MKUU
wa Mkoa wa Tanga, Magalula Saidi Magalula amewasimamisha kazi vigogo saba
Halamshauri ya wilaya ya Mkinga pamoja na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
hiyo, Amina Kiwanuka kuwachukuliwa hatua watumishi wengine 74 walipo chini ya mamlaka
yake,
Agizo
la Mkuu huyo wa Mkoa linafuatia ziara yake aliyotembelea wilaya hiyo hivi
karibuni wakati akijimbulisha kwa wananchi ambapo alibaini tatizo kubwa
lilikuwa ni watumishi wa Halmashauri hiyo kukataa kuhamia wilayani humo na
kuendelea kubaki kuishi Tanga mjini.
Kutokana
na hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa agizo la siku saba watumishi hao wawe
wamekwisha kuhamia kwenye wilaya hiyo jambo ambalo lilishindwa kufanyika
kutokana na watumishi hao kuendelea kubaki mjini.
Alisema
kuwa jana alikwenda wilayani humo kuangalia namna gani agizo hilo limekwenda
bado akakuta watumishi wakiwa wanaendelea na utaratibu wao wa kawaida wa
kuendelea kufanya kazi wilayani humo na kuandoka jioni kurejea Tanga mjini.
Waliosimamishwa
kazi na mkuu huyo wa mkoa ni Afisa Ardhi,Afisa Mifugo,Afisa Kilimo,Mkaguzi wa
Ndani,Afisa Uchaguzi,Afisa Manunuzi na Afisa Tehama kutokana na kukiuka
taratibu za utumishi.
“Mh Rais na Mh Waziri Mkuu waliagiza
watumishi hawa kuhamia wilayani humo lakini cha kushangaza mpaka leo hii wameshindwa
kufanya hivyo jambo ambalo linapelekea kudodora maendeleo kwenye wilaya hiyo
ambayo ilianzishwa miaka saba iliyopita “Alisema Magalula.
‘”Kutokana
na watumishi hao kuishi mbali na wilaya hiyo kumepelekea kukwamisha shughuli
mbalimbali za kimaendeleo na kuwafanya wananchi kushindwa kupata
mafanikio..hata ukiangalia ujenzi wa maabara bado upo kwenye hali ya chini sana
“Alisema RC Magalula.
Alisema kuwa kabla ya kufanya maamuzi hayo
alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kumpatia orodha ya watumishi wa
Halmashauri wanaotaka kuishi wilayani humo lakini walikataa kufanya hivyo.
Aidha
alisema kuwa amewasimamisha kazi ili kuona serikali ilivyokuwa makini katika masuala ya utendaji ikiwemo kuwataka
watumishi wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwani wakibainika
wahawatumiliwa.
Hata
hiyo alisema kuwa maamuzi hayo sio nguvu za soda kwa kuhakikisha
analishughulikia suala hilo ipasavyo kwa sababu lazima ufike wakati watumishi
watende haki kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo.
“Halmashauri ya Mkinga imeanzishwa miaka saba
iliyopita mpaka sasa bado maendeleo yameendelea kusuasua kutokana na watumishi
waliopenda kuwa karibu na kuwatumikia wananchi hii sio sawa hata kidogo.