KARIBUNI SANA

July 24, 2013
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIKAGUA TIMU YA URA YA UGANDA KABLA YA KUANZA MCHEZO HUO ANAYEFUATIA NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA,SAID SOUD NA KATIBU TAWALA WILAYA YA TANGA.

COASTAL IMARA

July 24, 2013
BENCHI LA Coastal Union akiwemo Kocha wao Mkuu,Hemed Morroco likiufuatilia kwa umakini mchezo kati yao na URA ya Uganda ambapo Coastal Union ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Keneth Masumbuko dakika 70.

URA YAKUBALI UTEJA KWA COASTAL UNION,YACHAPWA KIMOJA TU.

July 24, 2013
 KIKOSI cha Coastal Union kilichoifunga URA ya Uganda bao 1-0 leo kwenye uwanja wa Mkwakwani )

Na Oscar Assenga,Tanga.
BAO la dakika ya 70 lilofungwa na Keneth Masumbuko baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Uhuru Seleman kuwatoka mabeki wa URA na kutoa pasi kwa mfungaji huyo liliweza kuwapa heshima ya ushindi timu ya Coastal Union katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi yao na URA ya Uganda mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Mchezo huo ulikuwa na kasi ya vuta ni kuvute ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake,kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanja hapo zikiwa na hari na nguvu ya kutaka kuibuka na ushindi.

Kipindi cha pili Coastal Union walifanya mabadiliko yaliyoweza kuzaa matunda kwa kuwatoa Daniel Lyanga ambaye nafasi yake ilichukuliwa Selamani Kassim Selembe kwenye dakika ya 54 kuingia kwa mchezaji huyo kuliongeza nguvu ya mashambulizi na kuweza kufanikiwa kucheza nusu uwanja.

Wachezaji wengine walioingia kipindi cha pili na kuongeza kasi ya mashambulizi yaliyofanikiwa kudhaa matunda ni Abdi Banda aliyechukua nafasi ya Othumani Tamim dakika 55 huku dakika moja baadae akatoka Hamadi Juma na kuingia Mbwana Kibacha mabadiliko hayoa yaliweza kuleta mafanikio makubwa hasa kwenye kikosi hicho ambacho kinajiandaa na Ligi kuu Tanzania bara.

Wakionekana kucheza kwa kujipanga na kujituma ,Coastal Union waliweza kufanya mashambulio ya mara kwa mara langoni mwa URA huku wachezaji wake wakipiga mashuti yaliyokuwa yakiupanguliwa na mlinda mlando wa URA Bwete Brian.

Kutokana na mashambulio hayo Coastal Union waliweza nao kujipanga na kuweza kuthibiti vizuri safu yao ya ulinzi kwa kuwa makini na wachezaji wa URA hali ambayo iliwapa wakati mgumu kufika langoni mwa Coastal Union ambapo katika dakika ya 83 Coastal Union walifanya mabadiliko ya kumtoa Keneth Masumbuko na kumuingiza Pius Kisambale.

Huku URA walifanya mabadiko kwenye dakika ya 84 wakimtoaWalulya Derrick na kumuingiza Lugya Ronald ambapo licha ya kucheza vema lakini walishindwa kubadilisha matokeo kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili.

Wachezaji walioweza kuwakonga nyoyo vilivyo mashabiki wa Coastal Union ya Tanga ni Uhuru Selemani ambaye alikuwa mwiba kwa wachezaji wa Uganda huku mashabiki wa soka waliojitokeza kwenye mechi hiyo wakimshangilia vilivyo kila alipokuwa akigusa mpira,huku wachezaji wengine akiwemo Juma Nyoso,Haruna Moshi "Boban"wakiwafurahisha mashabiki kwa kucheza soka nzuri .

Kikosi cha Coastal Union leo kiliwakilishwa na mlinda mlango Shaban Kado,Hamad Juma,Othuman Tamim,Markus Ndehele,Juma Said "Nyoso"Jerry Santos,Uhuru Seleman,Crispian Odula,Daniel Lyanga,Haruna Moshi Boban na Keneth Masumbuko.

Kwa upande wa URA waliwakilishwa na Bwete Brian,Walulya Derrick,Sekijo Samweli,Munaaba Allan,Docca Musa,Agaba Oscar,Nkugwe Elkamack,Feri Ally,Ngama Emanuel,Lutimba Yayo,Kasibante James,Mugabi Yasin,Ganya Willy na Lugya  Ronald.