Ngoma Nzuri

April 21, 2013
MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid akiangalia ngoma ya wakina mama wa aliyokuwa ikichezwa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye Kata ya shume wilayani humo.

DC Mwanga akipata maelezo toka wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto

April 21, 2013
MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid Mwanga,akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto wakati akiwa katika ziara yake kwenye Tarafa ya Mlalo hivi karibuni.

DC Mwanga awaagiza wazazi kuchukuliwa hatua.

April 21, 2013

 

 Na Oscar Assenga, Lushoto.

MKUU wa wilaya ya Lushoto, Alhaj Majid Mwanga (juu Pichani)amewaagiza wevyeviti wa vijiji na maafisa watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka mahakamani wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wao shuleni na kuendelea kuwaacha majumbani pamoja na kuwapeleka mijini wakafanye kazi za ndani na kuuza karanga.

 Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni wakati akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Kata ya Shume (WDC) ambacho kilihudhuriwa na wataalamu wa kata pamoja na viongozi wa kata hiyo,DC Mwanga alisema ipo tabia iliyojengeka kwa wazazi kushindwa kuwapeleka watoto wao shuleni pindi wanapokuwa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na badala yake kuwapeleka wakafanya kazi hatutawavumilia lazima watachukuliwa hatua.

Alisema ni suala la ajabu sana mzazi ambaye anaona mtoto wake amefaulu na kuchukia badala ya kufurahia huku wengine wakiwashawishi kufanya vibaya mitihani yao ya mwisho ili watakapomaliza shule washindwe kuendelea na masomo hali hii lazima tuikemee kwa mikoni miwili kwani italeta adhari kubwa sana kwa vizazi zijavyo.

  “Lushoto sio sehemu ya kutafuta wafanyakazi wa ndani (Mahausigeli) wake houseboy hivyo wale wenye mawazo kama hayo wayaondoe kabisa kwani hawatafanikiwa hivyo wanachokifikiria “Alisema DC Mwanga.

Aidha aliwataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanya kwa uzalendo kwa kuwahi makazini kwa wakati pamoja na kuchukizwa kwa matokeo yaliyotokea mwaka uliopita hivyo waongeze bidii katika uwajibikaji wao ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwenye maeneo yao.

  “Wapo watu wanaowakatisha tamaa wanafunzi kutokana na matokeo mabaya kidato cha nne mwaka 2012 wasikubali kuwasikiliza badala yake wasome kwa bidii na matunda yake watayaona “Alisema DC Mwanga.

Aidha aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuacha kudanganyika na vijana ambao wanaweza kuwarubuni na kuwaaribia masomo yao pamoja badala yake wasome ili baadae waweze kupata matunda yanayotokana na elimu na kuwa na maisha mazuri.

               Mwisho.