KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

March 21, 2018

????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (katikati) akisisitiza jambo wakati akifungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu lililofanyika tarehe 21Machi, 2018 mjini Dodoma.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo mjini Dodoma kabla ya kufungua Kikao hicho.
????????????????????????????????????
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano  leo mjini Dodoma kabla ya kufunguliwa  kwa Kikao  cha baraza hilo .
????????????????????????????????????
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Bilauri akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akimsikiliza Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi hiyo Bw.Packshard Mkongwa mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifurahia jambo na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya mara baada ya kufungua kikao cha Baraza hilo mjini Dodoma.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Ernajoyce Hallo akiuliza swali wakati wa mkutano wa baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
PIX 8
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu)Bi. Maimuna Tarishi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo  leo mjini Dodoma  baada  ya kufungua Kikao hicho
PIX 9
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Packshard Mkongwa akiwasilisha mada ya Bajeti ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2018/19 wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Alex Ndimbo akiuliza swali wakati wa mkutano wa baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
…………………

Na.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kuwaasa wajumbe wa baraza kutoa maoni yatakayosaidia kufanikisha mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho Tarishi amesema kuwa Watumishi wote katika Ofisi hiyo wanao wajibu wakushiriki kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti ili kufanikisha azma ya Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Bila kujali nafasi zenu ni lazima mtambue kuwa mnao wajibu sawa katika kutoa maoni yatakayosaidia katika mchakato wa maandalizi ya bajeti” alisisitiza Bi.  Tarishi.
Akifafanua Tarishi amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikizingatia maoni ya wajumbe wa baraza hilo katika maandalizi ya bajeti hivyo ni wakati mwingine tena kwa watumishi hao kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika kikao cha baraza hilo kwa kutoa mchango utakaosaidia katika utendaji wa Ofisi hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti.
Aliongeza kuwa Baraza hilo linafanyika ikiwa ni utekelzaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayotaka Ofisi zote za Serikali kuwapa  nafasi watumishi wake kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo bajeti kupitia kwenye baraza la Wafanyakazi hali inayochochea maendeleo na tija katika utoaji wa huduma.
Naye Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya alieleza kuwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanapaswa kuwa kielelezo katika uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu yao ili kuwa mfano wa kuigwa hususan katika kukilinda na kuhakikisha uhai wa chama cha Wafanyakazi kwa kutenda haki kwa mujibu wa sheria zilizopo.
“Ni vyema kila mmoja wenu akawa wakili mzuri katika utendaji kuzingatia Ofisi hii ndiyo mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali bila kuacha kuzingazita uwepo wa TUGHE kwa kuwa ipo kwa mujibu wa Sheria namba 6 inayoeleza masuala ya ajira na usajiri wa vyama vya Wafanyakazi”.Alisema Bw.Mchenya
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo Bw.Yona Mwakilembe  amesema kuwa  maoni ya watumishi katika Ofisi hiyo yamekuwa yakizingatiwa kwa ukamilifu  hali inayoongeza morali kwa watumishi wa Ofisi hiyo.
“Tangu nimehamia hapa nimeshuhudia kwa kiwango kikubwa kwamba maoni tunayotoa kupitia baraza la wafanyakazi yanazingatiwa hivyo ni jambo la kujivunia na tunapongeza kwa hatua hii” Alisisitiza
Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu linafanyika mjini Dodoma leo Machi 21, 2018 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa uliowekwa na Serikali kupitia Wizara,  Mikoa,  Wilaya, Idara, Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma kuwapa nafasi watumishi kutoa maoni yao kupitia baraza la wafanyakazi ili kuongeza tija na uwajibikaji katika Taasisi husika.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WAKUU WA KAMPUNI YA TIGO, PIA AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA KAMPUNI YA FERROSTAAL KUTOKA UJERUMANI NA DENMARK IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

March 21, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mauricio Ramos Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Millicom International Service LLC (wanne kutoka kushoto) ambayo ina miliki Kampuni ya simu yaTigo aliyefika Ikulu pamo jana ujumbe wake.



RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Watendaji Wakuu wa Kampuni ya FERROSTAAL kutoka nchini Ujerumani na Denmark Ikulu jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto ni Balozi wa Denmark EinarHebogard Jensen aliyeongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzona Watendaji Wakuu wa Kampuni ya FERROSTAAL kutoka nchini Ujerumani na Denmark Ikulu jijini Dar es Salaam


Raiswa Jamhuri yaMuunganowa Tanzania MheshimiwaDkt. John PombeMagufuli akimpongeza Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda IGP Mstaafu Ernest Mangu mara baada ya hafla fupi ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamo jana Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi MejaJeneralimstaafu Simon Marco Mumwi(kushoto)pamo jana Balozi mpya wa Tanzania nchini Rwanda IGP Mstaafu Ernest Mangu
kulia) mara baada ya hafla fupi ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam



RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania MheshimiwaDkt. John PombeMagufuliakimsikilizaBalozimpyawa Tanzania nchini Rwanda IGP Mstaafu Ernest Mangu (hayupopichanialipokuwaakizungumza) marabaadayahaflafupiyauapishoIkulujijini Dar es Salaam.


RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali mstaafu Simon Marco Mumwi kumaliza kuzungumza katika hafla fupi ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozimpyawa Tanzania nchini Rwanda IGP Mstaafu Ernest ManguakiwakatikapichanaMkuuwaJeshi la Polisinchini, IGP Simon Sirro(wa kwanza kulia)KamishnaJeneraliwaUhamiajiDkt. Anna Makakalawa kwanza kushoto, MkuuwaJeshi la MagerezaKamishnaJeneraliwaMagerezaDkt. JumaMalewa(wapilikutokakulia)pamojanaviongoziwenginewaJeshi la polisimarabaadayahaflayaUapishoIkulujijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU