MAMA KIKWETE AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO NA KUTOKUBAGUANA BALI WASAMBAZE UPENDO

May 11, 2015

Na Anna Nkinda – Lindi

Vijana mkoani Lindi wametakiwa kuwa wazalendo na kutobaguana bali wasambaze upendo na kujiona wote ni sawa kwa kufanya hivyo wataondoa chuki na kudumisha amani, mshikamano na umoja katika jamii inayowazunguka.

Mwito huo umetolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua klabu zalendo zilizopo katika  Manispaa ya Lindi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kama jamii itajenga tabia ya ubaguzi italeta chuki na upendo utatoweka na hivyo kusababisha vurugu zitakazopoteza  amani iliyopo.

Alisema uzalendo ni kiini cha maendeleo hivyo huwezi kuwa mzalendo kama hupingi rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya, hutunzi mazingira, hushiriki kuchangia utoaji wa damu salama na kutokuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo katika jamii yako.

Mama Kikwete alisema, “Leo hii nimezindua klabu zalendo, Mzalendo ni mtu mwenye huruma na mtu anayeona thamani ya kitu alichonacho tunzeni vitu mlivyonavyo ikiwemo Amani ya nchi yetu na mjitoe kufanya kazi kwa bidii ili muweze kupata maendeleo.

Aidha Mama Kikwete  aliwahimiza wanafunzi kujitendea haki kwa kusoma kwa  bidii hadi elimu ya chuo kikuu kwa kufanya hivyo wataweza kuajiriwa na kujiajiri katika katika fani mbalimbali na kujiletea maendeleo katika mkoa wao wa Lindi.

Akisoma historia fupi ya klabu zalendo Mwalimu Mwajuma Malugu ambaye ni Mwenyekiti alisema lengo kuu la kuanzishwa kwa klabu hiyo ni kuutetea na kuulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibari ndiyo maana wanatumia namba za #26464#ikimaanisha tarehe 26 mwezi wa 4 mwaka 1964 siku ya muungano. 

Aliyataja malengo mengine kuwa ni kuhamasisha wanafunzi na vijana waliopo mtaani kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao kwa kufanya hivyo wataepukana na mambo yasiyofaa kwa maslai ya nchi yao.

“Mafanikio tuliyoyapata ni kujenga umoja na ushirikiano, kuongeza idadi ya wanachama na hii inatokana na kufunguliwa kwa matawi mengine ya uzalendo mashuleni na mitaani, kuongeza na kupanua uelewa kwa wanafunzi na raia kuhusu  klabu ya uzalendo, kuwahamasisha watu kuwa wazalendo na kujitoa katika uchangiaji wa damu, kupinga rushwa, madawa ya kulevya pamoja na kulinda Amani ya nchi.

Mwalimu Mwajuma alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni uhaba wa fedha kwa ajili ya kuandaa makongamao na mabonanza yatakayosaidia  kuimarisha harakati zote za klabu ya uzalendo na kushindwa kutuma wawakilishi katika mikutano na makongamano ya wanaklabu ngazi ya taifa. 

Pia kikundi kimekosa semina kwa wanaklabu hali inayoplekea wanachama  kukosa uelewa wa kutosha kuhusu madhumuni ya klabu hiyo.

Klabu zalendo ilianzishwa na walimu wa Shule ya Sekondari Lindi katikati mwa mwaka jana hadi sasa inawanachama 1450 kutoka shule za Sekondari Mkonge, Angaza, Ngongo, Ng’apa, Chikonji, Mingoyo, Kineng’ene , chuo cha ufundi VETA na walimu wa shule za msingi pamoja na wanafunzi wao.

Pia klabu hiyo imehusisha vijana kutoka mtaani wanaofanya kazi za udereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wavuvi na wanavikundi vya Sanaa.

Mama Kikwete aliahidi kukipatia kikundi hicho  mipira 20 na jezi seti 10 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ambao watashiriki katika mashindano mbalimbali `na kuangalia utaratibu wa kuwapatia mradi ambao utawasaidia kuwainua kichumi.

MH. PINDA AFUNGUA MAONYESHO YA ELIMU MKOANI DODOMA

May 11, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Sista  Flosy Sequeire, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Saint Francis ya Mbeya tuzo maalum ya kutambua  ufalu mzuri wa wanafunzi wa shule  hiyo  wakati alipofungua  maadhimisho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Wemgne kutoka kushoto ni  Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma  Mei 11, 2015  kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Mei 12, 2015.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wki ya elimu wenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Kulia ni Bibi Agnes Israel. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya  Mungula ya Mkarama,  Singida ambayo inawafundisha watoto wa kabila la Wahadzabe baadaya kufungua maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiza mtoto wa kabila la Wahadzabe,, Kone Paschal wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Bweni ya Mngulu mkoani Singida katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zaBritish Coucil wakati alipotembelea banda  la Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya Elimu aliyoyafungua kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHANONGO AHARIBIWA DILI NA YANGA TP MAZEMBE

May 11, 2015

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MPANGO wa kiungo mshambuliaji Haroun Chanongo wa Simba SC kwenda kucheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uko shakani, kufuatia mchezaji huyo kuumia kifundo cha mguu.
Winga huyo mwenye nguvu na kasi, aliumia mwishoni mwa Aprili akiichezea Stand United dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Chanongo alitakiwa kwenda Lubumbashi, DRC mwezi huu kwa ajili ya kufanya majaribio, lakini imeshindikana kwa sababu ya maumivu ya enka, amesema Meneja wake, Jamal Kisongo.
Haroun Chanongo kulia amefungwa PoP mguuni na kushoto akiichezea Taifa Stars dhidi ya Malawi hivi karibuni

“Chanongo kwa sasa amefungwa PoP (plasta gumu) kwenye kifundo cha mguu, maana yake hawezi kwenda Mazembe, kwa kweli ni pigo sana,”alisema Kisongo.
Meneja huyo wa Mbwana Samatta pia anayecheza TP Mazembe, amesema kwamba kwa uzoefu wake maumivu ya Chanongo huchukua hadi wiki sita mchezaji kupona.
“Hizo wiki sita anauguza maumivu, apone ndiyo aanze mazoezi mepesi kama wiki mbili. Yaani huyo hadi awe sawa si sasa hivi tena,”amesema kwa masikitiko Kisongo.
Kwa sasa Chanongo anacheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga kutoka klabu yake, Simba SC tangu Desemba mwaka jana.
Lakini tayari Simba SC imesema haitamuhitaji tena mchezaji huyo, baada ya kuwapo madai hana mapenzi na klabu hiyo.
CHANZO.bINZUBEIRY

KAVUMBANGU AOTA MBAWA YANGA SC, ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC

May 11, 2015

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
DIDIER Kavumbangu (pichani juu) ataendelea kuichezea Azam FC kwa mwaka mwingine mmoja, maana yake lile dili kurejea Yanga SC limekufa kifo cha kawaida.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kwamba Mrundi huyo ameongeza Mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo.
“Ni kweli tumemuongezea Mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wetu, Didier Kavumbangu, hii ni kutokana na kuvutiwa na kazi yake nzuri katika msimu wake wa kwanza,”amesema Kawemba.
Kabumbangu alisaini mwaka mmoja msimu huu kutoka Yanga SC, lakini mwishoni mwa msimu kukaibuka tetesi anarejea Jangwani.
Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ni shabiki mzuri wa Kavumbangu na ni kweli alitamani kufanya kazi tena na mkali huyo wa mabao.
Hata hivyo, Azam FC baada ya kuvutiwa na shughuli ya Mrundi huyo kwa msimu aliowatumikia, wameamua kuongeza naye Mkataba.
Katika msimu wake mmoja tu wa kwanza Azam FC, Kavumbangu ameifungia timu hiyo mabao 17 katika mechi 36 za mashindano yote, kati ya hato, 11 katika Ligi Kuu.
Wakati akiwa Yanga SC, Kavumbangu aliifungia timu hiyo mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote ndani ya misimu miwili.

MZEE MANGULA NA NAPE WAHANI MSIBA WA JOHN NYERERE

May 11, 2015

 Picha ya Marehemu John Nyerere aliyefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda.

Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi. AMENI
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akisaini kitabu cha rambi rambi nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam ambapo alifika kumpa pole Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia msiba wa mtoto wa Baba wa Taifa John Nyerere.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.
 Ndugu akitoa pole kwa Mama Maria Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa mkono wa pole Mama Maria Nyerere kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mama Maria Nyerere alipofika nyumbani kwake kumpa pole kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere, wengine pichani ni Makongoro Nyerere (kushoto), Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi, na Anna Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John Nyerere.
(Picha zote na Adam Mzee)

Taasisi ya Imetosha yatoa msaada kwa kituo cha Buhangija Shinyanga.

May 11, 2015


Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisis ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300. Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo  imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.
Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji kula kila siku.
 
Mkuu wa kituo hicho alisema anashukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.
 
Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
Baadhi ya missada iliyotolewa na Imetosha pembeni kulia ni mabelo mawili ya mguo.
Mkuu wa kituo hicho Bw Peter Ajali akiongea na watoto wa kituo hicho akieleza dhamira ya ya asasi ya Imetosha kwao.
Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet
 
Picha na habari kwa hisani ya TBN kanda ya kati.
RAIS KIKWETE KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE RASMI NCHINI ALGERIA

RAIS KIKWETE KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE RASMI NCHINI ALGERIA

May 11, 2015

3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari baada ya  kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa ameongozana na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah akiwasili katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers kwa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa  na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na kikundi cha utamaduni  katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya  dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na mabalozi wa nchi za Kiafrika katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya  dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
PICHA NA IKULU

WAKUU WA TAASISI ZA KUZUIA RUSHWA BARANI AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUANGALIA JINSI WATAWEZA KUPAMBANA NA KUFIKIA MALENGO YA KUTOKOMEZA RUSHWA NDANI YA BARA LA AFRICA

May 11, 2015

SAM_2509
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa kutoka Ghana Mh.Daniel Batidam akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2498
Makamu Mwenyekiti bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa Mh.Florince Ziyambi kutoka Zimbabwe
SAM_2494
Muongoza vikao kutoka Kenya Mh.John Tuta akitambulisha wajumbe
SAM_2497
SAM_2499SAM_2503
SAM_2514
Mwaandishi wa habari Merry Mwita akiuliza maswali katika mkutano huo
SAM_2504
Muonekano ndani ya ukumbi
SAM_2506
SAM_2522
Picha ya Pamoja
Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa barani Africa wamekutana  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.
Wakuu hao ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa barani Afrika AUABC iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za Afrika ambapo mwenyekiti wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema kuwa wanatarajia kwa mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa ndani ya bara hili.
Amesema kuwa kiwango kikubwa wanaangalia jinsi gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii kwa maana ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu za kiafrika.
Pamoja na hayo amesema kuwa tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni mfumo uliopo ambao unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo alisisistiza kwa wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa.
Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa
MAAMUZI YA KAMATI TFF YA RUFAA NA NIDHAMU

MAAMUZI YA KAMATI TFF YA RUFAA NA NIDHAMU

May 11, 2015

index 
Baada ya mahojiano kati ya mrufani Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF     Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:- 
  1. Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
  2. Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).
3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya  kusikilizwa.
Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani  angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.
4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.

Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.
Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.
Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/
Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.