WAJASILIAMALI WAHIMIZWA KUTUMIA INTERNET KUTANGAZA BIASHARA ZAO

September 06, 2015

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim akimkabidhi picha ya mlango wa asili ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi jijini Birmingham, Bw. Prince Kateka II ikiwa ni ishara ya kukaribishwa Zanzibar.
Wafanyabiashara wamehimizwa kutumia mtandao wa internet kutangaza bidhaa na huduma wanazotoa kwa kuwa njia hiyo ni nafuu na inawafikiwa watu wengi kwa haraka. Hayo yalibainishwa na Bw. Dickson Inachee, Raia wa Uganda alipokuwa anatoa mada katika kongamano la siku mbili la Watanzania wanaoishi Uingereza lililomalizika jijini Birmingham siku ya Jumamosi tarehe 05 Septemba 2015. 
Bw. Inachee alieleza kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya watu milioni 9.3 wanatumia internet nchini Tanzania. Kati ya hao watu milioni 2.4 wanatumia mtandao wa face book, hivyo ukitangaza katika face book, tangazo lako litawafakia watu wengi kuliko kutumia vyombo vilivyozoeleka kama magazeti. 
Aliendelea kueleza kuwa tangazo katika face book linatozwa Dola moja ya Marekani na kwa Tanzania litawafikia watu milioni 2.4 lakini tangazo hilo hilo ukilitoa katika gazeti linalopendwa sana nchini Tanzania utatakiwa kulipa Dola 300 na litawafikia watu elfu 50 tu. 

Bw. Inachee alimalizia mada yake kwa kusisitiza kuwa, endapo wajasiliamali nchini Tanzania wanataka kufanya biashara kwa kutumia mbinu mpya za kibiashara, basi hawana budi kutumia internet kutangaza bidhaa zao kwa kuwa njia hiyo itawaondolea mzigo wa kulipa fedha nyingi katika vyombo vilivyozoeleka sanjari na kuwafikia watu wengi zaidi.
Bw. Anthony Chaula akiwasilisha mada
Katika hatua nyingine, wanadiaspora walioshiriki kongamano hilo, wameridhishwa na hatua ya Serikali ya kuwapa hadhi maalum katika Katiba inayopendekezwa.

 Akiwasilisha mada katika kongamano hilo, Bw. Anthony, Chaula kutoka Idara ya Uhamiaji alisema kuwa Katiba inayopendekezwa itakapopitishwa, wanadiaspora watapewa hadhi maalum tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaonekana kama wageni wengine.
Wakati wa kongamano hilo, baadhi ya Watanzania wanaoishi Uingereza walitumia fursa hiyo kutangaza shughuli zao za kibunifu wanazofanya katika nchi hiyo. Bw, Ayoub Mzee alizindua rasmi progaramu yake inayoitwa AITV APP. Programu hiyo inamwezesha mteja, kwa kutumia simu ya mkononi au kifaa kingine chenye internet kuangalia vituo takriban vyote vya televisheni vya Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa gharama ya Dola za Marekani sita kwa mwezi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo yas Nje, Balozi Liberata Mulamula aksalimiana na Bw. Ayoub Mzee kabla ya kuzindua programu ya AITV APP.
Mtanzania mwingine Bw. Mediremtula ameanzisha kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa tablet. Anasema aina ya tablet anayotengeneza inafanya vizuri kibiashara katika nchi za Uingereza na Urusi na hivi sasa yupo katika mchakato wa kutengeneza aina nyingine ya tablet kwa ajili ya Tanzania.
Katika masuala ya sanaa hasa ya uigizaji wa filamu, Watanzania wa Uingereza hawakuachwa nyuma. Kuna Watanzania wamecheza filamu ijulikanayo Goingbongo. Filamu hiyo imeigizwa katika viwango vya kimataifa na walioafanikiwa kuiangalia wamethibitisha kuwa ni ya kimataifa kweli.
Kongamano hilo lilifungwa rasmi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Zanzibar, Bw. Salim Maulidi Salim ambaye alisisitiza umuhimu wa wanadiaspora kuwekeza nyumbani kwa madhumuni ya kukuza uchumi na kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa jamaa zao.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe akitoa cheti cha kutambua mchasngo wa mmoja wa wadhamini wa kongamano. Na Ally Kondo, Birmingham

NI MARUFUKU WATOTO KUMILIKI LESENI ZA MADINI

September 06, 2015

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama), akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani, Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao.
 Sehemu ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu. Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.
Washiriki mbalimbali wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao, wakiuliza maswali wakati wa semina hiyo. Semina ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.
 Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5, mwaka huu mjini Singida.
Viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mkoani Singida walioshiriki katika Semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao. Wa tatu kutoka kulia (Waliokaa kwenye viti) ni Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati – Singida na Kulia kwake ni Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani. Semina ilifanyika Septemba 5, mwaka huu.

SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA TUME YA UTUMISHI YA BUNGE LA NIGERIA OFISINI KWAKE LEO

September 06, 2015

  Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza.
 Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
 
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Ajira na Maendeleo ya Watumishi ya Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Salehe Pamba akifafanua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria (hawapo pichani) waliotembelea Bunge leo kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge. 
 Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Tume ya Utumishi ya Bunge la Nigeria Mhe. Yepwi Stephen Dako akiuliza namna ambavyo Tume ya Bunge la Tanzania husimamia Watumishi wa Bunge la Tanzania katika kuleta ufanisi kazini wakati walipokutana na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo wa tume ya Nigeria upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria na wenyeji wao kutoka Bunge la Tanzania mara baada ya kukutana nao Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akielezea baadhi ya masuala ya Kiutawala katika usimamizi wa Bunge kwa  wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge  la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. 
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiagana na Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako baada ya kumaliza mazungumzo yao.
BI. SAMIA SULUHU AHAIDI KUDHIBITI WIZI WA DAWA HOSPITALI ZA SERIKALI

BI. SAMIA SULUHU AHAIDI KUDHIBITI WIZI WA DAWA HOSPITALI ZA SERIKALI

September 06, 2015
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam janaBaadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.
 MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema Serikali watakayoiunda endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi watahakikisha wanadhibiti wizi wa dawa kwenye hospitali za Serikali ambazo zimekuwa zikiuziwa wananchi katika maduka ya dawa mitaani. Bi. Suluhu katoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia katika mikutano ya anuai ya hadhara Jimbo la Ilala kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo amebainisha kuwa dawa zote zitakuwa zinaingizwa katika mtandao maalum na kuzifuatilia na endapo zitatumika nje ya utaratibu itabainika na hatua kuchukuliwa. Alisema mtandao huo utafanikiwa kukabiliana na kero ya ukosefu wa dawa katika hospitali za serikali kwani dawa hizo zimekuwa zikiibwa kwenye hospitali za Serikali na kuuzwa nje katika maduka ya dawa binafsi na hospitali binafsi. "...Tunaamini mfumo huu utatusaidia kukabiliana na wizi wa dawa na rushwa hospitalini...unakuta daktari anakuandikia dawa alafu anakuelekeza duka la kwenda kununua sasa unajiuliza huyu mtu kajuaje kama sio yeye kapeleka pale," alisema Bi. Suluhu. Pamoja na hayo mgombea huyo mwenza, aliwashauri wananchi kuukubali utaratibu wa kutumia mfumo wa bima ya afya kwa matibabu ambao umekuwa ukimlazimu mwananchi kuchangia kiasi kidogo cha fedha na kutibiwa mwaka mzima bure katika hospitali zote zinazotumia utaratibu huo, kwani alidai utawasaidia wengi. "...Unajua ugonjwa unampata mtu ghafla na muda wowote haijalishi una fedha za kujitibu au la, lakini kama unabima ya afya waweza kutibiwa muda wowote hata kama hauna fedha wakati huo," alisisitiza Bi. Suluhu. Aidha, Bi. Suluhu alisema serikali watakayoiunda itajitahidi kupima maeneo mengi ya ardhi na kuyatoa kwa wananchi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi. Alisema Serikali yao pia imekamilisha utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni ambao wanadai fidia na itawalipa wananchi hao kwa thamani ya sasa ya ardhi kwani 2004 hadi sasa ni muda mrefu na ardhi imepanda thamani. Akizungumzia kero ya foleni, alisema ili kumaliza kero hiyo na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya kisasa pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la Kibaha ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es Salaam kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa barabara ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni katika barabara kubwa. Aidha Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili kupunguza msongamano katika barabara kubwa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

DALADALA LAACHA NJIA NA KUPARAMIA GENGE NA BAJAJ MAENEO YA KITUNDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

September 06, 2015
 Wananchi wakiangalia ajali ya daladala lenye namba za usajili T 456 BVT lililoacha njia kutokana na mwendokasi na kuparamia genge na bajaj yenye namba MC 611 ADC, maeneo ya Kitunda relini barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam leo asubuhi. Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa daladala kukimbilia abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
 wananchi wakiangalia ajali hiyo.
 Daladala hilo likiwa ndani ya genge baada ya kuacha njia.
Bajaj namba MC 611 ADC, likiwa kanda ya daladala hilo baada ya kugongwa. 

SAFARI YA MATUMINI IPO BUMBULI

September 06, 2015


 Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Devid Chanyeghea akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia vipaumbele vyake wakati akianza kampeni baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumrejesha kugombea jimbo hilo baada ya kuwekewa pingamizi na mpinzani wake. Kushoto ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga, Ismail Massoud



 Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Devid Chanyeghea, akiwaonyesha waandishi wa habari fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo amedai mpinzani wake aliongeza kipengele cha maandishi cha kugonbea Udiwani na Ubunge ambacho kilipelekea kuuzuiwa kugombea na kudai kuwa yeye ni mgombea wa Ubunge tu.

CHADEMA JIMBO LA MOSHI MJINI YATANGAZA WAGOMBEA UDIWAI WAKE.

September 06, 2015

Mkutano wa Hadhara wa Kampeni wa Utamburisho wa wagombea wa Udiwani katika jimbo la Moshi mjini.

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Korongoni ,manispaa ya Moshi,Ally Mwamba akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Korongoni (hawapo pichani).

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Rau ,manispaa ya Moshi,Peter Kimaro akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Rau (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Ng'ambo ,manispaa ya Moshi,Genesis Kiwelu akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Ng'ambo (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Miembeni,manispaa ya Moshi,Mbonea Mshana akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Miembeni (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Msaranga ,manispaa ya Moshi,Anna Mushi akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Msaranga.(hawapo pichani).

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Bomambuzi ,manispaa ya Moshi,Ludos Tarimo  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Bomambuzi(hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Majengo,manispaa ya Moshi,Peter Minja akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Majengo (hawapo pichani)
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kilimanjaro ,manispaa ya Moshi,Afrikan Mlay  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi kata ya Kilimanjaro (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Korongoni ,manispaa ya Moshi,Charles Mkome Mkalakala akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Pasua (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kaloleni ,manispaa ya Moshi,Francis Shio akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kaloleni (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kiusa ,manispaa ya Moshi,Stephen Ngasa akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kiusa .
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Kaloleni ,Manispaa ya Moshi,Reward Shelukindo akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Kaloleni  (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Shirimatunda,manispaa ya Moshi,Makupa Jonathan akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Shirimatunda. (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi,Hawa Mushi  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mawenzi (hawapo pichani)

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Mji Mpya ,manispaa ya Moshi,Abuu Shayo akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mji Mpya .

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Nganga mfumuni ,manispaa ya Moshi,Anthony Lyimo  akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Mfumuni(hawapo pichani

Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Soweto ,manispaa ya Moshi,Collins Tamimu akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Soweto.
Mgombea wa nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chadema na UKAWA katika kata ya Njoro ,manispaa ya Moshi,Jomba Koi akiomba kura mbele ya wakazi wa mji wa Moshi wanaoishi Soweto.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.