TANGA UWASA ,JUIN COMPAY LIMITED WAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO KUTEKELEZA MRADI WA MAJI WILAYANI LUSHOTO

March 01, 2018
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares kushoto akisaini mkataba wa kutekeleza mradi wa Maji wilayani Lushoto na Mkandarasi wa mradi huo Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambao utagharimu milioni 700 wanaoshuhudia nyumba kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares kushoto akisaini mkataba wa kutekeleza mradi wa Maji wilayani Lushoto na Mkandarasi wa mradi huo Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambao utagharimu milioni 700 wanaoshuhudia nyumba kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares kushoto akisaini mkataba wa kutekeleza mradi wa Maji wilayani Lushoto na Mkandarasi wa mradi huo Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambao utagharimu milioni 700 wanaoshuhudia nyumba kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares na Mkandarasi Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambaye atatakeleza mradi wa maji wilayani Lushoto mbao utagharimu milioni 700 wakibaliashana hati za makubaliano mara baada ya kusaini mkataba
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares na Mkandarasi Justice Kato  kutoka kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambaye atatakeleza mradi wa maji wilayani Lushoto mbao utagharimu milioni 700 wakionyesha hati za makubaliano mara baada ya kusaini mkataba
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares akizungumza wakati wa utiliaji saini wa makubaliano hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akizungumza wakati wa utiliaji saini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa maji wilayani Lushoto kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares
Mkandarasi Justice Kato  kutoka Kampuni ya Juin Company Limited Civili&Building Contractors ambaye atatakeleza mradi wa maji wilayani Lushoto ambao utagharimu milioni 700 akizungumza katika wa utiliaji saini wa makubaliano ya mkataba halfa iliyofanyika mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafiri wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Aram Phares kushoto ni Mkandarasi wa ambaye atatekeleza Mradi wa Maji wilayani Lushoto kutoka kampuni ya Juin Company Limited  Civili&Building Contractors Justice Kato
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi kulia akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Aram Phares

NEWS: TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana

NEWS: TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana

March 01, 2018

Zaidi ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.
Madiwani hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).
Madiwani hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi unaotekelezwa katika eneo hilo.
Pamoja na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.
Wakiwa kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.
Eneo hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.
Aidha katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kujifunza, faida za mabunge ya jamii, na kujifunza miradi ya maendeleo ya kuwezesha wananchi kiuchumi ambayo inatekelezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wananchi wa Kipunguni.
Katika mabadilishano ya uelewa mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya, Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao.
Alisema awali alikuwa akidhani kwamba asasi hiyo ina mlengo wa kisiasa kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwao lakini baada ya elimu hii amebadili uelekeo na kuitaka taasisi hiyo kupeleka elimu Tanzania nzima.
Alisema, "Anaona kwamba TGNP ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika nyanja zote."
Diwani huyo wa Ijombe ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii alisema pamoja na kubadili mwelekeo aliwataka wabunge kuona kwamba wanapoandaa miradi hawaandai mbunge mpya bali kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.
Katika mkutano huo walitoa maazimio kadhaa ya kufanyiwa kazi katika halmashauri.
Miongoni mwa maazimio hayo ni namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake kuhusu ile asilimia 5 na kutekeleza dhana ya viwanda.
Kwa mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.
Pia imeelezwa haja ya TGNP Mtandao kuendelea kutoa elimu kwa kusaidiwa na mabaraza ya halmashauri kuhusu rasilimali fedha na kufuatilia uwekezaji katika ujenzi wa hosteli kupunguza umbali wa watoto wa kike kutembea kufuata shule.
Mambo mengine ni kuona kwamba uandaazi wa bajeti unaanzia ngazi ya kijiji au mtaa badala ya kata na kukosekana kwa sauti za wananchi katika bajeti.
TGNP Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha miaka 25 sasa, kwa kipindi chote hicho kimeshirikiana na taasisi za serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Na Mwandishi wetu Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.Diwani wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Ukenyenge ya wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Anderson Mandia akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washiriki wakiendelea kujadiliana wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

VIDEO : MBUNGE MGIMWA ATOA VIFAA VYA UJENZI JIMBONI MWAKE

March 01, 2018
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo

WAFADHILI WARIDHISHWA NA MRADI NA MAENDELEO YA MRADI WA MAJARIBIO WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA WATOTO WALIO NA FURSA NDOGO

March 01, 2018
 Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiwaonyesha mmoja ya sehemu zinazotunzwa tablets ambazo zinatumiwa kufundishia wanafunzi akiwa na wafadhili wa mradi huo


  Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akiwaongoza wafadhili wa mradi huo kutembelea maeneo mbalimbali unapotekelezwa wilayani Pangani
  Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akiwa na wafadhili wa mradi huo wakiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kutumia teknolojia ya Tablets
Katibui Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kulia akiteta jambo na wafadhili wa mradi huo
Wadau wa mradi  wa  miaka mitano wenye lengo la kutumia  teknolojia ya kisasa kuwawezesha watoto waliona fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) wameeleza kuridhishwa kwao na maendeleo ya majaribio hayo.
Wadau ambao walikuwa na ziara ya siku moja kutembelea vijiji mbalimbali vya nradi huo katika wilaya za Muheza na Pangani wadau aho ambao walikuwa pamoja na Mwakilishi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Tanzania, Michael Dunford, Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya Kanda ya Afrika Mashariki, Anne Ndong-Jatta wakiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said.
Wakitoa maoni wakati wakipewa maelezo walisema ni wazi mradi umeanza kuonyesha uwezo wa teknolojia kuamsha ari ya kujifunza na kusoma.
Taarufa za awali za mradi na ushuhuda tuliouona inaonyesha kuwa mpango huu wa kiteknolojia una uwezo wa kuwasha mwamko wa elimu miongoni mwa watoto na wazazi na unapaswa kutiliwa maanani, alieleza  Mhandisi Said wakat wa ziara hiyo.
Pia Mhandisi Said alisema kuwa ni wazi pia kuwa kuwatambulisha wananchi katika teknolojia ya kisasa wakiwa na umtri mdogo kunawahakikishia  watoto hao kuwa hawawezi kunyanyaswa hapo baadaye wakiwa wakubwa.
Naye Ndong-Jatta alisema kuwa mradi unaonyesha haja ya kuangalia uwezekano wa kupunguza tatizo la kutojua kusoma na kuandika kwa wazazi kama njia mojawapo ya kuamsha mwamko wa elimu miongoni mwao na kuwawezesha kuwasukuma watoto kwenda shule.
Zaidi ya watoto 2,500 kutoka katika vituo 142 vilvyopo katika wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza na Pangani walipewa tablet mpya aina ya Google Pixel C, zilizotolewa kwa hisani ya Google. Tableti hizo zimewekewa mifumo ya elimu kutoka kwa washindi watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE. Washindi hawa walichaguliwa kutoka katika timu 198 napaneli ya majaji 11 wa kujitegemea na walio wataalamu na kutangazwa mwezi September, 2017 wakati wa wiki ya BarazaKuu la Umoja wa Mataifa
Mradi huo wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Mareka ni milioni 15. Mradihuu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wa bunifu kubuni na kuandaa zana za kusaidia kuondoa ujinga duniani na kuwasaidia watoto ambao hawajapata fursa ya kwenda shule kujifunza wakiwa nyumbani.

SERIKALI YAAGIZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI WA KIGENI KATIKA KISIWA CHA IZINGA MKOANI KAGERA

March 01, 2018

.........................................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 7 kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe kufanya Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa nchi jirani wanaodaiwa kulima na kufiga ndani kisiwa cha Izinga kilichopo ndani ya Pori la Akiba la Kimisi mkoani Kagera.

Ametoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake wilayani Karagwe mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kupokea taarifa na malalamiko ya kukamatwa kwa mifugo ya Watanzania ndani ya kisiwa cha Mubali huku kukiwepo mazao yanayodaiwa kulimwa na wananchi wa Rwanda katika kisiwa kingine cha Izinga.

“Ndani ya siku saba hicho kisiwa cha Zinga msafishe kila kitu, Mkuu wa Wilaya msaidie mtengeneze kikosi kiende kule kitoe takataka zote zilizoko kule, inakua ngumu kuadministrate (kutawala) wengine wa kwetu tunawatoa alafu wa nchi nyingine wamekaa, unatawalaje?”. Aliuliza kwa mshangao Dk. Kigwangalla.

Alisema watanzania wakienda upande wa Rwanda kuvua samaki ziwa Ihema wanauawa mara moja bila mjadala, wakati kwa upande wa Tanzani raia wa nchi hiyo wapo wengi na wengine wamepewa Uraia wa Kuasili (Citizenship by Naturalisation, CN) na huwa hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji wala mauaji  jambo ambalo alisema  ipo haja kama nchi kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kenyata alisema atatekeleza agizo hilo la Waziri Kigwangalla kwa haraka ndani ya muda uliotolewa ili kumaliza mgogoro huo.

Katika hatua nyingine Waziri Kigwangalla alikataa ombi la Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa la kuiomba Serikali iwamegee wananchi wa vijiji jirani sehemu ya eneo katika Pori la Akiba Kimisi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.

“Ardhi mimi sitatoa, sjui mlima sjui nini, siwezi kwenda kupeleka hilo ombi kwa Mhe. Rais, kabisa, hicho ni kitu ambacho hatuwezi kufanya kwa sasa’,” Alisisitiza Dk. Kigwangalla.

Mbunge huyo pia aliiomba Serikali kuweka uzio wa waya kwa ajili ya kutenganisha mpaka wa hifadhi hiyo na vijiji kwa madai ya kuepuka ukamataji wa mifugo ya wananchi unaofanywa na askari wa wanyamapori kwenye ardhi za vijiji na kuingizwa hifadhini na kutozwa faini, hoja iliyopigwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla alikataa ombi hilo na kusema kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ni mikubwa kuwezesha utekelezaji wa ombi hilo. Alisema Serikali itatengeneza mtandao wa barabara zinazounganisha hifadhi hiyo na vijiji kwa ajili ya kuimarisha doria na shughuli za utalii pamoja na kujenga ofisi ndogo za pori hilo katika kila wilaya inayohusika na pori hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka aliwataka wananchi wanaofanya vitendo vya kuingiza mifugo kwenye pori hilo wakati wa usiku kuacha mara moja kwa kuwa wakimatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema malalamiko ya wananchi hao kuwa askari wa wanyamapori wanakamata mifugo yao kwenye maeneo ya vijiji na kuiingiza hifadhini kwa lengo la kuwatoza faini kuwa sio ya kweli na kwamba malalamiko yanakuja kwakuwa hukamatwa asubuhi wakiwa wameshatoka kulisha mifugo hifadhini.

Kisiwa hicho cha Izinga ambacho kipo katika wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kina ukubwa wa Kilomita za Mraba 12 na kinapakana na nchi Rwanda.
Pori la Akiba Kimisi liliqnzishwa mwaka 2003 kwa Tangazo la Serikali na 116 na lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,030. Pori hilo lina wanyamapori mbalimbali wakiwemo Tembo, Twiga, Simba na Chui. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mwisheni alipofika kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashugwa kukagua Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka wakati akikagua Pori la Akiba Kimisi akiwa kwenye ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyesha mpaka wa Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. Kulia ni Mkuu wa Karagwe, Godfrey Mheluka na Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (kulia kwake).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia baadhi ya mifugo iliyokamatwa ndani ya Pori la Akiba Kimisi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya Ngara mkoani Kagera jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii).

MBUNGE LUCY MAYENGA AKUTANA NA AKINA MAMA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO MJINI SHINYANGA

March 01, 2018
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Lucy Mayenga (CCM) amefanya ziara ya kukutana na akina mama wafanyabiashara ndogo ndogo zaidi ya 250 wanaofanya shughuli zao katika Soko Kuu, Mtaa wa Sukari na Nguzo Nane mjini Shinyanga kwa lengo la kusikiliza shida zao na kujadili namna ya kuboresha biashara zao.

PRIVATE SECTOR ASSOCIATIONS AND CIVIL SOCIETY ORGANISATIONS CEO`S MEET TO DISCUSS SUSTAINABLE DEVELOPMENT GOALS (SGD'S) IN DAR ES SALAAM

March 01, 2018



GCNT National Coordinator Emanuel C.  Nnko presents a paper on SGD's goals to participants of  Half day workshop organised by UNDP supported project, Global Compact Local Network Tanzania, on February 28th, 2018 at Ramada Encore Hotel  .

UNDP Economic Advisor  Fitsum G. Abraha   presents a paper on Role of PSO/CSO On Advancing SGD's goals to participants of  Half day workshop organised by UNDP supported project, Global Compact Local Network Tanzania, on February 28th, 2018 at Ramada Encore Hotel .

SOME participants of workshop organized by UNDP in collaboration with Global Compact Local Network Tanzania follow the proceeding of the meeting.

SOME participants of  Half day workshop organised by UNDP supported project, Global Compact Loca ...