MWENYEKTI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) WA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

November 21, 2017


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili kuongoza Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akifungua  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
 Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani wakiwasili ukumbuni kuomba ridhaa ya kurudi CCM wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
 Waliokuwa wanachama wa vyama vya upinzani wakiwasili ukumbuni kuomba ridhaa ya kurudi CCM wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyepata kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo aliyepata kuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha ACT akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha akiomba na kukubaliwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwanachama wa CHADEMA Bw. Lawrence Masha akipeana mkono na  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Bi. Edna sunga  akiomba kurudi na kukaribishwa  CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

 Aliyekuwa mwanachama mwandamizi wa ACT Bi. Edna sunga  akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Bw. Samson Mwigamba akipeana mkono na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kiinana kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.
Aliyekuwa  Mshauri wa Chama cha ACT Wakili Albert Msando  akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017


Aliyekuwa  Mshauri wa Chama cha ACT Wakili Albert Msando  akipeana mkono na  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA)  Bw. Patrobas Katambi  akiomba na kukaribishwa kurudi CCM mbele ya  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho jijini Dar es salaam leo November 21, 2017

USHIRIKA WA WACHINJA KUKU KISUTU WENYE MALENGO MAKUBWA YA UWEKEZAJI

November 21, 2017
Kuku wakiendelea kuandaliwa ndani ya Soko la Kisutu. Picha zote na MaendeleoVijijini.

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini
SAUTI za kuku zinasikika hata ukiwa nje ya jengo dogo ndani ya Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, lakini ghafla zinakoma na zinasikika nyingine.
Siyo kwamba kuku hao wanahitaji chakula ama wanacheza, bali hapa ni machinjio, na sauti zinapokoma ujue tayari zimekwishapigwa kisu na zinaandaliwa kwa ajili ya kitoweo.

NAIBU WAZIRI,KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI WAZUNGUMZA NA WANANCHI

November 21, 2017
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi aliombatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(watatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli mbalimbali zilizopo chini ya idara za wizara na kukagua mipaka iliyopo katika mkoa huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, akizungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na wananchi wanaofanya shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiambata na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kulia) 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala(wapili kulia),Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima() na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga(kulia), wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo. 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala( kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima(watatu kulia) wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka Tanzanua na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo

Na Abubakari Akida-WMNN
NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka wananchi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao karibu na Kituo cha Mpaka wa Sirari unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mara kudhibiti matukio ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu hao kwa jeshi hilo.

Hayo ameyasema akiongea na wananchi wakati wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara, ikiwa na lengo la kutembelea mipaka iliyopo katika mkoa huo inayotenganisha nchi ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo katika ziara hiyo aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibiche na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

“Tumekuwa tukipata taarifa wananchi wa hapa kushirikiana na wahalifu katika kupitisha mali za magendo hapa hasa wakitumia vijana wanaoendesha bodaboda kupitisha mizigo yao na kuripotiwa matukio mbalimbali yanayohatarisha usalama wa raia wetu, natoa wito kwa wananchi wa hapa kushirkiana na jeshi la polisi kudhibiti matendo hayo ya kihalifu,” alisema Masauni

UMEME USIKATIKE BILA SABABU MAALUM- SUBIRA MGALU

November 21, 2017
Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa hawakati Umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.
Naibu Waziri aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme ambapo vituo vya kupozea Umeme alivyovitembelea ni Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.
“Umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea mfano kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu mkatoa taarifa mapema kwa wananchi,” alisema Subira Mgalu.
Aliongeza kuwa ukatikaji wa Umeme unasababisha malalamiko kutoka kwa Wananchi kwani kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato.
Aidha Naibu Waziri aliwaagiza watendaji wa TANESCO wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, 2017.
Vilevile alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika jiji la Dar es Salaam.
"Nawaomba watanzania wawe na matumaini na Serikali ya Awamu ya Tano kwani inajitahidi katika Ujenzi wa miundombinu ya Umeme, nia ikiwa ni nishati ya Umeme kupatikana muda wote," alisema Naibu Waziri.
kwa upande wake, Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona alisema kuwa Shirika hilo linafanya juhudi mbalimbali ili utekelezaji wa mradi huo ukamilike ndani ya muda ulioelekezwa.
Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya  19  vya  kupoza  Umeme  wa  Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Gharama za utekelezaji wa mradi husika ni  Dola za Marekani milioni 43, ambazo zimetolewa na Benki ya Dunia (WB) kupitia Mradi huo.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa kwanza kushoto) akiwa katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi wa uboreshaji wa Vituo vya Umeme na ujenzi wa njia za Umeme jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Emmanuel  Manirabona.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATASHASTA NDITIYE ATEMBELEA TUME YA TAIIFA YA TEHAMA NA TCRA-CCC

November 21, 2017

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, alipowasili ofisini hapo katika ziara yake ya kutembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Tumeya Taifa ya TEHAMA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), alipowasili katika tume hiyo, jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto),  wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akatoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia),  katika wa ziara hiyo. 
Shirika la Global Affairs Canada lazindua miradi muhimu Tanzania

Shirika la Global Affairs Canada lazindua miradi muhimu Tanzania

November 21, 2017
BMG Habari Shirika la Global Affairs Canada la nchini Canada limezindua miradi mitano ya afya nchini ikiwemo mradi wa Uzazi Uzima unaosimamiwa na Shirika la Amref Health Africa, lengo ikiwa ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Akizungumza jana kwenye uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es salaam, Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe.Ian Myles alisema miradi hiyo inagharimu zaidi ya Dolla Milioni 6O ambapo mashirika mengine yanayosimamia miradi hiyo ni pamoja na Aga Khan International, Care International na World Vision. Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu alieleza kufurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya serikali na wadau wa maendeleo katika kutatua changamoto za afya ikiwemo vifo vya akina mama na watoto na kwamba analipa kipaumbele eneo la Mama na Mtoto kwani ni muhimu katika sekta hiyo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Amref nchini Tanzania, Dkt.Florence Temu aliwashukuru wafadhili wa wa miradi hiyo kutoka nchini Canada na kubainisha kwamba ufadhili wao utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto hapa nchini. Shirika la Amref linatekeleza mradi wake katika wilaya tano za mkoa wa Simiyu ambazo ni Meatu, Itilima, Bariadi, Maswa na Busega ambapo mradi huo umeanza mwaka huu na utafikia tamati mwaka 2020 huku mashirika mengine yakitekeleza miradi yake katika mikoa ya Mwanza, Tabora pamoja na Rukwa.

KONGAMANO LA WASOMI WANATAALUMA KUFANYIKA JUMAMOSI HOTELI YA LANDMARK UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

November 21, 2017
 Mratibu wa Kongamamo la Wasomi Wanataaluma wa Kikristo liitwalo Tanzania for Jesus Prayer Movement ambalo mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus,  Ephrahim Mwambapa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Kanisa la Abundant Bressing Center (ABC), Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo litakalofanyika Hoteli ya Landmark siku ya Jumamosi. Kulia ni Mjumbe wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli.

Mratibu wa Kongamano hilo, Ephrahim Mwambapa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini Jumamosi ya Wiki hii wanatarajia kufanya kongamono kubwa la kihistoria kujadili namna watakavyoweza kutumia taaluma zao kusaidia jamii, kanisa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mratibu wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.

Alisema licha ya muungano huo kuundwa na vijana wa kikristo lakini vijana wote wasomi kutoka katika vyuo na shule za sekondari na madhehebu mbalimbali wanaalikwa ili kuchangia mada zitakazo jadiliwa na mgeni rasmi atakuwa ni Kiongzi Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Center nchini, Askofu Flaston Ndabila.

Mwambapa alisema kuwa katika kongamano hilo kutakuwepo na mada mbalimbali na kuona ni jinsi gani kila mmoja na taaluma yake ataweza kusaidia jamii badala ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kuifanyia kazi.

"Tunapokuwa vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii na ndio maana tumeona ni vizurio kuazisha muungano huu lengo likiwa kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema Mwambapa.

Alisema wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano ya mkutano mkuu wa kitaifa wa kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwambapa alisema kongamano hilo litafanyika Hoteli ya Landmark Ubungo jijini Dar es Salaam na litahudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali,sekondari baadhi wa viongozi.



Taasisi ya APHTA yatekeleza Vyema Mpango wa Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza Mashuleni

Taasisi ya APHTA yatekeleza Vyema Mpango wa Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza Mashuleni

November 21, 2017

Inaelezwa kwamba hadi kufikia mwaka 2020 magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kusababisha asilimia 73 ya vifo kote duniani ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa katika kupambana na magonjwa hayo ikiwemo Kisukari. Ni kutokana na athari za magonjwa hayo, Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHTA, kikazimia kuanzisha Mpango wa Kitaifa wa Afya Mashuleni, lengo likiwa ni kupambana na magonjwa hayo ambapo mpango huo unafadhiriwa na Taasisi ya “World Diabetes Foundation” ya nchini Canada. Na sasa mpango huo unatekelezwa vyema, fuatilia video hii. [embed]https://youtu.be/3VXQd_vNIl0 Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (kushoto), akizungumza kwenye ziara ya kujionea utekelezaji wa mpango huo mkoani Shinyanga. Wanafunzi wa shule ya Msingi Town Mjini Shinyanga, wakiimba Ngonjela wakati wa ziara hiyo. Viongozi mbalimbali kwenye ziara hiyo. Wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga wakiimba wakati wa ziara hiyo. Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga. Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B.

VYAKULA VITANO MUHIMU KWA UKUAJI WA AKILI YA MTOTO

November 21, 2017

Na Jumia Food Tanzania

Miongoni mwa changamoto zinazowakumba wazazi wengi wa kitanzania ni kushindwa kufahamu na kupangilia vyakula sahihi kwa ukuaji wa afya za watoto wao. Afya ya akili ya mtoto ni kitu muhimu na cha kuzingatia kwani humfanya mtoto aweze kufanya shughuli tofauti kwa ukamilifu ikiwemo uwezo wake wa kujifunza shuleni pamoja na kushiriki michezo mbalimbali na wenzake.
Baadhi ya wazazi kwa kutokufahamu huwapatia watoto wao vyakula ambavyo huwa haviwasaidii watoto kwenye hatua ya ukuaji. Inawezekana watoto huwa hawapendelei vyakula hivyo muhimu kwa afya zao, lakini inashauriwa kuanza taratibu na hatimaye wanazoea. Jumia Food imekukusanyia aina tano za vyakula ambavyo ukianza kumpatia mtoto wako utashangazwa na ukuaji wa afya ya akili yake.

Mayai. Virutubisho vinavyopatikana kwenye mayai ni muhimu kwenye utengezaji wa seli zinazotunza kumbukumbu kwenye ubongo. Kadiri tunavyokuwa na seli nyingi ndivyo tunakuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu. Hivyo ni vizuri kuzingatia kujumuisha aina hii ya chakula unapomtayarishia mtoto wako chakula, kwa mfano asubuhi kabla mtoto hajakwenda shuleni.  

Maziwa. Maziwa yasiyo na mafuta yanajulikana kuwa chanzo kikubwa cha protini, Vitamini D na fosforasi. Lakini pia kalsiamu inayopatikana ndani yake inasaidia namna miili yetu inavyodhiti nishati. Kalsiamu pia ina mchango mkubwa kwa uzalishaji wa insulini kwenye miili yetu. Mbali na kunywa maziwa kama yalivyo unaweza kunogesha kwa kuongeza chokoleti. Wataalamu wanasema kwamba kuna kiasi kidogo cha ‘kafeini’ kwenye maziwa ya chokoleti, na yanakuwa karibu na kiasi sawa cha sukari iliyopo kwenye juisi za matunda.  

Matunda. Ukuaji wa afya ya akili ya mtoto huhitaji matunda kwani humsaidia kwenye mchakato mzima wa kujifunza. Lakini pia matunda husaidia katika mchakato mzima wa kulainisha choo hivyo kusaidia kwa kiasi kikubwa watoto wengi wanaokumbwa na changamoto hiyo. Ukiachana na maji na mazoezi, matunda ni mbinu bora ya kuwafanya watoto kuwa na afya bora na hivyo akili kuwa tayari kwa kujifunza. Ili kutomtia mtoto uvivu katika kula matunda, unaweza kumuandalia kwa kuyakata kwa mtindo wa vipande vidogovidogo.   
Maji. Jambo ambalo wazazi wengi hawalifahamu ni ambavyo watoto wao hunywa kiasi kidogo sana cha maji kutwa nzima. Wataalamu wengi wamekuwa wakionya namna maji ambavyo huwa yanapuuzwa kama chakula muhimu kwenye mwili wa binadamu, si kwa watoto tu bali hata watu wazima. Watoto muda mwingi huwa wanakuwa kwenye pilikapilika zao bila ya kuwa na maji ya kutosha mwilini. Kutokunywa maji au kutumia kwa kiasi kidogo huwafanya watoto kuhisi njaa isiyo ya lazima. Hakikisha kuwa unajumuisha maji kwenye kila mlo unaomuandalia mtoto wako.
Nyama. Ukosefu wa madini ya chuma ni miongoni mwa tatizo sugu linalotokana na upungufu wa lishe, na huongoza kwa magonjwa yanayotokana na upungufu wa lishe duniani. Na kutokufanya vizuri kwa watoto shuleni huweza kuwa dalili mojawapo. Kiasi cha nyama unachokitumia kwenye mlo kila siku kina faida kubwa ambayo huwezi kuifikiria. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, hata kiasi kidogo unachokula kwa kimeonyesha utofauti mkubwa kwenye uwezo wa mwili kufyonza madini ya chuma kutoka vyanzo mbalimbali.

Inafahamika kwamba wazazi wengi huwapatia watoto wao vyakula ambavyo ni muhimu kwenye ukuaji wao. Kama mzazi au mlezi jaribu aina mbalimbali ya vyakula mbali na vilivyoorodheshwa humu, fuata ushauri wa wataalamu mbalimbali wa afya au kusoma zaidi majarida tofauti ya afya na lishe.  

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

November 21, 2017
WAMBURA AWATIA SHIME WAKUFUNZI WA WAAMUZI

Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura amesema, kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.

Wambura alisema hayo Jumatatu Novemba 20, 2017 kwenye Ukumbi wa ILO, Dar es Salaam wakati aifungua kozi Wakufunzi wa Waamuzi kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika.

Kozi ya wiki moja ya Wakufunzi wa waamuzi hatua ya tatu ‘Futuro III’ inayofanyika Tanzania kwa nchi 26 kushiriki. Jumla ya Washiriki 58 wanashiriki kozi hiyo kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania.

Kozi hiyo ina wakufunzi sita wakiwamo Carlos Henriques na Dominic Chiellens wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), ambao Wambura aliwataka wakufunzi wanaofundishwa mbinu mbalimbali kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza ndoto hiyo ya Afrika.

“Waamuzi wa Afrika wana uwezo. Ninyi wakufunzi ni wa kufanya waamuzi wetu kuwa na uwezo zaidi. Ni Aibu kwa Bara kubwa kama Afrika lenye nchi wanachama 54 wa FIFA kuwa na waamuzi wachache katika fainali za Kombe la Dunia.