HIVI NDIVYO MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA ALIVYOFURAHIA USHINDI WAKE NA WANACHAMA WA COASTAL UNION

July 23, 2015

MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA NA WANACHAMA WA KLABU HIYO MARA BAADA YA KUMALIZIKA UCHAGUZI MKUU AMBAPO ULIMCHAGUA KUONGOZA KLABU HIYO





MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA KUSHOTO AKISHIKANA MKONO NA MAKAMU MWENYEKITI WAKE,SALIM AMIRI KULIA NI MJUMBE WA KAMATI YA COASTAL UNION

MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKINYANYULIWA JUU NA WANACHAMA WA TIMU HIYO MARA BAADA YA KUIBA KIDEDEA KWENYE UCHAGUZI HUO
 RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA!

RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA!

July 23, 2015
 mail.google.comN
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Ambapo amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
G
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Y
……………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa – MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayofanyika Julai 25, 2015  Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Amesema Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha, amesema  kutakuwa na  Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua kutoka kwa viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini.
Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
Ameongeza kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo  Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo mbalimbali yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi ya vituo hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.
Akizungumzia baadhi ya malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji wa waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema kuwa Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.
Amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua watumishi hao wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na vurugu zinazoweza kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji wananchi inatakiwa kuanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa tarehe zilizopangwa.
Kuhusu taarifa za uwepo wa baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji wasiohusika kusimamia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji hao kuacha mara moja tabia hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na kwamba hatua kali za kisheria  zitachuliwa dhidi yao.
Pia amevitaka Vyama vya siasa kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au kuvaa mavazi yanayoashiria kampeni za siasa ili kuepusha vurugu

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI.

July 23, 2015


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata
utepe kuashiria kufungua
  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es
Salaam.
 Maonesho hayo yamefunguliwa
rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt.
Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha
Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya
Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya
Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi
leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio
Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani
waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu
alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya
Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho
hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William
Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya
kufundishia somo la Kompyuta, wakati

Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya
Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es
Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa
Plastiki zilizotengenezwa
  kwa kutumia
Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of
Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la
Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya
  Sayansi
ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho
hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia moja ya Mashine ya 3D Printer iliyobuniwa nchini Korea na
inayotumika kufundishia wanafunzi wa IT wa Chuo cha ‘The United African
University Of Tanzania’ (UAUT), wakati alipotembelea banda la maonesho la Chuo
hicho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu,
nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya
Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho, Chang
Kilee, akimpa maelezo kuhusu Mashine hiyo. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi
leo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata
maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,
  wakati alipotembelea banda lao la maonesho
katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba,
jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar, Hadi Mohamed
  (kushoto) na baadhi ya wanafunzi wake, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 10 ya Sayansi
ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, viongozi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, Kung Fu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom.
 Dkt. Bilal, akisalimiana na mmoja wa Walimu wa Chuo cha Liaoning Shi hua, Liju Shi, wakati alipotembelea katika Banda lao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya
Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo
yamefunguliwa rasmi leo.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

NAMNA COASTAL UNION ILIVYOINGIA MKATABA NA KOCHA MKUU MAYANJA NA KOCHA WA MAKIPA FREDY LUMU

July 23, 2015



KOCHA WA MAKIPA WA COASTAL UNION,FREDY LUMU AKISAINI MKATABA WA KUWAFUNDISHA MAKIPA WA TIMU HIYO HIVI KARIBUNI KULIA NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI


KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI AKIMUONYESHA SEHEMU YA KUSAINI KOCHA MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA MARA BAADA YA KUTUA MKOANI TANGA TAYARI KUKINOA KIKOSI HICHO.





KUSHOTO NI KOCHA MKUU MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA AKIMKABIDHI MKATABA WAKE KATIBU MKUU WA COASTAL UNION MARA BAADA YA KUUSAINI TAYARI KUITUMIA TIMU HIYO
Mabalozi India,Ubelgiji na Sweden wamuaga Rais Kikwete ikulu

Mabalozi India,Ubelgiji na Sweden wamuaga Rais Kikwete ikulu

July 23, 2015

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa India anayemaliza muda wake Mhe.Debnath Shaw wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania baada ya kumaliza muda wao wa kazi .
Mabalozi walioagana na Rais leo ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Mhe.Debnath Shaw wa India,Balozi Koenraad Adam  wa Ubelgiji na balozi Lennarth Hjelmaker wa Sweden.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Koenraad Adam wa Ubelgiji ikulu jijini Dar es Salaam leo alipokwenda kumuaga.
4
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa Sweden nchini aliyemaliza muda wake Mhe.Lennarth Hjelmaker ikulu jijini Dar es Salaam 
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Sweden nchini aliyemaliza muda wake Mhe.Lennarth Hjelmaker ikulu jijini Dar es Salaam leo
(picha na Freddy Maro)
BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA

BHALALUSESA ASISITIZA UMUHIMU WA UMAHIRI KATIKA TEHAMA

July 23, 2015
IMG_8834
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.
IMG_8915
Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.
Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa alisema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.
"Duniani kote, sekta ya uchumi, fani mbalimbali, taasisi na hata mifumo ya maisha yanategemea sana matumizi ya Tehama kwa sasa. Kadhalika, maendeleo makubwa katika Tehama yamebadili namna mambo yanavyofanyika,” alisema.
Alisema kwa kuhakikisha kwamba kuna maendeleo ya kutosha ni vyema walimu kuwa na umahiri unaotakiwa kwani Tehama inachangamoto nyingi zinazotakiwa kuangaliwa ili kuweza kuitumia ipasavyo kuleta mabadiliko katika jamiii.
Aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanapitia muswada huo kwa makini na kujazia maeneo yote ambayo wataalamu wameshindwa kumaliza na kusaidia kuweka mtaala huo vyema kwa mafunzo.
Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa kuimarisha uelewa kwa wanafunzi na wakufunzi vyuo vya walimu ili kuboresha matumizi ya Tehama katika mafunzo hasa masomo ya sayansi limeshirikisha wataalamu mbalimbali na kuendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na watu wa China.
Alisema kwamba serikali inatambua kuwa Tehama inaweza kutumika vyema katika kubadili na kuboresha mfumo wa elimu Tanzania.
Aidha alisema Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua umuhimu wa Tehama katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania.
Alisema moja ya malengo ya sera ni kuonesha mahitaji halisi ya Tehama nchini katika upande wa wataalamu na vifaa ili kufanikisha utoaji wa elimu hata ya masafa katika ngazi zote.
Kongamano hilo ni moja ya mradi wa China Funds in Trust Project (CFIT) wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua tehama na kuitumia.
Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu vitaingizwa.
IMG_8909 IMG_8842
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu wakati kongamano hilo likiendelea mjini Bagamoyo.
IMG_8843 IMG_8831
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (katikati). Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
IMG_8826
Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kulia), akifurahi jambo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
IMG_8928
Mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (walioketi wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo inayomalizika leo mjini Bagamoyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AKUTANA NA WANANCHI WA MLELE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda AKUTANA NA WANANCHI WA MLELE

July 23, 2015

 H
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  wasichana wa Kisukuma  nyumbani kwa Mzee Katinda kwenye kitongoji cha Tupindo wilayani  Mlele  akiwa  katika mapumziko mafupi  nyumbani kwake Kibaoni, Katavi   Juai 22, 2015.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
C
Watoto  wa familia ya  mzee Katinda wa  Kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  wakicheza ngoma ya Kisukuma mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda    Mheshiiwa Pinda yuko katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni, katavi.
mail.google.com
Mke wa Waziri Mama Tunu Pinda  akiwaonyesha picha mbalimbali alizopiga vijana wa kabila la Kisukuma aliokutana nao nyumbani kwa Mzee  Katinda katika kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  ambako yeye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wako katika mapumziko mafupi  kijijini Kibaoni.
mail.google.comM
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akifafanua jambo kwa kutumia  kompyuta ndogo (Ipad) wakati alipozungumza  na wanafamilia wa Mzee Katinda wa kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele akiwa katika mapumziko mafupi nyumbani kwake  Kibaoni, Katavi julai 22, 2015.