WAAHARIRI NA WANAHABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA UTALII WA TANZANIA

July 27, 2017
Wahariri na Wanahabari nchini wametakiwa kuendelea kutumia kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali ya utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Shirika la  Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 
 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 

 Amesema katika kufanikisha kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutegemea utalii Wanahabari wanapaswa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi kwa Watanzania na wageni kwa kutumia kalamu zao.
 

Aliwataka  waandishi kutokukubali  kuandika taarifa  ambazo hawazijui  kitaaluma, kwani kufanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa TANAPA, Allan kijazi amesema kuwa utalii Utalii unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80% ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.

Amesema kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka 2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.

"Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.

Akielezea Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.

Akielezea changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.

Kijazi alimaliza kwa kusema kuwa TANAPA ilianzishwa kisheria mwaka 1959 kukiwa na hifadhi moja tu ya Serengeti,lakini mpaka sasa hifadhi zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 16 mwaka 2014. 

 Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia  yaliyaokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanga'.

Mhariri wa Gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia kushoto akibadilishana mawazo na Mhariri wa Statv

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Limited,Absalam Kibanda

MH RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA MOROGORO AKIWA NJIANI KUELEKEA JIJINI DAR -ES SALAAM AKITOKEA MKOANI DODOMA MOROGORO JULAI 27,2017

July 27, 2017
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa eneo la Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro akitokea Mkoani Dodoma. Julai 27,2917.
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimsikiliza Bi Maria Gabrieli aliyemweleza Mh Rais Juuu ya kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27,2917.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimsikiliza Bi Halima Alli aliyemweleza Mh Rais Juuu ya kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27,2917

UNAITUMIAJE MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA BIASHARA YAKO ?

July 27, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Mitandao ya kijamii ni huduma zinazopatikana kwenye intaneti ambazo zinakuwezesha kuwasiliana, kutengeneza maudhui na kuwashirikisha watu wengine waliopo mitandaoni.

Tofauti na watu wanavyoitumia, Jumia Travel ingependa kukufunua macho kwamba mitandao ya kijamii imeleta fursa kubwa ya kutangaza biasahara za aina mbalimbali. Unaweza kuitumia mitandao hiyo kwa kufanikisha malengo kama vile; kukuza jina na biashara yako, kuwafahamisha wateja juu ya bidhaa na huduma zako, kujua wateja wanaichukuliaje biashara yako, kuwavutia wateja wapya pamoja na kujenga mahusiano thabiti na wateja ulionao.

Faida za kutumia mitandao ya kijamii

Kuwafikia watu wengi. Badala ya kutegemea wateja kuja moja kwa moja ofisini kwako mitandao ya kijamii huwafikia mamilioni ya watu sehemu mbalimbali ndani ya muda mfupi.

Kuwafikia wateja unaowakusudia. Uzuri wa mitandao ya kijamii ni kwamba hutofautiana kwa aina ya watumiaji wake kama vile vijana, watu wazima, wanasiasa, wanataaluma na matabaka mengine. Hivyo hii hutoa fursa kwa mfanyabiashara kulingana na huduma au bidhaa aliyonayo kujiwekea mkakati wa namna ya kuwafikia.

Unafuu. Haikuhitaji kuwa na fedha ndipo ufungue akaunti kwenye mtandao wa kijamii mara nyingi ni intaneti tu. Lakini kama unataka kuitumia kwa malengo ya kibiashara wamiliki wake hutoza kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rahisi kukimudu.

Kumfikia mtu binafsi. Mitandao ya kijamii inakuruhusu kujenga ukaribu au kuwasiliana na wateja wako kwa ukaribu zaidi. Uwezo wa kuyapokea na kuyajibu maswali yao au kuyasikiliza na kuyafanyia kazi maoni yao vina ushawishi mkubwa katika kuwafanya wateja kutumia huduma na bidhaa zako.

Uharaka. Ndani ya muda mfupi unaweza kusambaza taarifa juu ya huduma na bidhaa zako kwa watu wengi kwenda sehemu mbalimbali.

Urahisi. Haikuhitaji kuwa na ‘madigrii’ ya vyuo vikuu ili kuweza kutumia mitandao ya kijamii. Ni rahisi kuitumia kwa njia mbalimbali kama vile kompyuta, tabiti au simu za mikononi ambazo watu wengi wanamiliki.   
Mitandao mikuu ya kijamii unayoweza kuitumia

Facebook. Mtandao huu hutoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara kuwasiliana na wateja wao moja kwa moja, kuweka picha na video, kutangaza ofa walizonazo, bidhaa na huduma mpya na mambo mengine.

Twitter. Mara nyingi huduma hii hutumika kutuma na kupokea jumbe fupi kutoka kwa wateja wapya na waliopo. Siku hizi pia hutumika kama nyenzo muhimu kwa kuweka viungo ambavyo vitawapeleka wasomaji kwenye tovuti.

Youtube. Mtandao huu hutumika kwa kuweka video tofauti, zinaweza kuwa juu ya huduma na bidhaa ulizonazo, namna ya kuzitumia pamoja na taarifa mbalimbali ili wateja wako wazitazame.

Blogu. Kama mfanyabishara pia unaweza kufungua mtandao huu utakaokupatia fursa kubwa ya kuwashirikisha wasomaji wako juu ya huduma na bidha zako pamoja taarifa mbalimbali.

Instagram. Mbali na mtandao huu ipo mingine pia inayowawezesha watumiaji kuweka na kuwashirikisha watu wengine picha mbalimbali. Kwa mfano hivi karibuni Instagram wameuboresha mtandao wao kwa kuwawezesha watumiaji wake kuweka picha zaidi ya moja. Hivyo kutoa fursa nzuri kwa wafanyabishara kuweka picha mbalimbali za bidhaa na huduma zao.
Mbali na kuwepo kwa faida lukuki za mitandao ya kijamii, Jumia Travel ingependa kukuasa kwamba bado unahitajika umakini mkubwa katika nanma ya kuitumia. Miongoni mwa changamoto unazoweza kukumbana nazo ni pamoja na kupoteza muda na fedha zako kwa kuwekeza kwenye  kitu ambacho hakitoleta faida, kusambaa kwa habari zisizo sahihi kuhusu biashara yako kwa wateja na kukumbana na matatizo ya kisheria endapo usipofuata au kuvunja taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.