MKAZI WA KIJIJI CHA ISENGULE MKOANI KATAVI FATUMA ISSA (22) AJIFUNGUA WATOTO WANNE

March 16, 2017

Watoto wanne walizaliwa  na  mwanamke   aitwaye  Fatuma  Issa  22   Mkazi wa   Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema   mwambao  mwa  Ziwa   Tanganyika  Wilaya  ya  Tanganyika  Mkoa wa  Katavi wakiwa katika   chumba  maalumu  katika   Hospitali ya  Manispaa ya  Mpanda.
Huyu  ndiye  mwanamke   aitwaye   Fatuma  Issa  22  Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule   Tarafa ya  Karema   Wilaya  ya   Tanganyika    Mkoa wa  Katavi   akiwa   katika  chumba  maalumu  katika  Hospitali ya  Manispaa ya   Mpanda     baada ya kujifungua  watoto wanne kwa wakati mmoja  ambapo alijifungua  watoto hao  hapo machi 12  katika   Hospitali  hiyo  kati ya watoto hao mmoja ni wakike na watatu ni wakiume.

Mkuu  wa  Wilaya ya   Mpanda  Lilian  Matinga  akiwa  katika wodi ya  wazazi    katika   Hositali ya  Manispaa ya  Mpanda   aliwajulia  hali watoto wanne   mapacha  waliozaliwa hapo  Machi  12  mwaka huu kwa  wakati mmoja  na  mwanamke  aitwaye   Fatuma  issa  22   Mkazi wa  Kijiji  cha  Isengule  Tarafa ya  Karema  Wilaya ya  Tanganyika   Mkoa wa   Katavi
Picha  Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog

MARAIS WASTAAFU WAONGOZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU SIR GEORGE KAHAMA

March 16, 2017
AAASSS
 Mke wa Marehemu Sir Georeg Kahma, Janeth Kahama akiaga mwili wa Mumewe katika ukumbi Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu , Benjamini Mkapa  akitoa pole kwa watoto wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri wa Habari Sanaa  Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama.

TIGO, RITA KUANZA AWAMU YA NNE USAJILI WATOTO GEITA NA SHINYANGA

March 16, 2017
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika Septemba  mwaka jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA)pamoja na UNICEF inategemea kuzindua awamu ya nne ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga mapema wiki ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na RITA, Mpango huu wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano unatarajiwa kutekelezwa katika wilaya zote tatu (3) zilizo na halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga na Wilaya zote tano (5) zilizo na halmashauri sita (6) katika mkoa wa Geita.

“Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, ni asilimia 9.4 ya watoto wa mkoa wa Shinyanga na asilimia 8.6 katika mkoa wa Geita wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa. Lengo la RITA mara itakapoanza kutekeleza mpango huu ni kusajili watoto wote 740,912 ambao hawajasajiliwa na hawana vyeti vya kuzaliwa katika mikoa yote miwili kwa kipindi cha miezi 6,” alisemakaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Rita Emmy Hudson.

Ili kufanikisha utekelezaji mpango huu kutakuwa na vituo vya usajili zaidi ya 650 vitakavyokuwa na wasajili wasaidizi wapatao 1,250 kwa mikoa yote miwili. Wasajili hawa watawekwa katika ofisi za afisa mtendaji wa mtaa na vile vile katika maeneo ambayo kinamama huenda kupata huduma za kiafya za watoto.

“Matokeo tuliyoyapata mwaka jana katika utekelezaji wa mpango huu katika mikoa ya Iringa na Njombe yatatumika kuhakikisha watoto wote wanapata huduma hii katika mikoa ya Geita na Shinyanga,” alisema Hudson huku akiongeza kwamba mikoa hiyo iliweza kusajili watoto kwa asilimia mia moja (100%) kwa kipindi cha miezi mitano huko Iringa na Njombe.

Meneja wa Huduma za Jamii wa kampuni ya Tigo, Halima Okash alisema kampuni ya Tigo imekuwa mshirika mkuu wa mkakati wa Usajili wa Watoto wa chini ya miaka mitano toka mwaka 2012 ili kuiwezesha serikali kupunguza tatizo la muda mrefu la watoto kutosajiliwa na mamlaka husika pindi wanapozaliwa hivyo kuathiri mipango ya maendeleo ya muda mfupi na ile ya muda mrefu.
“Duniani kote takwimu sahihi na zinazopatikana kwa wakati ni jambo muhimu ili kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo ndio maana kati ya malengo makuu ya mkakati huu ni kutumia teknolojia ya simu za kiganjani katika kuchukua na kutuma taarika kwenda katika kanzidata (database) ya RITA mara mtoto anaposajiliwa kwenye vituo vilivyoaainishwa,” alisema Okash.
Okash aliongeza kwamba kampuni ya simu za mkononi ya Tigo inajivunia kuweza kutumia rasilimali ya ujuzi tulio nao katika kuwezesha kila mtoto nayezaliwa kutambuliwa na mamlaka husika hivyo serikali kufahamu kuna watoto kiasi gani katika umri fulani.
Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka ya awali ya utambulisho kwa mtoto inayomwezesha kutambuliwa uwepo wake na ni haki ya mtoto ya msingi. Hudson aliwaomba wadau wote ikiwa pamoja na viongozi wa mikoa, wilaya, halmashauri, tarafa, kata, mitaa/vijiji na vitongoji kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa mpango huu.

“Vilevile,tunawaomba Viongozi wa dini, wanasiasa, wanahabari na viongozi wa jadi ambao watusaidia kuelimisha wananchi kuhusu kujitokeza kwa wingi kuwasajili watoto ili wapate vyeti vya kuzaliwa,” alisema Hudson.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU MPYA KIJIJINI CHAMWINO, DODOMA

March 16, 2017
  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wahandisi na maafisa wa Wakala wa Majengo ya Serikali wakati alipowasili kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Sehemu ya matofali katika eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakati walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza wakati  Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea na wafanyakazi wa TBA  wakati wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili,akitambulishwa  kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiangalia ufyatuaji wa  matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakichanganya mchanga na saruji na kusaidia kufyatua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua mchanga unaotengezewa matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakimwangalia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Jenista Muhagama (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga   kagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017.
PICHA NA IKULU
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MBABANE SWAZILAND LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MBABANE SWAZILAND LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC

March 16, 2017
koromije
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
BANE 3
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia vikundi vya Burudani  mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane  Swaziland leo  march,16, 2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
BANE 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili  Heshima  kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
BANE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili  kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
…………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).  
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.
Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika  ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.
Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.
Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Imetolewa na                       
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.

TANGA UWASA INAHITAJI BILIONI 15 KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA

March 16, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia akiteta jambo na Meneja Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka hiyo,Haika Ndalama.

 Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani.
  Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani katikati mwenye hijabu ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania

 Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa wakiandaa baadhi ya dondooo kuhusiana na wiku ya maji

 Mwandishi wa Gazeti la Daily News Mkoani Tanga Amina Kingazi akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Raisa Saidi.
 Mwandishi wa Azam TV Mkoani Tanga,Mariam Shedaffa akifuatilia kwa umakini taarifa mbalimbali za mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)


 Waandishi wa Habari Mkoani Tanga Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wa pili kulia wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa kwenye semina hiyo
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,Amina Omari akuliza swali kwenye mkutano huo
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.
 
Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo kutumika tena.

Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu
itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia suala zima la uchafuzi wa mazingira.

“Tupo na mpango wa kuyatumia maji taka kwa shughuli nyingine kama kilimo cha mbogamboga, unaimani kwa kufanya hivyo tutaongeza kipato cha mtu mmoja moja…Lakini ili mpango huu uweze kutimia tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kutekelezwa,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mfumo wa kutumia majitaka kwa shughuli nyingine za kibinadamu umekuwa ukitumika katika nchi zilizoendelea kama China, Israel na kwingineko ambako teklonojia hiyo imeanza.

Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imeanza mpango wa kufunga mita za watumiaji maji wa malipo ya kabla zinazojulikana kwa jina la ‘Lipa Maji Kadiri Unavyotumia’ (LIMAKU) ambazo tayari wamezifunga katika baadhi ya maeneo yakiwemo vikosi vya jeshi hapa nchini.

Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamefunga katika vikosi vya jeshi vilipo mkoani hapa pamoja na shule 20 za msingi zilizopo katika Jiji la Tanga na maendeleo yake yanaenda vizuri.

“Tumeagiza mita nyingine za Limaku zipatazo 300 hizi pia tutazifunga katika taasisi za serikali na watu wengine hasa wateja wetu wenye madeni makubwa,” alisema Mgeyekwa.

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE

March 16, 2017

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo

 Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha  uzalishaji

Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha
Kilimanjaro ,Vivek Pandey  kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho  na hivyo kusitisha uzalishaji kulia ni Msimamizi wa Kiwanda hicho,Paskal Dimelo
Msimamizi wa Kiwanda cha kuzalishaji Saruji Mkoani
Tanga cha Kilimanjaro, Paskal Dimelo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitiza uzalishaji wake kushoto ni Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey,
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya  kiwanda hicho kufungwa.

Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300 kutokana na agizo lao la kusitiza uzalishaji katika kiwanda hicho kwa madai ya kukosa ubora unaotakiwa.


Alionyesha masikitiko yake hayo juu ya hataua iliyochukuliwa na shirika hilo la Ubora wa viwango Tanzania (TBS) ya kukifungia kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo Jijini Tanga kwa kudaiwahawajafikia ubora unatakiwa katika bidhaa hiyo bila ya kuangalia athari za mwekezaji huyo na ajira zilizopotea kiwandani hapo.

Aidha alisema ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa mamlaka hiyo husika(TBS)ambapo kwa namna moja au nyingine wanaonekana wanaikwamisha Serikali katika mpango wake wa kukua katika uchumi wa viwanda ambavyo vinaweza kuwa mkombozi wa ajira hapa nchini.

“Serikali inapambana na uchumi wa viwanda vitakavyoweza kusaidia ajira kwa vijana wetu sasa kinachotokea katika kiwanda hiki kunaonekana kuna watu wachache wanataka kumkwamisha muwekezaji huyu,hivi wizara husika iko wapi?nini hatma ya mwekezaji huyu na kufanya hivi hatuoni kama tunawafukuza hawa wawekezaji?”Alihoji Alhaj Mbaruku.

Hatua ya kusitiza huduma ya uzalishaji wa kiwanda hicho licha ya kuathiri ajira za wafanyakazi hao lakini pia itasababisha serikali kukosa mapato yanayoweza kusaidia kukuza uchumi wa Taifa na Mkoa wa Tanga .

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Vivek Pandey alisema kinachowaasumbua wao ni cheti bora kutoka kwa shirika la viwango cha kutambuliwa hivyo wanaomba suala hilo liingiliwe kati na mamlaka husika ikiwemo serikali ili waweze kuendelea na uzalishaji ambao utaweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.

Alisema baada ya taarifa zao kutoka kwenye vyombo vya habari alifika mmoja kati ya wataalamu kutoka katika shirika hilo Jijini Dar es saalm na kuondoka na sampo ya bidhaa hiyo ambapo mpaka sasa bado hawajapata majibu sahihi ya hatma yao.

“Baada ya taarifa zetu kuruka kwenye vyombo vya habari siku ya pili tu alitumwa mtu kutoka makao makuu ya TBS Jijini Dar es salaam na niliondoka nae sambamba na sampo ya bidhaa hiyo nahii leo ja (jana)kwenda tena ili kuona hatua gani zimechukuliwa dhidi
yetu”Alisema Pandey.

Aidha alisema hatua hiyo ya kusitisha uzalishaji mbali na kupoteza ajira kwa vijana lakini wamekisababisha hasara kiwanda kwa zaidi ya shilingi Milioni 200 ambazo zinatokana na tani elfu 11 zilizozalishwa kisha kuonekana zipo chini ya kiwango.

WATENDAJI WA SERIKALI WAAGIZWA KUWALINDA WAWEKEZAJI WAZAWA

WATENDAJI WA SERIKALI WAAGIZWA KUWALINDA WAWEKEZAJI WAZAWA

March 16, 2017
Serikali imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi. Aidha viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana. Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa. Prof. Mkenda amewasihi viongozi wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya nchini kujivunia uwepo wa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazawa kwani wao ni chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (anayetazama kamera) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu nje ya ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji na tovuti ya mkoa wa Simiyu.(Picha zote na Thebeauty.co.tz).[/caption] Amesema kuwa si vyema wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha zisizokuwa sahihi na kuonekana kama wana uadui na serikali, na badala yake watukuzwe ili kuweza kulipa kodi pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi. “hawa wafanyabishara hasa wazawa na wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu zetu na watu muhimu, kwani wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi ipate maendeleo, lakini wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa nchi ya viwanda, tuwathamni” alisema Prof.Mkenda. Katibu Mkuu huyo amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji wakubwa na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akisaliana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo S. Kiswaga mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, mkoani Simiyu kushiriki uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo pamoja na kuzindua tovuti ya mkoa huo.
 Awali akizungumza katika sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amesema kuwa ili Tanzania iweze kufanikiwa katika azma yake ya kuwa na viwanda lazima serikali iwekeze kwanza katika utafiti wa fursa zilizopo. Amesema kuwekeza katika utafiti utasaidia kutoa uthubutu wa kufanya na kutenda mambo mbalimbali yatakayoifanya nchi kuwa na uchumi wa kati na kuwaletea wananchi maendeleo. “nchi hii tusingelihitaji kuona wakuu wa mikoa kuwa wabobezi katika kila sekta na badala yake wawaache wataalam na watafiti wafanye kazi zao kitaalamu ili kuepuka mvurugano wa shughuli za kimaendeleo ndani ya nchi” amesema Mtaka