MUHEZA KUPATA MIL 500 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

MUHEZA KUPATA MIL 500 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

October 14, 2014

IMG_1498 
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu wakiwa wamesimama kwenye mashine ya kuchimbia visima iliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa takribani Sh. Mil 240.
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla ameahidi Sh. Milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Mhe. Makalla alitoa kauli hiyo jana, alipotembelea Wilaya hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maji na hali ya  huduma ya maji wilayani humo.
 “Nawapongeza sana Halmashauri yenu na uongozi wake kwa kununua mashine kwa ajili ya kuchimba visima vya maji, sijawahi kutembelea Wilaya yoyote nchini nikakuta jambo hili. Kitendo cha Halmashauri kukusanya mapato yake na kufanya hivi, mnastahili pongezi na kuwa mfano kwa Halmashauri nyingine nchini,” alisema Makalla.
“Nimeridhishwa na jitahada zenu na nitahakikisha mnapata mgao wa Sh. Milioni 500 ili kufanikisha lengo la kupatia ufumbuzi tatizo la maji Muheza,” aliongeza Makalla.
Naibu Waziri alisema kwamba kama kiongozi mwenye dhamana kwenye Serikali Kuu, atahimiza maamuzi yafanyike upesi ili jitihada zinazofanywa na Wilaya ya Muheza zifikie lengo walilojiwekea kuwapatia wananchi maji.
Aidha, Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake kwa kutembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga UWASA) na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.
Mhe. Makalla alisikia taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo na kufurahishwa nayo, hasa kwa jinsi walivyofanikiwa kupiga hatua kubwa ya kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa na ukusanyaji mzuri wa mapato kutoka kwa wateja wake.
“Kwa kweli nimefurahishwa mno na jitihada zenu za kupunguza upotevu wa maji na kwa kufikia kiasi cha asilimia 23 ni kiwango kizuri, ukilinganisha na Mamlaka nyingine nchini. Hasa ikizingatiwa hii ni changamoto kubwa na kama Wizara tunafanya jitahada kupata suluhisho lake,” alisema Makalla.
Pia, aliongeza ukusanyaji mzuri wa mapato ni hatua kubwa kwa Mamlaka hii, kwani itarahisisha na kuchangia utendaji mzuri wa kazi na maendeleo ya Mamlaka hiyo katika kuhakikisha inainua Sekta ya Maji jijini Tanga na mkoa mzima kwa ujumla.
Katika ziara hiyo Mhe. Makalla amefanikiwa kutembelea miradi ya maji ya vijiji vya Misengeni, Mikwamba na Michungwani, wilayani Muheza. Na vilevile, chanzo cha maji cha Mibayani, kituo cha kusukuma na kutibu majisafi cha Mowe na eneo la ujenzi wa mabwawa ya majitaka lililopo Utofu, Tanga Mjini.
Mhe. Makalla ameanza ziara yake ya siku 6 jana mkoani Tanga, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha utekelezaji wa programu ya wa Big Results Now na miradi yote ya maji inatekelezwa kwa kasi na ufanisi ili kuleta matokeo yenye tija na kwa wakati.
chanzo:fullshangweblog

Taswira mbalimbali za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake

October 14, 2014


Mwalimu akisalimiana na Rais Iddi Amini Dadah wa Uganda wakati wa kikao cha OAU mjini Addis Ababa, Ethiopia enzi hizo. Kushoto kwa Mwalimu ni Waziri wa Mambo ya Nje Mhe John Malecela
Mwalimu akiwa na mume wa Malkia wa Uingereza, Prince Philip
Mwalimu akimlaki Waziri Mkuu wa wa Kwanza wa China Chou Enlai ambaye mtindo wake wa mashati ilirithiwa na Watanzania na kujulikana kama Chunlai
Mwalimu katika mazungumzo na Rais Iddi Amin Dadah wa Uganda. Kushoto ni Mama Maria Nyerere
Mwalimu Nyerere alkiongoza matembezi ya kuunga mkono Azimio la Arush
Familia ya Mwalimu Nyerere
Picha rasmi ya Mwalimu na Mama Maria Nyerere
Mwalimu na Madiba
Mwalimu na Mhe John Samwel Malecela
Mwalimu akimkumbatia Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kutoa hotuba ya kukubali matokeo ya Urais alipogombea kwa mara ya kwanza mwaka 1995. Mhe Benjamin Mkapa alishinda
Rais Kikwete azindua kijiji cha Mfano cha Vijana Sikonge

Rais Kikwete azindua kijiji cha Mfano cha Vijana Sikonge

October 14, 2014

1 (3) 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge leo.Rais Kikwete yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge hapo kesho.watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selenga.
D92A0453 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana wajasiriamali katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora leo.
D92A0545 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.
D92A0579 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano(picha na Freddy Maro).
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA DHAMINI KONGAMANO LA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) KWA SIKU TATU

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA DHAMINI KONGAMANO LA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) KWA SIKU TATU

October 14, 2014

02 (1) 
Washiriki wa kongamano lamafunzo ya mfumo mpya wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO)kutoka nchi za Nigeria,Mali,Ivort coast,Senager,Rwanda,Cape Verde,Gabon na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano hilo la siku tatu linalofabnyika kwenye hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
03 (1) 
Afisa wa Kanda ya Afrika wa ICAO  Papa Issa Mbengue (kushoto)akisisitiza jambo juu ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege wakati wa Kongamano la mafunzo ya ufanisi wa masuala ya uongozaji wa ndege linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wanaomsikiliza ni  Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(watatu kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia) Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand. (wapilia kutoka kulia) na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues 
10 
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha akisalimiana na baadhi ya washitiki wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa hapo  kongamano hilo limedhaminiwa na TCAA linalofanyika kwa siku tatu kuanzia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
01 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (kulia)akisalimiana na  Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues  Ould, baada ya kufungua kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa kulenga wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo linafanyika kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand.(African Flight Proceducare Manager)
Rais Kikwete atoa hotuba Kilele cha Mbio za Mwenge Tabora

Rais Kikwete atoa hotuba Kilele cha Mbio za Mwenge Tabora

October 14, 2014

11 (1) 22 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha mbio za mwenge 2014 ziilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo(picha na Freddy Maro)

2 (1) 
Kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ulius  na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Dkt.Fenela Mkangara.
4 (2) 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenge wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ziizofanyika mkoani Tabora leo.
5 (3) 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora lei(picha na Freddy Maro)

MAASKOFU KATOLIKI WAJADILI USHOGA

October 14, 2014

MAKASISI wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa.

Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa kanisa katoliki wanakutana kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu,katika mkutano huo ni papa Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba,vidonge vya uzazi wa mpango,mapenzi ya jinsia moja na talaka.
Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa hilo kuzingatia Zaidi suala la wapenzi wa jinsia moja chanya kuliko kuwa kinza na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo wa sinodi.