MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Oktoba 31, 2015
Simba SC Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Mwadui FC
Prisons Vs Ndanda FC
Coastal Union Vs Mbeya City
Novemba 1, 2015
African Sports Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Toto Africans
Novemba 2, 2015
Mgambo Shooting Vs Stand United
|
Kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall amesema mbio za ubingwa sasa zimeshika kasi katika timu yake |
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KOCHA
Mkuu Azam FC, Muingereza Stewart John Hall amesema kwamba anataka
kuendeleza wimbi la ushindi ili kuhakikisha anatimiza ndoto za kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam
FC jana imepanda kileleni kwa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa mabao 4-2
dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, hivyo kufikisha
pointi 22, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC, baada ya timu
zote hizo kucheza mechi nane.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana, kocha huyo aliyeipa Azam FC ubingwa
wa Afrika Mashariki, Kombe la Kagame Agosti mwaka huu, amesema kwamba
lengo si kuwa kileleni mwa Ligi Kuu kwa muda, bali kutwaa ubingwa.
“Si
suala la kuwa juu tu, nataka kufikia malengo tuliyojiwekea, hivyo kazi
kubwa iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu za kila
mechi tutakazocheza,” alisema.
|
John Bocco jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 wa Azam FC |
Stewart
amefurahishwa na safu yake ya ushambuliaji kwa kucheza kwa ‘njaa ya
kufunga’ na kufuata maelekezo anayowapa kabla ya mchezo.
“Nina
imani na safu yangu ya ushambuliaji, kama bao la nne lililofungwa na
Kipre Tchetche ni la aina yake, ile ilikuwa moja ya maagizo
niliyomuagiza na kufanyia kazi,” amesema.
Azam
FC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumapili kumenyana na Toto Africans
katika mfululizo wa ligi hiyo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam.
Kwa
ujumla Ligi Kuu inaendelea mwishoni mwa wiki, Jumamosi Simba SC
ikimenyana na Majimaji FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga SC na
Kagera Sugar Uwanja wa Mwinyi, Tabora, Mtibwa Sugar na Mwadui FC Uwanja
wa Manungu, Turiani, Morogoro, Prisons na Ndanda FC Uwanja wa Sokoine,
Mbeya na Coastal Union na Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mechi
nyingine zitachezwa Jumapili, na mbali ya Azam FC na Toto, Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga African Sports itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu wakati
Jumatatu, Mgambo Shooting itaikaribisha Stand United Uwanja wa
Mkwakwani.