FURSA NYINGINE YA SCHOLARSHIP YAJA: SHULE ZA SEKONDARI ZATAKIWA KUTUMA MAOMBI SASA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SAYANSI YA YST 2018!

January 17, 2018

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI D JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM.

January 17, 2018

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia kwa Umakini kikao hicho.
kikao kikiendelea.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao cha Viongozi wa Seneti  Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam , kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wajumbe wa Vyuo na Vyuo Vikuu wakifurahia jambo(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
 ....................................................................................................................................................................

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) leo amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti amesisitiza kuwa  nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.  ''Suala la ushindi wa CCM katika uchaguzi huu wa marudio halina mjadala tutashinda kwa heshima, Amani na  demokrasia vijana wa CCM tumejipanga vyema kufanikisha hilo ngazi zote" Alisisitiza  Mwenyekiti Kheri

Wakati huo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam. ''Tunatambua na kuthamini mchango wa Vijana wenzetu wote katika jamii mkiwemo ninyi wa Vyuo na Vyuo Vikuu tunawategemea sana hivyo tutaendelea kufanya kazi nanyi katika maeneo yote katika kutimiza wajibu wetu wa msingi” Alibainisha Mwenyekiti Kheir.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Dar es Salaam Asha Feruzi pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Alex Gwantwa.
 



AGAPE YAKABIDHI BAISKELI KWA VIJANA 15 WALIOHITIMU MAFUNZO YA HISA SHINYANGA

January 17, 2018
Shirika lisilo la kiserikali la Agape AIDS Control Programme (AACP) limetoa mafunzo ya Hisa kwa vijana 15 kutoka katika kata za Mwamalili,Didia na Masekelo zilizopo katika wilaya ya Shinyanga. 

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MIRADI YA UKUTA WA BAHARI KATIKA ENEO LA KIGAMBONI NA OCEAN ROAD

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MIRADI YA UKUTA WA BAHARI KATIKA ENEO LA KIGAMBONI NA OCEAN ROAD

January 17, 2018

3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Mradi na Miundo Mbinu wa UNOPS Bw. Bernard Odhuno wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameketi kwenye moja ya sehemu za kupumzikia pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Kigamboni wenye urefu wa mita 500. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
9
Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa bahari Ocean Road. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
KU1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari ambao mradi unatekelezwa katika eneo la Kingo ya Bahari iliyopo Chuoni hapo yenye urefu takribani mita 400. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira a Muungano January Makamba.
KU2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unatekelezwa katika eneo la  Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)  yenye urefu takribani mita 400. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira a Muungano January Makamba.
KU3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari katika eneo la  Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)  yenye urefu takribani mita 400 leo jijini Dar es Salaam.
KU4
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akielezea jambo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi ambao unatekelezwa katika eneo la  Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)  yenye urefu takribani mita 400.
KU5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wa mradi huo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa Kuimarisha Kingo za Bahari unatekelezwa katika kingo za Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) Kigamboni yenye urefu wa mita 400, Sea View yenye urefu wa mita 900 na Pangani Tanga.
KU6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipita juu ya Kingo ya Bahari iliyojengwa kupitia mradi wa uimarishaji wa Kingo za Bahari alipotembelea Fukwe ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo. Fukwe hiyo imefanyiwa maboresho ambapo kingo yake imejengewa njia ya wapita kwa miguu na sehemu za kupumzikia.
KU7
Sehemu ya Kingo iliyojengwa katika fukwe ya bahari ya hindi eneo la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
KU8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kigamboni alipokutana nao wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Uimarishaji wa Kingo za Bahari, mradi unaotekelezwa katika eneo la  Kingo ya Bahari iliyopo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)  yenye urefu takribani mita 400. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Kate Mfutakamba. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)
11
Ujenzi wa Ukuta wa bahari katika eneo la umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MKAZI WA DAR NA KIGOMA WAJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 10 KILA MMOJA

January 17, 2018

.Akizungumza na waandishi habari wakati wa kukabidhi hundi hizo kwa washindi hao , mapema leo mbelee ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Mmoja wa Maofisa Habari wa Tatu Mzuka, Millard Ayo alisema droo hiyo inachezwa kila siku,huku wenye bahati zao wakiendelea kujinyakulia vitita vyao vya Tatumzuka.Milard amewaasa Watanzania waendelee kucheza kwa wingi na mara kwa mara mchezo huo,kwani ukiibuka mshindi maisha yake huinuka na kuwa bora zaidi tofauti na alivyokuwa hapo awali.Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umetoa washindi wawili wa sh. Milioni 10 katika droo inayochezwa kila siku,mmoja akitokea jijini Dar na mwingine akitokea mkoani Kigoma
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka,Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka inayofanyika kila siku ,Harieth Steven (21) mkazi wa Kigoma ambaye anajishugulisha na kazi za ndani (housegirl),mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .
Harieth Mwenye mtoto mmoja alifurahia kujishindia donge hilo kupitia mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka,kwani baada ya kutaarifiwa kuwa amejishindia kiasi hicho cha fedha,akajipa matumaini ya kuwa ndoto yake ya kufanya biashara ya vitenge sasa inakwenda kutimia rasmi,na kuacha kufanya kazi za ndani.
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka,Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka ,Ally Rashid (26) mkazi wa Yombo Buza ambaye anajishugulisha na biashara ya kuuza Mboga mboga jijini Dar,mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

WCF YAWANOA WAAMUZI, WASULUHISHI NA MAKATIBU MUHTASI KUTOKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

January 17, 2018

 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.

Hayo yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.

“Katika jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda,  makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la utoaji huduma za Mfuko kwa wadau  litaongezeka na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba  alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.

“Jambo hili si rahisi kwa sababu ndio linaanza kwa hivyo tunahitaji ushirikiano wa karibu sana kutoka kwa wadau mbalimbali mkiwemo ninyi CMA, na katika hilo ushirikiano tu hautoshi Mfuko umekuwa ukitoa elimu ili kuwawezesha watu  wajue Mfuko umeanzishwa kwa sababu gani, kazi zake, lakini pia kujua taratibu za kudai fidia pale mfanyakazi anapopatwa na majanga ya kuumia au kuugua wakati akitekeleza wajibu wake wa kikazi.” Aliongeza Bw. Mshomba.

“Ndio maana leo hii tunao wataalamu wetu watakaotoa mada mbalimbali zikiwemo, Sheria za Fidia, Namna Fidia inavyolipwa lakini shughuli za Mfuko.” Alibainisha Mkurugenzi Mkuu Bw. Mshomba.

Aidha aliishukuru Tume kwa kuwashirikisha WCF ili kuwaelimisha wafanyakazi wake kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

“Ni muhimu kwetu sisi kuwaelimisha wadau kuhusu shughulim zetu na ndio maana huwa tuko tayari wadau wetu wanapotualika ili kutoa elimu hiyo.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ……..kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Bw. Eric F. Shitindi amewahimiza washiriki wa kuzingatia elimu watakayoipata kwenye mafunzo hayo ili hatimaye watekeleze ipasavyo malengo ya serikali ya awamu ya nne ya kujenga uchumi wa kati ifikapo mwak 2025.

“Ni matarajio yetu kwamba Tume na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, mnao wajibu mkubwa sana katika kufanikisha azma hiyo ya serikali kama nyinyi mtatekeleza wajibu wenu.” Alisema.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Edrisa Mavura, akitoa hotuba yake.
Maafisa wa CMA wakiteta jambo.
Bw. Mshomba, (kulia), na Bw.Nungu, wakijadili jambo.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akikaribishwa na Wakurugenzi wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia) na wa CMA, Bw.Shanes Nungu, alipofika kufungua mafunzo hayo
 Bw. Mshomba akijibu baadhi ya maswali ya washiriki kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya washirtiki wakifuatilia mafunzo.
Kamishna wa Tume, Bi.Suzanne Ndomba, (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo. Wengine ni Makamishna wenzake, kutoka kushoto, Bw.Kibwana Njaa, Bw.Jones Majura na Bw.Jaffary Ally Omar.
Picha ya pamoja.
Bw. Mashomba akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar.
Washiriki wakipitia vipeperushi vya WCF.
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com 

WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

January 17, 2018
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye. Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo.
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.

MPINA AKAMATA MAROBOTA 1152 YA NYAVU HARAMU MWANZA NA SINGIDA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 894.

January 17, 2018
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwa na Kiongozi wa Operesheni ya maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa Ziwa Victoria, Shafii Ramadhani Kiteri wakikagua  shehena ya marobota 600 ya nyavu  haramu  zenye thamani ya shilingi  milioni mia tano inayomilikiwa na Meshaki Chacha jijini Mwanza leo. Nyavu hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa  na  mmliki  akitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni hamsini ndani ya masaa 24. (Na John Mapepele)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (mwenye miwani na kofia )akisikiliza  jambo kutoka  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati (kushoto) wakiwa kwenye boti ya doria kutoka katika kijiji Kakukuru wakielekea  kwenye kambi ya uvuvi ya Kisiwa cha Galinzila ambapo Mhe.Waziri alifanya mkutano na wavuvi . Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomiah Chang’a. (Na John Mapepele)
Mmliki wa ghala lenye  shehena ya marobota 600 ya nyavu  haramu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa kisheria zenye thamani ya shilingi  milioni mia tano,  Meshaki Chacha  akihojiwa na Mwandishi wa Habari wa ITV baada kikosi kazi kilichoundwa na  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(mwenye kofia) kuvamia ghala lake lililopo jijini Mwanza  leo. Ametakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 ndani ya masaa 24 leo. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina  (mwenye miwani)akikagua nyavu haramu za kuvulia samaki katika kijiji cha Kakukuru wilayani Ukerewe ambapo alichoma moto nyavu haramu za zenye  thamani ya  shilingi bilioni mbili. Kulia ni Lameki Mongo, Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  na kushoto ni Abbakary Murshidi, Afisa Uvuvi  wa Wilaya ya Ukerewe (Na John Mapepele)
  • Aapa kutokomeza uvuvi  haramu nchini
  • Asema imebaki 3% tu ya  Sangara wanaokubalika kuvuliwa katika ziwa Victoria
Na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Joelson Mpina  amekamata  marobota 1152 ya aina mbalimbali za nyavu haramu zisizoruhusiwa  kisheria  kutumika kuvulia samaki zenye thamani ya shilingi  milioni 894 jijini Mwanza na Singida ambapo baadhi ya nyavu  hizo zimetaifishwa na nyingine kuteketezwa na wamiliki wakitakiwa kulipa  faini ya shilingi milioni 120 ndani ya masaa 24 kwa makosa ya kufanya biashara ya nyavu hizo kinyume cha sheria.
Akiongea na  Vyombo vya Habari jijini Mwanza katika ghala la nyavu  la Meshack Chacha mara baada ya kukamata shehena  ya marobota 600 ya nyavu haramu kwenye ghala lake, Mhe. Mpina alisema nyavu haramu 294 kati ya 894 zilikamatwa na kikosi kazi maalum cha kudhibiti uvuvi haramu katika kanda ya Ziwa Victoria  alichokiunda hivi karibuni wakati mmoja wa wafanyabiashara hao Masagati Majani alijaribu kutorosha vyavu hizo kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.452 BBS kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam.
Gari hilo lipo katika kituo cha polisi cha Singida kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo kulingana  na sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, imetoa  mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia  kifungu cha 37(a) (ii) na (iii)
Aliwataja wamiliki wengine ambao walikamatwa kutokana na kujihusisha na biashara  haramu ya uagizaji na uuzaji wa vyavu zisizoruhusiwa kisheria kuwa ni Josia Jonam Obielo, Jeremiah Asam na Dastun Venant ambapo alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba  wafanyabiashara  wote  wanao agiza na kuuza zana haramu za uvuvi wanakamatwa na sheria kali zinachukuliwa ili kudhibiti uvuvi haramu nchini.
“Niliapa kusimamia ulinzi wa raslimali za uvuvi  nchini hivyo nitahakikisha operesheni  hii inakuwa ya  kudumu katika kupambana na uvuvi haramu hadi uvuvi haramu utakapokwisha” alisisitiza Mpina
Katika hatua nyingine Waziri Mpina  amelaani kitendo Kiwanda cha Sunflag cha mkoani  Arusha kwa kuendelea kufadhili uvuvi haramu nchini kutengeneza na kuuza   vyavu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa kisheria wakati Serikali imekuwa ikisisitiza viwanda vyote nchini kuacha tabia ya kufadhili uvuvi haramu kwa kutengeneza zana haramu za uvuvi.
Waziri Mpina ameagiza watalam kwenda mara moja katika kiwanda hicho kuchunguza  ukweli wa jambo hilo ili sheria zichukue mkondo wake.
Hivi karibuni Waziri Mpina aliunda Kikosi maalum cha kupambana na uvuvi haramu ambapo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne zaidi ya zana haramu za uvuvi ikiwa ni pamoja na nyavu zenye jumla ya bilioni tatu zimeteketezwa katika kanda ya ziwa Victoria peke yake huku viwanda  vitano vya kusindika samaki vilivyopo jijini Mwanza vikitakiwa kulipa jumla ya shilingi milioni 180 ndani ya masaa 24.
Viwanda hivyo vilitozwa faini hiyo kutokana na kuendelea kuwa wafadhili wakuu wa uvuvi haramu kwa kununua na kuchakata samaki aina Sangara wachanga na wazazi kinyume cha Sheria ya Uvuvi.
Waziri Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003  na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama  kwa mlaji na  kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.
Waziri Mpina alisema samaki aina ya Sangara kwenye Ziwa Victoria wapo katika hatari ya kutoweka kabisa katika kipindi cha miaka miwili endapo hali ya uvuvi haramu ukiachwa uendelee  bila kuchukua hatua za haraka na madhubuti kudhibiti janga hili.
Alisema kulingana na  utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki Tanzania (TAFIRI) 2017 unaonesha kuwa samaki wachanga waliochini ya sentimita 50 wasioruhusiwa kuvuliwa ni asilimia 96.6 ,  samaki wazazi walio zaidi ya sentimita 85 ambao pia hawarusiwi kuvuliwa ni asilimia 0.4 na samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu hivyo juhudi za pamoja za wadau wote wa sekta ya uvuvi zinahitajika ili kurejesha raslimali ya uvuvi katika Ziwa Victoria kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.