RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA KINYEREZI II JIJINI DAR.

March 16, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akianza ukaguzi katika Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni akitoa maelekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mitambo ya kufua umeme kwa kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kinyerezi hawapo pichani kabla ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba akifafanua jinsi ujenzi wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II kitakavyokuwa mara baada ya kukamilika  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM Ramadhani Madabida kabla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi  wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye ofisi za kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia huko Kinyerezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA TAKUKURU NA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA TAKUKURU NA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

March 16, 2016

1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala yaliyoulizwa wakati wa kikao.
2Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola akitoa maelezo kuhusu taasisi anayoiongoza kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
3Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akitambulisha kamati anayoiongoza.
4 
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Ruth Mollel (Mb) akitoa mchango wake katika kikao.
5 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (mkono wa kushoto) wakisalimiana na wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kabla ya kikao.
6 
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xvier Daudi akiwasilisha mada kuhusu taasisi anayoiongoza kwa wajumbe wa kamati ya Bunge, hawapo pichani.
7 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, kushoto, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa kikao na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
8 
Waziri wa Nchi, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kulia, akifafanua jambo wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Rais Magufuli aweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kinyerezi II

Rais Magufuli aweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kinyerezi II

March 16, 2016

indexZZ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
…………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Machi, 2016 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi namba mbili, uliopo katika wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam, ambao utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 240 za umeme.
Mradi huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia inayosafirishwa kwa bomba kutoka Mtwara, unatarajiwa kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha kuanzia miezi 21 hadi 28 utakapokamilika kabisa.
Kuanza kwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme huo, kunafuatia juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kufanikisha upatikanaji wa shilingi bilioni 120, ikiwa ni asilimia 15 ya fedha zilizopaswa kutolewa na Tanzania na fedha nyingine shilingi Bilioni 292 zimetolewa na Japan.
Mradi huu umetanguliwa na mradi wa Kinyerezi namba moja ambao una uwezo wa kuzalisha megawatts 150 za umeme, na mitambo yake tayari imeanza uzalishaji wa megawatts 105 zilizoingizwa katika gridi ya Taifa.
Pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Kinyerezi namba mbili, Rais Magufuli amekagua mitambo ya kuzalisha umeme ya mradi wa Kinyerezi namba moja, ambapo Mkuu wa Kituo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) cha Kinyerezi Mhandisi John Mageni, ametoa maelezo kuwa shirika hilo lina mpango wa kupanua uzalishaji wa umeme katika mradi huo kutoka megawatts 150 hadi kufikia megawatta 335, kwa kuongeza mitambo ya kufua umeme kwa teknolojia inayojumuisha matumizi ya gesi asilia na mvuke uzalishwao na mitambo hiyo.
Baadaya ya kupokea maelezo hayo, Rais Magufuli ameridhia kuwa serikali yake itatoa Dola za kimarekani milioni 20, kwa ajili ya kufanikisha upanuzi wa mradi huo na ameagiza kuwa wataalamu wa TANESCO washirikiane na Mkandalasi kuhakikisha upanuzi huo unafanyika haraka iwezekanavyo, badala ya muda wa miezi 12 uliopangwa.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO, kuanza kuachana na mitambo ya kukodi kwa ajili ya kuzalisha umeme, na badala yake nchi ijenge mitambo yake yenyewe ili kuondokana na gharama kubwa za nishati hiyo muhimu.
“Waziri, ukiona mtaalamu anakuletea mapendekezo ya kutaka kukodi mitambo ya kuzalisha umeme, badala ya kuleta mapendekezo ya kununua mitambo yetu wenyewe ujue mtaalamu huyo hafai, mtoe” Amesisitiza Rais Magufuli
Ameongeza kuwa tafiti zimethibitisha kuwa hadi sasa Tanzania ina zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 za gesi asilia, ambayo itazalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya ndani, na umeme mwingine kuuzwa nje ya nchi ikiwemo Kenya ambayo tayari imeomba kuuziwa umeme kutoka Tanzania.
Aidha, Rais Magufuli ametoa onyo kwa TANESCO kuwa hatarajii kusikia bwawa la maji la Mtera limeishiwa maji, kwa kuwa katika msimu huu wa mvua maeneo ya Iringa yalikuwa na mvua nyingi ambazo zimesababisha hadi mafuriko mafurukio.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, juhudi zilizofanyika zimefanikisha kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawatts 800 hadi kufikia megawatts 1,000 kiasi ambacho ni pungufu kwa megawatts 20 tu, ikilinganishwa na mahitaji ya megawatts 1020 za sasa.
Ameongeza kuwa pamoja na kuweka jiwe la msingi la mradi wa Kinyerezi namba mbili, hivi karibuni serikali inatarajia kujenga miradi mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, ikiwemo Kinyerezi namba tatu utakaozalisha megawatts 600, Kinyerezi namba nne utakaozalisha megawatts 300, na mingine itakayojengwa Lindi na Mtwara.
Prof. Muhongo amebainisha kuwa mpaka sasa gesi asilia inazalisha kati ya asilimia 50 na 60 ya umeme wote hapa nchini, Maji yanazalisha asilimia 30 hadi 40, na umeme unaozalishwa kwa mafuta hauvuki asilimia 10.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa Japani hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida, Wabunge wa kamati ya Nishati na Madini, wafadhili wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Afrika na Shirika misaada la Japan (JICA.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
WAZIRI PROF. MBARAWA AIPONGEZA TTCL

WAZIRI PROF. MBARAWA AIPONGEZA TTCL

March 16, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Morogoro.Mkuu wa Biasahara Kanda, Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa TTCL mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
Mkuu wa Biasahara Kanda, Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa TTCL mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro
…………………………………………………………………………………
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, ameipongeza Kampuni ya simu TTCL kwa juhudi inazofanya katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini na kuitaka kutumia kikamilifu fursa ilizonazo ili kujiendesha kibiashara na kutoa gawio kwa Serikali.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo Mkoani Morogoro Jumatatu hii alipokuwa katika ziara yake ya kukagua kazi zinazofanywa na Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kutoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji wa taasisi hizo.
Ziara ya Profesa Mbarawa katika Kampuni ya simu TTCL ilimwezesha kupata taarifa fupi ya utendaji wa Kampuni ya TTCL Mkoa wa Morogoro kwa mwaka 2015 pamoja na mipango na malengo ya Mkoa huo kwa mwaka 2016 ikiwa ni pamoja na mikakati itakayowezesha kuyafikia malengo hayo. Aidha Waziri Mbarawa alipata taarifa kuhusu utendaji wa Mkongo wa Taifa wa mawasiliano na changamoto zinazokwamisha Mkongo huo kufanya kazi kwa ufanisi.
Uongozi wa TTCL Mkoa wa Morogoro ulimjulisha Waziri Profesa Mbarawa kuwa, kikwazo kikubwa kinachokwamisha utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano uharibifu wa kukatwa kwa mtandao wa Mkongo huo kunakofanywa na baadhi ya wakandarasi wa barabara na wakandarasi wanaojenga mkongo wa kampuni ya simu ya Haloteli pamoja maporomoko ya ardhi huko Njombe na Igavisenga.
Akijibu hoja hizo, Profesa Mbarawa aliahidi kushirikiana na Menejimenti na bodi ya TTCL katika kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuwataka Wafanyakazi wote kubadilika, kufanya kazi kwa juhudi kubwa na moyo wa uzalendo ili kuiwezesha TTCL kuwa namba moja katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini na kumudu ushindani ulipo katika sekta hiyo hivi sasa.
Aidha, Waziri Mbarawa aliiagiza Menejimenti ya TTCL kuongeza kasi ya kupanua huduma zote zinazotolewa na kampuni hiyo na hasa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kukidhi mahitaji makubwa ya huduma hiyo na fursa kubwa ya kibiashara iliyopo kutoka kwa makampuni yanayotoa huduma za tehema.
Baadhi ya Wafanyakazi wa TTCL walimuuliza Waziri Mbarawa kuhusu tetesi zilizopo kuwa anakusudia kuanzisha taasisi nyingine na kuikabidhi jukumu la kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao tangu kuanzishwa kwake, umekuwa chini ya usimamizi wa TTCL ambapo Waziri Mbarawa alikanusha tetesi hizo na kusema kuwa, Serikali ilishafanya uamuzi kwa kuikabidhi TTCL jukumu la kuusimamia na kuuendesha Mkongo wa Taifa wa Mawasiano na hivyo hakuna mpango mwingine tofauti na uamuzi huo.
Waziri Mbarawa aliongeza kuwa kuwa, Serikali itaiongezea TTCL jukumu jingine la kusimamia kituo cha kutunzia kumbukumbu (Data Center) kinachotarajia kuanza kazi muda mfupi ujao pamoja na na kuahidi kusaidia kuiwezsha TTCL kupata masafa ili kuongeza uwezo wake wa kutoa huduma.
NAIBU WAZIRI DK. KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA MADAKTARI NA WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA MATENDO YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA.

NAIBU WAZIRI DK. KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA MADAKTARI NA WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA MATENDO YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA.

March 16, 2016

    NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wanataalum wa sekta ya afya kuacha mara moja vitendo vya kupokea na kuomba rushwa kwani endapo watabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Dk. Kigwangalla emesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kuadhimisha siku ya kinywa na meno duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya tiba ya kinywa na Meno, Muhimbili.

Ambapo amesema kuwa kwa utawala huu wa sasa Serikali ya awamu ya tano ni dhama nyingine na hawatamvumilia mtu.

“Ninaona tu, bado kuna wachache wanaojihusisha na vitendo vya kuomba rushwa hapa na pale. Kwa dhama hizi ukikutwa hatutakuurumia na hatutamuurumia mtu kwa hili. Tunapaswa kuweka maslai mapana kwa wananchi tunaowahudumia kwenye mioyo yetu” alieleza Dk. Kigwangalla.

Maadhimiho hayo kwa mwaka huu yenye kauli mbiu “Afya njema ya kinywa ni afya ya mwili mzima” kilele chake kinatarajiwa kufikia tamati Mkoani Morogoro ambapo kwa siku zote hizi hadi kilele, Madaktari watatembelea shule maalum kadhaa za ikiwemo ya Mtoni Maalum, Sinza Maalum, Buguruni Maalum na zingine za Mkoa wa Shinyanga na Morogoro ambapo pia watafanya uchunguzi na matibabu ya bure katika siku zote hizo.

Awali katika ufunguzi huo, kulitanguliwa na matembezi maalum ya KM 10, yaliyoongozwa na Naibu Waziri Dk. Kigwangalla ilikuhamasisha afya njema ya kinywa na mwili katika mapambano hayo.
Matembezi maalum ya ufunguzi wa siku ya maadhimisho ya kinywa na meno yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yakipita eneo la Maktaba Kuu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) aliyeyaongoza matembezi hayo pamoja na viongozi wengine waandamizi akiweo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Maseru (kushoto) na Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro wakiwasili katika viunga vya Eneo la Chuo cha tiba ya meno Muhimbili baada ya kutembea kwa umbali wa KM 10.
Baadhi ya viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembea kwa umbali mrefu wa KM 10 kama ishara ya kufungua maadhimisho ya siku ya tiba ya meno duniani.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akisoma hotuba maalum ya ufunguzi huo
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba kwa wananchi na wageni waalikwa katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba hiyo.
Mkuu wa Shule ya Kinywa na Meno, DK. Elison Simon akitoa hutuba yake katika tukio hilo.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi, Dk. Hamisi Kingwangalla wakati wa tukio hilo.

Baadhi ya viongozi waandamizi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajia kufanyika Mkoani Morogoro Machi 20.2016, ambapo watatoa huduma bure ya tiba ya kinywa na meno. (Picha zote na Andrew Chale).
Simbachawene awataka ma RC wafanye kazi kulingana na kasi ya Rais

Simbachawene awataka ma RC wafanye kazi kulingana na kasi ya Rais

March 16, 2016

41Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka TAMISEMI Bi. Suzani Chekani akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasilisha mada kuhusu kuwajibika kwa kuzingatia sheria za nchi kwa wakuu wa mikoa wapya katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam  kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.
42 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa(Hawapo pichani) kuhusu suala la kutatua changamoto zilizopo katika mikoa katika katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam
46 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Suleiman Jafo akizungumza na wakuu wa mikoa (Hawapo pichani) akiwataka kwenda kuwajibika kwa kwa kuzingatia sheria na kutatua changamoto za wananchi katika mikoa yao katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam  .
43 44  
Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifatilia maelekezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) katika kikao cha kuwakumbusha majukumu yao kama wakuu wa mikoa.45 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene  (kutoka wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa jana kulia mwa Waziri ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi  MAELEZO
……………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mhe.George Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa walioapishwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia muda mwingi kutatua kero zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Mhe.Simbachawene ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokutana na Wakuu hao wa Mikoa ambapo amewasisitiza kwenda na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kutimiza malengo yaliyopangwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.
“Mfumo wa sasa wa uongozi ni tofauti na mfumo wa zamani, namna Mhe. Rais anavyotaka tufanye kazi ni tofauti na zama zingine zilizopita,Wakuu wa Mikoa mnapaswa kujua kila kinachoendelea kila siku katika Mikoa yenu na mnapaswa muwajibike kwa wananchi wenu”alisema Simbachawene.
Mhe.Simbachawene ameongeza kuwa,Wakuu wa Mikoa wamepewa madaraka ya kusimamia mfumo wa ufanyaji kazi kwa kuhakikisha watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo kwakua nchi haiwezi kubadilika kama hakutakua na utendaji mzuri.
Aidha,Mhe.Simbachawene amewakumbusha Wakuu wa Mikoa wazingatie na kusimamia haki za wananchi kwakua kuna baadhi ya mamlaka za Serikali za Mitaa zinaripotiwa kuwaonea sana wananchi hasa wanawake katika kupata haki zao maana ndio wanaongoza kwa kunyanyaswa.
Pia amewataka Wakuu wa Mikoa kutumia mamlaka waliyopewa kuvunja mabaraza yote ya usuluhishi yasiyozingatia sheria katika kutoa maamuzi na kuunda mabaraza mapya yenye sifa za kutatua kesi za wananchi.
Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo ameahidi kuwapa Wakuu wa Mikoa ushirikiano wa kutosha kutoka Ofisi ya TAMISEMI ili kuhakikisha kazi zao zinafanyika kwa ufanisi.