VIONJO ,VYAKULA VYA ASILI KUPATIKANA NDANI YA TAMASHA LA HANDENI KWETU JUMAMOSI HII

December 12, 2013
Na Mwandishi Wetu, Handeni
BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.
AJALI ... BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI MBAYA LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR,WATU ZAIDI YA 12 WAHOFIWA KUFARIKI NA MAJERUHI ZAIDI YA 50.

AJALI ... BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI MBAYA LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR,WATU ZAIDI YA 12 WAHOFIWA KUFARIKI NA MAJERUHI ZAIDI YA 50.

December 12, 2013

Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.

Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.
Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.
Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, MRISHO GAMBO.