KINANA AWASILI PEMBA

May 03, 2014


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Pemba, Katibu Mkuu anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara Pemba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Viongozi wa CCM Pemba mara baada ya kuwasili Pemba leo ambapo anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika Gombani ya Kale.
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatiza mitaa ya Madungu Flat.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini vitabu vya wageni kwenye afisi kuu ya CCM Pemba Chake Chake pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wengine ofisini ni Naibu Katibu Mkuu CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Ndugu Abdala Mshindo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Ndugu Mzee Mbelwa.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia Buku la Wageni ( Kitabu cha Kusaini Wageni) cha Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Pemba
Buku la Wageni ( Kitabu cha Kusaini Wageni) cha Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Pemba

MRISHO MPOTO AWALIZA WAANDISHI NA WIMBO WAKE MPYA

May 03, 2014

Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani kwa washiriki wa mkutano unaoenda sanjari na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini msanii Mrisho Mpoto aliyekuwa akiimba wimbo mpya unaohusu waandishi wa habari,wimbo ambao umo katika albamu yake mpya aliyozindua leo .
Jaji Mstaafu Mark Bomani akizundua video mpya ya msanii Mrisho Mpoto ya wimbo wake unaohusu waandishi wa habari , katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha kunako fanyika mkutano unaenda sanjari na siku ya uhuru wa habari duniani.
Washiriki wa mkutano huo wakitizama Video mpya ya Msanii Mrisho Mpoto ya wimbo wake mpya unaohusu waandishi wa habari.
Wimbo mpya wa msanii Mrisho Mpoto uliwatia wengi Simanzi baada ya kutizama Video hiyo.
Msanii Mrisho Mpoto akimkabidhi Mh Jaji Mstaafu Mark Bomani VCD ya video ya albamu yake mpya ijulikanao kama "WAITE"kwa ajili ya uzinduzi.
Mh,Jaji Mstaafu akizindua rasmi albamu ya pili ya msanii Mrisho Mpoto ,Ijulikanayo kama "Waite"
Msanii Mrisho Mpoto akizungumza muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa albamu yake mpya ya WAITE.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
SUPER STAR DIAMOND PLATZNUM AAAHIDI KUTENDA HAKI KWA WANANCHI WA MTWARA ONA ALICHOSEMA LIVE!!

SUPER STAR DIAMOND PLATZNUM AAAHIDI KUTENDA HAKI KWA WANANCHI WA MTWARA ONA ALICHOSEMA LIVE!!

May 03, 2014

Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum,akiwapagawisha mashabiki wake wa mkoa wa mtwara waliofurika katika Tamasha la Ties & Heels lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye ukumbi wa Makonde beach Mkoani Mtwara jana.
Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum,akicheza na madansa wake wakati wa  Tamasha la Ties & Heels lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye ukumbi wa Makonde beach Mkoani Mtwara jana.
 
Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Diamond Platinum ameahidi kuwatendea haki wakazi wa mikoa ya kusini kila mwaka kwa kile anachodai mafanikio makubwa ya ndoto yake ya kuwa mwanamuzi bora hapa nchini imeanzia mkoa wa Mtwara.
 
Mwanamuziki huyo  aliambatana na  kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’ au Madame kama mashabiki wake walivyokuwa wakimuita amethibitisha kauli hiyo  kwa mashabiki wake waliofurika katika tamasha maalumu la Ties & Heels lililofanyika katika ukumbi wa makonde  beach Mkoani Mtwara na kudhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
 
Amesema tangu kuanza kwake kujiingiza kuwa mwanamuzi wa muziki wa kizazi kipya alianza kwa shoo yake mkoani mtwara ambapo ilionyesha kuwakuna wapenzi wengi na aliendelea kujulikana maeneo mengi hapa nchini kutokana na wapenzi walivyoanza kukumkubali, na ndipo aliwaahidi wapenzi hao kuwa ataendelea kuwasili mkoani humo kila mwaka kwa kulipa fadhila kwa mafanikio anayoyapata.
 
Akizungumzia juu ya shoo hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Kanda ya kusini wa Vodacom Tanzania, Henry Tzamburakis amebainisha kuwa tukio hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu.
 
“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini.” Alisema Tzamburakis.
 
Kwa kuongezea Tzamburakis amewashukuru  wakazi na mashabiki wote wa Diamond na wapenzi wa muziki wa Bongo Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na burudani wamenufaika na baadhi ya huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom.
 
Nae Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu alieambatana na mpenzi wake alisema hakuona shida kumsindikiza asali wake wa moyo mtwara yote haya kwaajili ya mashabiki wao. Kwa tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati kubwa ya kutembelewa nasi na tutadumisha utamaduni huu kila mwaka.

BREAKINGI NEWS??JANUARI MAKAMBA ASIMIKWA KUWA MLEZI WA UWT MKOA WA TANGA.

May 03, 2014
NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA AKILAKIWA NA MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA,AISHA KIGODA MARA BAADA YA KUWASILI LEO KWENYE HAFLA YA KUSIMIKIWA KUWA MLEZI WA JUMUIYA HIYO KULIA WA KWANZA NI KATIBU WA UWT MKOA WA TANGA,

NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA KUSHOTO AKISALIMIA NA KATIBU WA CCM MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA ANAYESHUHUDIA KATIKATI NI MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA,AISHA KIGODA

NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA KUSHOTO AKISALIMIA NA BAADHI YA WAKINA MAMA WA UWT MKOA WA TANGA LEO MARA BAADA YA KUWASILI.

NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA AKIWA TAYARI KUKAGUA GWARIDE LA GREEN GUARD WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA TANGA MARA BAADA YA KUWASILI LEO





HAPA NI NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA AKIVIKWA SKAFU MARA BAADA YA KUWASILI KWENYE HAFLA HIYO LEO

HAPA NI GREEN GUARD WAKIKE WAKIMVALISHA NAIBU WAZIRI WA MASWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA,JANUARI MAKAMBA SKAFU LEO KABLA YA KUANZA KIKAO CHA KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT MKOA AMBAPO WALIMPITISHA KUWA MLEZI WAO KUSHOTO NI KATIBU WA CCM MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA


HAPA MAKAMBA AKIWA AMESIMAMA AKIFUATILIA GWARIDE LA VIJANA WA GREEN GUARD WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUSHOTO NI KATIBU WA CCM MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA NA KULIA NI MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA,AISHA KIGODA




WAJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT MKOA WA TANGA WAKIIMBA KWEA FURAHA MARA BAADA YA MAKAMBA KUINGIA UKUMBINI LEO

HAPA WAJUMBE MBALIMBALI WAKIFUATILIA KWA MAKINI KIKAO HICHO

KUSHOTO NI NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOGIA JANUARI MAKAMBA AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA JIMBO LA KILINDI,BEATRICE SHELUKINDO KWENYE KIKAO HICHO LEO KATIKATI NI MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA,AISHA KIGODA


MWENYEKITI WA UWT WILAYA YA TANGA,MWASHAMBA PASHUA AKIFUATILIA KWA UMAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI KWENYE HALFA HIYO,JANUARI MAKAMBA KUSHOTO NI DIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,MAMA MAPINDA.














KATIBU WA UWT MKOA WA TANGA,AKITETA JAMBO KABLA YA KUANZA KIKAO HICHO LEO


KATIKATI NI NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOGIA ,JANUARI MAKAMBA KUSHOTO NI MWENYEKITI WA UWT MKOA WA TANGA AISHA KIGODA KULIA NI KATIBU WA CCM MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA WAKIFUATILIA MAMBO MBALIMBALI KWENYE KIKAO HICHO LEO

HAPA MWENEYEKITI WA UWT MKOA AISHA KIGODA AKITETA JAMBO NA NAIBU WAZIRI JANUARI MAKAMBA LEO