Makomandoo Kupamba Sherehe za Maadhimisho Miaka 55 ya Uhuru

Makomandoo Kupamba Sherehe za Maadhimisho Miaka 55 ya Uhuru

December 05, 2016
jenista
Na: Frank Shija – MAELEZO.
 
MAKOMANDOO wa Jeshi la Ulinzi wanatarajiwa kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo wwatacheza  gwaride  la kimyakimya.
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa  leo Jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Jenista amesema kuwa  mbali na maonyesho hayo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya Bendi ya Muziki wa kizazi kipya na Kizazi cha zamani, ngoma za asili za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.
 
Waziri Mhagama ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Aidha ametoa  wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Uhuru siku hiyo ya tarehe 9 Desemba ili kusjumuika na Watanzania wote katika kuadhimisha sherehe hizo.
 
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu”
 
MAJALIWA AZINDUA BENKI YA UCHUMI COMMERCIAL KATIKA MJI MDOGO WA KARATU

MAJALIWA AZINDUA BENKI YA UCHUMI COMMERCIAL KATIKA MJI MDOGO WA KARATU

December 05, 2016
bujiku
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajumbe wa bodi ya Benki ya Uchumi Commercial, tawi la Karatu kabla ya kufungua benki hiyo Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bujk
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Benki ya Uchumi Commercial tawi la Karatu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza kabla ya kufungua tawi hilo Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
piki
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Benki ya Uchumi Commercial tawi la Karatu Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pok
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Uchumi Commercial  tawi la Karatu baada ya kuifungua Desemba 5, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
telle

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea Benki ya Uchumi Commercial, tawi la Karatu  baada ya kuifungua Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHADEMA YAWANOA VIONGO WAKE WA MABARAZA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA.

December 05, 2016

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Lengo lilikuwa ni kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake ikiwemo kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama chadema ili kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu nchini.

Chama hicho kililaani zoezi la kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la Mwanza huku mazingira rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus alisema hatua hiyo inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa mwelekeo wa kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza machinga hao kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Na BMG Habari
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Diwani wa Kaya ya Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

SERIKALI YATAKIWA KUBAINISHA STENDI ZA DALADALA JIJINI MWANZA

December 05, 2016

 Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akihojiwa na waandishi wa habari

Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa wamezisimamisha Daladala kwa kosa la kupakia abira eneo ambalo sio rasmi

 Jinsi magari yanavyogeuza katika eneo la Buhongwa
 Eneo la stendi isiyokuwa rasmi ya Buhongwa ilivyo katika kadhia ya ubovu
 Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akikagua eneo la barabara ya Buhongwa ambayo inatumiwa na madereva Daladala kama stendi
 Gari likigeuza katikati ya barabara kutokana na kukosekana kwa eneo maalumu la stendi


 Wajasiriamali wakiwa katika eneo la biashara huku Daladala zikitumia eneo hilo pia kupakia na kushusha abiria
 Gari inageuza kituoni ambapo ni barabarani huku watu wakiendelea kuvuka barabara
 Dede akikagua barabara iliyoharibika
 Gari ikiwa imepaki katika eneo bovu la barabara ya Buhongwa



 Mwandishi wa habari wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akimhoji moja ya madereva katika eneo la Buhongwa

 Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede akisalimia na wakazi wa eneo la Nyashishi mara baada ya kuzuru katika eneo hilo ambalo ndilo amependekeza kuwa stendi ya daladala, kushoto kwake ni Mwandishi wa habari wa www.blogspot.com Ndg Mathias Canal

Na Mathias Canal, Mwanza

Uongozi wa Mkoa wa Mwanza umetakiwa kubainisha stendi za Daladala, maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara za mbogamboga na matunda kwa kina mama sambamba na kubainisha maeneo maalumu ambayo daladala haziruhusiwi kusimama kwani kufanya hivyo kutaondoa urasimu uliopo baina ya madereva wa Daladala na askari wa usalama barabarani.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede wakati alipozuru kujionea kadhia wanazokumbana nazo madereva wawapo barabarani sambamba na kujionea kandia wanayoipata kutokana na ubovu wa barabara na kutokuwa na stendi ya Daladala katika Mtaa wa Buhongwa nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana.

Dede alisema kuwa ni ajabu kwa nchi yetu kuwa na kituo cha daladala chenye mwanzo lakini hakina mwisho hivyo kuwafanya madereva kugeuza mahala pasipokuwa rasmi ambapo ni hatari kwa uhai na magari na madereva hao.

Katika eneo la Buhongwa zinapogeuzia daladala kama kituo, barabara yake ni mbovu huku pembeni kukiwa na machinga sambamba na wajasiriamali wanaouza mbogamboga na matunda jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa wafanyabiashara hao endapo kama gari litaharibika kutokana na hitilafu ya breki.

Hata hivyo alisema kuwa kumekuwa na wimbi la ukamataji na kutozwa faini na askari wa usalama barabarani kwa madereva hao kutokana na kuegesha magari katika eneo la barabara kwa ajili ya kupakia abiria jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani hakuna kituo katika eneo hilo pamoja na madereva hao kulipia ushuru kila siku.

Dede alisema kuwa katika njia itokayo Kishiri, Airport, Ilemela na Kisesa kuelekea Buhongwa kuna jumla ya Daladala 1900 ambayo kwa siku moja kila gari inalipia ushuru wa shilingi 1000 ambapo kwa gari zote 1900 kwa siku serikali inakusanya kodi ya jumla ya shilingi 1,900,000/=.

Katika kipindi cha mwezi mmoja serikali inakusanya jumla ya shilingi 57,000,000/= huku ikiwa inakusanya jumla ya shilingi 693,500,000 kwa mwaka.

Dede amehoji fedha zote hizo serikali inafanyia nini kama imeshindwa kukarabati barabara itokayo Mwanza Mjini kuelekea Airport sambamba na kukarabati na kubainisha eneo maalumu la stedi kwa ajili ya Daladala.

Sambamba na hayo pia Dede amependekeza serikali kuhamisha kituo cha daladala kisichokuwa rasmi cha Buhongwa kuhamia katika eneo la Nyashishi lililopo mwanzoni mwa Wilaya ya Misungwi kwani kupitia kuwepo kwa eneo hilo daladala zote zitafanikiwa kuingia katika stendi hiyo na serikali itakusanya mapato mengi kwani itakuwa rahisi kuwabana madereva wote.

Katika Barabara itokayo Makao makuu ya Mkoa wa Mwanza (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa) kuelekea eneo hilo la Buhongwa kuna vituo rasmi visivyopungua sita huku vituo visivyo rasmi vipo zaidi ya 15 hivyo ni vyema uongozi wa Mkoa wa Mwanza kupitia ofisi ya usalama barabarani kusimamia jambo hilo na kuweka alama mahususi zitakazobainisha vituo hivyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAUZO WA KAMPUNI YA NDEGE YA BOEING, MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) PAMOJA NA BALOZI WA CUBA HAPA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

December 05, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw. Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James.

Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano imedhamiria kununua ndege nyingine nne zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.

"Sisi hapa tunazungumza kuwa watalii hawajafika hata milioni 2 kwa mwaka, lakini nchi kama Morocco inapata watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka, hii yote ni kwa sababu hatuna mashirika ya ndege ya kwetu, watalii wakitaka kuja hapa ni lazima waje kwa kuungaunga, wafikie nchi nyingine halafu ndipo wapate moyo wa kuja huku, licha ya kwamba sisi Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 duniani zenye maeneo mazuri yenye utalii

"Kwa hiyo niwaombe tu Watanzania wapende mali zao, kwa sababu wakati mwingine nikiangalia mitandao na magazeti ni ajabu huwezi kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta wanasifia tu ndege za watu wengine na wanazibeza za kwao" amesisitiza Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ametaja aina ya ndege mpya ambazo Serikali itazinunua kuwa ni ndege 1 aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kufika nchini Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018 na ndege moja aina ya Boeing 787 Dash 8 Dream Liner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 na inayotarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika.

Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi za Serikali zenye lengo la kuinua utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.

"Tumeleta ndege aina ya Bombardier hapa, zimepunguza gharama za safari mfano kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, sasa wanalipa kati ya 160,000/ hadi 200,000/- wakati nauli ilishafika Shilingi laki 8 na kitu, lakini watu wengine utakuta wanazungumzazungumza wee maneno ya hovyo kwa kutumiwa, tumeshaamua na tutafanya hivyo" amesisitiza Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika hapa nchini (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye amepandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika ofisi zake zilizopo Afrika Kusini.

Rais Magufuli amemshukuru Dkt. Tonia Kandiero kwa juhudi kubwa alizozifanya akiwa Mwakilishi Mkazi wa AfDB hapa nchini ambapo miradi mikubwa na muhimu katika maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa.

Akizungumza baada ya kuagana na Rais Magufuli Dkt. Tonia Kandiero amemshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha miaka 6 aliyokuwa hapa nchini na amesema anaondoka akiwa ameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimahusiano na AfDB ambapo miradi yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni imetekelezwa hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo anayemaliza muda wake baada ya kuiwakilisha nchi ya Cuba kwa miaka minne.

Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo kwa uhusiano na ushirikiano mzuri aliouendeleza kati ya Tanzania na Cuba uliojengwa na waasisi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Fidel Castro wa Cuba.

Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo amemshukuru Rais Magufuli na Serikali kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Cuba na amesema anaondoka akiwa anaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizi utaendelea kuwanufaisha wananchi ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za kijamii.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

05 Desemba, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo pamoja na ujumbe wake.

BLOGGERS TANZANIA WAPEWA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA UENDESHAJI WA MITANDAO YA KIJAMII

December 05, 2016



Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Dk. Hassan Abbas(wa pili kulia) akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Tanzania Bloggers Network(TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar.
Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi(aliyesimama)  akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tanzania Bloggers Network(TBN) uliofanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar leo

Baadhi ya Bloggers wakiwa kwenye mkutano wao 


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Dk. Hassan Abba  akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya bloggers.