DC MUHEZA :SIJARIDHISHWA NA HALI YA UFAULU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

April 19, 2017

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema hajaridhishwa na hali ya ufaulu kwa shule za msingi na sekondari wilayani humo kwa kuwataka walimu ambao shule zao zitafanya vibaya wawajibishwe.

DC Mwanasha aliyasema hayo mwishoni mwa wiki 
ambapo alisema licha ya kutambua zipo changamoto mbalimbali lakini sio sababu inayoweza kuchangia hali hiyo .

Alisema wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya ambazo zina historia kubwa
  kwa elimu hapa nchini hivyo wanapaswa kuienzi kwa wanafunzi kufanya vizuri ili kuweza kuinua kiwango cha taaluma kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Nafahamu zipo changamoto mbalimbali ikiwemo za elimu lakini suala
  hilo linafanyiwa kazi na serikali ili kuona namna ya kulipatia ufumbuzi  kama jamii ni sehemu ya elimu tushirikiane jinsi ya kuboresha miundombinu “Alisema.

Hata hivyo aliitaka jamii kuwafichua watoto wenye ulemavu ambao
  wamekuwa wakihifadhiwa majumbani na kushindwa kupata elimu ili waweze kupatiwa elimu ambayo inaweza kuwasaidia kukabiliana na maisha yao ya baadae.

“Tusiwafiche watoto wenye mahitaji maalumu majumbani badala yake tuone
  jinsi ya kuwapeleka shuleni ili waweze kupata elimu bora  ambayo inaweza kuwasaidia maishani”Alisema.

Naye kwa upande wake,Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya

Muheza,Julita Akko alisema wao wapo kwenye mikakati ya kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka  licha ya kukabiliwa na uhaba wa upungufu wa miundombinu.

Alisema  licha ya hivyo wanakabiiliwa pia na uhaba wa vifaa vya

kujifunzia kwa shule za msingi na sekondari hasa kwenye masomo ya sayansi na hisabati.

VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO

April 19, 2017
 Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia  wakionesha cd hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)

 Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Marick Omary,akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwasaidia na kutowafungia vijana hao kuuza cd hizo kwa kuwa zinawapatia ridhiki ya kihalali tofauti na kufanya kazi zingine zisizo za kihalali.

 Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Andhuhuri Mohamedy,akichangia hoja kwa waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwaruhusu wafanyabiashara hao (Machinga) kuendelea na biashara hizo ambayo inawawezesha kulisha na kusaidia familia zao na kusema kama kuna maboresho ni bora serikali wakae kwa pamoja wazungumze siyo kupiga marufuku watakufa njaa.

 Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Halima Bakari,akizungumza kwa majonzi kuhusu kuiomba serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwaruhusu wafanyabiashara hao waendelee na uuzaji wa tamthilia na filamu za nje kuendelea kuuza kwa kuwa kuna wanawake wengi wameachana na suala la kuuza miili yao (Biashara ya Ngono) ambayo siyo halali wakajiingiza kuuza cd hizo ili wapate kipato cha kihalali kwa hiyo kuwafungia ni kuwarudisha nyuma kifikra.
 Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

  Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia  wakionesha cd hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

UTALII WA BALOON WAWA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.

April 19, 2017
Kikapu maalumu kinachotumika katika Baloon kwa ajili ya kubeba watalii kikishushwa katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya Utalii wa Baloon.
Waandaaji wa Baloon wakifanya maandalizi ya kuliandaa Baloon hilo kwa ajili ya kubeba wageni wakati wa maandalizi ya kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Rubani wa Baloon linalo milikiwa na Kampuni ya Serengeti Balon Safari  ,Masoud Mohamed akitoa maelekezo kwa crew yake wakati wa maandalizi ya balon hiyo.
Watangazaji wa Kipindi cha Clouds 360 James Tupatupa na Sam Sasali wakiwa mbele ya Baloon wakati liwekewa hewa kabla ya kuanza safari ya utalii.
Baloon likiwekewa hewa .
Sehemu ya ndani ya Baloon ikionekana wakati likijazwa hewa kabla ya kuanza safari.