RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI YA TAKUKURU YA 2015/2016

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI YA TAKUKURU YA 2015/2016

April 11, 2017
RAS1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akitoa muhtasari wa Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017
RAS2
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017
RAS3 RAS4
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kupokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwa mwaka 2016/2017 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017
RAS6 RAS7 RAS8 RAS9
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola na watendaji wa taasisi hiyo baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwa mwaka 2015/2016
Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKAJI KUZINDUA KLABU ZA ELIMU YA UZIMAJI MOTO SHULE ZA SEKONDARI NCHINI

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKAJI KUZINDUA KLABU ZA ELIMU YA UZIMAJI MOTO SHULE ZA SEKONDARI NCHINI

April 11, 2017
AND1
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo),jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
AND2
Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wakuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, akiuliza swali kwa Kamishna Jenerali wa jeshi hilo,Thobias Andengenye(hayupo pichani), wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
AND3
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wakuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye  wakati wa mkutano huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MABALOZI WAPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAMUAGA RAIS DK. SHEIN

MABALOZI WAPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAMUAGA RAIS DK. SHEIN

April 11, 2017
MAB1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mabalozi wapya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha  Tanzania  katika Nchi mbali mbali walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 11/04/2017.
MAB2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha  Tanzania katika Nchi mbali mbali,  walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo/ [Picha na Ikulu.] 11/04/2017. 
RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA WAJUMBE WA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYOMO KWENYE MCHANGA KUTOKA MIGODINI

RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA WAJUMBE WA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYOMO KWENYE MCHANGA KUTOKA MIGODINI

April 11, 2017
AP1
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Nehemiah Eliachim Osoro kuwa mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017 
AP2
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa mjube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP3 AP4
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Oswald Joseph Mashindano  kuwa mjube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP5
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Casmir Sumba Kyuki kuwa mjube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP6
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Usaje Benard Usubisye kuwa mjube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP7 AP8
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Butamo Kasuka Philip kuwa mkube wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP06
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akisalimiana na Gabriel Pascal Malata na wana-Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017
AP10
AP11
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Nadrew Wilson Massawe kuwa mjumbe Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017 
AP12 AP13
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akiongea na wajumbe wa Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini baada ya kuwaapisha kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017 
AP14
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania John Pombe Magufuli akiongea na wajumbe wa Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini baada ya kuwaapisha kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017 
PICHA NA IKULU

Huduma za Benki ya NMB Zasogea Mtaani Kwako

April 11, 2017



Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi. Kulia ni Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama.
 Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipokuwa wakizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi zenye gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria. Kwa huduma hizo mteja wa NMB anaweza kuweka na kutoa fedha mtaani kwake, kuangalia salio na hata kufanya malipo ya tozo mbalimbali akiwa katika mawakala wa NMB popote alipo.


UPATIKANAJI wa huduma za Benki ya NMB umezidi kuboreshwa na sasa umesogezwa zaidi mtaani kwako. 

Mteja wa NMB na asiyekuwa mteja kupitia huduma ya NMB Wakala sasa anaweza kuweka kutoa fedha na hata kulipia huduma mbalimbali akiwa mtaani kwake bila ya uhitaji wa kufika katika tawi la benki ya NMB. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alipokuwa akitambulisha huduma hiyo iliyoboreshwa zaidi, Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria alisema kuboreshwa kwa huduma hiyo sasa kunawawezesha wateja kupata huduma za benki hiyo kwa haraka na kwa usalama na uhakika popote walipo.

Alisema huduma hiyo pia inamwezesha mteja wa NMB kuweza kuweka fedha, kutoa, kujua salio lake kwa gharama nafuu zaidi, huku ikitolewa na mawakala zaidi ya 2000 ambao wanapatikana maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo maeneo ya vijijini. 

Alisema lengo la NMB ni kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake tena kwa gharama nafuu. Alisema huduma zingine ambazo wateja wengine hata wasiokuwa na akaunti za NMB wanaweza kufanya kwa mawakala hao ni pamoja na kulipa ada za shule, kulipia tozo za luku, ving'amuzi, malipo ya TRA, leseni na bili za maji.
 

Tigo, Jackson Group kushirikiana uzinduzi wa Kitabu Ap

April 11, 2017
  Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa  uzinduzi wa Kitabu App ambayo  iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania Pembeni yake ni mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa.

Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa  akielezea namna ya kupakua KItabu App kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android  uzinduzi wa Kitabu App ambayo  iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania pembeni yake ni   Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael

Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna  ya matumizi ya Kitabu App kwa waandishi (Hawapo pichani) mara wakati wa  uzinduzi wa Kitabu App ambayo  iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania. katikati mtunzi wa hadithi Frank David na pembeni mwishoni ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael

Dar es Salaam, Tuesday, Aprili 11, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Kampuni ya Jackson Group kuzindua  App mpya ya mtandao  inayofahamika kama Kitabu App ambayo  iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania.
App hiyo  inaingia sokoni kama suluhisho  sio tu kwa wasomaji  bali pia kwa waandishi wa vitabu  ambao sasa wanaweza   kuuza na kufuatilia na mauzo ya vitabu vyao  kupitia simu zao za mkononi, kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE ambao ni mkubwa, wa kasi na mpana nchini.
Kujumuisha  vitabu kwa njia ya sauti  katika jukwaa moja  inatarajiwa kuwa App hiyo itabadilisha jinsi ambavyo Watanzania watakavyojijengea mazoea kujisomea,  hali ambayo itakuwa ni kinyume na kupungua kwa mazoea hayo ambapo kwa kiwango kikubwa  kumekuwa kunahusishwa na  kuwepo kwa utamaduni mbovu wa kujisomea miongoni mwa wananchi.     
Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa App hiyo Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael alisema, “Kampuni yetu inaendelea  kuthibitisha  kujikita kwake katika kuwekeza n katika kuboresha utamaduni wa kujisomea nchini Tanzania. Tuna imani kwamba App hii  itahamasisha mvuto wa kujisomea  miongoni mwa jamii na hivyo kufufua  kudorora  kwa utamaduni  hapa nchini.”
Shisael alisema, “Tayari wateja wetu wengi  wanapenda kutumia simu kuchati na marafiki pamoja na wanafamilia,” na kuongeza, “Kupitia Kitabu App tunatoa jukwaa muhimu kwa waandishi, wachoraji na wasomaji kwa ujumla kufikia sehemu rahisi  ya kusoma mada mbalimbali kupitia simu ya mkononi. 
Akizungumzia kufurahia kwake  kushirikiana App  hiyo na wateja wa Tigo Shisael alibainisha kwamba  hivi sasa wanaweza kuvipata vitabu  wavipendavyo wakati wakifanya mambo mengine kwenye simu zao
Akitoa maoni yake kuhusu App hiyo Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa  alisema, “ App yetu ya Kitabu App ni ubunifu ulioendeshwa kimkakati  ukiwa unahamasishwa na kukua katika kujumuishwa kiteknolojia. Kupitia App hii tunawaruhusu waandishi wa vitabu kufikia kiwango cha hali ya juu cha usoamaji  kupitia simu zao za kisasa. Wakati tuna waandeishi wengi wenye vipaji katika  aina mbalimbali za vitabu, hali kadhalika kuna uhitaji mkubwa wa  uelewa ndani yake.”
 Alisema, “Tunaamini kwa kuangalia  zaidi katika kukua kwa orodha yetu tunaweza kuleta mabadiliko ndani ya usambazaji kote nchini na kuirudisha tena furaha ya kujisomea  kwa Watanznania.”
Twissa aliongeza, “ Kitabu ni App  ya kuelimisha, kuburudisha  na kuunganisha na mada za kidini. Elimu  ni moja ya mitazamo yetu ya msingi, hivyo tunajenga ushirikiano  na tunatoa wito kwa taasisi za kielimu  kupakua mada zao, kuhifadhi kwa ajili ya kuchapisha na kusambaza vitabu.”

App ya Kitabu App inaweza kupakuliwa bure  na kwa hivi sasa  inapatikana katika simu za Android  ambapo mtumiaji  anatakiwa  tu  kutoa malipo kupitia TigoPesa kwa mada zinazohitajijka na mtu  binafsi.


LHRC YAWANOA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

April 11, 2017
 Mkurugenzi wa Baraza la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa katiba mpya inayoendelea Hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI MACHI 2017 UMEONGEZEKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 6.4

April 11, 2017
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dar es Salaam leo kupata taarifa ya mfumuko huo wa bei kwa mwezi Machi.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Veronica Kazimoto (kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwapatia taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongeza hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari 2017.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi wa Februari 2017.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi Machi 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi 2016.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari 2017.

Taarifa hiyo imeonesha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi 2017 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2016.

WASANII WAAHIDI BURUDANI KALI TAMASHA LA BURUDANI "NYANZA FESTIVAL 2017" JIJINI MWANZA

April 11, 2017
#BMGHabari
Wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali kwenye tamasha la kwanza na la aina yake la Nyanza Festival litakalofanyika April 15 na 16, 2017 Uwanja wa CCM Kirumba.

"Zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu". Amesema Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi.

Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo nikiwa ni kuukuza na kuuendeleza muziki wa Kanda ya Ziwa.