MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAZINGIRA JIJINI TANGA YASEMA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI NI MOJA KATI YA CHANGAMOTO INAYOIKABILI.

March 17, 2014


  MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAZINGIRA JIJINI TANGA,MHANDISI,JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
UHARIBIFU na Uchafuzi wa vyanzo vya mto zigi ambao ndio chanzo pekee cha maji kwa jiji la Tanga kunakosababisha ujaaji tope kwenye bwawa la maji na kupungua ubora wa maji ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Tanga(Tanga UWASA).

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji yatayoanza kesho mpaka Machi 22 mwaka uu jijini Tanga.
     
Wa kwanza kulia ni PRA wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Jijini Tanga,Mwanauwani Bawaziri akiwa na waandishi wa habari kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya wiki ya maji katikati ni mwandishi wa gazeti la mtanzani mkoa wa Tanga,Amina Omari na Nestory Ngwega wa Daily News
Amesema ili kuweza kukabiliana na hilo mamlaka hiyo ina kamati ya mazingira kuzunguka bwawa hilo kwa kushirikiana na WWF(T) imeshaingia makubaliano na kikundi cha umoja wa wakulima wahifadhi mazingira kuhihwi Zigi (UWAMAKIZI tangu Novemba  mwaka jana kwa kipindi cha miaka mitatu ili kukindi hicho kiweze kufanya hifadhi ya vyanzo vya mto zigi.

Katika maeneo ya vijiji vya Kimbo,Mashewa, Kwaisaka, Shembekeza  na Mashewa ambapo watu wapatao 374 wamejiunga na kikundi hicho ambapo Tanga UWASA itachangia sh.milioni 100 kwa kikundi hicho katika kipindi cha miaka mitatu.

 Aidha amesema changamoto nyengine inayowakabili ni utegemezi wa umeme wa TANESCO ambapo inatarajiwa hapo baadae kupitia “Water Sector Development Program –WSDP huu ni mpango wa kuboresha miundombinu ya maji unaofadhiliwa na benki ya dunia na serikali ya Tanzania kutanunuliwa “Standby Generators ili pale penye katiko la umeme la muda mrefu kuwashwe kupitia Generator hilo.

Akizungumzia mafanikio,Mhandisi Mgeyekwa amesema tokea kuanzishwa  mamlaka hiyo miaka kumi na tano iliyopita wamefanikiwa kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 23.4 kufikia desemba mwaka jana.

POLISI YANASA KIWANDA CHA KUTENGENEZA KONYAGI FEKI.

March 17, 2014
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitizama sehemu ya mbele ya kiwanda cha kutengenezea Konyagi feki ambapo muonekano wake ni maduka na saloon.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAZINGIRA JIJINI TANGA KUAZIMISHA KWA KUFANYA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII

March 17, 2014
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAZINGIRA JIJI LA TANGA,MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISI KWAKE JUZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI
March 17, 2014

MAGADI SODA KULIINGIZIA TAIFA SHILINGI BILIONI 480 KWA MWAKA

1 (10) 
Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya habari Frank Mvungi 
2 (6) 
Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga  
3 (6) 
Mhandisi wa mradi wa  magadi soda  Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia  kiasi cha dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga 
PICHA ZOTE  NA. Georgina Misama-MAELEZO
March 17, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL A AFUNGUA MKUTANO WA WAWEKEZAJI KATI YA ISRAEL NA TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM

1 (9) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Picha na OMR
3 (5)  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo. Picha na OMR
March 17, 2014

Viongozi wa Barclays Africa Group walivyotembelea nchini

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa, Kennedy Bungane (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini, Bi.  Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga wakati wa mkutano uliondaliwa kwa wateja na wadau wakati viongozi wakuu wa Kundi la Barclays  Afrika (the Group),  wakitembelea nchini, jijini  Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Ofisa Mkuu Vihatarishi (Risk) wa Barclays Afrika, Anil Hinduja.
March 17, 2014