CCM NA CHADEMA WAANZA KUWANADI WAGOMBEA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KIBORILONI.

January 20, 2014

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanajro, Iddi Juma, (aliyeshika kipaza sauti), akimnadi mgombea wa CCm katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani, Wlly Adriano katika uchaguzi uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwanbi wa Kata ya Kiborloni, Vincent Rimoy, alyefariki dunia ghafla Novemba 6 mwaka jana.
Katibu Mweznezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Michael Mwita (Kushoto) akiteta jambo na Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Kiboriloni wa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Willy Adriano, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata hiyo,, Marehemu Vincent Rimoy aliyefariki dunia Novemba 6, mwaka jana.
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi (kushoto), akiwa akimtambulisha Mgombea wa Udiwani katika kata ya Kiboriloni, Willy Adriano aliyesimama katikati, kulia kwake ni Mke wake.

Na Fadhili Athumani, Moshi

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA), mwishoni mwa wiki walifanya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi  mdogo wa udiwani katika kata ya Kiboriloni liliachwa wazi kufuatia  kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Vincent Rimoy (CHADEMA),  aliyefariki ghafla Novemba 6 mwaka jana.

Wa kwanza kufanya uzinduzi ni Chadema, waliozindua kampeni yao kwa  mbwembwe wakimtambulisha mgombea wao, Frank Kagoma ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi, uzinduzi ulioongozwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa chama hicho mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemon Ndesamburo.

Wakizungumza katika Nyakati tofauti katika uzinduzi huo uliofanyika, Jumamosi ya Januari 18, mwaka huu, katika stendi ya kidia, viongozi wa Chadema walianza kumnadi mgombea wao ambap[o walimtaja kama mtu sahihi ambaye anaweza kuendeleza mapambano ya chama hicho ndani ya baraza la madiwani kupinga ufisadi na uonevu katika manispaa ya Moshi.

Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafari Michael, aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa Chadema kwani ndiye mwenye uwezo wa kutekeleza yale yote aliyoyaanzisha Marehemu Rimoy ndani ya kata hiyo na baraza la madiwani.

“Wananchi wa kiboriloni msidanganyike, chaguo la kweli katika maendeleo ya kata hii ni Kagoma, katika kipindi chake kama mwenyekiti Kagoma alifanikiwa kuvunja magenge yote ya ujambazi na sasa mnatembea vifua mbele bia wasiwasi, tupeni kagoma tuendeleze moto wa Chadema ndani ya Baraza la Madiwani, tupeni kagoma tukamalizie kazi aliyoianzisha Rimoy,” alisema Rimoy.

Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Filemona Ndesamburo alisema kazi ya kuleta maendeleo katika kata hiyo na mkoa kwa ujumla  unaweza kufanywa na watu makini wenye uthubutu kama alivyo na uthubutu Mgombe wa kiti hicho, Frank Kagoma.

Kwa upande wao, Chama cha Mapinduzi CCM, waliofanya uzinduzi wao juzi, kwa kumtambulisha mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Wlly Adriano walisema Maendeleo ya kata ya Kiborloni ni zaidi ya itikadi za siasa na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya uamuzi sahihi.

Akizungumza na maelefu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya Kidia, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi alisema wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa njia mbalimbali, ikiwemo  kufanya vurugu na maandamano.

 “Unajua ukisikia nchi fulani ina maendeleo kiuchumi, kisiasa na mambo mengine ni kwa sababu kuna amani, kwa hiyo hili jambo ndugu zangu ni muhimu sana kulizingatia ili kutuwezesha kuendelea na kazi zetu za kijamii vizuri” alisema Kazidi.

Kwa upande wake Mchumi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, aliwataka  vijana kutokuuza shada zao za kupigia kura kwani kufanya hivyo ni kuuuza maendeleo yake.

Aidha Matemu aliongeza kwa kusema  kuwa siasa bila maendeleo hakuna kujenga msingi wa kuleta maendeleo, na kuwataka wananchi wa kata ya kiboriloni kuchagua Willy Adriano ili aweze kuwawakilisha katika baraza la madiwa la Manispaa ya Moshi.

Naye Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano, alisema Siasa za Tanzania haziwezi kupiga hatua endapo wananchi hawatabadilika na kuacha tabia ya kuchaguana kwa kuangalia kigezo cha itikadi za kisiasa.

Uchaguzi mdogo wa udiiwani  katika kata ya Kiboriloni uunarajiwa kufanyika Februari 9 mwaka huu kuziba pengo lililoachwa wazi kufuatia kifocha aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa tikiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Vincent Rimoy.

Rimoy ambaye alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, alifariki dunia ghafla, Novemba 6 mwaka jana, baada ya kudondoka akiwa shambani kwake eneo la mandaka wilaya ya Moshi.

Mwisho.
January 20, 2014

*HAFLA FUPI YA KUWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU DAR JANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na mkewe aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta na  familia yake, baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kulia kwa Makamu ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba. 
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwigulu Nchemba, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. 
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Charles Kitwanga, kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo.
January 20, 2014

MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

MWANAJESHI FEKI ATIWA MBARONI AKIMTAPELI DC

January 20, 2014
 'Koplo' feki akichukuliwa maelezo na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko.
 
Na Mashaka Mhando,TANGA 
VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa,vinamshikilia Edwin John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa.

 "Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT).

UVCCM TANGA YAWATANGAZIA KIAMA MADIWANI,WENYEVITI MIZIGO.

January 20, 2014
Na Oscar Assenga, Kilindi.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange amewataka madiwani na wenyeviti wa serikali za vijiji na vitongoji wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa wananchi kuacha kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

Makange alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha cha Makasia Kata ya Kwediboma wilayani hapa ambapo alisema viongozi wengi baada ya kupata nafasi za uongozi wamejisahau na kushindwa kutatua kero zinazo wakabili wananchi wao waliowachangua kitendo ambacho kinapelekea wananchi kuichukia serikali.

KISAUJI AWAFUNDA WANACHAMA WA CCM TAWI LA CHUO KIKUU ECKENFORDE TANGA.

January 20, 2014
Na Safari Chuwa ,Tanga.
VIJANA mkoani Tanga wametakiwa kusimama imara ikiwemo kuthubutu kujituma na kubuni ajira ambazo zitawawezesha kuyaendesha maisha yao badala ya kuendelea kukaa na kusubiria ajira ambazo huchukua muda mrefu kupatikana.

Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
  ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (MNEC) Salim Kisauji wakati wa sherehe za ufunguzi wa tawi jipya la chama hicho lililopo kwenye chuo kikuu cha Eckenforde mkoani Tanga.

KINGWENDU KUPAGAWISHA KWENYE BONANZA LA MICHEZO JUMAMOSI TANGA.

January 20, 2014
Na Burhan Yakubu,Tanga.

Msanii marufu wa sanaa za maigizo na uchekeshaji ,Kingwendu

anatarajiwa kushiriki katika bonanza litakalofanyika uwanja wa shule ya msingi majani mapana Jijini Tanga jumamosi ijayo januaria 25 mwaka huu.

Kingwendu atakuwa msanii mkaribishwa katika bonanza hilo ambalo
limekuwa likifanyika kila jumamosi ikiwa ni utekelezaji wa kamati ya uratibuinyaoongozwa na diwani wa kata ya Nguvumali,Mustapha Selebos iliyopanga kuwa itakuwa ikiwaalika wasanii na wachezaji mbalimbali kutoa burudani mjini Tanga.