MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 50 KUTOKA KAMPUNI YA TSN NA MIPIRA 50 KUTOKA KAMPUNI YA SMART SPORTS KWA AJILI YA MASHINDANO YA KINONDONI CUP

April 29, 2015


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
  Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo (wa pili kulia), akimkabidhi jezi na vifaa vya michezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yaliyoanzishwa na Makonda. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN , Koiya Kibanga.
Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo akimvalishe moja ya jezi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya mashindano hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN ambayo imetoa msaada wa vifaa hivyo vya michezo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  kinachosambazwa na Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), Khamis Tembo,Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TSN Group, Koiya Kibanga, Meneja Masoko na Mauzo wa TSN, Nafsa Soud na Mshauri wa TSN, Francis Bonda 'Kaka Bonda'
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka kampuni ya TSN pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kulia), ambaye ametoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.

 Suleiman Msuya

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.

Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.

Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.

"Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao," alisema.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.

Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

DKT. SHEIN AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI RUVUMA LEO

April 29, 2015


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015. Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent, Songea.

SHINDANO LA MAMA SHUJAA LAZINDULIWA WILAYANI KISARAWE

April 29, 2015



Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

Subira ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika  katika kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Subira amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake kushiriki  kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu  na kutaka zawadi ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.

 Aliongeza kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za kilimo bora.

Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema  kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.


Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu  akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
  Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
 Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
 Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengine pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapoanza.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga.
  Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
  Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.

 Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo wakto akizindua shindano la Mama Shujaa lililofanyika leo katika Kijiji cha Kisanga wilayani humo.
Dk.Shein azindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Ruvuma April 29, 2015.

Dk.Shein azindua mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Ruvuma April 29, 2015.

April 29, 2015
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015.
3
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
4
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
 Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent, Songea
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE.

April 29, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD2 AD3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD4 
R
ais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia mkutano huo. AD5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR
AD7 AD8 AD9 
Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania, waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR
………………………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Aprili 29, 2015, ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa dharura wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Harare, chini ya Uenyekiti wa Rais Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, Mwenyekiti wa sasa wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mkutano huo wa siku moja pia umehudhuriwa na Rais Seretse Ian Khama, Rais wa Botswana na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mfalme Muswati III wa Swaziland, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Namibia Hage Geingob, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Awali akifungua mkutano huo Rais Mugabe alisisitiza umuhimu wa nchi za SADC kuwa na mpango madhubuti wa Viwanda kwa kuwa uwepo wa viwanda utasaidia kupunguza tatizo kubwa linalozikabili nchi hizi hasa ajira, pamoja na uchumi duni unaotokana na ukosefu wa viwanda vya kuboresha bidhaa zinazozalishwa katika nchi za ukanda huu. Mkakati huu uliopitishwa na Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaanza mwaka huu 2015 hadi mwaka 2063. Katika mkakati huu nchi za SADC zinalenga kutanua uhuru wa soko katika utatu wa kanda za Kibiashara yaani SADC, EAC na COMESA ikiwa ni pamoja na kutenga eneo huru la ukanda wa kiuchumi wa nchi za kanda hizi, huku lengo likiwa kufanikiwa upatikanaji wa eneo huru la ukanda wa biashara kwa nchi za Afrika. Masuala mengine ni pamoja na kukuza bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizi katika masoko ya Asia ambao ni walaji na watumaji wakubwa wa malighafi zinazozalishwa katika nchi hizi.
Rais Mugabe alifafanua pia kuwa, nchi hizi kwa umoja wake zikiunganishwa utakuta ndizo zina rasimali kubwa ya madini ya Dhahabu, Almasi na hata Gesi na kwamba kama mtengamano huu utakamilika nguvu ya pamoja inaweza kugeuza hali ya maisha ya wananchi wa nchi hizi sambamba na maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo.
Awali akizungumza kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Mugabe, Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Lawrence Tax aliishukuru serikali ya Zimbabwe kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu ambao ulikuwa ni mwendelezo wa ule uliofanyika Victoria Falls, Zimbabwe Agosti 17, 2014 mkutano uliotaka nchi wanachama wa SADC pamoja na kupitisha mkakati wake wa Kimaendeleo, upange dira ya utanuaji na uendedlezaji viwanda katika ukanda huu.
Matukio mengine katika mkutano huu ni pamoja na makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, makabidhiano yaliyofanywa na nchi ya Zimbabwe chini ya Rais wake Robert Mugabe kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Pia Rais Mugabe alitumia muda huo kuutaka Mkutano huu wa Dharura kutoa heshima zao kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi kwa kutambua mchango wake katika uhuru wa nchi zilizomo SADC na pia mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi. Raia Mugabe alimtaja Hayati Brigedia Mbita kama mpiganaji mahiri na kiongozi aliyefanya kazi kwa maslahi ya watu wengi bila kuchoka na kwamba Afrika na SADC vitamkumbuka daima kwa mchango wake huo.
Imetolewa na:    Ofisi ya Makamu wa Rais
                                 Harare, Zimbabwe
                                       Aprili 29, 2015
WATUHUMIWA WA KESI ZA UGAIDI ARUSHA WAIBUA MAMBO MAHAKAMANI

WATUHUMIWA WA KESI ZA UGAIDI ARUSHA WAIBUA MAMBO MAHAKAMANI

April 29, 2015

images 
Mahmoud Ahmad,Arusha
…………………………………………
 
Watuhumiwa 60 wa kesi za ugaidi jijini Arusha wamemuomba Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Nestory Barro kuchukua uamuzi mgumu wa kufanyia kazi kwa vitendo makosa yaliyomo kwenye Sheria dhidi ya tuhuma zinazowakabili.
 
Madai hayo waliyatoa mwishoni mwa wiki iliyopita  wakati kesi zao zilipokuwa zimepangwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo Mwendesha Mashitaka wa Serikali Augustine Kombe aliziahirisha hadi Mei 8, Mwaka huu kutokana upelelezi wa polisi kutokamilika.
 
Akizungumza mahakamani hapo kwa niaba ya wenzake mara baada ya kunyoosha mkono na kupewa nafasi na Hakimu Barro, mtuhumiwa Jafar Lema aliyeomba kujulishwa wanapokuwa mahakamani hapo wanakuwa chini ya mamlaka ipi.
 
Hatua ya kuuliza swali ilikuja baada ya mtuhumiwa mwenzake kutaka kujua suala la dhamana dhidi ya mashitaka yanayowakabili ilihali akidai wapo watuhumiwa wenzao waliopewa dhamana wakiwa polisi na wanaendelea kuripoti kituoni hadi leo.
Akitoa ufafanuzi kwa mtuhumiwa na wenzake Hakimu alisema, kosa waliloshitakiwa nalo halina dhamana, kwani hata hao aliodai walipewa dhamana polisi na kutakiwa kuripoti wanaweza kuwa wana mambo yao na ndio maana hawapo mahakamani.
“Unajua sheria yetu hii bado ina makosa kwasababu mtuhumiwa unatakiwa uwe mahabusu wakati kesi yako ikiwa imeanza kusikilizwa na si wakati wa upelelezi,” alisema Hakimu Mkazi Baro.
 
Hata hivyo majibu hayo yalimpa fursa mtuhumiwa Lema kuomba kufahamishwa kwamba wanapokuwa mahakamani hapo wanakuwa chini ya nani, Polisi au Mahakama, ambapo Hakimu Mkazi Barro alimueleza kuwa ni Mahakama.
“Mheshimiwa Hakimu, sasa nakuomba usiogope, hakuna mtu atakayekufunga kwani Taifa litakuona wewe ni shujaa, nakuomba na wenzangu ufanyie kazi kwa vitendo makosa hayo yaliyopo kwenye sheria,”alidai mtuhumiwa Lema na kuongeza:
“Nakuomba umwambie Mwendesha Mashitaka wa Serikali Kombe ayarudishe majalada yote ya kesi hizi hadi hapo upelelezi utakapokamilika, kama watakusumbua nipo tayari mimi na wewe tushirikiane kufungua kesi ya Kikatiba,”alidai Lema
Hata hivyo Hakimu Mkazi Barro alilazimika tena kutoa ufafanuzi kwa mtuhumiwa huyo na wenzake akieleza kwamba alichokuwa akikisema mtuhumiwa kina ukweli kwamba sheria ina makosa lakini kwa shauri hilo yeye hana mamlaka yoyote.
“Katika mashitaka haya ya PI aisee sina mamlaka nayo, labda kama ingekuwa na makosa ya wizi wa kuku na mengine kama hayo huku nina mamlaka napo, sio katika hili,” alisema Hakimu Mkazi Barro.
Kwa upande wake Mwendesha Mashitaka Kombe akijibu maadhi ya madai ya watuhumiwa hao  aliwashauri kuandika barua kwa Mkurugenzi Mashitaka nchini (DPP), kuelezea kuhusu kuchelewa kukamilika kwa upelelezi wa kesi zao.
 
Watuhumiwa hao wameshitakiwa kwa makosa yaliyo chini ya Sheria ya kuzuia ugaidi, ambapo Sheria namba 22  ya Mwaka 2002 inasema upelelezi wa shauri hilo ukishakamilika, Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi. Watuhumiwa hao 60  waliopo katika kesi mbalimbali wanakabiliwa na mashitaka ya kuua, kujaribu kuua, kusajili na kusafirisha vijana kujiunga na kikundi cha ugaidi cha Al-Shabaab.
 
 Mbali na mashitaka hayo wanahusishwa na  tukio la  milipuko ya mabomu Bar ya  Arusha Night Park, mlipuko wa Bomu Viwanja vya Soweto na mlipuko uliotokea Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasite  jijini Arusha ambapo ilisababisha vifo na majeruhi.

WAZIRI WA MEMBE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM

April 29, 2015
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Membe akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 28, 2015. Rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinton Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).