Reli ya ‘Standard Gauge” Sasa Dar Mpaka Rwanda

January 14, 2018
Na. Judith Mhina 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuunganisha Reli ya Kisasa (Standard Gauge) kutoka Isaka mkoani Shinyanga mpaka Kigali nchini Rwanda, ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizi mbili.

Rais Magufuli ameeleza hayo leo Ikulu Jijini Daar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame aliyekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.“Mimi na Rais Kagame kumeongea mambo mengi ya ushirikiano na kwa pamoja tumekubaliana kuanza ujenzi wa Reli ya Standard Gauge kutoka Isaka mpaka Kigali,” ameeleza Rais Magufuli.

Ameeleza kuwa ili kuharakisha ujenzi wa reli hiyo, kwa pamoja wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na sekta ya ujenzi na wale wale wa Mambo ya Nje wa nchi hizi mbili kukutana haraka wiki ijayo kusughulikia masuala kadhaa yanayohusu ujenzi wa reli hiyo ikiwa ni pamoja na kujadili namna ya upatikanaji wa fedha za ujenzi.

Akielezea umuhimu wa kukuza uchumi na biashara baina nchi hizi mbili, Rais Magufuli amesema mpaka sasa mwenendo wa biashara kati ya nchi hizi umekuwa wa kusuasua na kwamba reli hiyo itasaidia kuimarisha biashara na ushirikiano wa Tanzania na Rwanda.

“Tunataka ikifika mwezi Desemba mwaka huu, mimi na Rais Kagame tuwe tayari tumeweka mawe ya msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hii,” alisisitiza Rais Magufuli.

Amesisitiza kuwa mbali na kuimarisha uchumi, ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa takribani kilometa 400 pia utatoa ajira kwa vijana wengi na kusaidia usafirishaji wa madini ya Nickel kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Tanzania ambapo madini hayo yanashindwa kuchimbwa kutokana na kukosekana usafiri madhubuti wa reli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kwamba Tanzania inamuunga mkono Rais Kagame kwa asilimia mia moja katika kuchukua Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba itafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi marafiki pia zimuunge mkono Rais huyo wa Rwanda.

Kwa upande wake, Rais Paul Kagame amemshukuru Rais Magufuli na Watanzania kwa kumuunga mkono katika nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na kwamba atafanya kila linalowezekana kuzishawishi nchi za Afrika kuongeza uwekezaji na kila nchi kuweka kikakati ya kuongeza ajira ili kuwafanya vijana waachane na dhana ya kukimbili nchi za Ulaya kutafuta maisha bora.

“Tatizo la vijaqna kukimbilia nchi za Ulaya linaweza kumalizika iwapo sisi Waafrika kwa umoja wetu tutashirikiana na kutafuta ufumbuzi, ikiwa ni pamoja na nchi moja moja kuweka mikakati madhubuti ya kuwapa elimu na ujuzi sahihi ili vijana hawa waweze kumudu mazingira yao na kujiendeleza.” Ameeleza Rais Kagame.

Aidha, Rais Kagame amesifu utendaji kazi wa Rais Magufuli na kuahidi kuja mara kwa mara nchini Tanzania kwa ajili ya ushauri na kujifunza zaidi. “Naahidi kuwa nitakuwa nakujamara kwa mara kuomba ushauri kutoka kwa Rais Magufuli ili kuweza kusaidia nchi zetu na Bara la Afrika kwa ujumla. Alimalizia Kagame

Hii ni ziara ya tatu kwa Rais Kagame kuzuru Tanzania tangu Rais Magufuli aingie Madarakani mwaka 2015. Mara ya kwanza alikuja kuhudhuria sherehe za kuapishwa John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI

January 14, 2018
MAAFISA Ugani wa Kata na Vijiji wilayani Lushoto mkoani Tanga wametakiwa kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake wahakikisha wanakwenda kwa wakulima ili kuwapa elimu ya namna ya kulima kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wakati wa ziara yake wa kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji na kusikiliza kero zinazowakabili.

Akiwa kwenye kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola, Mbunge huyo alisema wapo baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kwenda wa wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ili waweze kuwapa elimu ya namna ya kulima kisasa jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha maendeleo yao nyuma.

“Ndugu zangu maafisa ugani tambueni kuwa mnajukumu kubwa la kuhakisha mnakwenda kwa wananchi kuwaelimisha juu ya kulima kilimo chenye tija kwao kwani hiyo itawasaidia kuweza kupata mafanikio kuliko wanavyofanya sasa lakini pia acheni kukaa ofisini “Alisema.

“Kwani elimu ambayo mnaweza kuitoa inaweza kuwa chachu ya wakulima kuweza kulima mazao mazuri yatakayokuwa ya ushindani na soko la kisasa hivyo jambo hilo ni muhimu sana “Alisema.

Alisema iwapo wakulima wataweza kufikiwa kwa wakati wataweza kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kuweza kujiandaa vema na ujio ya fursa mbalimbali za miradi mikubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.

“Niwaambie ndugu zangu hii ni fursa muhimu kwa mkoa wa Tanga na wakulima ambao walikuwa wanazalisha mazao yao na kupeleka Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa laki nane hadi tisa lakini sasa mtakuwa mkitumia hata laki nne mpaka Tanga mjini kwani mradi ukianza kutakuwa na soko la uhakika”Alisema.

Aidha pia mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima
kubadilika kwa kuongeza uzalishaji kutokana na uwepo wa soko la uhakika kwenye mazao yao katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa kwa lengo la kuinua vipato vyao.

Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani humo,Juma Khamisi alimuhaidi mbunge huyo kuwa watashirikiana na maafisa ugani waliopo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya kulima kilimo chenye tija ili waweze kunufaika.

“Mh Mbunge tumepokea kauli yako kwa mikono miwili na sisi kama viongozi wa kijiji hiki tutahakikisha tunashirikiana na maafisa ugani,wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji ambao utakuwa chachu ya kuweza kuwainua kiuchumi kwa kuchochoea kasi ya maendeleo kwao “Alisema.

RAIS DKT MAGUFULI AAGANA NA RAIS KAGAME BAADA YA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI

January 14, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mazungumzo rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018


 Rais Paul Kagame wa Rwanda akiongea na vyombo vya habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akiongea na vyombo vya habari baada ya mazungumzo yake  rasmi na Rais Paul Kagame wa Rwanda  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018

Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiagana na viongozi mbalimbali  baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  mgeni wake  Rais Paul Kagame wa Rwanda baada ya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini  leo Januari 14, 2018.PICHA NA IKULU
THUWAIBA: ATOA MAAGIZO MAZITO KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA UWT ZANZIBAR

THUWAIBA: ATOA MAAGIZO MAZITO KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA UWT ZANZIBAR

January 14, 2018

IMG_0785
MAKAMU Mwenyekiti wa  UWT Taifa Bi.Thuwaiba Kisasi akizungumza na wanawake wa Umoja huo katika Mikoa ya Mjini na Magharibi Unguja katika mwendelezo wa ziara yake visiwani Zanzibar.
PICHA NA ABEID MACHANO
………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
VIONGOZI na watendaji mbali mbali wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) wametakiwa kukusanya taarifa na takwimu sahihi za wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Umoja huo kwa lengo la kupata wanachama wa uhakika watakaoleta ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Dola wa mwaka 2020.
Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Thuwaiba Kisasi wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Mikoa ya Mjini na Magharibi Zanzibar huko katika ukumbi wa Mkoa Mjini uliopo Amani, amesema ili CCM ishinde kwa kishindo katika Chaguzi mbali mbali za dola ni lazima kuwepo na mfumo rasmi wenye takwimu sahihi za wanachama hai.
Alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kinakabiliwa na changamoto zisizokuwa za lazima kwa baadhi ya uchaguzi mbali mbali uliopita kutokana na kuwepo kwa tabia chafu za baadhi ya watendaji kupotosha takwimu,hali inayopelekea kuwepo kwa wanachama ambao sio halisi.
“Hatutowavumilia baadhi ya watendaji ambao wanapotosha takwimu za wanachama wetu kwa kusudi ama kutumiwa na baadhi ya watu wengine kwa maslahi yao binafsi lazima tuwe waadilifu na wenye kuipenda jumuiya na Chama chetu kwa ujumla.
Kitendo cha kupotosha takwimu ni sawa na kukisaliti chama chetu na kupelekea kitumie nguvu nyingi wakati wa uchaguzi hali ya kuwa tuna rasilimali kubwa ya wanachama wanaokipenda na kukiunga mkono chama chetu”, amesema Makamu Mwenyekiti huyo na kuwasisitiza viongozi na watendaji wa UWT kuanzia ngazi za mashina hadi taifa kuhakikisha wanaratibu takwimu sahihi za wanachama hai hasa wapya wanaojiunga na chama hicho.
Pia alieleza kuwa Chama cha Mapinduzi kwa sasa kipo katika utaratibu mzuri wa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kadi za wanachama za Kielectoniki zitakazokuwa na taarifa zote za mwanachama kwa lengo la kurahisisha masuala mbali mbali ya kiutendaji ndani taasisi hiyo.
Alifafanua kwamba kupitia kadi hizo itakuwa rahisi kupata taarifa za wanachama hasa wa UWT ili iwe rahisi kuwapatia mikopo mbali mbali kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali na fursa zingine zitakazowawezesha kujiajiri wenyewe.
Kupitia mkutano huo ambo ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Makamu Mwenyekiti huyo yenye lengo la kuwashukru wanawake wa Umoja huo kwa busara zao za kumchagua kwa kura nyingi katika  uchaguzi wa UWT ngazi ya taifa pamoja na kukumbushana utekelezaji wa mikakati mbali mbali ya kiutendaji ndani ya umoja huo.
Pia liwambia  Akina Mama hao kuwa uchaguzi umekwisha hivyo makundi yaliyoundwa wakati wa vuguvugu la uchaguzi yavunjwe na badala yake washikamane kwa mustakabali wa maendeleo ya umoja huo na CCM kwa ujumla.
“ Tunashukru katika uchaguzi wa jumuiya zetu hazikutokea figisufigisu kama zilizotokea kwa baadhi ya uchaguzi wa jumuiya za wenzetu hivyo tusirudi nyuma bali tupendane, tushirikiane na kushauriana mambo mema yatakayoimarisha UWT kwa maslahi ya wanawake wote wa Tanzania.”, alieleza Thuiwaba.
Akizungumzia mikakati ya kiutendaji ya umoja huo kuwa ni pamoja na kuwapatia viongozi, watendaji na wanachama wa ngazi mbali mbali mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Naye Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Bi. Tunu Kondo amesema UWT  kwa Zanzibar imejipanga vizuri katika kwenda sambamba na mabadiliko mbali mbali ya kiutendaji yanayotokea katika chama na umoja huo.
Aliahidi kuwa maagizo mbali mbali yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti kwa upande wa Umoja huo yatatekelezwa kwa wakati mwafaka huku wakiendelea kufanya kazi kwa kasi,uadilifu na ufanisi wa hali ya juu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa UWT anayefanyia kazi zake Tanzania bara, Eva Kiwele Mwingizi ameeleza kufurahishwa kwake na ari na hamasa za kiutendaji za wanawake wa Umoja huo katika Mikoa mbali mbali Zanzibar na  kueleza kuwa hiyo ni ishara ya mafanikio.
Amesema huu ndio wakati wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania nzima kushirikiana katika masuala mbali mbali ya kiamendeleo, kijamii na kisiasa kwa lengo la kuidhibitishia dunia kuwa wanawake ni wachapakazi na sio watu wa kukaa ndani tu bila kufanya kazi.
Katika mwendelezo wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo anamalizia ziara yake hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa upande wa Kisiwa cha Unguja.

NAIBU WAZIRI WA MADINI BITEKO ,AMEWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI

January 14, 2018
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili  Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,akisaini kwenye kitabu cha wageni wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita. 
Afisa madini wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akitoa taarifa ya shughuli za madini mbele ya Naibu waziri wa madini Doto Biteko .
Naibu waziri wa madini Doto Biteko Akizungumza na Viongozi na Watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko   pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea 
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini   namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko  akitoa mkono wa pole kwa familia ambayo imekumbwa na msiba wa kuondokewa na kijana wao ambaye alifukiwa na kifusi wakati akiwa kwenye kazi ya uchimbaji.

Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akisalimiana na kutoa pole kwa kaka yake na marehemu wakati alipofika nyumbani kwao na marehemu.(PICHA NA JOEL MADUKA)
 
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akifurahia na wananchi wa kijiji cha Ikalanga wakati alipokwenda kuzungumza nao juu ya mikakati ya maendeleo.
Na,Joel Maduka,Geita.

Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao
wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria  ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka
mazingira mazuri ya utendaji  kazi kwenye
maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na  majanga
ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye  mgodi mdogokijiji cha Buntubili  eneo ambalo hivi
karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.
Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni
kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza  huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi
yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye
mazingira hayo.
“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja
anakufa katika  mazingira ya uzembe tunatamani
tuone  watanzania wote wanachimba
wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili
,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali
popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele
na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao
wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye
mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.
 
Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini
amewataka
wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na  ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza
kujisabasha hatari ya kupoteza maisha  kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali
nzuri ya uchimbaji.
Akisoma taarifa kwa Naibu waziri wa madini,mlinzi wa eneo hilo
la mgodi ,Bw Christopha Mazige .amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na ubishi wa
vijana watatu ambao walivamia mgodini hapo kwa lengo la kutafuta mali lakini
ghafla  wakiwa kwenye mabishano sehemu
moja ya ardhi alipokuwa amesimama kijana ambaye alifukiwa na kifusi ilikatika
na kushuka naye kwenye shimo kutokana na hali hiyo wenzake walikimbia.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Mhandisi Ally Maganga amesema
bado kuna changamoto zinazoikabili Sekta ya madini kama baadhi ya Wachimbaji wadogo
kushindwa kulipa kwa wakati tozo stahiki za madini kama vile ada za mwaka za
leseni na Mrabaha wa madini.

NAIBU WAZIRI KIJAJI AFANYA UZINDUZI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

January 14, 2018
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)amabye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la Wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu Arusha,alisema madhumuni ya baraza hilo ni kuwapa fursa watumishi kupitia wawakilishi wao pamoja na kujadiliana juu ya masuala mbalimbali.(Habari Picha na Pamela Mollel)
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akizungumza katika uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Makamu Mweneyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Bw.Juma Kaniki akisoma risala katika uzinduzi huo 
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi akiteta
jambo
na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro katika uzinduzi wa
baraza la pili la wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha
Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)katikati akinyoosha juu mkataba wa kuunda baraza ambao umehakikiwa na kusainiwa na Kamishna wa kazi,wa pili kulia niKaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,Dk.Faraji Kasidi,na wakwanza kushoto ni Didas Malekia Mwenyekiti wa tawi la IAA chama kilichounda baraza la wafanyakazi(THTU)
Sehemu ya Baraza la Wafanyakazi Chuo cha Uhasibu Arusha

Baadhi ya wanafunzi chuo cha Uhsibu Arusha wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa umakini ambapo pamoja na mambo mengi Naibu Waziri wa fedha na Mipango
Dkt.Ashatu Kijaji aliwasisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa mshiriki mkubwa wa
kupambana na rushwa ambayo inajikita katika kupotosha na kumomonyoa maadili.

Naibu Waziri wa fedha na mipango Mh.Dkt Ashatu Kijaji(Mb)
akiwa katika picha ya pamoja na baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu
Arusha Tarehe 10 Januari 2018
RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

January 14, 2018

1 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
3 5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye Gadi ya Jeshi ya heshma pamoja na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumpokea katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili (hazionekani pichani ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia frame ya Picha ya Kiasili aliyokabidhiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
13 14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kumpokea mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU