WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA ATCL DAR/DODOMA

January 16, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Januari 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ​ baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Mstaafu John Malecela akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania kati ya uwanja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Makamba atoa maelekezo katika kikao kazi

Waziri Makamba atoa maelekezo katika kikao kazi

January 16, 2017

TOAA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba akiwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.  Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
TOA 1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake. 
TOA 2
Sehemu ya Menejimenti timu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba kabla ya kuanza kikao kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro.
TOA 3
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) na Eng. Bonaventure Baya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
TOA 4
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bw. Ntime Mwalyambi akiwasilisha mada katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Video: Binti aliye mdatisha mwanaume mtandaoni kwa picha zisizo zake aibishwa

January 16, 2017
Ni jambo la kusisimua kutokana na huruka za vijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni mara baada ya kuona matumizi mabaya ya mitandao kama Facebook,Twitter, Instagram nk vikiongezeka. Vijana wengi  wanashindwa kutumia mitandao ya kijamii  kwa ajili ya masilahi yao badala yake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kutafuta wapenzi,utapeli, umbeya, kuanika nyeti zao yaani kuweka picha chafu nk.

Katika video hii Kijana Moses alipata urafiki na msichana ambaye anaitwa “Zaydar” mtandaoni, moses alivutiwa zaidi baada ya kuona picha za mrembo Zaydar kwenye Instagram na ndipo alizidi kukoleza urafiki, kuomba namba na kumtaka awe mpenzi wake, Zaydar hakukataa kwani na yeye  alikuwa anatafuta mwanaume wa kumchuna kisawaswa.

 Picha alizo kuwa akipost ‘Zaydar’ kwenye mitandao yake ya kijamii hazikuwa zake, alikuwa anaweka picha za warembo wengine ambao ni wazuri zaidi. Hivyo huruka ya moses alijua kuwa msichana anaye wasiliana naye ndiye yule kwenye picha kumbe sio. Timbwili zito ni badaa ya Moses na Zaydar kupanga (apointment) ya kuonana live Dar es salaam – Buguruni – Sokoni … angalia video .. tunaomba Support sanaa ya Tanzania Asante Tunamengi ya kukuelimisha kila wiki.

MBUNGE WA TANGA AWAOKOA ASKARI WA JIJI LA TANGA NA KIPIGO KUTOKA KWA WASAFIRISHAJI

January 16, 2017
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimika kuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwa na wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madai ya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.

Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimu Mbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasi na Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiashara hao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.

Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu na Assad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya gari linaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.

Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupo mkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoani Dodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio na kuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisi zao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.

Akizungumza  na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwa watulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzi kutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketi hivi karibuni mjini hapa.

  Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukua ushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambaye alisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo na wanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zote ambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.

Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo na atakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine za kielektroniki.

Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za Tanga Mombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi ni kutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jambo ambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs na hawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashine hizo.

Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari na kulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu za kutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs

 
Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

January 16, 2017

Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.
Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.
MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3.
Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.

DC HAI ,GELASIUS BYAKANWA AMUACHIA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO HATMA YA WATUMISHI WABADHILIFU

January 16, 2017
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinaonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanawa (katikati) akiwa na katibu tawala wa wilaya hiyo,Upendo Wela (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya hiyo Yohana Sintoo (kushoto).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho . 
 
Na Dixon Busagaga,Hai.
 
 MKUU wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.
 
 Akiwa ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.

 Akihitimisha taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu Mkurugenzi ,Mhandisi Kweka.

 “Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa  Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani ,lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa ,Ofisi hizi mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.

 “Niishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.

 Mkuu huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo ya fremu za madawati badala ya madawati.

 Tuhuma nyingine inaihusu timu ya ukaguzi  iliyokiri kukamilika kwa kazi bila ya kuonesha kama walipokea madawati au walienda kukagua kazi ya mzabuni  licha ya mzabuni kuomba malipo ya fremu za madawati badala ya  Madawati kamili.

 Ofisi ya elimu msingi,ofisi ya mkurugenzi,ofisi ya Mhasibu wa Halamshauri na kitengo cha manunuzi pia zinatuhumiwa kushindwa kubaini nyaraka zilizowasilishwa na mzabuni endapo zilikuwa ni kwa ajili ya fremu za Madawati badala ya  Madawati kamili.

Katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Byakanwa alisema kampuni iliyopewa zabuni ya kutengeneza madawati ni ya Ujenzi na haijawahi kufanya kazi ya kutengeneza madawati, kuwa na karakana wala  vifaa vya uselemala .

Byakanwa alisema kwa malipo yaliyofanyika Halmashauri ilipoteza zaidi ya sh Mil 12 huku akishangazwa na hatua ya mmoja wa watumishi wanaotuhumiwa kuomba malipo badala ya mzabuni.

Akionyesha namna watumishi hao walivyokiuka taratibu Byakanwa alisema taarifa ya uchunguzi inaonyesha Halmashauri iliunda timu ya ukaguzi ambayo katika cheti cha ukaguzi na mapokezi ya bidhaa kinaonyesha bidhaa au madawati yalipelekwa ,Julai 16, 2016 ,siku 12 tangu siku ya mkataba na mzabuni.

“Mmoja w wajumbe wa kamati hiyo ya ukaguzi alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kuratibu zoezi la Madawati ,alikuwa na jukumu la kusambaza mbao kwa wazabuni na alikuwa anajua kuwa hajapeleka mbao za kutosha kwa mzabuni ,katika maelezo yake mbele ya tume anakiri kuwa mzabuni hajamaliza kazi kwa sababu Halmashauri haijampa mbao.”alisema Byakanwa.

Alisema mzabuni aliieleza tume kuwa anadaiwa madawati 246 na halmashauri na kuwa amekamilisha kutegeneza madawati 154 na ueleza kua alishindwa kukamilisha kutokana na kukosa mbao kutoka halmashauri.

“June 9,2016 malipo ya Sh Mil 19.2 yakalipwa kwa ajili ya fremu za madawati siyo Madawati.Vocha ya malipo ikasainiwa na DT na kuandaliwa na mtumishi mwingine (jina tunalo)  ikakamilisha mchezo.”alisema Byakanwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kufanya hivyo ilikuwa ni kinyume cha taratibu za malipo kwa kuwa wahusika walipaswa kujiridhisha na nyaraka walizokuwa wakitumia ,kwa nini mzabuni aliamua kudanganya Halmashauri.

Byakanwa aliishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yahana Sintoo alisema licha ya kwamba amefika wakati zoezi la uchunguzi lina kamilika bado atafanyia kazi taarifa hizo kwa umakini mkubwa ili kujiridhisha na utendajji kazi wa watumishi wa halmashauri hiyo.


VILIO, SIMANZI, MAJONZI VYATAWALA VIFO VYA WATOTO WA MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WALIOKOSA HEWA NDANI YA GARI JIJINI DAR ES SALAAM

January 16, 2017
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Therese wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mwanafunzi mwenzao Maria Masala wakati wa ibada ya kuuaga mwili huo iliyofanyika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Therese Ukonga Madafu Dar es Salaam jana.

Mkoa wa Mbeya wafikiwa na kompyuta za Bayport

January 16, 2017
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta nane Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock kwa ajili ya kuzigawa kwa Halmashauri nne za Mkoa huo wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kusini wa Bayport Financial Services, Emmanuel Nzuttu. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Bayport Mbeya, Mohamed Kisoki akifuatiwa na wakala wake Kurwa Lighton. Picha na Mpiga Picha wetu Mbeya.

Mbeya wataka kompyuta za Bayport ziongeze ufanisi wa kazi

Na Mwandishi Wetu,Mbeya
SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya, zimewataka watumishi wa umma katika mkoa wao,hususan kupitia ofisi zitakazonufaika na msaada wa kompyuta nane kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, kuongeza ufanisi wa kazi kwa kupitia vitendea kazi hivyo vilivyotolewa.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya, Nyasenga Enock, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, kwenye makabidhiano ya kompyuta zilizotolewa na Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Tunduma, Ileje, Mbeya na Rungwe, huku kila ofisi ikipokea kompyuta mbili.
Majadiliano yakiendelea katika makabidhiano hayo ya kompyuta kutoka Bayport Financial Services mwishoni mwa wiki, mkoani Mbeya.

Akizungumzia hilo, Enock alisema kwamba haitakuwa na maana kama msaada wa kompyuta za Bayport hautaongeza ufanisi kazini na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia vyema vitendea kazi hivyo vipya vinavyoweza kuleta tija kama kila mtumishi atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuwatumikia wananchi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock akigawa kompyuta hizo kwa wahusika baada ya kukabidhiwa na Bayport Financial Services.
Ugawaji wa kompyuta ukiendelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya.
“Huu ni msaada mkubwa kwa mkoa wetu, hususan wale ambao kwa namna moja ama nyingine watazipokea kompyuta hizi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ukizingatia kwamba mpango huu ulizinduliwa kwao tangu mwaka jana.

“Nawaomba wale ambao watapokea kompyuta hizi wakafanye kazi kwa nguvu zote tukiamini kuwa wenzetu wa Bayport watakapoamua kufanya utafiti wa vifaa vyao jinsi vilivyotumika, basi kuwe na tija ili waendelee kushirikiana na sisi kwa mambo mengine,” Alisema Enock.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema ni furaha yao kuzifikisha kompyuta hizo kwa mkoa Mbeya, ikiwa ni siku chache baada ya kuingia mwaka mpya wa 2017.

“Tunaamini kwa kiasi kikubwa kuwa wenzetu wa Mbeya watazitumia kompyuta tulizo wapa kama sehemu ya kupanua wigo wa kuwatumikia wananchi kwa ajili ya kukuza uchumi wao na Watanzania kwa ujumla kwa namna moja ama nyingine.

“Baada ya kuingia mwaka mpya wa 2017, Mkoa wa Mbea wamekuwa wa kwanza kupokea kompyuta zetu na tunaamini utaratibu huu utaendelea kwa mikoa nyingine kama tulivyojipanga kuhakikisha kwamba tunapunguza changamoto za ukosefu wa kompyuta kwa ofisi za serikali kwa sababu ni jambo la msingi na serikali haiwezi kufanya kila kitu,” alisema Mercy.

Taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa, imeamua kusambaza kompyuta 80 kwa ofisi za serikalini mikoani, huku Wizara ya Utumishi Makao Makuu tukiacha kompyuta 125, huku kompyuta zote hizo zikiwa na thamani ya Sh Milioni 500.