WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016

December 10, 2017
Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

CPA. Mwakapalila alisema kuwa taarifa bora za fedha ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi kwa kuwa walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine hutegemea taarifa hizo katika kufanya maamuzi.

‘Kama taarifa za fedha hazitatolewa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati mwafaka kunaweza kusababisha athari katika uthabiti wa mifumo ya kifedha nchini’, alieleza CPA. Mwakapalila

Aidha Mwakapalila amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

Amesema suala la Uchumi wa viwanda ni muhimu katika kuongeza kipato na kupata fedha za kigeni kwa njia ya kuuza bidhaa nje na pia kupata mapato ya kodi na yasiyo ya kodi hivyo akatoa rai kwa wananchi kuendelea kujadili masuala ya uchumi wa viwanda na kupata namna sahihi ya kuufikia ili ndoto ya uchumi huo ziweze kuwa za kweli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno amesema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kimataifa.

Amesema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha Hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.

Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Nkupama, amesema kuwa tuzo hiyo inawapa morali ya kufanyakazi kwa umahili zaidi na kuwapongeza watumishi walioko katika idara yake kwa kufanyakazi kubwa na bila kuchoka kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu za uhasibu wanapotekeleza majukumu yao.

Mshindi wa Jumla katika tuzo hizo kwa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 ni Twiga Cement Plc na kwa upande wa Wizara na Idara za Serikali ni Wizara ya Fedha na Mipango fungu hamsini (V. 50), tuzo ambayo ilipokelewa na Mhasibu Mkuu wa fungu hilo Bw. Christopher Nkupama, ikifuatiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji fungu arobaini na nne (V.44) na Ofisi ya Waziri Mkuu fungu ishirini na tano (V. 25)

Washiriki wa Tuzo hizo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Wizara na Idara za Serikali na Sekta Binafsi ambapo kwa mwaka huu waliojitokeza kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa walikua sita na Wizara na Idara za Serikali walikua sita.

Jumla ya washidani waliojitokeza ni 56 na waliofanikiwa kuvuka kigezo cha kuwa na zaidi ya asilimia 75 walikua washidi 36 na hao walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu kulingana na makundi.

Vilevile Idadi ya Wahasibu ambao wamehudhuria katika Mkutano wa mwaka ambao hufanyika kila mwaka kabla ya kutolewa tuzo hizo imepanda kwa asilimia 60 ambapo mwaka 2016 walihudhuria wajumbe 1700 ilihali mwaka huu 2017 wamehudhuria zaidi ya wajumbe 2700.
Wahasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 wakiwa katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto) baada ya kupokea Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zilizotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam .
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahasibu wa Wizara hiyo fungu 50 baada ya kuwakabidhi tuzo hiyo katika eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliyeshika tuzo ni Mhasibu Mkuu wa Fungu hilo Bw. Christopher Nkupama.
Washindi wa Kwanza wa makundi mbalimbali ya Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mmoja wa wahasibu walioambatana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50, Bw. Christopher Nkupama (hayupo pichani) akisalimiana na meza kuu baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 iliyotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (wa kwanza kulia) akimklabidhi Mhasibu wa Wizara ya Fedha na Mipango-fungu 50 (Vote 50), Bw. Christopher Nkupama (kushoto) tuzo kwa kuwa mshindi wa kwanza wa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 kwa kundi la Wizara na Idara za Serikali iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA. Pius Maneno.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila akieleza kuwa Uhasibu ni taaluma muhimu katika maendeleo ya Viwanda kwa kuwa wawekezaji hutumia taarifa za fedha zinazoandaliwa ili kutoa maamuzi, wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwaka wa Wahasibu na kugawa tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa washindi wa mwaka 2016, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA. Pius Maneno muda mfupi kabla ya kutoa tuzo za taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango
MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA

December 10, 2017
30
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya  Ndugu Rodgers William Sianga wakati akiwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahame Tom Nyanduga (kulia) alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
16
Sehemu ya wahudhuriaji wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Taasisi zote zenye usimamizi kuhakikisha zinasimamia vyema jukumu lao la kutumia nafasi zao kuongeza juhudi katika kuimarisha misingi ya Utawala Bora, Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji.
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
Makamu wa Rais alisema Vita dhidi ya ukiukwaji wa Maadili haiwezi kupiganwa na Serikali peke yake, “Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na maovu mengine vinatokomezwa”
Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kisera na kisheria ambayo itahakikisha vijana wanakuzwa kimaadili kwani hakuna Taifa Duniani linaweza kupata maendeleo bila kuwa na utamaduni unaozingatia maadili alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa ili kujenga Utawala Bora ni lazima  kuweka uwiano wa yanayofanyika na serikali kuu hadi serikali ya mitaa nchi nzima.Serikali ilizindua  Rasmi mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji  Awamu ya Tatu (NACSAP III) Desemba 2016.
Makamu wa Rais alisema kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya Ofisi za Serikali, Serikali imeamua kufuatilia uhalali wa vyeti vya Watumishi, Idadi halali ya Watumishi wa Umma na ulipaji wa Mishahara Hewa na kusisitiza zoezi ili litakuwa endelevu.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi na Watumishi wa Umma kwa ujumla kuwa Maadili ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. “Ni imani yangu kuwa Wakuu wa Taasisi hizi kuwa mtahakikisha misingi ya haki za binadamu, utawala bora na viwango vya Maadili ya Viongozi wa Umma vinasimamiwa ipasavyo ili kuimarisha nidhamu ya Maafisa na Watumishi wa Umma”.
Kuimarishwa na kudumishwa kwa nidhamu ya utendaji, huduma zitolewazo Serikalini, Ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya fedha za Serikali kutaleta mafanikio katika kuelekea uchumi wa kati.

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

December 10, 2017
 Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
 
Shirika la
Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa
Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.
 
Akizungumza
mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)
wa Tanesco, Demetruce Dashina amesema
kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku
kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka
ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
 
“Jana
tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo
ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo
huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya
hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema
Dashina
 
Amesema kuwa
shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha
mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
Kwa upande
wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa
usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo
iliyozoeleka.
 
Muhaji
amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo 
  kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya
kuwahudumia  kama inavyohitajika.
 Kaimu
Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)
 wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina Akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku 
   Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Leila Muhaji akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari juu ya kuimarika kwa Mfumo wa Ununuzi wa luku mara baada ya kuhamia sehemu nyingine. 
Waandishi wa habari habari walifika katika mkutano huo wakifatilia kwa Makini.
IGP SIRRO ATEMBELEA KIKOSI 673 CHA JESHI LA WANANCHI MKOANI DODOMA.

IGP SIRRO ATEMBELEA KIKOSI 673 CHA JESHI LA WANANCHI MKOANI DODOMA.

December 10, 2017
PICHA NO 1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akikagua maandalizi ya JWTZ Kikosi cha 673 katika harakati za maandalizi ya  kuamia mkoani Dodoma na alietangulia  mwenye nguo nyeusi  CEO Meltus Franci akimuonyesha IGP maeneo mbali mbali ya kikosi hicho.  Picha na Jeshi la Polisi.
PICHA NO 2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro  kushoto akiwa na mwenyeji wake CEO Meltus Franci, akikagua ujenzi wa gharama nafuu  katika Kikosi 673 ili kuupata ujuzi huo kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi watumie ili kupunguza gharama za Nyumba za Askari mkoani Dodoma katika harakati za kuamia mkoani humo.  Picha na Jeshi la Polisi.
PICHA NO 3
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro  kushoto akiwa na mwenyeji wake CEO Meltus Franci, akikagua ujenzi wa gharama nafuu  katika Kikosi 673 ili kuupata ujuzi huo kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi watumie ili kupunguza gharama za Nyumba za Askari mkoani Dodoma katika harakati za kuamia mkoani humo.  Picha na Jeshi la Polisi.

MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM

December 10, 2017
 Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Mchungaji Kulwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.
 Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
 Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.

Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.


 Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
 Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.
 Mtoto mkubwa wa marehemu,  Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.
 Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.
 Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho.

Na Dotto Mwaibale

VILIO Majonzi na simanzi vilitawala   wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.

Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.

"Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.

Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.

Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.

Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.

Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.