RC GALLAWA AWAONGOZA WAKAZI WA MKOA WA TANGA MAPOKEZI YA TIMU YA COASTAL UNION BINGWA WA UHAI CUP

December 02, 2013



MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,HEMED AURORA KULIA AKIPOKEA KOMBE LA UHAI CUP TOKA KWA NAHODHA WA TIMU HIYO NZARA NDARO LEO

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU  GALLAWA KUSHOTO AKIPOKEA KOMBE LA UHAI CUP TOKA KWA NAHODHA WA TIMU YA COASTAL UNION NZARA NDARO LEO MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI HAPA

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIWAPUNGIA MIKONO MASHABIKI WA SOKA MKOANI TANGA WALIOFURIKA KUWAPOKEA MABINGWA WA KOMBE LA UHAI 2013 COASTAL UNION YA TANGA.

MAPOKEZI YA COASTAL UNION TANGA YAVUNJA REKODI

December 02, 2013
KATIKATI MWENYE SUTI NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,BENEDICT OLE KUYANI AKIWA NA BAADA YA VIONGOZI WA MKOA NA WILAYA NJE YA UWANJA WA MKWAKWANI WAKIWASUBIRI WACHEZAJI WA COSATLA UNION



WALILIA BARABARA

December 02, 2013
OFISI ya Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Tanga inaombwa kuangalia uwezekano wa kuiingiza kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha barabara ya Mombo- Bangala chini- Kidundai- Kiluwai- Vuga yenye urefu wa km 9 ili kuwapunguzia kero ya usafiri wananchi wa maeneo hayo.

Wanaomba barabara hiyo ya kiwango cha vumbi kwa kuanzaia angalau itengewe fedha za kuifanyia ukarabati maalum utakaohusisha kazi za kuchonga, kupasua miamba (mawe makubwa) na kunyoosha ili kuwapa fursa wanakivijiji wanaoishi mlimani kusafirisha kwa Mpunga na Mahindi ambayo wanayalima katika mashamba yalioko katika skimu ya umwagiliaji ya Mombo.

KIDUNDAI WALILIA MAJI SAFI

December 02, 2013
WAKAZI zaidi ya 1,500 wa kijiji cha Kidundai kilichopo kata ya Vuga katika halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wanaiomba serikali kulitafutia ufumbuzi tatizo la kukosekana kwa huduma ya maji safi kijijini humo ili nao waweze kuishi kama watanzania wengine.

Wamesema wamechoka kudhaliliaka kwa kulazimika kuchangia chanzo pekee cha maji yasiyo salama na mifugo yao kwa zaidi ya miaka 20 sasa, maji ambayo yanapatikana katika mfereji wa Mbokoi ulioko umbali wa km. 3 kutoka kijijini kwao.

Wametoa kauli hiyo walipozungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa Tanga Raha alipotembelea kijijini humo mwishoni mwa wiki.

AGONGWA NA FUSO DARAJA LA MTO ZIGI.

December 02, 2013
Na Paskal Mbunga,Tanga..

MTU mmoja amejeruhiwa vibaya sana jana asubuhi baada ya kugongwa na gari la mizigo aina ya Fusso katika daraja la mto Zigi eneo la Amboni, nje kidogo ya jiji la Tanga.


Arif Mauji (58) mkazi wa Kibafuta wilayani hapa. 

aligongwa wakati akeendesha pikipiki kwenye daraja hilo ambapo ghafla lilitokea gari aina ya Fusso nyuma yake na kumgonga kasha kumburuta umbali wa mita 50 na kumtupa nje ya daraja na kuangukia kwenye kingo za daraja hilo akiwa taabani.


Arif aliumia sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja uso, miguu na miguu na pikipiki yake kuharibika vibaya sana kiasi cha kutoweza kutengenezwa tena.


Majeruhi alikimbizwa katika hospitali kuu ya Bombo ambako amelazwa.


MAKANGALE ACADEMYA SASA YAONYESHA CHECHE ZAKE

December 02, 2013
MCHEZAJI IDD KHAMIS IDDI MWABWIJU AKITIA SAINI KWENYE MKATABA WA KUJIUNGA NA ACADEMY YA MAKANGALE ILIYOPO PEMBA AMBAYO INAMILKIWA NA MWANDISHI WA HABARI MASANJA MABULA HUKU VIONGOZI WA ACADEMY HIYO WAKISHUGHUDIA (PICHA NA MASANJA MABAULA -PEMBA )





       

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

December 02, 2013
Release No. 203
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 2, 2013

KIINGILIO MECHI YA TANZANITE 1,000/
Washabiki watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini watalipa kiingilio cha sh. 1,000.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Kiingilio cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange. Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

HANDENI WALIVYOAZIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

December 02, 2013
Na Kambi Mbwana, Handeni
WANAUME wametakiwa kujenga tabia ya kucheki afya zao badala ya kuwaachia akina mama peke yao, ikiwa ni njia ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi uliozimishwa leo Dunia nzima, huku kiwilaya ya Handeni, yakifanyika katika Kata ya Kwasunga, wilayani Handeni.
Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, wa pili kulia mwenye koti jeusi akionyesha ujuzi wa kusakata rhumba katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kiwilaya, yalifanyika Kata ya Kwasunga, ambapoi alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alihudhuria majukumu mengine ya Kitaifa. Picha zote kwa hisani ya Handeni Kwetu Blog.
 Kaimu Mkurugenzi wa Handeni, Mr Mdoe, aliyesimama, akizungumza jambo katika madhimisho ya Ukimwi katika Kata ta Kwasunga, wilayani Handeni mkoani Tanga.
 Kamanda wa Polisi wa Handeni, OCD Zuberi Chembera, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, ambapo kiwilaya yalifanyika katika Kata ya Kwasunga wilayani Handeni mkoani Tanga. Chembera alimuwakilisha DC Muhingo Rweyemamu.