SERENGETI BOYS YATUA AFRIKA KUSINI

August 04, 2016

Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar walikoweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)

Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys na viongozi walipowasili Hoteli ya Garden Court Milapark  ambako imepiga kambi kabla ya kuivaa Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Baadhi ya Viongozi wa wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar. Kutoka kushoto ni Ayoub Nyenzi, Pelegrinus Rutayuga na Mshauri wa Ufundi, Kim Poulsen. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
PROF. MBARAWA ASISITIZA TATHIMINI UWANJA WA NDEGE SONGWE

PROF. MBARAWA ASISITIZA TATHIMINI UWANJA WA NDEGE SONGWE

August 04, 2016


br1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
br2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege zinavyoongozwa wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
br3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.
br4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo  kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
br5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
br6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
br7 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo  kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya ujenzi.
Amebainisha kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
“Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha inaendana na jengo lenyewe”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameeleza  ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na taratibu   za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
“Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya Taifa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa
Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAMUA ASILIMIA MBILI YA USHURU WA PAMBA IJENGE MADARASA

August 04, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga  
  Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima), Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi).
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Maswa, Mhe. Dila Mayeka akitoa mchango wake wa mawazo katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, kilichofanyika Mjini Bariadi


Na Stella Kalinga
Serikali Mkoani Simiyu imesema  asilimia mbili ya ushuru wa zao la pamba inayopatikana katika Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu ielekezwe katika ujenzi wa Miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari,hususani vyumba vya madarasa.
Uamuzi huo umefikiwa kufuatia majadiliano ya pamoja kati ya Uongozi wa Mkoa na Halmashauri zote katika kikao  kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka akiwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wilaya na Wajumbe wa Kamati za Fedha za Halmashauri ili kujadili mstakabali wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.
Mtaka amewaelekeza Wakurugezi wote wakafanye uhakiki na kuainisha takwimu sahihi  za mahitaji ya vyumba vya madarasa ili kupata uhakika wa vyumba vinavyohitajika katika mkoa mzima na kupanga mkakati wa namna vyumba hivyo vitakavyojengwa ikiwa ni pamoja na teknolojia itakayotumika katika kufyatua matofali  pamoja na gharama zake na kuwasilisha taarifa katika Ofisi yake tarehe 9 Agosti, 2016, ambapo baada ya kupata taarifa hiyo na kujiridhisha zoezi la ufyatuaji matofali kimkoa litazinduliwa rasmi Wilayani Maswa tarehe itakayopangwa na mkoa.
“ Sina uhakika sana na takwimu hizi, niwaagize tena Wakurugenzi wote mkafanye mapitio upya na uhakiki wa kina katika maeneo yenu juu ya idadi ya vyumba vya madarasa vinavyohitajika kwa Elimu ya Msingi na Sekondari. Mkae na wataalam wenu wa ujenzi mfanye tathmini ya namna mtakavyojenga kama mtatumia matofali ya kuchoma, matofali ya block au matofali yakufungamana (interlocking blocks) yanayofyatuliwa na vijana waliopewa mafunzo na Shirika la Nyumba la Taifa,ambao wako katika kila halmashauri pamoja na gharama zitakazotumika”, alisema Mtaka.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka Wakurugenzi kufanya utaratibu wa kubadilisha matumizi ya fedha haraka  pale inapobidi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu kufanikisha zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwatengenezea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia na kuwezesha madawati yaliyotengenezwa ambayo hayana mahali pa kuwekwa yasihar

nyumba zote zilizojengwa kwenye hifadhi ya reli na barabara kuu zote nchini kutembezewa nyundozz

August 04, 2016

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Reli ya Tanzani na Zambia (TAZARA), Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), zianze kubomoa nyumba zote zilizojengwa kwenye hifadhi  ya reli na barabara kuu zote nchini ili kuilinda miundombinu hiyo isiharibiwe.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mkoani Mbeya mara baada ya kukagua  Daraja la Reli ya Tazara  lililopo Mbalizi nje kidogo ya mji huo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu “Sheria iko wazi, lazima muisimamie msisubiri mpaka Waziri aseme. Mwananchi yeyote aliyeifata miundombinu ya reli lazima mmvunjie nyumba yake ili miundombinu iliyojengwa kwa kutumia fedha nyingi iweze kudumu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Meneja wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoa wa Mbeya Bw. Fuad Abdallah akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu uharibifu wa Daraja la Reli ya TAZARA eneo la Mbalizi Mkaoni Mbeya kutokana na shughuli za kibinadamu, alipotembelea daraja hilo leo.

Prof. Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za kuboresha miundombinu ya reli ya kati na reli ya Tazara ili kuhakikisha mizigo yote ya ndani na nje ya nchi inayopitia kwenye bandari ya Dar es Salaam na kupita katika barabara inapita katika reli.

“Mizigo inayopita katika reli ni asilimia 4 tu kutoka bandarini hivyo lazima tujipange kuanza kutafuta masoko na kuchukua mizigo hiyo ili kulinda miundombinu ya barabara inayoharibiwa na uzito mkubwa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa karakana ya Mbeya.

Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameuhimiza uongozi wa TAZARA kuongeza juhudi katika utoaji elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya uchimbaji mchanga, kokoto kwenye hifadhi ya miundombinu ya reli hasa kwenye mito na chini ya madaraja ili kuzuia uharibifu kuhatarisha usalama wa usafiri wa treni.

Naye Meneja wa TAZARA wa mkoa wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah amemueleza Waziri Mbarawa zoezi la kubomoa nyumba litatekelezwa kama  sheria ya reli inavyosema kwa wananchi kuacha  ya mita 30 kwa vijijini na mita 15 kwa mjini.

Ameongeza kuwa mamlaka itaendelea kutoa elimu ya utunzaji wa  miundombinu ili wawe sehemu ya utunzaji kwa kuacha kufanya shughuli zao kwenye maeneo hayo.

Katia ziara hiyo, Waziri Prof. Mbarawa amekagua pia  Karakana ya TAZARA ya Mbeya ambayo inatoa huduma ya matengenezo ya vichwa vya treni 39 aina ya Diesel Electric (DE) pekee na kubaini ukosefu wa baadhi ya mitambo, uchakavu wa mitambo iliyopo na ukosefu wa vipuri.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua mashine ya kichwa kimojawapo cha treni wakati alipokagua ukarabati wa vichwa hivyo katika karakana ya Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na mmoja wa abiria wakati alipokagua huduma za Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA), (hawapo pichani) wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati alipozungumza nao, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.

KIWANDA CHA MO ENTERPRISES CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI KUMI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

August 04, 2016

 Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (katikati)alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda  cha Mo Enterprises kilichopo kiwalani jijini  Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa kiwanda hicho ya jinsi gani kiwanda hicho kinavyotiririsha maji machafu kutoka kiwandani hapo.
EVELYN MKOKOI

AFISA HABARI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Kiwanda cha kutengeneza maji na juice cha cha MO ENTERPRISES kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi kwa kosa la kumwaga maji machafu katika makazi ya watu, bila kupata kibali cha Baraza la taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC na kibali cha Bonde la wami ruvu, kinachoruhusu kuachia maji yaliyotibiwa kwenye mazingira. Hayo yamebainika katika muendelezo wa oparesheni  ya ukaguzi wa mazingira na viwanda jijini Dar Es Salaam inayofanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina.

Kiwanda hicho kinatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni kumi kwa muda wa siku saba, pamoja na kufanya marekebisho ya miundominu kiwandani hapo na kupata kibali cha kutiririsha maji wanayoyatibu toka kiwandani hapo, kutoka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC.

Katika ziara Hiyo, NEMC pia imewatoza faini ya shilingi milioni tano kila moja wakazi tisa wa eneo la kiwalani Bam Bam kwa kile kinachodaiwa ni kutapisha maji ya vyoo katika mfereji mkubwa wa maji ya mvua maarufu kwa jina la mfereji wa Airport, Nakutakiwa kulipa faini hiyo ya jumla ya shilingi milioni arobaini na tano kwa muda wa wiki moja , kinyume na hapo watafikishwa mahakamani.

Aidha, Naibu Waziri Mpina pia alitembelea kiwanda cha Step Entertainment kinachotengengeza CD, tape na DVD na kujionea uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha maji ya chooni katika mazingira na kuwatoza faini ya shilingi milioni saba ambayo inatakiwa kulipwa ndani ya siku saba pamoja na kuwataka kuziba matoleo yote ya mifereji inayotoa maji machafu na kufanya usafi wa mazingira mara moja.

Timu hiyo ya Naibu Waziri Mpina pia ilitembelea kiwanda cha Royal na kukipa AMRI kali la kufanya kusafi wa mazingira katika mtaro wao kwa muda wa siku mbili.

MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI KWA MARA NYINGINE NCHINI MAREKANI.

August 04, 2016
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro.