SPLM YAANZA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA ARUSHA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa
Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini
Ujumbe wa
Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini yalifanya
mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana mjini Dar es Salaam jana.
Mazungumzo
haya yalilenga kuandaa utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa mjini Arusha mwezi wa januari tarehe 21 ambayo yanalenga
kuyaunganisha makundi matatu katika chama cha SPLM kurudisha Amani na kuunda
Serikali itakayowajumuisha viongozi kutoka makundi yote.
Katika
mazungumzo ya jana makundi haya yamekubaliana kuendelea na mkakati wa utekelezaji wa makubaliano ya Arusha kwa
lengo la kuandaa utaratibu wa viongozi
wa makundi yote kurudi Sudan ya Kusini mapema iwezekanavyo.
Mizengo Pinda aimiza Wabunge kushiriki mazoezi na michezo kulinda afya zao
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwapongeza wachezaji wa timu za Bunge la
Jamuhuri kwenye tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 katika
majengo ya Bunge hilo Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter
Pinda aliwapongeza wanamichezo wa Timu za Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kuliletea sifa kubwa Bunge hilo kwenye mashindano ya
michezo mbali mbali ya Kitaifa na Kimataifa.
Mh.
Pinda alitoa pongezi hizo katika Tafrija maalum ya kuukaribisha mwaka
mpya zilizofanyika katika majengo ya Bunge la Jamuhuri Mjini Dodoma
hafla iliyokwenda sambamba na kuwapongeza wanamichezo wa Bunge hilo
baada ya kushinda michezo tofauti katika mashindano ya Mabunge ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Mjini Arusha Tanzania.
Waziri
Mkuu Pinda alisema kwamba michezo inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano
ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na
sekta ya michezo.
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda
akiwa pamoja na Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda na Baadhi ya Wabunge
wakifurahia vikombe mbali mbali vilivyoibuliwa na Timu za Bunge la
Jamuhuri katika Mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aliishauri
Kamati ya Uongozi wa Michezo ya Bunge hilo kufikiria umuhimu wa
kuwashirikisha wawakilishi wa wanamichezo wa mabunge wanachama kwenye
tafrija kama hizo kwa lengo la kusherehekea nao pamoja ili kudumisha
ushirikiano pamoja na ujirani mwema.
Alieleza
kwamba michezo ina nafasi pana ya kupunguza joto la kisiasa, hitilafu
au ugomvi unaotokea baina ya nchi na nchi na kupelekea watu wa pande
zinazohitilafiana kurejea kwenye ushirikiano na mafungamano baina yao.
Mh.
Pinda alifahamisha kwamba kwa kuwa mabunge mengi yana utaratibu mzuri
wa kuandaa mashindano ni vyema kwa waheshimiwa wabunge kuzitumia fursa
kama hizo katika kushiriki kwenye mazoezi na hatimae mashindano kwa
lengo la kudumisha afya zao.
Baadhi
ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wakiwa kwenye tafrija ya
kuupokea mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika katika majengo ya Bunge Mjini
Dodoma sambamba na kuzipongeza Timu za Bunge hilo zilizoshinda kwenye
mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki.
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliwatakia mwaka
mwema wa 2015 Waheshimiwa wote wa Bunge la Jamuhuri hasa mwezi Oktoba
mwaka huu ambao kama wamefanya vyema majimboni mwao utawarejesha tena
kwenye wadhifa wao.
Alisema
kurejea kwa Wabunge hao kwa kiasi kikubwa kunaweza kuleta faraja kubwa
kwa vile tayari wameshazoeana kutokana na kushirikiana pamoja katika
vikao vya Bunge hilo kwa takriban miaka mitano.
Mapema
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Iddi Azan alisema ongezeko la michezo
mbali mbali kwenye mashindano ya Timu za Mabunge ya Afrika ya Mashariki
linatokana na azimio la Mabunge ya Jumuiya hiyo la kuzitaka Nchi
Wanachama kuongeza michezo mengine kwenye mashindano hayo.
Waziri
Mkuu akiwaongoza waheshimiwa wenzake kwenye mduara ulioporomoshwa na
bendi ya Utalii katika tafrija ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 Mjini
Dodoma.(Picha na – OMPR – ZNZ).
Mwenyekiti
Azan alisema mshindano ya Mabunge hayo yalikuwa yakishirikisha michezo
miwili tuu ile ya Kandanda na Pete ambapo kwa sasa ipo riadha, mbio za
vijiti, kuvuta kamba, kufukuza kuku ikiwemo pia ile ya watu wenye
mahitaji maalum { Walemavu }.
Mwenyekiti
huyo wa Bunge Sports Club alielezea faraja yake kutokana na ushiriki
mzuri wa wanamichezo wa Timu za Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kwenye mashindano mbali mbali ya Mabunge na kuleta ushindi
katika michezo tofauti.
Katika
mashindano hayo ya mwaka 2014 ya Timu za Mabunge ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki yaliyoshirikisha wachezaji 150 Timu ya Mpira wa Pete Wanawake
ya Bunge la Tanzania ilitokea mshindi wa kwanza, Riadha wanawake
washindi wa kwanza, riadha wanaume washindi wa Tatu, mpira wa miguu
washindi wa Pili na kuvuta kamba Timu za wanawake na wanaume Tanzania
zimeshika nafasi ya kwanza.
Penzi la Wema Sepetu na Ommy Dimpoz Lawekwa Hadharani.......Wapiga Picha wakiwa bafuni Usiku
Hatimaye
zile tetesi kwamba mwigizaji Wema Sepetu na msanii wa muziki Ommy
Dimpoz wanatoka kimapenzi zimekuwa kweli kwa zaidi ya asilimia 200....
Tetesi
hizo zimethibitishwa na picha waliyopiga jana usiku wakiwa bafuni
huku Wema akiwa amevaa taulo tu na Ommy Dimpoz akionekana kwa mbali
kama ananawa mikono.
Picha
hii iliamsha watu kibao usiku wa jana hasa wale Team Wema, kwani
comments na likes zilivyo tiririka utadhani picha imewekwa saa sita
mchana, kumbe ni usiku wa manane.
Baadhi ya picha zao
“SUMATRA TANGA WAWATANGAZIA KIAMA WAMILIKI WA MABASI MKOANI TANGA”
MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri nchi
Kavu na Majini Mkoani Tanga (Sumatra) umewapa muda wa siku mbili wamiliki wa
mabasi mkoani hapa kuhakikisha wanahamia kwenye kituo kipya cha mabasi
kilichopo kange jijini Tanga ndani ya siku mbili zijazo la sivyo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Agizo la hilo lilitolewa na
Ofisa Mfawizi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Walukani Luhamba wakati alipofanya
ziara ya kutembea kituo hicho kuangali namna ya agizo la Mkuu wa mkoa wa Tanga,
Said Magalula namna linavyokwenda.
Alisema kuwa kimsingi wamiliki hao
kuendelea kubaki kwenye stendi ya zamani ikiwemo wengine kupaki magari
pembezoni mwa ofisi zao zilizopo karibu na maeneo hayo ni kukiuka amri
iliyotolewa na mamlaka hiyo hivyo watakaobainika kufanya hivyo baada ya muda
uliotolewa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha alisema licha ya kuchukuliwa
sheria kali kwa watakaobainika kukaidi agizo hilo lakini pia watawatoza faini
ya sh.lakini mbili (200,000) pamoja na kuvutiwa leseni ili kuweza kuwa fundisho
kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Ofisa huyo alisema kuwa serikali
imetumia fedha nyingi kuhakikisha stendi hiyo inakuwa katika kiwango kizuri kwa
ajili ya kupunguza msongamano eneo la mjini kwa kuijenga lakini wao wameshindwa
kufikiria suala hilo na kuendelea kubaki mjini.
Awali akizungumza ,Mwenyekiti wa
Muungano wa Wasafirishaji wa Daladala
Jijini Tanga,Atwabi Shabani aliwataka wamiliki hao kuhakikisha
wanazingatia agizo hilo ili kuweza kuepukana na adhabu wanazoweza kukumbana
nazo.
Kwa upande wao baadhi ya madereva
wanaofanya safari zao kati ya Tanga na mikoa mengine waliotii agizo hilo
waitaka mamlaka hiyo kwa kushiriki Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama
barabarani kuhakikisha wanasimamia suala hilo ipasavyo ili kuepusha malalamiko.
Mmoja kati ya madereva hao,Omary
Chuchuli alisema kuwa utaratibu huo ni nzuro kwa sababu unaondoa manung;uniko
kwa baadhi ya wasafirishaji wengine ambao walikwisha kutii agizo la kuhamia
kwenye kituo hicho cha mabasi.
Naye Fadhili Jumanne alisema lazima
vyombo vinavyohusika na jambo hilo kuhakikisha vinashirikiana kwa pamoja ili
kuweza kuondoa changamoto hiyo iliyopo.
Subscribe to:
Posts (Atom)