MRADI WA SECAP LUSHOTO HATARINI KUTOWEKA

September 15, 2014

MRADI wa Hifadhi ya Mmomonyoko wa Udongo na Kilimo ijulikanayo kama ‘Soil Erosion Control and Agroforest Project (SECAP), unaojumuisha vijiji saba vya Mlalo na Lushoto uko kwenye hatari ya kutoweka endapo hatua za haraka kuunusuru hazitachukuliwa.
Mradi huo ulianzishwa mwaka 1980 na ulikuwa na malengo ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kuendesha kilimo cha kisasa na kupanda miti, ambako ulilenga eneo la maili 610 hadi 2300 kwa kuwashirikisha wananchi zaidi.
Imedaiwa kuwa, wafanyabiashara wanaovuna miti katika hifadhi za miti za mradi huo hutoa kiasi cha sh 500,000 hadi sh milioni 1 kwa baadhi ya viongozi, kuhakikisha wanawalinda na mbao zao kwa madai walishaweka mambo sawa kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya uvunaji Wilaya ya Lushoto.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Lushoto, Jumanne Shauri, Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo, Lucas Shendolwa na Mbunge Henry Shekifu, wameahidi kuchukua hatua za haraka kuzuia uharibifu huo wa mazingira kuendelea walipozingumza na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti.
Tanzania daima ilipotembelea vijiji hivyo, ambavyo ni Hemtoye, Msale, Kifulio, Makole, Kwekanga, Kihifu na Kigulunde, ilishuhudia wafanyabiashara zaidi 15 wakikata miti katika msitu huo.
Uchunguzi umeonyesha kuwa, wafanyabiashara hao waliomba vibali vya kukata miti aina ya ‘Kaltas’ kwa maelezo kuwa imekuwa ikitumia maji mengi ardhini, jambo ambalo limetoa upenyo kukata miti ya mivule na mingineyo na hakuna mapato yanayonufaisha vijiji husika.
Mkuu wa wilaya hiyo, Majid Mwanga, alisema kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya uvunaji wilaya, amekuwa akitoa vibali vya uvunaji miti baada ya kupata taarifa kutoka ngazi za vijiji na Idara ya maliasili na kwamba, mtu anapokiuka ni vema watendaji na wananchi wampe taarifa.
“Mimi niko hapa ofisini sijui nini kinatokea msituni huko…nawaomba wananchi wenye mapenzi mema kama nyinyi waandishi, mtupatie taarifa na kama wabovu ni maliasili, viongozi wa vijiji, kata au idara ya misitu… tutachukua hatua kama serikali,” alisema.
 Chanzo;Tanzania Daima

CHADEMA YAPATA VIONGOZI WA KAMATI YA UTENDAJI

September 15, 2014

Kutoka kushoto ni Naibu Mkuu zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma, Katikati ni Naibu katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika na Kulia ni Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.
 Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa 
Naibu Katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KIBITI

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KIBITI

September 15, 2014
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji katika Chanzo cha maji kwenye kijiji cha Muyuyu kata ya wilaya ya Rufiji wakati wa Ziara ya kiongozi huyo inayoendelea katika mkoa wa Pwani, ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani  ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongoza na Katibu wa NEC Siasa, Uenezi na Itikadi,(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-KIBITI)4 
Mbunge wa jimbo la Kibiti . Mh. Abdul Marombwa akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa watumishi wa zahanati ya kijiji cha Muyuyu wakati ziara ya  katika mkoa wa Pwani7 
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akipanda mti katika zahanati ya kijiji cha Nyamatanga wilayani Kibiti mkwani Pwani 
Jengo la zahanati ya kijiji cha Nyamatanga 16 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizumza na wananchi wa kijiji Nyamatanga kata ya Nyamatanga 19 
MsKatibu wa CCM Mkoa wa Pwani mama Joyce Masunga akizungumza na waanchinchi wa Kibiti. 26 
Mkuu wa wilaya  ya Rufiji Bw. Nurdin Babu akiteta jammbo na Mbenge wa jimbo la Kibiti Mh. Abdul Marombwa huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mwisheshe Mlao.30 
RAIS DKT. SHEIN APOKELEWA COMORO

RAIS DKT. SHEIN APOKELEWA COMORO

September 15, 2014


IMG_4092 
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN AKISALIMIAANA NA BALOZI COMORO NCHINI TANZANIA ALIPOWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA COMORO AKIWA KATIKA ZIARA YA KISERIKALI AKIWA AMEFUATANA NA MKEWE MAMA MWANAMWEMA SHEIN NA VIONGOZI MBALI MBALI [PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]
IMG_4102 
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN  AKIWA NA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA COMORO MOAMED  ALI SOILIHI WAKATI WIMBO WA TAIFA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAA TANZANIA NAWIMBO WA MUUNGANO WA COMORO UKIPIGWA [PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]

*KINANA ASONONESHWA NA MIKOROSHO YA WAKULIMA ILIVYOKAUKA KWA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI MKURANGA, AAHIDI KUWASAIDIA WAKULIMA WAFIDIWE

September 15, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akionyeshwa mikorosho iliyokauka katika mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba 14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua mikorosho iliyokauka katika mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba 14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha yao.
 Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili katika wilaya ya Rufiji, Septemba 14, 2014, wakati akiendelea na ziara yake katika mkoa wa Pwani. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ameambatana naye katika ziara hiyo.
 Kinana akimsalimia Mbunge wa rufiji alipowasilikatika wilaya hiyo
 Kinana akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurudin Babu alipowasili katika wilaya hiyo, leo Septemba 14, 2014.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurudin Babu alipowasilina Kinana katika wilaya hiyo.

WAREMBO WA SHINDANO LA MISS TANZANIA WAJIFUA GYM KUJIWEKA FITI

September 15, 2014


 Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hii wamefanya mazoezi katika chumba maalum cha mazoezi 'Gym', ungana na mpigapicha wa Father Kidevu Blog katika picha mbalimbali za warembo hao katika kambi yao.

*RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE TOKA KWA RAIS WA SUDANI YA KUSINI MHE SALVAR KIIR JIJINI DAR ES SALAAM

September 15, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, jana amepokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Salvar Kiir Mayardit wa Sudani ya Kusini ulioletwa na mjumbe malumu Jenerali James Kok Ruea, juzi Ikulu jijini Dar es salaam. 
Mjumbe huyo aliongozana pia na Mkuu wa Kituo cha Martti Ahtisari (Martti Ahtisari Centre) kwa nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, Bw. Itonde Kakoma (pichani kushoto)

MATUKIO KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

September 15, 2014


 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba  wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wakielekea kuhudhuria  kikao cha arobaini cha Bunge hilo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba  Ally Kessy (kulia) na Mohammed Raza (kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha arobaini cha Bunge hilo. Picha na MAELEZO_DODOMA

*SIMBA CHAWENE AWATAKA WATANZANIA KUACHWA KUFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA MCHAKATO WA KATIBA

September 15, 2014

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Simba Chawene akichangia mada bungeni mjini Dodoma. Picha na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
*************************************
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. George Simba Chawene amesikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya Wajumbe walioko nje ya bunge hilo kuhusiana na uhalali wa bunge hilo lililoko Kisheria.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo huku akisisitiza kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa na watu hao wanapaswa kuangaliwa kuhusu uzalendo wao.
Mhe. Chawene ameeleza kuwa inasikitisha zaidi hasa pale shutuma zinapoelekezwa kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta, kuwa bunge hilo sasa linaonekana ni mali ya Mwenyekiti wa bunge hilo wakati si kweli.
“Gazeti linachukua kurasa tatu hadi nne kuzungumzia habari Sitta king’ang’anizi, hivi hili bunge lipo kama liliitishwa na Sitta ama na Rais wa nchi?, hili bunge liko kisheria”, alisema Mhe. Chawene. 
Aliongeza kuwa kwa niaba ya Watanzania wanafanya kazi ya bunge hilo kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza kuwa wajumbe waliotoka nje ya bunge hilo wamevunja sheria na kwamba hawawezi kutafuta uhalali nje ya sheria.
“Wanamlazimisha Rais avunje bunge hili, Rais wa kufuata utawala bora anavunja kwa mamlaka yapi? Mamlaka ya Rais yako kwa mujibu wa sheria”, alisema Mhe. Chawene.
Aidha, ameeleza kuwa Sheria inayoendesha mchakato wa Katiba ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imetungwa kutoka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye hatua tatu zikiwemo hatua ya kukusanya maoni ambayo Tume ya Warioba ilifanya kazi hiyo na kumaliza, hatua ya Pili ni bunge hilo kujadili kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa uwakilishi uliopo ndani ya bunge hilo na hatua ya tatu ni wananchi kwenda kutunga Katiba.
“Sisi hapa tunatoa Katiba inayopendekezwa, inayofuata ni Watanzania kwenda kutunga Katiba kwa kutunga kwa kupiga kura ya kusema ndiyo au hapana yale tuliyoyajadili na kuletwa na Tume”, alisisitiza Mhe. Chawene.
Aidha, amewataka watanzania kuwaona watu hao kuwa ni watu wabaya na wasio na nia nzuri na nchi na kuepuka kuingia barabarani kufanya maandamano ya kuipinga Katiba hiyo.

*SERIKALI YAENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI KWA AJILI YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

September 15, 2014

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bw. Marcel Katemba akiongea na waandishi wa habari( Hawapo pichani)kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuyajengea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo katika  jamii, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro.PICHA NA GEORGINA MISAMA
***********************************
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Serikali kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam.
Mercel alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2005.
“Sera hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na ushirikano” Alisema Marcel.
Marcel aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea kusimamia sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta hiyo.
Aidha Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za maadili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala, kutandaa na kuboresha huduma zinazotolewa na mashirika hayo.
Akifafanua zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s umeimarika kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo yakiserikali.
Pia Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
Juhudi za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa wananchi kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya wananchi 35,000 ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679 kote nchini.

WATANO MGAMBO KUIKOSA MECHI YA LIGI KUU DHIDI YA KAGERA SUGAR.

September 15, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
WACHEZAJI watano wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga wanatarajiwa kuikosa mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya timu hiyo na Kagera Sugar itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani hapa.

Mchezo huo unatarajiwa kucheza Septemba 20 ikiwa ni ufunguzi wa pazia la michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 14 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari shime alisema kuwa wachezaji hao wanakosa mechi hiyo kutokana na kuwepo kwenye timu za majeshi ambao ni Hassani Kibakuli, Salum Chambo, Full Maganga ambao huenda wasicheze mchezo huo wa ufunguzi wa ligi hiyo.

Alisema wachezaji wengine wawili wakiwemo beki wao wa kati Antony Chacha na Chande Magoja wapo kwenye kozi ya kijeshi hivyo wakimaliza wataungana na timu hiyo kwenye mechi zao za ligi kuu soka Tanzania bara.

Akizungumzia namna walivyojipanga kukabiliana na upungufu huo,Shime alisema kuwa wachezaji waliosalia kwenye kikosi hicho wana uwezo mkubwa katika nafasi hizo hivyo wana matumaini makubwa kucheza kwa mafanikio msimu ujao.

Alisema kuwa timu hiyo inaendelea vema na maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ambapo Ijumaa iliyopita walicheza na JKT Oljoro ya Arusha kwenye uwanja wa Sheirh Abeid Mkoani Arusha na kutoka suluhu pacha na Jumamosi walicheza na Panoni FC ya Kilimanjaro na kutoka Sare
ya 1-1.

Aidha alitoa wito kwa wadau wa soka mkoa wa Tanga kuzisapoti timu zao zilizopo mkoani hapa lengo likiwa kuhakikisha zinabaki kwenye michuano hiyo ili kuweza kukuza kiwango cha soka kwa kuzishabiki.

KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI, OKWI MWENDO MDUNDO, LOGA AIBUA JAMBO MSIMBAZI!

September 15, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.

Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za ligi hizo zinavyoelekeza.

Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.

Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa kutofanyiwa uhamisho.

Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.

Kamati vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14 kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee tena mbele ya Kamati.


Logarusic aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.

FREEMAN AIKAEL MBOWE ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI CHADEMA TAIFA

September 15, 2014
Hatimaye Mhe Freeman Aikael Mbowe Amechaguliwa Tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kupata kura 789 sawa na asilimia 97.3 ya kura zote. Aliyeshinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara ni Profesa Abdallah Safari kwa kupata kura 775 sawa a asillimia 95 na nafasi ya Makamu mwenyekiti Zanzibar ameshinda Mh Saidi Issa Mohamedi kwa kupata kura 645 sawa na asilimia 79.
MATOKEO YA UCHAGUZI