MISS TANGA KUPATIKANA JUNI 21,2014 JIJINI TANGA,MSHINDI KUONDOKA NA GARI LENYE THAMANI YA MILIONI 10

May 22, 2014


 Bi Regina Gwae ( wapili kushoto), Akiongea na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely jijini Dar es Salaam kuhusu shindano la miss Tanga linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge hotel (watatu kulia),Meneja Mauzo Nice and lovely Bw.Brian Kelly.
 waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Bi Regina Gwae (kushoto),akiwaonyesha waandishi wa habari gari lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely  litakalo shindaniwa katika shindano hilo (kulia), meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw.Brian Kelly.
========  ====  ======
Wito umetolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano kubwa na la aina yake la kuwania taji la ulimbwende linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge hotel.

Akiongea na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely Bi Rejina Gwae amesema kuwa wanajivunia kupata nafasi ya kuwa waandaji wa shindano hilo na kutoa wito kwa warembo wote wenye nia ya kushiriki kujitokeza kwa wingi.

Kuhusu zawadi kwa mshindi Bi Rejina amesema kuwa mshindi ataondoka na gari lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely akasema kuwa pia kuna zawadi nyingine za pesa taslimu toka kwa washindi wengine ambazo wanatarajia kuzitangaza baadae.

Kwa upande wake meneja mauzo wa Loreal  wamilikiwa wa bidhaa za Nice and lovely Briyan Kelly alianza kwa kuishukuru kampuni ya Mac D promotion kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wa nafasi hiyo na kuahidi kuitendea haki nafasi hiyo.

Akamalizia kwa kutoa wito kwa wote wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana Mkonge hotel, D,boutique tanga mjini,Breez fm,Tanga beach resort, Five brothers, Mwambao fm, Sophia records, Danny fashion barabara ya 13, ofisi za the guardian tanga barabara ya 15 na  Yolanda salon mtaa wa Eckenford na Nyumbani hotel.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MIKUTANO YA MH.WAZIRI WA FEDHA AMBAYE ANAHUDHURIA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFDB) UNAOFANYIKA KIGALI -RWANDA

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MIKUTANO YA MH.WAZIRI WA FEDHA AMBAYE ANAHUDHURIA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFDB) UNAOFANYIKA KIGALI -RWANDA

May 22, 2014

PIC 1 
Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa katika majadiliano na viongozi wa Benki ya HSBC kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ‘Terminal III’. Majadiliano hayo yalifanyika katika Hotel ya Mills Colonie Mjini Kigali Rwanda.
PIC 2  
Mh.Saada Mkuya Salum,Waziri wa Fedha akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya HSBC baada ya majadiliano yaliyofanyika katika Hotel ya Mills Colonie Kigali Rwanda.
PIC 3 
Waziri wa Fedha Mh.Saada M.Salum akimsikiliza kwa makini Bi.Erika Rubin mratibu wa mfuko wa Mkoba Fund wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Hotel ya Serena Mjini Kigali Rwanda. Kulia kwa Mh.Waziri ni Nd.Jovin Rugemarila Afisa anayeshughulikia masuala ya ADB na mbele yake ni Kamishina msaidizi wa Fedha za nje –Wizara ya Fedha Nd.Jarome Bureta.
PIC 4 
Mh.Saada Salum Mkuya akiwa kwenye mazungumzo ya faragha na mratibu wa Mkoba Fund Bi.Erika Rubin mara baada ya mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Muhabura Mjini Kigali Rwanda.
PIC 5 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedhda Dkt.Silvacius Likwilile akieleza kwa muhtasari yale yaliyojadiliwa katika mikutano ya Benki ya maendeleo ya Afrika inayoendelea Nchini Rwanda. Anayemhoji Katibu Mkuu ni mtangazaji wa TBC Nd. Stanley Ganzel.
New American Ambassador to Tanzania Mark Childress Presents his Credentials

New American Ambassador to Tanzania Mark Childress Presents his Credentials

May 22, 2014


D92A4199 
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete this morning received credentials from new American ambassador to Tanzania Mark Childress during a brief official ceremony held at Dar es Salaam State House in the presence of senior State House and Foreign Affairs officials.
Prior to his appointment Mark Childress held various posts in the US administration including Assistant to the President and Deputy Chief of Staff for Planning at the White House. From 2011 to 2012, he served as Senior Counselor for Access to Justice at the Department of justice and from 2010 to 2011 he was Principal Deputy General Counsel at the Department of Health and Human Services among others.
His International experience includes two years in Nigeria working on agricultural development issues on a Rotary scholarship and as an attorney for aboriginal rights issues with the Cape York Development Corporation in Cairns, Australia from 2005-2006.
Ambassador Mark received a B.A From yale University and a J.D. from the University of Carolina Law School.
In the Picture President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete receives credentials from new American ambassador to Tanzania Mark Childress(photos by Freddy Maro). 

MKUTANO WA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA NYADA ZA JUU KUSINI ULIOANDALIWA NA TFDA

May 22, 2014

Mkurugenzi  wa TFDA akitoa  maelezo ya utangulizi  kuhusu  warsha  hiyo leo katika  ukumbi wa RMO mkoani Mbeya

Utambulisho  wa  washiriki  ukifanyika
Mgeni  rasmi  na  wawakilishi wa TFDA wakiingia  ukumbini
Wanahabari  wakiwa katika warsha  hiyo ya  siku  moja leo
Warsha ya  wanahabari na  wahariri mikoa ya nyanda za juu kusini
Warsha  ikiendelea  katika  ukumbi wa RMO Mbeya Picha na www.mwadhishiwetu.blogspot.com

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusiana Na Ugonjwa Wa Dengue Katika Mkoa Wa Tanga

May 22, 2014
 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akitoa  taarifa  kwa Waandishi wa habari  ( Hawapo pichani ) wakati wa Mkutano na vyombo vya habari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga kuhusiana na ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Tanga .Amewataka wakazi wa Tanga na wananchi kwa ujumla  kuondoa hofu ya kuwepo kwa ugonjwa huo katika Mkoa wa Tanga  kwa sababu hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuhusishwa na ugonjwa huo. Aidha Dr Asha anawasisitiza  wakazi wa Tanga kuendelea kufanya usafi katika  mazingira yote kwani ugonjwa wa Dengue huambukizwa na Mbu anaeitwa Aedes ambaye mara nyingi hupatikana  maeneo yaliyotuama maji masafi mfano kwenye ndoo za maji, vifuu, matairi ya gari n.k. Kushoto ni Afisa Habari wa Mkoa wa Tanga  Bi. Monica Laurent
 
 
Afisa Habari Mkoa wa Tanga Bi Monica Laurent akijibu moja ya maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani). Wakazi wa Tanga waelewe kuwa  tayari Mkoa wa Tanga umepokea  vipimo vya Ugonjwa wa Dengue  na kwa sasa vinapatikana katika hospitali ya Rufaa Bombo na kuna uwezekana wa kuvisambaza katika Wilaya za Mkoa wa Tanga. Ni jukumu la kila mmoja kuwahi katika vituo vya afya mara ahisipo dalili za ugonjwa wa Dengue


Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa mkutano