KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2023 APANDA MITI BWAWA LA MAJI MABAYANI

June 13, 2023

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Ndugu Abdallah Shaibu Kaim akipanda mti katika Bwawa la kuhifadhi Maji Mabayani lililopo eneo la Pande wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkoani Tanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Ndugu Abdallah Shaibu Kaim akipanda mti katika Bwawa la kuhifadhi Maji Mabayani lililopo eneo la Pande wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkoani Tanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Ndugu Abdallah Shaibu Kaim akipanda mti katika Bwawa la kuhifadhi Maji Mabayani lililopo eneo la Pande wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkoani Tanga.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Ndugu Abdallah Shaibu Kaim amepanda mti katika Bwawa la kuhifadhi Maji Mabayani lililopo eneo la Pande wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkoani Tanga.

Ambapo sambamba na ukaguzi na uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya kimkakati, ziara hiyo imejikita pia katika ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya utunzaji mazingira, hususani vyanzo vya maji.


Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge Kitaifa wakati wa ziara hiyo ameipongeza TANGA UWASA kwa jitihada za utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira wakati akipokea taarifa ya shughuli za uhifadhi wa vyanzo vya maji katika ziara yake eneo la Mabayani.


"Nawapongeza TANGA UWASA kwa kazi nzuri na jitihada za uhifadhi wa vyanzo vya maji na tuendelee kuwahamisha wananchi kulinda na kutunza Mazingira", ameeleza Ndugu Kaim.


Mkoa wa Tanga umeupokea Mwenge wa Uhuru 2023 tarehe 09.06.2023 kutokea Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo kauli mbiu kwa Mwaka huu ni: " TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA".

TASAC YAKUTANA NA TAASISI MBALIMBALI WANAZOSHIRIKIANA NAZO KUFANYA KAZI ZA USAFIRI WA MAJINI

June 13, 2023


Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua akizungumza leo wakati wa kikao cha wadau wa taasisi mbalimbali wanazoshirikiana nao kufanya kazi za usafiri majini ili kujenga mahusiano na kukumbushana baadhi ya wajibu wao.


Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua akizungumza leo wakati wa kikao cha wadau wa taasisi mbalimbali wanazoshirikiana nao kufanya kazi za usafiri majini ili kujenga mahusiano na kukumbushana baadhi ya wajibu wao.


Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua akizungumza leo wakati wa kikao cha wadau wa taasisi mbalimbali wanazoshirikiana nao kufanya kazi za usafiri majini ili kujenga mahusiano na kukumbushana baadhi ya wajibu wao.
mmoja wa wadau hao akiuliza swali katika kikao hicho
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho


Na Oscar Assenga,Tanga

SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) wamekutana na wadau wa taasisi mbalimbali wanazo shirikiana nao kufanya kazi za usafiri majini ili kujenga mahusiano na kukumbushana baadhi ya wajibu wao.

Hayo yalibainishwa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua wakati wa kikao hicho cha pamoja ambapo alisema kwamba wajibu wao ambao unawataka kuyatimiza majukumu yao ya kisheria.

Kapteb Shalua ambaye pia ni Afisa Mkaguzi wa vyombo vya majini Mkoani Tanga wajibu huo unawataka kuhakikisha usafiri wa maji unakuwa ni salama pamoja na uwepo wa utunzaji wa mazingira 

“Kwa hiyo tulikutana na taasisi mbalimbali ikiwemo TPA,Marine Park ambao ni wabia wenzetu katika utunzaji wa mazingira ya bahari ,Afya,Maafisa Uvuvi kwa ajili ya kujadiliana na kusikiliza maoni kutoka kwao namna ya kuweza kuboresha mashirikiano yao ili kila taasisi waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa”Alisema

Hata hivyo alisema malengo hayo yatasaidia kuhakikisha usafiri wa majini au shughuli za majini zinatendeka kwa hali ya usalama na amani lakini pia pia kuwepo na utekelezaji wa sheria.

RAIS DKT. SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA TFF

June 13, 2023


Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (kulia) akipokea Tuzo ya Heshima kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF)  Ndg. Wallace Karia (kushoto) ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza Soka nchini.Tuzo hiyo ameipokea katika Usiku wa Tuzo Juni 12, 2023 Jijini Tanga.

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Tanga

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mchango wake wa kupenda, kuthammini na kuendeleza michezo nchini.

 

Tuzo hiyo imetolewa kwa Rais Dkt. Samia ikiwa ni mwendelezo wake kwenye sekta ya michezo kukutana na kuwapongeza wanamichezo wanapofanya vizuri kwenye michezo tangu aingie madarakani pamoja na kuunga mkono na kutia hamasa vilabu vya Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutunuku kila goli lililofungwa katika mashindano ya Klabu Bingwa na Shirikisho la Mpira Afrika kwa kila goli lililofungwa maarufu kama "Goli la Mama".

 

Akipokea tuzo hiyo Juni 12, 2023 jijini Tanga kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgeni Rasmi katika usiku wa Tuzo za Shirikisho la Mpira nchini (TFF) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameahidi kuifikisha tuzo hiyo na kusema imetolewa kwa Rais wa nchi akiwa ni shabiki namba moja na mpenda michezo nchini.

 

Naibu Waziri Mwinjuma ameongeza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri kuendeleza miundombinu ya michezo nchini kwa kukarabati viwanja saba vya Mkwakwani Tanga, CCM Kirumba Mwanza, Sokoine Mbeya, Jamhuri Dodoma, Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru vya jijini Dar es salaam na Uwanja wa Amani Zanzibar pamoja na kujenga viwanja vipya viwili nchini katika mikoa ya Arusha na Dodoma kabla ya mwaka 2027 ambapo Tanzania, Kenya na Uganda zimeomba kuwa wenyeji wa Mashindano ya Afrika (AFCON).

 

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Bw. Wales Karia amesema  wanautaratibu wa kuwatambua na kuwatuza watu mbalimbali waliotoa mchango wao katika kukuza na kuendeleza soka nchini kila wanapofunga msimu wa ligi zote za mpira wa miguu chini.

 

Hafla hiyo ya utoaji tuzo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu pamoja na Viongozi mbalimbali, wachezaji na wageni waalikwa walioshamirisha hafla hiyo.