MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MAMA SIZAKELE ZUMA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM

MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MAMA SIZAKELE ZUMA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM

May 11, 2017
unnamed
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  wakielekea kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
A
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
A 1
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, wakipata picha ya kumbukumbu na wasaidizi wao  kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
A 2
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimsindikiza Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, aliyemtembelea kwenye  ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
A 3
 Kikundi cha matarumbeta cha Usambara kikiwakaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) na  Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele, Zuma alipomkaribisha mgeni wake huyo kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
PICHA NA IKULU

HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KATIKA KUZIPA HADHI HOTELI

May 11, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini hoteli fulani inatajwa kuwa ni ya nyota tatu, nne au tano? Najua itakuwa ni vigumu kuelewa kama haupo katika tasnia ya masuala ya hoteli au utalii mpaka upatiwe ufafanuzi wa kutosha.
Government Launches 'Nipo Tayari' Campaign

Government Launches 'Nipo Tayari' Campaign

May 11, 2017
Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Honorable Ummy Mwalimu (MP) speaks during the launches of sanitation campaign in Dodoma.[/caption]   TANZANIA needs to end open defecation and have all people using improved toilets, to reflect the status of a middle-income country. The Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Honorable Ummy Mwalimu (MP) and stakeholders conveyed this in Dodoma during a Call to Action event. The minister called for the national sanitation campaign, “To carry out a much bigger campaign far beyond the dimensions of the Mtu ni Afya.” The National Sanitation Campaign launched in 2012 is ramping up its efforts to accelerate household sanitation improvements. The use of poor quality toilets and the practice of open defecation is a leading cause of illness and death from cholera, diarrheal diseases, and costs the country 1% of its GDP each year. Poor sanitation is also a major contributor to stunted growth of about 2.7 million children in Tanzania. Children who are more likely than their peers to struggle in school and earn less as adults. The campaign is setting out new activities ranging from promoting improved toilets, hand washing with soap, water treatment at point of use, sanitation in schools and health care facilities to the provision of adequate toilets on highways and bus stops. “I would request each one of you to join the government efforts of ensuring access to improved sanitation and hygiene,” said the Minister,to the assembled government staff, development partners, the private sector and public. Over the past 25 years, open defecation has remained a problem. For instance, in 1990 the report shows that 10% of rural population had no toilets, 13% in 2000, 16% in 2011 and 13% in 2016. And over 55% of Tanzanians use unimproved toilets that are as damaging to health and the economy. A World Bank assessment indicates that Tanzania is losing 1 percent of its GDP due to poor sanitation and hygiene. This is too high for a country like Tanzania that is aspiring for a mid-income economy by 2025. Moreover, UNICEF estimates a loss of 1.7 million children each year due globally to diarrhea and pneumonia which can both be prevented by a simple act of hand washing with soap and use of improved toilets. As a step toward addressing the financing gap, the government has started allocating local funds into sanitation as exemplified by the 2017/18 budget for Ministry responsible for Regional Administration and Local governments. To facilitate the country achieve the access to improved Sanitation and Hygiene, the minister has called upon all the stakeholders to join the government efforts of ensuring access to improved sanitation becomes a reality.

SENSA YA WAFANYAKAZI WA NYUMBANI KUFANYIKA MKOANI MWANZA

May 11, 2017
Jackline Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la kutetea Haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini, WOTESAWA, akizungumza na Lake Fm, baada ya semina kwa viongozi wa serikali za Kata/Mitaa pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ili kuwajengea uwezo wa kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani katika maeneo yao.
Na Binagi Media Group
Semina kwa viongozi wa serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ikiendelea Jijini Mwanza
Semina hiyo imeandaliwa na shirika la WOTESAWA kwa siku tatu tangu Mei 09 hadi leo Mei 11,2017
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza mwanahabari Nashon Kenedy, wakati akichangia mada kwenye semina hiyo
Wadau wa Maendeleo mkoani Mwanza wameidhinisha mikakati mbalimbali ikiwemo kufanya sensa ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na utungwaji wa sheria ndogo ndogo za kuwalinda watoto, lengo likiwa ni kusaidia mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto hao.

Wamefikia makubaliano hayo leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa serikali za mitaa kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela yaliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani la WOTESAWA lililopo Jijini Mwanza.

Akizungumzia mikakati hiyo, Jackline Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la WOTESAWA amebainisha kwamba, mikakati hiyo itasaidia kuwalinda watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwanusuru na utumikishwaji wa kazi nzito huku wakilipwa ujira mdogo.

Wadau walioafiki mikakati hiyo ni Madiwani, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii ambapo wameongeza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuielimisha jamii kupitia mikutano ya hadhara ili kuepukana na ukatili kwa watoto hususani wafanyakazi wa nyumbani.

Baadhi ya watoto wamekuwa wakikosa fursa ya kusoma kutokana na kuajiriwa katika kazi za nyumbani kinyume na sheria huku wakilipwa ujira mdogo tofauti na waraka wamishahara wa mwaka 2013 unavyoelekeza.

Waraka huo unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni raia wa kigeni. Tazama picha zaidi hapa

Chalinze na kompyuta za Bayport

May 11, 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri mpya ya Chalinze mkoani Pwani, Edes Lukoa mwenye koti jeusi, akipokea msaada wa kompyuta mbili kutoka kwa Mratibu wa Masoko wa Bayport Fiancial Services, Mercy Mgongolwa. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Kanda ya Kati Christopher Kihwele kushoto kwa Mercy na Meneja wa wa Bayport Bagamoyo Francis Sumila na Katibu wa Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete Idd Swala kulia kwa Mkurugenzi wa Chalinze.

Bayport yaikomboa Halmshauri mpya ya Chalinze kwa kuwapatia kompyuta

Na Mwandishi Wetu, Chalinze
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana iliikomboa Halmashauri mpya ya wilaya Chalinze kwa kuipatia kompyuta mbili kwa ajili ya kupunguza changamoto za upungufu wa vifaa vya kiutendaji, ikiwa ni miezi michache tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo mpya.

Kompyuta hizo zilipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa katika ofisi yake, ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwatumikia wana Chalinze na Watanzania kwa ujumla kwa kutumia kompyuta hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akipokea kompyuta mbili kutoka kwa Taasisi ya Bayport Financial Services ikiwakilishwa na Mratibu wa Masoko Mercy Mgongolwa.
Akizungumza jana katika makabidhiano hayo wilayani Chalinze, Mratibu wa Masoko wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema kwamba lengo la kuipatia kompyuta hizo linatokana na dhamira ya kuona wilaya hiyo inasonga mbele kimaendeleo.

Alisema kugawa kompyuta hizo ni mwendelezo wa nia yao baada ya kuzindua ugawaji wa kompyuta hizo 205 zilizoanza kusambazwa katika ofisi mbalimbali za serikali baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki.

“Tumefika katika Halmashauri hii kutoa kompyuta kwa Halmashauri ya Chalinze huku ikiwa tumeshafikisha msaada kama huu katika maeneo mbalimbali ya Tanzania kama vile Morogoro, Mwanza, Mara, Mbeya, Kilimanjaro na kwingineko.

"Tunaamini kwamba msaada huu utakuwa na dira nzuri kwa watumishi wa umma wa Halmashauri hii ambayo ni mpya, hivyo ni madhumuni yetu kuona wanapata vitendea kazi vizuri ili wafanikiwe kuwatumikia Watanzania,” Alisema Mercy.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa aliwashukuru Bayport kwa msaada wa kompyuta kwa ajili ya ofisi yao ambayo ni mpya baada ya kugawanywa kutoka katika Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo.

“Tumepokea kwa furaha msaada wa kompyuta hizi na tunaamini kwa dhati kabisa itapunguza au kurahisisha utendaji kazi katika ofisi zetu za Halmashauri ya Chalinze kama wenyewe mlivyokusudia kwa kuanzisha utaratibu wa msaada huu.

“Tunaahidi kwamba tutazitumia vizuri kompyuta hizi pamoja na kufikisha huduma iliyokusudiwa kwa watu wote, ukizingatia kwamba kukua kwa sayansi na teknolojia kunalazimisha ofisi kutumia kompyuta ili kurahisisha utendaji kazi,” Alisema Lukoa.

Zoezi la kutoa msaada wa kompyuta katika ofisi mbalimbali za serikali lilianza mwishoni mwa mwaka jana, ambapo katika maeneo yote ambayo wamepeleka vifaa hivyo wamepokea vizuri na kuahidi utendaji kazi mzuri kwa utumia rasilimali hizo, huku Bayport ikiendelea kusambaza vifaa hivyo katika maeneo mengine yaliyopangwa na serikali kwa kupitia Wizara ya Utumishi.
RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA AWASILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFIULI

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA AWASILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFIULI

May 11, 2017
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa Nyimbo za Mataifa mawili (Tanzania & Afrika Kusini)  zikipigwa katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
A
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipita kukagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza ndani ya viwanja vya Ikulu kwa Heshima ya ugeni huo wa Rais wa Afrika Kusini.
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Kimaendeleo yahusuyo mataifa hayo mawili ya Tanzania na Afrika Kusini.
A 3
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
A
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 1
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 2
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 3
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli
A 4
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kufika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 5
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeambatana na msaidizi wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 6
Vikundi vya Matarumbeta vikitoa burudani wakati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

DC KASESELA AFUNGUA WARSHA YA KUJENGA UELEWA KUHUSU PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ADSP 2)

May 11, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Na Mathias Canal, Dar es salaam akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Na Mathias Canal, Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.

Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.

Dc Kasesela amesema kuwa Utekelezaji wa ASDP 2 utazingatia malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2021), Mkakati wa Taifa wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Dira ya maendeleo ya Tanzania (2025).

Alisema kuwa Programu hiyo imezingatia vipaombele vya vizara ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi na imelenga kutatua changamoto na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo, Kuongeza pato la Taifa, Kuboresha kipato cha wakulima wadogo na usalama wa chakula na lishe nchini.

Sambamba na hayo pia alisema kuwa wadau wote wa ASDP 2 wanapaswa kusimamia na kutekeleza kwa weledi maeneo makuu manne ya utekelezaji wa Programu hiyo ambayo ni Usimamizi wa Matumizi ya maji na ardhi (Sustainable Water and Land use Management),, Kuongeza tija na faida katika kilimo, mifugo na uvuvi (Enhanced Agricultural productivity and profitability).

Maeneo mengine ya kusimamiwa vyema na wadau ni Biashara na Uongezaji wa thamani kwenye mazao (Commercialization and Value Addition, na Viwezeshi vya sekta, Uratibu, Ufuatiliaji, na Tathmini ya sekta (Sector Enablers, Coordination and Monitoring and Evaluation).