MWALIMU MKUU WA SHULE HIYO AMATE RAPHAEL KIMARIO AKIZUNGUMZA KWENYE MAHAFALI HAYO KABLA YA KUMKARIBDISHA MGENI RAMSI |
NEC:VIFAA VILIVYOKAMATWA SIO BVR, WALA HAVIHUSIANI VYOVYOTE NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Siku
moja baada ya kunaswa mashine zilizosadikiwa kuwa ni za uandikishaji
wapiga kura kwa njia ya kielektroniki (BVR), zilizokuwa zikiandikisha
wafanyakazi wa Kiwanda cha MM Steel jijini Dar es Salaam, Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) imeibuka na kueleza kuwa mashine hizo ni 'feki' na
wala hazihusiani kwa namna yoyote na vifaa vyao.
Jaji
mstaafu Damian Lubuva akizungumza na viongozi wa Chadema. Kutoka kulia
ni Wakili wa chama hicho, John Malya na Reginald Munisi.
Mkurugenzi
wa NEC, Ramadhani Kailima, ndiye aliyetoa ufafanuzi huo wakati
akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na mashine hizo ambazo zilikamatwa
juzi wakati zikiendelea kutumiwa kwa shughuli ya uandikishaji wa
wafanyakazi wa kiwanda hicho kilichopo katika eneo la Mikocheni.
Wakati
Polisi wakizikamata jana kwa ushirikiano na maofisa kadhaa wa NEC,
tayari mashine hizo zinavyofanana na BVR zilishaandikisha wafanyakazi
zaidi ya 100 wa Kiwanda cha MM Steel.
Akielezea
zaidi kuhusiana na tukio hilo, Kailima alisema kuwa, mara baada ya
kupata taarifa za kuwapo kwa mashine hizo, walienda kuzikagua na kubaini
kuwa hazina uhusiano na zile za Biometric Voter Registation (BVR),
zilizotumiwa na wao (NEC) kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
“Hakuna
ukweli wowote kuwa zile ni mashine za BVR na tumebaini ni feki, tena ni
sawa na zile zinazotumika kwenye ofisi mbalimbali kuandikisha
wafanyakazi wake... hawa waliosema ni mashine za kuandikishia wapiga
kura hawako sahihi... si kweli,” alisema Kailima.
Alisema
endapo watu wataendelea kuwa na shaka juu ya namna NEC inavyofanya kazi
kwa sababu tu ya kuona mashine kama hizo, basi wanaweza pia kukamata
mashine za ofisi nyingi zikiwamo za kwenye viwanja vya ndege, hospitali
na hata manispaa kama ya Kinondoni ambayo hutumia mashine kama hizo kwa
shughuli zake mbalimbali.
“Mashine
tulizozikuta kwenye hiyo ofisi jana (juzi) ni computer mpakato (laptop)
na mashine za kuchukua alama za vidole. Hata wale wafanyakazi
tulipowahoji walibainisha kuwa wanazitumia kuorodhesha wafanyakazi wao
kwa ajili ya usalama wa ofisi... na tena zipo ofisi nyingi zinatumia
mashine hizo,” alisema Kailima.
Kailima
alitoa tahadhari kwa wataalamu wanaovishauri vyama vya siasa kuwa
makini na kuacha kupotosha kwa kuwaleza mambo yasiyo na ukweli, hasa
kuhusiana na NEC kwani wao wanafanya kazi zao kisayansi zaidi na hakuna
fursa ya kuwapo kwa ubabaishaji wa aina yoyote.
Aliongeza
kuwa hawafanyi kazi zao kwa misikumo ya kisiasa, bali huzingatia
utaalamu na hivyo wanaotumiwa kwa ushauri na vyama waache kuwadanganya
wanasiasa.
“Hawa wanasiasa wanadanganywa na watu wanaojiita wataalamu... mashine hizi (zilizokamatwa) hazihusiani na BVR," alisisitiza.
CHADEMA WAHUSISHWA UCHUNGUZI
Akieleza
zaidi juu ya hatua walizochukua baada ya tukio la juzi, Kailima alisema
kuwa (jana) walifanya uchunguzi wa mashine hizo kwa kushirikiana na
wawakilishi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao
ndiyo walitoa malalamiko kwao kuhusiana na madai ya kuwapo kwa mashine
kama BVR zinazotumiwa kuandikisha watu.
“Wataalamu
wao (Chadema) walikuja na tukathibitisha (wote) zile ni feki na
hazihusiani kabisa na mashine zetu za BVR,” alisema Kailima.
Kwa
upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) John Mnyika, aliitaka NEC ivikabidhi vyama vya siasa nakala za
daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepukana na njama za wizi wa kura
alizodai zinaweza kufanywa na chama tawala -- Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Akizungumia
tukio la juzi kuhusu kukamatwa kwa vifaa vinavyofanana na mashine za
BVR, Mnyika alisema suala hilo walilikabidhi kwa maofisa wa NEC na Jeshi
la Polisi ambao wanalichunguza kwa kushirikiana na maofisa wa Chadema
ili kubaini ukweli.
Kadhalika,
Mnyika aliitaka NEC kushughulikia suala hilo haraka na kutishia kuwa
wasipotoa majibu ya kina ndani ya siku tatu, atashauri wanachama wenzake
kuishinikiza ifanye hivyo ili kuondoa shaka iliyopo.
Hata
hivyo, Mnyika aliyasema hayo kabla ya kutolewa kwa maelezo ya Kailima
kuhusiana na uchunguzi walioufanya kwa mashine hizo zilizokamatwa
Mikocheni.
Juzi,
Chadema walipata taarifa kutoka vyanzo vyao vyao kuwa kuna mashine
zinazofanana na BVR zinaandikisha watu na hivyo wakashirikiana na Polisi
na NEC kuvikamata kabla ya kwenda kuvichunguza. Meneja Mawasiliano wa
MM Steel, Aboubakar Mlawa, alieleza kuwa kampuni yao imeamua kuandikisha
wafanyakazi wao kwa nia ya kudhibiti usalama vitendo vya wizi, na
kwamba tayari walishaandikisha wafanyakazi zaidi ya 100 kati ya 900
waliokuwa wakitarajiwa kutoka kwenye viwanda vyao saba.
BENKI YA CRDB YASAIDIA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA GEITA
Benki ya CRDB kupitia
tawi lake la mjini Geita imechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika Shule za Msingi Mwatulole na Shule ya Msingi Geita ambayo baadhi
ya majengo yalibomolewa na mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali
mwanzoni mwa mwake huu mkoani Geita.
Sambamba
na kusaidia ujenzi na ukarabati wa madarasa Benki ya crdb ilichangia
maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika mjini
Geita kwa sababu benki hiyo inawajali wateja wake. Maadhimisho ya wiki
Huduma kwa Wateja ilianza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 10 ambapo Benki
ya CRDB ilishiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Benki ya CRDB imewashuru wateja wake kupitia tawi la Geita.
Meneja wa CRDB Geita, Amini
Mwakang'ata (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja Mkuu
wa Shule ya Msingi Mwatulole iliyopo Mkoani Geita, Catherine Mugusi kwa
ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto) akipokea
maoni kutoka kwa mteja wa wa Benki ya CRDB tawi la Geita wakati wa
Maadhiisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mjini Geita.
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akizungumza na
wateja wa benki hiyo (hayupo pichani) katika maadhimisho ya Wiki ya
Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika tawi la Geita.
KINANA APIGA KAZI YA NGUVU MKOANI KIGOMA
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa shule
ya msingi Katanga,Kasulu mkoani Kigoma tayari kunadi sera za CCM kwa
mwaka 2015-2020.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea ubunge wa jimbo
la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika viwanja vya shule ya msingi Katanga, Kasulu,mkoani Kigoma.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole akiomba kura
kwa wakazi wa Kasulu Kusini mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja
vya shule ya msingi Katanga.
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Kasulu mjini Ndugu Daniel Nswanzigwanko akizungumza
na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuhutubia
wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kasulu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika
kwenye uwanja wa CCM Kasulu mjini.
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika
kwenye uwanja wa CCM Kasulu mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi
Kasulu mjini na kuwaeleza kuwa CCM imeleta mgombea anayejali wananchi, mtendaji na mfuatiliaji asiyependa rushwa na anatanguliza maslahi ya nchi kwanza kwa manufaa ya wote.
Kasulu mjini na kuwaeleza kuwa CCM imeleta mgombea anayejali wananchi, mtendaji na mfuatiliaji asiyependa rushwa na anatanguliza maslahi ya nchi kwanza kwa manufaa ya wote.
LOWASA AAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA KILIMANJARO
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) taifa ,Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Moshi.
|
Maelefu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kutia Chadema kwa mwavuli wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,wakionesha ishara ya mabadiliko. |
Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,James Mbatia akiwa amemnyanyua mkono na kumuombea kura mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael |
BUZWAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA.
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti Bwana James Jisena kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa kampuni kwa utumishi wa muda mrefu. |
Bwana Amos John(Kushoto) ambaye ni Meneja wa Idara ya Biashara Mgodi wa Buzwagi akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi wa Idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu. |
Meneja wa Idara ya Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana George Mkanza akimkabidhi cheti Bwana Abdalah kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu. |
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko akimkabidhi cheti Wilbert Masawe kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu |
Meneja wa Idara ya Huduma za kitaalamu za madini Bwana Sam Eshun akimkabidhi cheti mmoja wa watumishi katika idara yake kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu. |
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko akimkabidhi cheti Cosmas Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu. |
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Victor Mtutwa kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi.
|
Meneja Mkuu wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni ya Acacia Bi. Janet Ruben akimkabidhi Shamsa Mohamed kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu katika idara ya Ufanisi wa Kampuni katika Mgodi wa Buzwagi |
Meneja wa Idara ya Assets Reliability Eng. Peter Mbawala akikabidhi cheti Agness Joseph kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi cha miaka mitano |
Mkuu wa kitengo cha Idara ya Raslimali watu Bwana Ivocatus Masanja akitangaza majina ya washindi wa Tuzo mbalimbali ambazo zilitolewa wakati wa halfa ya siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi. |
Mshauri Mkuu wa Idara ya Uendelevu wa kampuni ya Acacia Steve Kisyaki (kushoto) akimkabidhi cheti Bwana Franco Eliya Mwakalinga kwa kuitumikia kampuni kwa kipindi kirefu. |
BURUDANI YA KUKATA NA SHOKA NAYO HAIKUKOSEKANA VIJANA WA JJ BAND KUTOKA MWANZA WAKAUFANYA USIKU WA FAMILIA YA BUZWAGI KUWA WA AINA YAKE. |
Subscribe to:
Posts (Atom)