TAGCO KUKUTANA MACHI 12 KATIKA MKUTANI WA 13 JIJINI ARUSHA

TAGCO KUKUTANA MACHI 12 KATIKA MKUTANI WA 13 JIJINI ARUSHA

January 16, 2018

TG1
Mweyekiti wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Paschal Shelutete akizungumza kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarjiwa kufanyika kuanzia tarehe 13 Machi Jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mwenezi wa TAGCO Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus na Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi.
TG2
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO Abdul Njaidi na Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete
TG3
Kaimu Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akisistiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini (TAGCO) na waandishi wa habari kuhusu Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Katibu Mkuu wa TAGCO, Abdul Njaidi, Mweyekiti wa Chama hicho Paschal Shelutete na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus
TG4
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa viongozi wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na MELEZO
……………………………………………………………………
Na Florah Raphael-Fullshangwe-Dar es Salaam

Mkutano Mkuu wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo ,  unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 12-16 Machi mwaka huu mkoani Arusha ambapo jumla ya maofisa 300 wanatarajiwa kishiriki katika mkutano huo.

Akiongea Na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa chama hicho Paschal Shelutete amesema kuwa lengo kuu kuelekea mkutano huo  ni  kukumbushana wajibu na majukumu yao serikalini.

Aidha amesema kuwa kikao hicho kina kazi ya kuwajengea washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za serikali na kuhakikisha idara ya mawasikiano na uhusiano serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Pia ameongeza na kusema kuwa katika mkutano huo jumla ya mada 14 zitaongelewa ambazo zitajikita zaidi kwenye masuala mbalimbali  yahusuyo habari, mawasiliano na itifaki.
Pia amesema kuwa mada hizo zitawasilishwa na wataalam watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano na kuongeza kuwa kutakuwepo mijadala na fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya maaafisa mawasiliano na wadau wengine wa habari.

Mwisho kabisa amewaasa Maafisa Uabari, mawasiliano, uhusiano na Itifaki kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 7 machi mwaka huu.

DK. KIGWANGALLA APONGEZA USHIRIKIANO WA FINLAND KATIKA UHIFADHI WA MISITU NCHINI

January 16, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini. 

Na Hamza Temba - Dodoma
.............................................................. 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla ameipongeza Serikali ya Finland kwa ushirikiano na misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiitoa kuunga mkono juhudi za Serikali katika uhifadhi wa maliasili na uendelezaji wa misitu nchini.

Dk. Kigwangalla ametoa pongezi hizo leo Januari 16, 2018 kwa Balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Mhe. Peka Huka ambaye amemtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na maendeleo ya misitu nchini.

“Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Serikali ya Finland,  mmekuwa washirika wetu wakubwa wa maendeleo kwa muda mrefu ambao mmetusaidia mambo mbalimbali ikiwemo kuendeleza misitu nchini, kuendeleza Chuo cha Mafunzo ya Misitu Olmotonyi na hata mapitio ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, ni matumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha ushirikiano huu”, alisema Dk. Kigwangalla.

Alimueleza balozi huyo kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika uhifadhi wa misitu nchini ikiwemo uhaba wa rasilimali fedha na teknolojia kwa ajili ya kuwezesha uhifadhi endelevu. Alisema changamoto nyingine ni uvunaji haramu wa mazao ya misitu ambayo husababisha eneo la hekta 372,000 za misitu kupotea kila mwaka.

Alisema mbali na nguvu kubwa inayotumiwa na Serikali katika udhibiti wa uvunaji holela wa mazao ya misitu Wizara yake kwa kushirikiana na taasisi zilizoko chini yake inaendelea kuweka mikakati thabiti kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kiserikali kwa ajili ya kutafuta nishati mbadala pamoja na kuanzisha mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa miti ya mkaa kwa njia endelevu.

Akizungumzia umuhimu wa misitu nchini, Dk. Kigwangalla alisema takribani kila kitu hapa nchini kinategemea uwepo wa misitu. Alisema zaidi ya asilimia 80 ya chanzo cha nishati ya umeme nchini ni maji ambayo hutegemea uwepo wa misitu, alitaja pia kilimo na ufugaji ambao pia hutegemea mvua na maji ambayo hutegemea pia uwepo wa misitu.

Kutokana na umuhimu huo, Dk. Kigwangalla amemuomba Balozi huyo kuhamasisha wawekezaji wa Finland  kuja kuwekeza Tanzania katika uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu nchini na kuahidi kuwapa ushirikiano.

Kwa upande wake Balozi Huka, alimueleza Dk. Kigwangalla kuwa nchi yake imekua ikifadhili miradi mbali mbali ya uendelezaji wa misitu katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mikoa ya nyanda za juu kusini na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Alimueleza Waziri Kigwangalla kuwa changamoto iliyopo ya uharibifu wa misitu nchini inahitaji uwepo wa nishati mbadala ambayo mchakato wa upatikanaji wake unatakiwa kushirikisha wadau na Mamlaka nyingine za Kiserikali ikiwemo Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimkaribisha Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo alipotembelewa na balozi huyo kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo katika uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka ofisini kwake mjini Dodoma leo.
 Balozi Peka Huka akimsikiliza Waziri Kigwangalla katika kikao hicho.
 Waziri Kigwangalla akifafanua jambo kwa Balozi Peka Huka (hayuko pichani) katika kikao hicho mapema leo mjini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimuaga Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Peka Huka baada ya mazungumzo ofisini kwake leo mjini Dodoma . 
RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA JUMUIYA ZA CHAMA IKULU

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AZUNGUMZA NA WENYEVITI WA JUMUIYA ZA CHAMA IKULU

January 16, 2018

DSC_3576
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumza na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuchukua nafasi hiyo kuiongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
DSC_3611
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzu Dk. Ali Mohamed akiwa na mgeni wake Mwnyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dkt. Mndolwa Bernad Edmund, akimshindikiza baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar alipofika kujitambulisha
DSC_3797
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, akitowa maelezo na kumtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James walipifika kwa mazungumzo na kujitambulisha Ikulu Zanzibar leo.
DSC_3861
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akia katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao na kujitambulisha Ikulu Zanzibar
DSC_3914
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania (UWT) Thuwaiba Editon Kisasi alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo
DSC_3934
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar walipofika kujitambulisha.
Picha Ikulu

SEKRETARIETI YAPELEKA WANNE MAADILI

January 16, 2018
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu. 
 
Viongozi walioshtakiwa kwenye Kamati ya Maadili ni msimamizi wa Kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, Muhasibu msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele. 
 
Sekretarieti inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya Simba ya Dar es Salaam iliyochezwa Disemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
 
Kwa tuhuma hizo viongozi hao watatakiwa kufika mbele ya kamati Januari 18, 2018.
 
Kamati ya maadili iko chini ya mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa

WAZAZI WASIOFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO CHANZO CHA KUFELI KWA WATOTO WAO

January 16, 2018
 Mratibu wa Asasi ya Kiraia ya Jijini Tanga “Tree of hope” Goodluck Malilo wakati wa akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Komsala Kata ya Mgambo wilayani Handeni kuhusiana na mradi wa uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu ambao umefadhiliwa na Shirika la The Foundation For Civili Society ambao unatekelezwa kwenye vijiji vine vya Michungwani, Kwedizinga, Kabuku Nje na Komsanga wilayani Handeni
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo
 Kikundi cha Burudani cha Kabuku Sanaa Group wakitumbuiza kwenye mkutano huo wa uhamasishaji
Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo

WAZAZI na Walezi ambao wamekuwa wakishindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni wamedaiwa kuwa chanzo cha kupelekea matokeo mabaya ikiwemo wengine kupata sifuri katika mitihani yao.

Hayo yalisemwa leo na Mratibu wa Asasi ya Kiraia ya Jijini Tanga “Tree of hope” Goodluck Mwalilo wakati wa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Komsala Kata ya Mgambo wilayani Handeni kuhusiana na mradi wa uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu.

Mradi huo umefadhiliwa na Shirika la The Foundation For Civili Society ambao unatekelezwa kwenye vijiji vine vya Michungwani, Kwedizinga, Kabuku Nje na Komsanga wilayani Handeni

Alisema vitendo vya wazazi kushindwa kuwajibika kwa kufuatilia
maendeleo ya watoto wao shuleni licha ya kusababisha matokeo mabaya lakini pia limekuwa likisababisha kuwepo kwa utoro wa mara kwa mara ambao umekuwa tatizo kubwa la kupelekea kushindwa kupata elimu bora ambayo ingeweza kuwasaidia kwenye maisha yao.

“Ndugu zangu wananchi mnawajibu mkubwa wa kuhakikisha mnafuatilia maendeleo ya watoto wenu shuleni kwani hii ndio inaweza kuwa chachu ya wao kufikia maendeleo yao kwani mtajua changamoto zinazowakabili na kuona namna ya kuweza kuzipatia ufumbuzi haraka “Alisema

Alisema iwapo watakuwa mstari wa mbele kufuatilia maendeleo ya watoto wao itawasaidia kuweza kufanya vizuri katika masomo yao jambo ambalo linaweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwao.

“Lakini mafanikio mazuri ya wanafunzi shuleni yanatokana na
ufuatiliaji wa wazazi,walezi na walimu ambao wakisaidiana kwa pamoja itakuwa chachu kubwa ya kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa vijana wao “Alisema.

Hata hivyo alisema licha ya hivyo lakini pia wananchi wanapaswa kufuatilia na kuhoji ruzuku zinazopelekwa kwenye shuleni zao ili kuona namna ambavyo zimetumika kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwa chachu ya kupata maendeleo kwenye sekta ya elimu.

Alisema licha ya kufuatilia lakini pia wanapaswa kusimamia miradi inayoendeshwa kwenye shule husika ikiwemo kuifuatilia ili kuona kama inatekelezwa kwa ubora kutokana na fedha ambazo zimetolewa.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Kassim Kajembe alisema alisema kupitia elimu ambayo wameipata imewapa mwanga mzuri wa kuweza kujua namna ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na kuhoji miradi ya maendeleo itakayotekelezwa kwenye shule zao.

TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA

January 16, 2018
  Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua Ujenzi wa jengo la maabara lililojengwa katika  kituo cha afya cha Nyangamara Mkoani Lindi.
Mwonekano wa Nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo katika Kata ya Nyamara, wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi.

Angela Msimbira- OR-TAMISEMI LINDI.
Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Lindi Bw. Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya usimamizi wa huduma ya afya Wilaya ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia  ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya  cha  Nyangamara kilichopo kata ya Nyangamara, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.

Bw. Makenge amesema Kamati ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalojukumu kubwa la kusimamia shughuli zote za afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana budi kuhakikisha Miradi inayotekelezwa na Serikali inasimamiwa kikamilifu ikiwepo Ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.

Amesema kuwa Kamati hiyo inahitajika kusimamia wahudumu wa afya katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyopo  katika sekta ya afya.

Ameiagiza kamati hiyo kusimamia utendaji bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa kuwahimiza wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuondoa kero mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya nchini.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Bikilo Zuberi amesema kuwa mpaka sasa tayari serikali imeshatoa shilingi milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi, Ujenzi wa Maabara, Chumba cha Upasuaji, wodi ya wazazi na chumba cha kuifadhia maiti jambo ambalo litapunguza kero kwa wananchi na kuongeza huduma za afya nchini.

Ameishukuru serikali kwa kuweza kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Lindi kwa kutoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha afya cha Nyangamara kwa kuwa awali kituo kilikuwa na changamato ya kutokuwa na majengo ya kutosha ya kutolea huduma kwa wananchi ikiwemo ukosefu wa jengo la maabara, wodi ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara na chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake,Diwani wa Kata ya Nyangamara Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi Mhe. Ramadhani Malingumu ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kushirikisha wananchi kwenye ujenzi wa vituo vya afya nchini jambo ambalo litasaidia katika kutunza na kusimamia vituo vya afya vilivyojengwa.

Aidha amesema wananchi wa kata hiyo wameshirikishwa katika ujenzi wa kituo hicho kwa asilimia mia jambo ambalo linaimarisha ushirikiano kati ya wananchi na serikali katika kuleta maendeleo katika jamii.

POLISI ARUSHA YATHIBITI UVUNJAJI MARA DUFU

January 16, 2018
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeweza kudhibiti matukio ya uhalifu kwa 17.9% mwaka jana 2017 tofauti na mwaka 2016 ambapo kulikuwa na matukio 2,817 wakati  mwaka 2017 kulikuwa na matukio 1,963 pungufu ya matukio 854, huku matukio ya uvunjaji yakipungua toka 604 hadi 294 ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya mwaka 2016.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda Polisi wa mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, matukio hayo ya uhalifu yamezidi kupungua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2016 matukio yalipungua kwa 6.8% ikilinganishwa na mwaka juzi 2015, na kuongeza kwamba hayo yote yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na Jeshi hilo.

Makosa mengine ambayo yamepungua ni pamoja na Unyang’anyi wa kutumia nguvu ambayo mwaka 2016 yalikuwa 86 na mwaka jana 2017 yameshuka hadi 40 huku makosa ya kutupa watoto yalikuwa 38 lakini mwaka 2017 yameshuka hadi kufikia 13.

“Matukio ya Mauaji nayo yalipungua kutoka 65 hadi 58 kwa mwaka 2017, wizi wa Watoto yalikuwa 20 na yamepungua hadi matukio mawili, na yalioongezeka ni Ubakaji na Ulawiti ambapo mwaka 2016 matukio ya Ubakaji yalikuwa 144 na mwaka jana yameongezeka matukio matano wakati makosa ya Kulawiti yalikuwa 58 yameongeza kufikia 62”. Alisema Kamanda Mkumbo.

Aidha katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya Jeshi hilo liliweza kukamata Cocaine gramu 480, Bhangi kilogramu 211 na gramu 760 na Mirungi  kilogramu 317 na gramu 710 pamoja na watuhumiwa 554.

Kwa upande wa Usalama Barabarani Jeshi hilo limeweza kukusanya jumla ya shilingi 3,825,180,000 kutokana na makosa mbalimbali ambapo kwa mwaka 2016 Jeshi hilo lilikusanya jumla ya shilingi 4,708,680,000 kutokana na makosa hayo.

Hata hivyo Kamanda Mkumbo alisema kwamba kushuka kwa makosa ya Usalama Barabrani  kumetokana na watumiaji wengi wa barabara hususani madereva wa vyombo vya usafiri kufuata vyema sheria za Usalama Barabarani hali hiyo imetokana na elimu iliyokuwa inatolewa na Jeshi hilo kitengo Usalama Barabarani kupitia Radio mbalimbali za hapa jijini Arusha, elimu kwa wanafunzi lakini pia elimu ya kituo hadi kituo kwa wadereva wa Pikipiki za abiria.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza uhalifu, Kamanda Mkumbo ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa za uhalifu na wao kuzifanyia kazi mara moja lakini pia ametoa onyo kwa yoyote atakayedhubutu kushiriki kutenda uhalifu, atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
KOKA ATOA MIL .MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGUA S/M KONGOWE

KOKA ATOA MIL .MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGUA S/M KONGOWE

January 16, 2018
IMG_20180115_170449
Mkazi wa Ngungwa,kata ya Kongowe wilayani Kibaha ,Mkoani Pwani,Bahati Semwe akimuonyesha mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka,maji ya kisima ambayo wanatumia ,hivyo amemuomba kusimamia kero hiyo ili wapate maji safi na salama
IMG_20180115_164828
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka,akizungumza katika mkutano wa hadhara ,huko Miembesaba ‘A’ kata ya Kongowe wakati wa muendelezo wa ziara yake ya jimbo,ambapo hadi sasa ameshatembelea kata ya Visiga,Misugusugu na Kongowe.
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini , Silvestry Koka,ametoa kiasi cha sh.milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.
Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ,shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme .
Koka alitoa mchango huo ,wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ,Miembesaba ‘A’kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.
Aliomba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi lengwa.
Akizungumzia changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni .
“Kulikuwa na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi”
“Lakini tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa awamu” alifafanua Koka.
Koka aliwaasa wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na darasa la kwanza kuwapeleka shule .
Alisema elimu ndio nguzo na hazina ya watoto ,hivyo ni jukumu la wazazi kuona umuhimu wa kuwapa haki hiyo watoto hao.
Kuhusu tatizo la kutumia maji ya visima badala ya maji safi na salama kutoka Dawasco huko eneo la Ngungwa kata ya Kongowe ,alisema linashughulikiwa .
Alisema tatizo la maji lililokuwepo awali Kibaha ,sivyo ilivyo sasa kwani wamepiga hatua ,mradi wa Ruvu Juu na Ruvu Chini imekamilika hivyo kazi iliyobakia ni kusambaza .
Katika afya ,Koka alielezea anaendelea kusimamia changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi,vifaa tiba na madawa.
Alisema kutokana na hilo ,mwezi June mwaka jana ,alileta kontena la vifaa tiba mbalimbali lililogharimu mil.400 na vifaa hivyo vilisambazwa kituo cha afya mkoani na zahanati zilizopo jimboni hapo. 
Alieleza ataendelea kusimamia asilimia 10 ya vijana ,wazee,wanawake,walemavu kwenye mapato ya ndani ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,ili inufaishe makundi hayo.
Koka alisema kwasasa ,asilimia 10 inatakiwa igawanywe asilimia 4 akinamama,asilimia 4 vijana,wazee na walemavu asilimia moja ,moja.
Nae afisa elimu kata ya Kongowe,Aziza Matekenya alisema wakati baadhi ya majengo ya shule ya msingi Kongowe yakiungua shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 1,840.
Alisema halmashauri ilitoa milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo na imeahidi kuongeza milioni 20 kwa ajili ya umaliziaji.
Aziza alieleza,kwasasa shule ina jumla ya vyumba 12 vya madarasa vinavyotumika ,vitatu vichakavu ambapo inahitaji vyumba vya madarasa 40 ili kukidhi mahitaji.
Shule hiyo ilijengwa miaka ya 70 ,kwasasa ina wanafunzi 2,820 na walimu 35 .
RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

January 16, 2018

e01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe.Sahabu Isah Gada Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe. Mhe.Sahabu Isah Gada  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba kwa balozi mpya wa Poland Mhe. Krysztof Buzalski Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Poland nchini Mhe. Krysztof Buzalski Ikulu jijini Dar es salaam leo
e8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Nigeria nchini Mhe. Ikulu jijini Dar es salaam leo
e10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi 16, 2018
e11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa mwambata wa kijeshi wa Ubalozi wa Uturuki nchini Navy Commander Murat Ozen  baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa  Urturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto)   Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 16, 2018
e14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na balozi mpya wa  Urturuki nchini Mhe. Ali Davutoglu akiwa na Mwambata wa Kijeshi Navy Commander Murat Ozen na Katibu wa pili ubalozini Nihat Kumhur baada ya kupokea hati ya yake ya utambulisho. Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Israel hap  nchini Mhe. Noah Gal Gendler  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Israel  Mhe. Noah Gal Gendler Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e23
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea  hati ya utambulisho toka kwa balozi mpya wa Australia nchini Mhe. Alison Chartres Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
e24
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bw.  Robert Sirotka, mume wa balozi mpya wa Australia nchini, Mhe. Alison Chartres  (kati) baada ya kupokea hati  za  utambulisho toka kwa balozi huyo mpya  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018. Kulia ni Katibu wa Pili Ubalozini Deanna  
e25
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na  Bw.  Robert Sirotka, mume wa balozi mpya wa Australia nchini, Mhe. Alison Chartres  (kati) baada ya kupokea hati  za  utambulisho toka kwa balozi huyo mpya  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2018
PICHA NA IKULU

NEC yawakumbusha wasiamamizi wa Uchaguzi kuzingtia Sheria

January 16, 2018
 Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Februari.
 Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi Mdogo.
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge, akiwasilisha Mada ya Maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kwa wasiamamizi wa Kinondoni.Picha na Hussein Makame-NEC

Na Hussein Makame -NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi ili kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.

Hayo yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo la jiji la Dar es Salaam.

Alisema wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni mchakato unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.

“Hivyo mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria...,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza” alisema Elisante.

Aliwakumbusha wasimamizi hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekuwa ikisisitiza kwamba Sheria za Uchaguzi hazikuacha ombwe katika kueleza jinsi gani masuala ya Uchaguzi yanatakiwa yatatuliwe.

Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge akiwasilisha mada ya Maelekezo kwa wasimamizi hao, aliwataka kutoruhusu matumizi ya utambulisho mwingine mbadala tofauti na ule ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeruhusu kutumika.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 61 (3) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na kifungu cha 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, kimeipa mamlaka Tume kuidhinisha matumizi ya utambulisho mwingine tofauti iwapo mpiga atakosa kadi ya kupigia kura” alisema Victoria na kusisitiza kuwa:

“Vitambulisho vilivyoruhusiwa na Tume ni vitatu, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya Kusafiria kwa maana ya Passport na Leseni ya Udereva, hivyo mtu akikosa kadi ya kupigia kura au vitambulisho hivyo hakuna utambulisho wowote utakaoruhusiwa ili mtu aweze kupiga kura”

Mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kwa ngazi ya Jimbo la Kinondoni na kata zilizoko kwenye jimbo hilo, yalijumuisha viapo kwa wasiamamizi hao walioapa kutunza sira na kujivua au kukiri kuwa si mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kinondoni pamoja na Jimbo la Siha na Udiwani katika kata 10 za Tanzania, unatarajiwa kufanyika tarehe 17 Februari mwaka 2018.

MHE BITEKO AITAKA STAMICO KUITHIBITISHIA SERIKALI KWANINI IENDELEE KUWEPO

January 16, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya  pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umetakiwa kutoa maelezo kwa serikali katika kipindi cha muda mfupi kueleza sababu za kuendelea kusalia kuwepo kwa shirika hilo kutokana na kukosa umakini katika utendaji.

Kauli ya kuchukizwa na utendaji wa Shirika hilo imetolewa Leo 16 Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko Wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika hilo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam.

Mhe Biteko alisema kuwa serikali ilikuwa na makusudi mazuri kufuatia mabadiliko ya Sera za kiuchumi katika miaka ya 1980 kwa STAMICO kuwekwa kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa na hatimaye kubinafsishwa rasmi mwaka 1996 lakini katika kipindi chote cha utendaji hakuna msaada wowote ambao Shirika hilo limeipatia serikali zaidi ya kuingiza hasara maradufu.

Alisema kuwa pamoja na STAMICO kuwa na jukumu la kuendeleza migodi ya Madini na kufanya biashara za Madini ikiwemo mradi wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo Biharamlo Mkoani Kagera na Mgodi wa Makaa ya Mawe KABULO uliopo Mkoani Ruvuma lakini Taasisi hiyo imeshindwa kuendeleza migodi kwa ufanisi huku wachimbaji wadogo wakisalia kuwa katika uduni wa mbinu rafiki na tija katika utendaji kazi wao.

Alisema kuwa Shirika hilo linapaswa kutafakari kwa umakini utendaji wake kwani limeongeza hasara kwa serikali ya deni la shilingi Bilioni 1.77 hivyo serikali haiwezi kuendelea kusalia kuwa na Shirika linalozalisha madeni kuliko matokeo makubwa na faida.

Aliongeza kuwa wataalamu wote katika sekta ya Madini wanapaswa kutambua kuwa biashara ya Madini ni zaidi ya kutoa leseni hivyo watambue kuwa kuna kila sababu ya kuwa na matumizi bora ya mapato na kutazama namna bora ya kuifanya sekta ya Madini kuchangia asilimia 10% ya pato la Taifa.

Mhe Biteko alisema kuwa imani bila matendo ni uduni wa fikra hivyo kuwa na cheo kikubwa serikalini halafu uzalishaji ni mdogo ni kipimo halisi cha utendaji wa mazoea walionao watumishi wengi ambao wamekosa uzalendo na bidii katika utendaji kazi.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kusimamia vyema rasilimali za wananchi hivyo watendaji katika sekta mbalimbali wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Rais Magufuli katika kuteleleza adhma ya serikali.