WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA ZIFF AZINDUA TAMASHA LA UONESHAJI FILAMU BURE MKOANI GEITA

November 19, 2016
Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.

Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Na BMG
Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.

Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.
Katibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alibainisha kwamba ZIFF imekuwa ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani Consult kwa lengo la kuziwezesha kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya kuonesha filamu bure na kufikisha elimu iliyokusudiwa.
Katibu Tawala Wilayani Geita, Thomas Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo Ufugaji na utunzaji wa Mazingira.
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita, akisalimia kwenye uzinduzi huo.
Kulia ni Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita, akisoma risala kuhusiana na Mradi wa Uoneshaji Filamu Bure mkoani Geita.

Alisema mradi huo umelenga kutoa chachu kwa wanajamii kutumia fursa mbalimbali ikiwemo ufugaji kujipatia kipato badala ya kutegemea shughuli moja kama vile madini. Pia kuwahimiza kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Yote hayo pamoja na mengine yanafikishwa kwa wananchi kwa njia ya filamu.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (kulia) akipokea taarifa ya mradi wa uoneshaji wa filamu bure mkoani Geita kutoka kwa Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita (kushoto).
Mkuu wa idara ya Habari, Kijani Consult Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure katika maeneo ya wazi mkoani Geita.
Kutoka Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi wa Denimark nchini Tanzania, Dotto Kahindi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo na Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu kuhusu masuala mbalimbali kwa wanajamii.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
Maafisa Habari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanahabari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanatasnia wa Filamu mkoani Geita
Burudani za asili mkoani Geita
Burudani za asili zikiendelea
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Uoneshaji wa Filamu bure mkoani humo ili kufikisha elimu ya masuala mabalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira pamoja na ufugaji kwa njia ya filamu
Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto walioshiriki shindano fupi la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kuonesha Filamu bure mkoani Geita.
Mgeni Rasmi Mhe.Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto, Maisala Ibrahimu anayesoma kidato cha pili shule ya Sekondari Kangalala (ke) na Joshua Tito anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Kivukoni Geita (Me) ambao walioonesha vipaji vya hali ya juu katika kucheza muziki. 

ZIFF imetoa fursa ya kuwanunulia mavazi ya shule watoto hao huku pia wakipata fursa ya Kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Filamu katika Visiwa vya Zanzibar hapo mwakani.

Bonyeza HAPA Kutazama picha za kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu Tanzania.
MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AANZA ZIARA YA SIKU KUMI MKOA WA DAR ES SALAAM

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AANZA ZIARA YA SIKU KUMI MKOA WA DAR ES SALAAM

November 19, 2016
kond1
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akitoa maelekezo wakati akikagua  uharibifu wa mazingira katika mtaa wa Maweni Mjimwema  uliosababishwa na wachimba kokoto.
……………………………………………………………………..
(NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wanachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika.
“Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua 80% ya wafanyakazi wa serikali hawafanyikazi, asilimia 80 ya watumishi wa umma hawafanyikazi, niwapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara,” alisema Mkonda.
Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali ina wafanyakazi kuanzia ngazi ya vitongoji.
Aidha mkuu huyo ataelekea mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo ataangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na wachimba kokoto.
  kond3
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na wakuu wa wilaya za Kigamboni na Temeke pamoja na viongozi mbalimbali  wakati akikagua uharibifu wa mazingira katika mtaa wa Maweni Mjimwema  uliosababishwa na wachimba kokoto
kond5
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Kigamboni hawapo pichani wakati aliofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi wilayani humo.
kond6
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya wialaya katika ziara ya mkuu huyo wa mkoa katika wilaya hiyo.
kond7
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi kulia akiwa pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul makonda hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoa wa Dar es salaam.
kond8
Mkuu wa mkoa wa Dar es samaa Mh. Paul Makonda akizindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa katikati  wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
UISLAMU SIO UGAIDI ASEMA-RC GAMBO

UISLAMU SIO UGAIDI ASEMA-RC GAMBO

November 19, 2016
1
Na Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesema Uislamu sio ugaidi hivyo dini isihusishwe na ugaidi na wala Uislamu usitumike kama ngao ya kufanya uhalifu bali ugaidi ni uhalifu na atakaejihusisha na ugaidi ashughulikiwe kama wahalifu wengine .
Yameelezwa jana na mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo, kwenye kongamano la Kiislamu lililoandaliwa na Marakazi ya Al Azhar Sharif, Changombe ,Dar Es Salaam, lililofanyika ukumbi wa ccm, mkoa wa Arusha, lililokuwa likizungumzia athari za Fatua zinazohalalisha umwagaji wa damu zilizohifadhiwa na kutyumbisha amani na utulivu.
Kwenye hotuba hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Monduli, Iddy Kimanta, amesema vipo vitendo vingi vinafanywa na baadhi ya watu kwa kisingizio cha dini ya Kiislamu jambo ambalo sio sahihi hatakidogo kwa kuwa dini inakataza kumwaga damu au kuua nafsi isiyo kuwa na hatia .
Akasema wanaojihusisha na ugaidi watashughulikiwa kama magaidi na kamwe wasihusishwe na uislamu kwa kuwa dini haina uhusiano wowote na ugaidi.KUhusu elimu, Kimanta,amewataka wazazi kuhakikisha wanasomesha watoto wao elimu zote mbili ya Dunia na Akhera, na hivyo kuwajenga kwenye malezi yaliyo bora ambayo yana maadili ya uislamu.kwa kuwa yatawawezesha kujiepusha kujiingiza kwenye uhalifu na ugaidi.
”Arusha ni eneo lipo kwenye hatari zaidi kwa kuwa tunakaribiana na maeneo ambayo kama kama vijana wasipopelekwa kwenye malezi yenye maadili watatumika kwenye ugaidi ,mfano anakuja mtu anachukua vijanakwa madai anawapeleka nje kusoma na mzazi hahoji mtoto wake anaenda kusoma kitu gani ”alisema, kimanta.
AmeseKUhusu matumizi ya mitandao, amesema ipo mitandao mingi lakini sio yote yenye nia njema na Uislamu hivyo wazazi lazima wawe makini kwa kuwa mitandao mingi inalenga kuvuruga na kuwagawa na hatimae ni kuporomoka kwa maadili katika jamii.
Amesema kibaya zaidi wazazi nao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao na hivyokusahau majukumu yao ya malezi na mitandao ina nguvu kubwa kuliko Quraan tukufu na hivyo sasa wazazi na watoto wanaishi kimtandao tandao badala ya kusomesha watoto ili wapate elimu yenye manufaa.
Awali Shekhe wa mkoa wa Arusha, Shaaban bin Jumaa, amesema hivi sasa kuna vikundi vingi vimezuka ambavyo vinakuwa vikitoa Fatua(MATAMKO) juu ya dini ambayo yanapotosha na kusababisha mitafaruku na migogoro .Amesema Fatua inatakiwa kutolewa na kiongozi mwenye elimu kubwa aliyebobea kwenye dini na sio hali ilivyo ambaposasa mtu yeyote ambae hana elimu kubwa wala sio kiongozi anatoa fatua.
Amesema kinachosababisha hayo kutokea ni kutokuheshimiana ambapo kila mmoja sasa anataka madaraka wakatihana sifa hiyo hivyo kilichopo ni kila mmoja kumheshimu mwingine aliyemzidi elimu ya dini na hivyofatua zittaondoka.
Amesema elimu ndogo ndio inayopelekea watu kufanya vitendo vya ugaidi na kusingizia dini wakidai ni jihadi jambo ambalo sio sahihi hata kidogo.

DKT. SHEIN ALIFUNGUA RASMI KONGAMANO LA KIBIASHARA BAINA YA TANZANIA NA COMORO, ZANZIBAR LEO

November 19, 2016
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Mhe,Mohamed Bacar Dossar (katikati) wakisimama pamoja na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Comoro ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Visiwa vya Comoro wakisimama ulipopigwa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Comoro katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipowasili kufungua Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahamoud pamoja na Viongozi mbali mbali alipowasili kufungua Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi na Maafisa mbali mbali wa taasisi za Serikali na Binafsi wakikwa ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi na Maafisa mbali mbali wa taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipokuwa akitoa maelezo katika Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne katikati).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,kwa Viongozi na Wafanyabishara mbali mbali lililofanyika katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,kwa Viongozi na Wafanyabishara mbali mbali lililofanyika katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara baina ya Comoro na Tanzania,kwa Viongozi na Wafanyabishara mbali mbali lililofanyika katika ukumbi wa Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.[Picha na Ikulu.]

NDEREMO,VIFIJO VYATAWALA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA TUMAINI DAR

November 19, 2016
 Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo, alitunuku  jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo,akimtunuku Evelyn Wallace Shundi Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Wahitimu Agnes Nsokolo (kulia) na Asha Kidendei wakiwa na furaha baada ya  kuwa miongoni mwa wahitimu 43 waliotunukiwa  Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Evelyn Shundi ambaye ni mfanyakazi wa Ewura akiwa na furaha wakati wa mahafali hayo.
 Wahitimu wakivaa kofia baada ya kutukiwa
 Mmoja wa wanafunzi akipatiwa cheti wakati wa mahafali hayo
 Wakivaa kofia ikiwa ni ishara ya kunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamekaa baada ya kutunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamesimama mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakisubiri kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Domina Rwemanyila (kushoto) na Diana Tengia wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa Sahada ya Sanaa ya  Mawasiliano ya Umma
 Ni furaha iliyoje kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Dk Frederick Shoo na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliotunukiwa Sahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara
 Wapigapicha wakiwa kazini wakati wa mahafali hayo
 Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakipiga wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha mahafali hayo
 Julieth (katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuhitimu katika chuo hicho. KWA MAWASILIANO ZAIDI;0715 264202/0754 264203