ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO

September 17, 2017
Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo  vinavyochangia katika  upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.
 Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo  vinavyochangia katika  upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo  vinavyochangia katika  upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria wa  udhibiti wa  pembejeo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.

“tunatekeleza mradi wa miaka miwili  unaolenga uimarishaji  utekelezaji wa  sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu)  kudhibiti  soko na kuhamasisha upatikanaji  wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa utafiti ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.

“Kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema Lugano.

Aidha Lugano alisema kuwa utafiti huo umefanywa kwenye mikoa 10 ilichaguliwa kutoka katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani pamoja wilaya mbili kila mkoa zilichaguliwa kwa kuzingatia umbali kutoka makao makuu ya mkoa ili kuwezesha kulinganisha uhusiano wa umbali na upatikanaji wa pembejeo.

“Mikoa ambayo tumefanya utafiti ni pamoja  Ruvuma, Kagera, Mbeya, Morogoro, Manyara, Rukwa, Iringa, Shinyanga na Simiyu hii ndio tuliona sahihi kufanyia utafiti kwakuwa ipo katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora kimekuwa kikwazo moja wapo kwa wakulima wadogo wadogo hasa wale ambao hawana elimu ya kilimo na kusababisha hasa kwa wakulima na wengine kukata tamaa ya kilimo.

“Mahitaji ya mbegu kwa mwaka nchini inakadiriwa kuwa tani 120,000. Kati ya hizo, 25% (tani 30,000) huzalishwa na sekta rasmi, kiasi kinachosalia huagizwa kutoka nje ya nchi na makapuni za kibiashara” alisema Lugano

 Lugano alisema kuwa makisilio ya mahitaji na upatikanaji ya viuatilifu kwa mwaka ni changamoto kutokana na kuwa usambazaji hivyo hutegemea mahitaji mahsusi kwa eneo maalum lenye uhitaji kwa wakati maalum

“Mahitaji ya viatilifu huongozwa na Mfumo wa ‘Integrated Pesticides Management (IPM)’ Sera ya taifa ya kilimo (2013) inahimiza menejiment sahihi ya viuatilifu ambao unazingatia kanuni za kilimo bora zinazozingatia usalama na uhifadhi wa mazingira takriban viuatilifu vyote vinavyotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi” alisema Lugano
 
Naye afisa kilimo wa manispaa ya Iringa Gerlad Mwamila aliupongeza utafiti uliofanywa na jukwa la kilimo la ANSAF kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuweza kuyafumbua maeneo yenye changamoto na jinsi gani ya kuzitatua kwa kutuwekea wazi mapendekezo yake.

"ukiangalia utafiti huu umewakusa sana wakulima na unamanufa kwa wakulima hivyo sisi viongozi ambao tupo serikalini tunapaswa kufikisha elimu hii kwa viongozi wetu wa juu pamoja na wakulima ili kukuza kilimo cha wakulima wadogo" alisema Mwamila

Mwamila alisema kuwa serikali inatakiwa kujipanga kufanikisha zoezi la upimaji ardhi ili kuwasaidia wakulima wadogo kulima kwa uhakika na sio kulima kwa kubahatisha kama ambavyo saizi wanavyolima.

"kwa kweli halmashauri zetu hazina pesa za kutosha kufanikisha zoezi la upimaji ardhi kwa wakulima wote,lakini kama halmashuri zikifanya kazi sambamba na taasisi binafsi tunaweza kufanikisha lengo la kumkomboa mkulima mdogo" alisema Mwamila

Kwa upande wake afisa kilimo wa halmashuri yawilaya ya Iringa Merry Mushi alisema kumekuwa na changamoto kwa wakulima kuuziwa pembejeo ambazo hazina ubora hivyo halmashauri imejipanga kutatua tatizo hilo.

"mara kwa mara tumekuwa tutoa elimu kwa wakulima juu ya kutumia pembejeo zisizo na ubora hivyo wakulima wameanza kuelewa na kufikisha malalamiko yake kwenye ofisi za kilimo za wilaya hiyo ni hatua kubwa sana kwetu"alisema Mushi


Mwakilishi na Mbunge wa Jimbu la Tunguu Wakabidhi Fedha Kwa Vikundi 13 Vya Ushirika Shehia za Unguja Ukuu

September 17, 2017

Mwakilishi wa Jimbo Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika vya Wananchi wa Kae Pwani Unguja. Mchango huo umetolewa na Mbunge na Mqwakilishi kuchangia vikundi hivyo kwa ajili ya kutunisha mifuko ya vikundi vya vinavyojishughulisha na ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa na kilimo na kukupeshana, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Ungua Ukuu Kae Pwani.
 Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.

Baadhi wa Viongozi wa Vikundi vya Ushirika katika Shehia za Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla hiyo.  
Sheha wa Shehia ya Kae Pwani Ndg. Khamis Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa Vikundi vya Ushirika vua Shehia hiyo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikamano wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Aso Mtu Ana Mungu, wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Tuwe Nao,wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.. 
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi vya Ushirika wakifuatilia hafla hiyo. ya kukabidhiwa fedha kutunisha mfuko wa vikundi vya jumla ya vikundi 13 vimekabidhiwa fedha taslim zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo lao la Tunguu Zanzibar. Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza baada ya kukabidhi fedha kwa Vikundi vya Ushirika vya Kae Pwani Unguja Ukuu Unguja fedha hizo zimetolewa kwa pomoja yeye na Mbunge wake kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo lao kukuza Mtaji wa Vikundi vyao vya ushiriki vinavyojishughulisha na kilimo cha mboga mbogo, kuweka na kukopa na vikundi vya Ujasiriamali, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM uNGUJA Ukuu Kae Pwani.

Baadhi ya Viongozi wa Vikundi vya Ushirika wakifuatilia hafla hiyo. ya kukabidhiwa fedha kutunisha mfuko wa vikundi vya jumla ya vikundi 13 vimekabidhiwa fedha taslim zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo lao la Tunguu Zanzibar. Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kae Pwani Ndg.Ali Muhidini akizungumza na kutoa nasaha zake kwa Wananchi wa Vikundi vya Ushiriki kushikamano na kuvikuza vikundi vya katika kujiletea maendeleo ya kipato kupitia katika vikundi vyao.
Katibu wa CCM Tawi la CCM Kae Pwani Ndg. Daruweshi Ali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika katika Shehia ya Kae Pwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimsalimia Mtoto Mulhat Ai Ramadhani wakati alipofanya ziara kutembelea Wananchi wa Jimbo lake la Tunguu na kukabidhi fedha kwa vikundi 13 ili kutunisha mfuko wa vikundi vyao, katika shehia ya Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.

RPC LINDI AWAAPISHA GIRL GUIDES 230, WABAKAJI WATOTO SASA KUKIONA

September 17, 2017

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 
 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. 

Na Richard Mwaikenda,Lindi
 JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga 

katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana.

Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote 

wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali  za kisheria.

"Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike 

wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga na kuwataka 

waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike.

Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya 

kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni.

Akielezea walichonufaika katika wakati wa mafunzo yaliyodumu kwa takribani siku nne, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa 

Lindi, alisema kuwa waischana walifaidika kwa kupata mafunzo ya ukakamavu, kujiamiini, kuepukana na vikwazo 

mbalimbali wanavyokumbana navyo wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani ikiwemo kurubuniwa kwa kupewa 

mimba za utotoni.

Alitaja mambo mengini waliyonufaika nayo ni ujasiriamali, utunzaji wa mwili, utunzaji wa mazingira, uongozi, maadili, 

kujitolea , kuwa na upendo na uzalendo kwa nchi yao.

Mwenyekiti aliimpongeza Kamanda Mzinga kwa kuwapatia askari wa kike ambaye anafanya kazi nzuri ya kukutana na 

watoto wanaoelezea matatizo yao bila woga baada ya kupata mafunzo ya TGGA, ambapo alidai baadhi ya wanafunzi 

hao wanadiriki kusema wazi kwamba wazazi wao wana tabia ya kutaka kuwabaka.

Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, aliwaasa wasichana waliopata mafunzo hayo, kulinda kiapo walichokipata 

kwa kuwa watiifu na kuweka mbele uzalendo, awe na imani iliyo thabiti katika maisha yake, nchi yake na Jamii.

"Hivyo basi msilichukulie jambo la kawaida,  libaki mioyoni mwenu mbele ya Mungu na muepukane na ulevi, kutumia 

dawa za kulevya, matumizi mabaya ya mitandao, tunataka muwe na misimamo katika maisha yao yote."Alisema Shaba.

Alisema TGGA ina utaratibu wa kuwaingiza uanachama kuanzia watoto wa miaka mitatu na kuendelea ambapo 

huwapatia  mafunzo ya kujiamini, kujithamini, ujasiriamali na kuipenda nchi yao.

Pia alitangaza  kwa wanachama wao walio likizo na waliomaliza shule wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kuomba 

kujiunga na programu ya Yess kwenda nje ya nchi kupata mafunzo ya uongozi, utamaduni na maadili katika nchi tano 

wanachama kwa ufadhili wa Makao Makuu ya Girl Guides ulimwenguni.

Alisema wanachama watakaofanikiwa kwenye programu hiyo inayoendeshwa kuanzia miezi mitatu, sita au mwaka 

mzima watafaidika kwa kujiongezea upeo wa mambo mbalimbali.


 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akimkaribisha mgeni rasmi, RPC wa Lindi, Renatha Mzinga kwenye hafla hiyo.

 Baadhi ya wazazi wa Girl Guides waliokuwa wakiapishwa wakiwa katika hafla hiyo

 Timu ya soka ya wanawake mkoani Lindi wakitambulishwa katika hafla hiyo. Nao wanatarajia kujiunga na Girl Guides
 Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
 Young Leader wa Dar es Salaam, Valentina Gonza akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akijitambulisha
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth Namatanga akimvisha beji mwanachama mpya
 Girl Guides wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
 Mgeni rasmi, RPC Mzinga akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Lindi, Sharifa Mkwango akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
  Mkufunzi Mkuu wa TGGA, Emmiliana Stanslaus akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
 Girl Guides mpya akivishwa beji

BLOGGER TUPOKIGWE ABNERY KUZINDUA KITABU CHA RIWAYA "MAPENZI KABURINI" JIJINI ARUSHA

September 17, 2017


Tupokigwe Abnery Mwampondele amezaliwa,Seronera - Serengeti mkoani Mara.Alisomea shahada ya Isimu ya lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya Sekondari ya Wasichana Precious blood iliyopo mkoani Arusha-Tanzania. N’je na kazi ya uwalimu Tupokigwe Abnery ni mtunzi wa vitabu vya hadithi, mbunifu wa mavazi ya kiasili, mjasiriamali na mwandishi wa gazeti tando (blogger) inayoitwa Sinyati Blog.

Tupokigwe Abnery alikuwa na kawaida ya kupenda kujibembeleza au kujifariji akiwa anatembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zake ili kuweza kulala au kufika anakoelekea bila kuchoka,ndipo siku moja baada ya kushiriki shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma Kikwete iliyoandaliwa na TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) aliibuka mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

BENKI YA CRDB YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI MWANZA

September 17, 2017
Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Na  Binagi Media Group
Benki ya CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza mitaji yao.
Akisoma hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.

Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi 20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya 649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13 pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia wateja wake kwa urahisi.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza
Meneja Mwandamizi wa benki ya CRDB, kwa wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuka akizungumza kwenye mkutano huo Jijini Mwanza
Meneja Biashara benki ya CRDB, Danford Muyango akizungumza kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo
Benki ya CRDB imeendelea kuwahakikishia wajasiriamali kwamba itaendelea kushirikiana nao kwa kuwapatia mikono yenye riba nafuu ili kukuza biashara zao
Mjasiriamali Doroth Baltazari ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Chabati Pop Food, akiwaonyesha baadhi ya wanahabari bidhaa anazotengeneza.

WATALII ZANZIBAR HAWAJAKAUKA LICHA YA MSIMU ULIOPO KUZOELEKA KUWA WACHACHE

September 17, 2017


Na Jumia Travel Tanzania

Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio lukuki takribani kila sehemu utakayoipendelea. Mji Mkongwe uliopo visiwani Zanzibar ni mojawapo ya maeneo hayo yenye utajiri wa vivutio vya watalii kama vile maisha na vyakula vya wakazi wake, biashara pamoja na majengo ambayo yanayoakisi tamaduni za mataifa tofauti kama vile Waarabu, Waajemi, Wareno, Waafrika na Waingereza ambayo yamekuwepo tangu karne za 18 na 19.

Katika kuhakikisha maeneo hayo yanajulikana miongoni mwa watanzania na wageni wanaotembelea nchini, Jumia Travel wamezindua kampeni ambayo itakuwa ikiangazia maeneo mbalimbali. Ikiwa imejikita kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar, kampuni hii ambayo inajishughulisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ilifanya mahojiano na Meneja Operesheni wa Africa House Hotel, Bw. Justus Kisome na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU MAHUSUSI WA KOROSHO TANZANIA

September 17, 2017
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wadau mahususi wa korosho katika hotel ya Tanga Beach mjini Tanga unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dkt Charles Tizeba akizungumza katika mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Octoba 1 mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Hassani Jarufu akizungumza wakati wa mkutano huo 
unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Mama Anna Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo 
unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri
 Wasjhiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo 
 Wadau wakifuatilia makrabasha mbalimbali kwenye mkutano huo

 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Mwanga kushoto akifurahia jambo wakati wa mkutano huo
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete kulia akiteta jambo na baadhi wa washiriki wa mkutano huo leo uliofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga

 Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Mnauye akiteta jambo kabla ya kuanza kikao hicho

 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM) Hawa Ghasia akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mlalo (CCM) Rashidi Shangazi wakati  wa kikao hicho mapema leo ambao ulifunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akisalimia na Mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao hicho
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu akisaliana na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kabla ya kuanza mkutano huo
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete


 Sehemu wa washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia kwa umakini mkutano huo
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini 
 Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Mathew Mtigumu katikati akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakati wa kikao hicho kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mazingira,Januari Makamba
 Baadhi ya washiriki wakiendena na mkutano 

Sehemu ya washirki wakifuatilia mkutano huo leo

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo leo
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.