KOMBE LA SHIRIKISHO MZUNGUKO WA TATU

KOMBE LA SHIRIKISHO MZUNGUKO WA TATU

January 22, 2016
Mzunguko wa tatu wa michuano wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) unatarajiwa kuendelea wikiendi hii mpaka katikati ya juma lijalo kwa michezo 13 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Kesho Jumamosi michezo mitatu itachezwa, mjini Morogoro Burkinfaso FC watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini humo,  Pamba FC watawakaribisha Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, huku Ndanda FC wakichea dhidi ya Mshikamno FC katika uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara.
Jumapili michuano hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Friends Rangers uwanja wa Taifa, Njombe Mji watakua wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Amani Njombe, huku Stand United wakicheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Michuano hiyo itaendelea Jumatatu, Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC dhidi ya Madini FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi na Africa Lyon wakiwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumanne Mtibwa Sugar watawakaribisha Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Wambi Mafinga, Africa Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga, na Geita Gold watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Singida United watacheza dhidi ya Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa Namfua mjini Singida, na mchezo wa mwisho utachezwa Februari Mosi katika ya Wenda FC dhidi ya Mbeya City uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mpaka sasa timu ya JKT Mlale pekee ndio imeshafuzu kwa mzunguko wa nne baada ya kuiondosha Majimaji kwa mabao 2-1, katia mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KLABU YA PRISONS

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KLABU YA PRISONS

January 22, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake Hassan Mlilo kilichotokea jana katika hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu Hassan Mlilo, ndugu, jamaa, marafiki na klabu ya Tanzania Prisons, na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini amesema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Mwili wa marehemu Hassan Mlilo unatarajiwa kusafirishwa leo mchana kuelekea mkoani Mbeya, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika mji wa Rujewa mkoani humo.

MAONESHO YA BIASHARA YA ESTHER LAND SHOW AFRIKA KUSINI YAVUTIA WAFANYABIASHARA WENGI ZAIDI KUTOKA TANZANIA

January 22, 2016

Na EmanuelMadafa,Mbeya,Mbeya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika kusini  (Esther Land Show) ambayo hufanyika kila mwaka nchini humo yameendelea kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kutoka nchini Tanzania.

Pia Maonesho hayo hufanyika  katika mji wa Johnsburg ambapo kwa mwaka huu yanatalaji kuanzia Mwezi Machi  23 hadi  April 03 mwaka huu huku idadi ya wafanyabiasahara hao waliojitokeza imetajwa kufikia  zaidi ya watu  100 ,hasa kutoka  katika mikoa ya Kanda ya Ntanda za juu kusini.

Katika kufanikisha safari ya wafanyabiashara hao  kampuni ya  Blue  Bird Buleau De Change iliyopo Jijini Mbeya imeamua kudhamini safari hiyo kwa kutoa usafiri wa kwenda na kurudi kwa basi  la Twiga Intarnational  ambapo kila mfanyabiashara atachangia kiasi cha shilingi laki nne na nusu  (450000).

Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Jankey Ndingo, amesema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa zilizomo kwenye maeneo yao.
“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.
  
Amesema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la kimataifa.

Amesema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza kusafirisha bidhaa hizo.

“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.

Aidha, amesema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi  kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.



Hata hivyo, amesema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa ya siku 13.





Mwisho.
Jamiimojablog

BALOZI WA NORWAY NCHINI ATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME KATIKA KITUO CHA KIKULETWA WILAYANI HAI.

January 22, 2016
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad wakati akimpokea ofisini kwake kwa ajili ya ziara ya kutembelea kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha,(Arusha Techinical) Dkt Richard Masika aliyeongozana na balozi wa Norway katika ziara ya kutembelea kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa.
DC Mtaka akiongozana na Balozi Kaarstad kuelekea ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha ,Dkt Richard Masika akiteta jambo na Balozi wa Norway Kaarstad ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Anthony Mtaka akizungumza na ugeni wa balozi wa Norway ofisini kwake .
Baloozi Kaarstad akimueleza jambo DC Mtaka.
Ugeni wa Balozi wa Norway ukiwa umetembelea kivutio cha Utalii cha Chemka ambako kuna Chemichemi ya maji yenye uvuguvugu ambako watalii wamekuwa wakitembelea na kuogelea.
Kivutio cha Utalii cha Chemka ambacho maji yake yanatokana na Chemichemi .
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha ambao ndio waendeshaji wa kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa  akitoa maelezo kuhusu mradi wa ukarabati mkubwa uanaotaraji kufanywa kwa msaada wa serikali ya Norway.
Mooja ya mioundo mbinu katika kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa.
Balozi Kaarstad akiongozwa kutembelea maeneo mbalimbali katika kituo cha Kufulia umeme cha Kikuletwa.
Sehemu ya Mitambo ya kufua umeme katika kituo cha Kikuletwa inavyoonekana kwa sasa baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo na Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Profesa Idd Mkilaha walipkutana wakati wa kutembelea Kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Ugeni wa Balozi wa Norway Kaarstad ukitembelea maeneo mbalimbali ya mradi huo .
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha,Dkt Masika akimuonesha Balozi Kaarstad mfereji mkuu wa kupeleka maji katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Kazi ya uondoaji tope ikiendelea katika mfereji huo.
Sehemu ya maporomoko ya maji yanayotiririka katika mto Kikuletwa.
Balozi wa Norway ,Henne-Marie Kaarstad akizungumza na wanahabari katika eneo ambalo maji yanapita kwa kasi katika mto Kikuletwa.
Ugeni wa Balozi wa Norway ukitizama moja ya mito inayotirisha maji kuelekea katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Mto unaotenganisha wilaya ya HAi na Simanjro mkoani Manyara unaopeleka maji katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
DC Mtaka akimuongoza balozi Kaarstad kupita katika moja ya daraja lilopo eneo la mradi .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Benki ya NMB na John Deere kuwakopesha wakulima matrekta

Benki ya NMB na John Deere kuwakopesha wakulima matrekta

January 22, 2016
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kusaini hati ya makubaliano na Benki ya NMB itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen (kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kusaini hati ya makubaliano na Benki ya NMB itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao.Kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha na Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen wakiwa katika tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha na Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen wakiwa katika tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Sehemu ya waandishi wa habari wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Sehemu ya waandishi wa habari wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wanufaika wa mkopo huo wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wanufaika wa mkopo huo wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen akizungumza katika tukio la kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.[/caption] IMG_0315 Sehemu ya waandishi wa habari wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Sehemu ya waandishi wa habari wakishuhudia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Benki ya NMB na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) kuwawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es SalaamMkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akisaini hati ya makubaliano na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha wakishuhudia. Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akisaini hati ya makubaliano na Kampuni ya John Deere (wauzaji wa matrekta) itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha wakishuhudia.[/caption] [caption id="attachment_66174" align="alignnone" width="800"]Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Benki ya NMB itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha, tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Benki ya NMB itakayo wawezesha wakulima kupata mkopo wa matrekta kwa ajili ya shughuli zao. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lonagro Tatnzania Ltd, Lukas Botha, tukio hilo lilifanyika jana kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.[/caption] Na Mwandishi Wetu BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni maarufu kwa uuzaji wa matrekta ya John Deere zimeingia makubaliano ili kufanikisha kuwakopesha matrekta wakulia wanaochipuki kwa lengo la kuwawezesha waendelee kufanya vizuri kwenye kilimo cha kisasa. Katika makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Banki ya NMB imekubali kutoa mkopo ambao utamuwezesha mkulima kununua trekta hilo huku akiurejesha taratibu, Hata hivyo Kampuni ya John Deere itatoa mafunzo ya kilimo cha biashara kwa mkulima aliyenufaika na mkopo huo pamoja na kumfundisha matumizi bora ya kifaa hicho cha kilimo. Akizungumza mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema benki yao inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo na inavyochangia kukuza uchumi wa Tanzania hivyo kuamua kuwawezesha wakulima ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa ujumla. "...Upatikanaji wa mikopo kwa wakulima siku za nyuma ulikuwa ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kilimo...hivyo makubaliano haya yanakuja kuleta suluhisho kwa wakulima hasa katika eneo la kupata vifaa muhimu vya kilimo cha kisasa kama matrekta yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia," alisema Mponzi. Alisema kwa kutambua mchango wa sekta ya kilimo tayari Benki ya NMB imewasaidia wakulima wadogo zaini ya 600,000 kupata mitaji ya mikopo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao anuai ya kilimo pamoja na kuendesha mafunzo ya kijasiliamali kuwajengea uwezo makundi yote. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen alisema mikopo hiyo inayotolewa kwa wakulima inalengo la kuwainua wakulima wadogo ili waweze kubadili kilimo chao kuwa kilimo endelevu kinachotumia vifaa vya kisasa yakiwemo matrekta ya kilimo, kuvunia na kusafirisha mazao kutoka shambani hadi eneo linalokusudiwa. "Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo katika nchi za Afrika, John Deere kwa kushirikiana na NMB tunategemea kuweka mifumo itakayowawezesha wakulima wadogo ili kuleta ufanisi katika shughuli nzima ya kilimo. Ufanisi katika manunuzi ya pembejeo, uzalishaji na pia matumizi ya teknolojia za kisasa (mbegu, mbolea na hata vitendea kazi-mashine) na hata ufanisi katika kutafuta masoko ya mazao yao mojakwa moja," alisema Westhuizen. ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com