DKT. SHEIN AFANYA ZIARA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAAFA YA MVUA, ZANZIBAR JANA

May 06, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na wasaidizi wake alipofika Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya hafla kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Hapa ni Mtaa wa Mwanakwerekwe ambapo pamefanyika shimo kubwa akama linavyoonekanwa kutokana na mvua iliyonyesha juzi na kupelekea uharifu ambao fedha nyingi zitatumika kufukia eneo hili pia Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea wakati alipofanya ziara ya makusudi leo kutembelea maafa mbali mbali yaliyotokea kutokana na Mvua hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed leo wakati wakati alipofanya ziara ya hafla ya kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed (kulia) wakati wakati alipofanya ziara ya hafla ya leo kutembelea Bwawa la Maji la Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia namana lilivyofurika Maji ya mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali kwa Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohamed Iddi (kulia) alipofika leo kuangalia maafa yaliyomkuta Bibi Mwanahamis Takrima Mohammed (aliyekaa) kwa kuvunjikiwa na nyumba yake kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (wa pili kulia) Mkuu wa Wilaya Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud.
Baadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingiliwa na maji ya mvua mkubwa iliyonyesha juzi na kepelekea hasara mbali mbali kwa Wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa ziwa hilo ambapo leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea na kuona hasara zilizotokea akiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud wakati alipotembelea baadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingia na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kepelekea hasara mbali mbali, katika ziara hiyo Mhe, Rais alifuatana na Viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimfariji Bibi Fatma Abdalla Turufino Mkaazi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.(Picha na Ikulu.)

WANANCHI NA TAASISI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WANAPOTAKA KUPIMA MAENEO YAO YA ARDHI KUEPUKA KUTAPELIWA

May 06, 2015

Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalam wa Upimaji na Ramani wa wizara hiyo wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro na kubainika kuwa chini ya kiwango.
Wataalam wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifanya uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani lililopimwa chini ya kiwango. Katikati (aliyesimama) ni Bw. Bernard Malugu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro iliyoifanya kazi hiyo chini ya kiwango.
Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Huruma Lugalla (kushoto) akifuatilia moja ya eneo ambalo lilitakiwa kuwa na alama ya mpaka ambalo halikuwa na alama yoyote wakati wa uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani iliyopimwa na Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro ambayo ilibainika kuwa chini ya kiwango. Kulia ni Bw.Allex Kachoka Mpima Ardhi wa wizara hiyo.
Moja ya alama ya mpaka ya ambayo iligundulika kujengwa chini ya kiwango wakati wa uhakiki uliofanywa na wataalam wa Wizara ya Ardhi kwenye moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani.Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) ya Morogoro ambayo ilipewa kazi ya Upimaji wa eneo hilo imeifanya kazi hiyo chini ya kiwango.
Wapima Ardhi na Mipaka wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiendelea na zoezi la uhakiki wa alama za mipaka kwa kutumia kifaa kiitwacho Hand Heled GPS kwenye moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze,Bagamoyo Pwani.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeto tahadhari kwa Taasisi na wananchi wanaotaka kupimiwa maeneo yao ya ardhi kuhakikisha kuwa wanafuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia masuala ya upimaji wa ardhi ili kuepuka kupata hasara na kuingia kwenye migogoro ya ardhi isiyo ya lazima kutokana na kutumia watu au makampuni yasiyosajiliwa kishera.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya makampuni yanayojishughulisha na upimaji wa Ardhi na ramani kugundulika kufanya kazi za wateja wao chini ya viwango kufuatia ramani zilizowasilishwa na makampuni  hayo  wizarani hapo kwa ajili ya kuidhinishwa kukosa sifa pindi zinapofanyiwa uhakiki na wataalam wa wizara hiyo. 

Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani vijijini wa wizara hiyo Bw. Huruma Lugalla akizungumza mara baada ya timu ya wataalam wa wizara hiyo kufanya uhakiki wa moja ya ramani ya eneo linalopaswa kuwa la makazi ya watu na taasisi nje kidogo ya mji wa Chalinze, Bagamoyo mkoani  Pwani ambalo  upimaji wake umekiuka kanuni na taratibu amesema Serikali haitayafumbia macho makampuni yote yanayochukua fedha za wananchi na Taasisi na kisha kufanya upimaji usiokidhi viwango vilivyowekwa na wizara hiyo kwa mujibu wa Sheria.

Amesema wizara hiyo itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuyafungia   makampuni yote yanayobainika kufanya kazi chini ya kiwango, kukiuka kwa makusudi taratibu za upimaji wa ardhi na kufanya uzembe wa kushindwa kuweka mipaka na alama sahihi za maeneo wanayoyapima jambo linalochangia mivutano na migogoro pindi maeneo husika yanapogawiwa kwa wananchi.

“Nawaomba wananchi na Taasisi mbalimbali zinazotaka kupimiwa maeneo yao kwa kutumia makampuni kuwa makini na kuchukua tahadhari ili kuepuka hasara ya kulipa gharama za upimaji mara mbili, msichukue watu wa kati au kampuni zisizosajiliwa kisheria  ambazo haziko kwenye orodha ya Katibu wa Baraza la Taifa la Wapima Ardhi” Amesisitiza.

Bw. Lugalla ameeleza kuwa Kampuni ya Intergrated Property Consultancy and Services (IPCS) kutoka Morogoro iliyohusika na  zoezi la upimaji na ramani katika eneo hilo haikufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria kufuatia ramani iliyowasilishwa na Mkurugenzi wake Bw. Bernard Malugu wizarani hapo kushindwa kukidhi vigezo vya ubora unaotakiwa mara baada ya kuhakikiwa na wataalam wa Upimaji na ramani wa Wizara. 

Amesema wataalam wa upimaji na ramani wa Wizara hiyo mara baada ya kufanya  uhakiki wa eneo hilo wamebaini   ukosefu wa alama (bikoni) za baadhi viwanja, kukosekana kwa pini za kugawa viwanja na tofauti umbali wa eneo la kiwanja kimoja hadi kingine iliyokuwepo kwenye ramani ambayo haikuendana na uhalisia wa eneo husika wakati wa zoezi la uhakiki.

 Aidha, amebainisha kuwa ramani ya eneo hilo ilisainiwa kimakosa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kufuatia kampuni yake  ambayo imesajiliwa kisheria dhamana  kuamua kumtafuta mtu wa kati wa kuifanya kazi hiyo badala yake na kisha Mkurugenzi wake Bw. Bernard Malugu kuidhinisha ramani hiyo kwa kuisaini huku ili ipelekwe wizarani kupatiwa kibali huku akijua wazi kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo hazimruhusu kutoa kazi kwa mtu au kampuni nyingine. 

“Ili kuepusha migogoro ya ardhi inayoweza kutokea katika eneo lile taratibu zitafuatwa ili kampuni hiyo iifanye kazi ile upya kwa gharama zake na kisha kuwaita wataalam wa wizara kufanya uhakiki upya ili kujiridhisha kabla ya kutoa kibali cha viwanja hivi, Sisi kama wizara hatutakubali kuendelea kulaumiwa na wananchi kwa uzembe unaofanywa na makampuni haya” Amesisitiza. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya IPCS iliyopewa kazi ya kupima eneo hilo akitoa utetezi kwa kampuni yake mara baada ya kufanyika kwa uhakiki huo alikiri kuwa kampuni yake imefanya  makosa na kukiuka sheria, miiko na maadili yanayosimamia shughuli za upimaji na ramani nchini.
Amesema  yeye kama Mkurugenzi wa kampuni hiyo alisaini ramani ya eneo hilo Machi 19, 2015 kimakosa hivyo kampuni yake  imeonyesha uzembe na udhaifu wa usimamizi ikiwemo yeye mwenyewe kutomfahamu mtu wa kati aliyeifanya kazi hiyo.

Aidha, amesema kampuni yake iko tayari kuyabeba mapungufu yote yaliyojitokeza na kukubali kurudia kazi ya kupima na kuweka mipaka iliyokosekana endapo itaruhusiwa na wizara hiyo kufanya hivyo.

Wajumbe wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar wawafariji waloiathirika na mvua

May 06, 2015

WAJUMBE wa Sekreatrieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya (NEC) ya CCM, jana walitembelea maeneno yaliyofikwa na mafuriko ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo la kuangalia na kuwafariji wananchi walioathirika na mkasa huo.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wao, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai, wajumbe hao wa Sekreatrieti walitembelea maeneo mbali mbali mkoani humo ikiwemo Mpendae kwa Binti Amrani, Tomondo na Mwanakwerekwe, ambayo yalikumbwa na kadhia hiyo.
Walitumia nafasi hiyo kuwafariji baadhi ya wananchi waliathirika na mafuriko hayo, ambapo baadhi nyumba zimejaa maji na nyengine kuanguka kuta zake, na kusabababisha hasara kubwa.

Wajumbe hao wamewataka wale wote waliokumbwa na janga hilo, kuwa na moyo wa subra na kuiachia Serikali kupitia kitengo cha maafa kutafakari na kuona nini la kufanya. Aidha, wametoa wito na haja kwa jamii nzima ya Wazanzibari kuchukua tahadhari hasa wakati huu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha.

Mvua hiyo kubwa iliyonyesha kwa muda wa masaa matatu mfululizo, kuanzia saa 3:30, iliwafanya wananchi wa Manispaa ya Zanzibar na vVitongoji vyake kushindwa kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.







MEYA MWENDA WA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA AFRIKA

May 06, 2015

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.

Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.

Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities).

Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).

Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.

Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.

Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana. Mwingine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty pamoja na watendaji wengine wakifuatilia kwa makini wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa amenyanyua Tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Marekani 100,000 kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kumkabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA) kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
SHAMRA SHAMRA ZA MAANDAMANO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI ZILIVYOFANA MJINI MUSOMA

SHAMRA SHAMRA ZA MAANDAMANO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI ZILIVYOFANA MJINI MUSOMA

May 06, 2015
DSC_0056
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi mkoani Mara wakijiaanda kuanza maandamano kutoka Hospitali Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Musoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
DSC_0060
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi wilayani Musoma wakiwa wamekusanyika nje ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma kwenye viwanja vya Mkendo, mkoani Mara.
DSC_0083
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga kutoka mikoa mbalimbali ya nchini wakijumuika na wenyeji wao kwenye maandamano ya maadhimisho hayo.
DSC_0086
DSC_0103
Baadhi ya Wakunga wakijumuika na wakinama wa mjini Musoma njiani kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo wakati maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakishereheshe maandamano hayo.
DSC_0108
Wakunga wa kiume kutoka wilaya ya Serengeti wakiwa wamejumuika na wenyeji wao kwenye maandamano hayo.
DSC_0127
DSC_0136
Shangwe zikiendelea kuelekea viwanja vya Mkendo.
DSC_0153
Kinababa nao hawakubaki nyuma waliwaunga mkono Wakunga kwenye maandamano hayo.
DSC_0161
Mkazi wa mjini Musoma mwenye ulemavu aliyejumuika kwenye maandamano hayo akisukumwa na mmoja wa Wakunga kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo zinakofanyika sherehe za maadhimisho hayo.
DSC_0164
DSC_0177
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige naye alishiriki maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma mkoani Mara.
DSC_0180
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) Tanzania, Sawiche Wamunza (wa kwanza kulia) akishiriki kwenye maandamano hayo.
DSC_0185
DSC_0222
Mpiga picha wa Clouds TV Ntibashima Edward akiwa amepanda juu ya gari aina ya canter kwa ajili ya kuchukia matukio ya maandanamano hayo.
DSC_0289
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) wakipokea maandamano kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mjini Musoma, Mkoani Mara. Kutoka kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali, Dk. Ama Kasangala, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Musoma, Stephen Zelote pamoja na Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Bi. Feddy Mwanga.
DSC_0275
Maandamano kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yakiwasili kwenye viwanja vya Mkendo na kupokea na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) yakitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma.
DSC_0285
DSC_0293
DSC_0300
DSC_0304
DSC_0307