WAZIRI MAKAMBA AWASILI ARUSHA NA KUTEMBELEA WILAYA YA MERU

March 27, 2017
 Faida ya Hifadhi endelevu ya Mazingira. Pichani ni eneo la Ngaresero Wilaya ya Meru ambapo kuna uhifadhi mzuri wa mazingira. Hata hivyo eneo hilo limeanza kuvamiwa na wananchi kwa shughuli za kibinadamu na kuhatarisha uhai wake. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo na kumtaka Bw. Timoth Leach mmiliki wa Ngaresero Mountain Lodge kufanya ukaguzi wa mazingira mara moja ili kubaina matumizi sahihi ya rasilimali maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Edward Moringe Sokoine. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha na alitembelea  msitu wa Enguiki na Lendikinya kisha alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

DC GONDWE APOKEA VIFAA VYA MICHEZO TOKA ZIZZOU FASHION

March 27, 2017
BCO
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea sehemu ya vifaa vya michezo kutoka kwa Mdau Mkubwa wa Michezo nchini, Athuman Tippo maarufu kama Zizzou, kwa ajili ya kuhamasisha Michezo kwa vijana wa Wilaya hiyo, kupitia Kampeni ya Michezo kwa vijana ya Uchumi Cup iliyoianzisha DC Gondwe kwa ajili ya kuwahamasisha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia fursa ya Michezo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Duka la Vifaa vya Michezo la Zizzou Fashion, Sinza Jijini  Dar es salaam.
Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA JUMUIYA YA WANAWAKE WALIOJIAJIRI (SEWA) KUTOKA INDIA

March 27, 2017
ABO Mh Makamu wa Rais akipokea taarifa ya ziara kutoka kwa Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala pamoja na Pushpa Rathod – SEWA


Makamu wa Rais baada ya kuvishwa alama ya heshima kwa mila za Kihindi kutoka kwa Pushpa Rathod


“Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong,wa pili kutoka kulia mwenye suti katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassa, Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania.


SEWA – “Self Employed Women Association” ni Jumuiya ya Wanawake Waliojiajiri ambayo miongoni mwa viongozi wake wakuu ni Bi. Renana Jhabvala (Chair Women in Informal Employment WIEGO.
Aidha, Bi Renana na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Jopo la Juu Duniani katika Kuwezesha Wanawake Kiuchumi chini ya Umoja wa Mataifa.
Ushirikiano wa viongozi hawa unandelea kuleta mafanikio makubwa kwa Wanawake hasa wa ngazi ya chini hapa Tanzania.
Baada ya ujumbe huo kutua Tanzania tangu tarehe 21 – 26 Machi, 2017, wanawake wa Zanzibar na Tanzania Bara wamepata mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali. Taasisi zilizoshiriki ni TEWO SACCOS, JUWABIKA, UWAKE, BACCA, BAMITA na MKUDUWODEA.
Mhe. Makamu wa Rais baada ya kukutana na ujumbe huo tarehe 27/3/2017 ukioongozwa na “Deputy High Commissioner” India Bw. Robert Shetkintong, akiongozana na Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala, Pushpa Rathod , Sophia Kinega kiongozi wa wanawake waliojiajiri na Mhe. Siriel Mchembe msaidizi wa Mama Samia kwenye jopo la juu la dunia katika kuwezesha wanawake kiuchumi amekubali kuanzisha Jumuiya hiyo hapa Tanzania.
Mchakato wa kuanzisha Jumuiya ya wanawake waliojiajiri India na Tanzania (SEWA) unaanza mara moja chini ya ulezi wake.Wanawake waliojiajiri Tanzania hongereni kwa kupata sauti Duniani.

MWANAHABARI GEORGE BINAGI WA LAKE FM MWANZA AUAGA UKAPELA

March 27, 2017
Jana March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.

Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.

"Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. 

Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani, hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.

BMG inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za kanisani.

PROFESA MUHONGO ASAINI LESENI ZA MADINI

March 27, 2017
Na Veronica Simba – Dodoma

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesaini leseni za madini kutoka kwa wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kutimiza taratibu zote zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Leseni ya kwanza iliyosainiwa ni ya uchimbaji wa kati wa dhahabu katika eneo la Masagalu, Handeni yenye namba ML 570/2016. Leseni hiyo imehamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investments Tanzania Ltd.

Aidha, Waziri Muhongo alisaini leseni namba ML 572/2017 ya Sisti Mganga. Leseni hiyo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo la Itiso, Chamwino mkoani Dodoma.

Leseni nyingine iliyosainiwa na Waziri Muhongo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi aina ya kokoto, ambayo mmiliki wake ni Said Abdallah. Leseni hiyo namba ML 573/2017 ipo eneo la Chipite, Masasi.

Profesa Muhongo aliwataka waombaji na wamiliki wote wa leseni za madini nchini, kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo taratibu zote kama zilivyobainishwa katika Sheria ya Madini ikiwemo ulipaji wa mrabaha na kodi mbalimbali, kujenga mahusiano mema na jamii zinazowazunguka pamoja na kuzingatia utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Zoezi hilo la utiaji saini lilifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma na kushuhudiwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisaini leseni za madini za wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa. Anayeshuhudia ni Mwanasheria wa Wizara, Khadija Ramadhan.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia), akikabidhi leseni iliyohamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investment Tanzania Ltd.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia), akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo la Itiso – Chamwino kwa mmiliki wake Sisti Mganga. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Rayson Nkya.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG), IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

March 27, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya  Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016, kutoka kwa CAG  Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 . Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hizo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hizo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU