MATUKIO KATIKA PICHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MEATU

MATUKIO KATIKA PICHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MEATU

October 09, 2016
o1
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt  Seif Shekalaghe kushoto akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu Kulia  Mhe. Elieza Chilagali katika kata ya  Kobondo wilayani Meatu mkoani Simiyu mwishoni mwa wiki.
o2
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkimbiza mwenge kitaifa kutoka kwa Bw. James Sadick Munguji kutoka Simiyu, katika Mbio za Mwenge Wilayani Meatu mwishoni mwa wiki.
o3
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  (kushoto) kulia ni kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bw. George Jackson Mbijima na wajumbe wengine wakimsikiliza Bi Regina Anthon katikati alikyeshika kipaza sauti ambaeni ni katibu wa kikundi cha lishe cha mshikamao wilayani Meatu, wakati wa maonyesho ya shughuli za kikundi hicho baadaya kuupokea Mwenge wa Uhuru katika mji mdogo wa Mwandoya jimboni Kisesa.
o4
Katika Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kushoto kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bw. George Jackson Mbijima na wajumbe wengine pichani wakisikiliza ripoti ya nidhamu katika Eneo la Nyakanja jimboni Kisesa Wilayani wakati wa Mbio za mwenge mwishoni mwa Wiki. (Picha zote na Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais)

TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA LAFANA.

October 09, 2016
Jana Jumapili Oktoba 09, 2016 kuanzia majira ya saa nane mchana hadi saa 12 jioni kulifanyika Tamasha Kubwa la Kusifu na Kuabudu, katika Kanisa la Kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mamia ya watu/waumini walijitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo hakika lilifanya na kugusa nyoyo za wengi.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani) alielezea kufurahishwa na tamasha hilo na namna lilivyofana huku akisisitiza wanadamu kuwa na desturi ya Kusifu na Kumuabudu Mungu kwani kupitia ibada hiyo, milango ya mbinguni hufunguka.
Na BMG
Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili hususani za kusifu na kuabudu, Yusuph Nghumba, akiimba katika tamasha hilo. Kulia ni mkewe. 

Licha ya kwamba mwimbaji huyo anakabiriwa na tatizo la kutoona lililomkumba ghafla ukubwani, lakini bado anamsifu na kumuabudu Mungu katika roho na kweli na anaendelea kubarikiwa licha ya jaribu hilo la kimwili kwani ipo siku atauona ukuu wa Mungu.
Wa pili kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili hususani za kusifu na kuabudu, Yusuph Nghumba, akiimba katika tamasha hilo. Wa pili kulia ni mkewe na wa kwanza kushoto ni mmoja wa watoto wao. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana kanisa la EAGT Lumala Mpya ambaye pia ni mwimbaji mahiri wa kusifu na kuabudu.

Licha ya kwamba mwimbaji huyo anakabiriwa na tatizo la kutoona lililomkumba ghafla ukubwani, lakini bado anamsifu na kumuabudu Mungu katika roho na kweli na anaendelea kubarikiwa licha ya jaribu hilo la kimwili kwani ipo siku atauona ukuu wa Mungu.
Praise and Worship Team kutoka Kanisa jirani la CAG Sabasaba Jijini Mwanza, wakihudumu kwenye tamasha hilo.
Praise and Worship Team kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Jijini Mwanza, waliokuwa wenyeji wa tamasha la Kusifu na Kuabudu, wakihudumu.
Mamia ya waliohudhuria tamasha hilo, wakimsifu Mungu 
Praise and Worship Team kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Jijini Mwanza, waliokuwa wenyeji wa tamasha la Kusifu na Kuabudu, wakihudumu.
Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (mwenye suti) akiungana na waumini wengine kumsifu Mungu kwa roho na kweli.
Mmoja wa waimbaji mahiri kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya akihudumu kwenye tamasha la Kusifu na kuabudu lililofanyika jana kwenye kanisa hilo.
Mwenyekiti wa Vijana kanisa la EAGT Lumala Mpya ambaye pia ni mmoja wa waimbaji mahiri wa kusifu na kuabudu akihudumu kwenye tamasha hilo.
Wote wanaomsifu na kumuabudu Mungu kwa roho na kweli, hubarikiwa
Hakika Tamasha la Kusifu na Kuabudu lilifanya sana ndani ya Kanisa la Kimataifa la EAGT Lumala Mpya hivyo usikose tamasha lijalo ambalo utajuzwa pia kupitia mtandao huu.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi.

+SAUTI: BAADA YA NYASA BOY KUTOKA JIJINI MWANZA KUFANYA KAZI NA SAJNA, APATA NAFASI YA KUFANYA KAZI NA BARAKA DA PRINCE.

October 09, 2016
Nyasa Boy si jina geni miongoni mwa wasanii chipukizi kutoka Jijini Mwanza. Alianza kujulikana Jijini Mwanza mwaka mmoja uliopita baada ya kufanya kazi na Mc Darada, iliyoita Chongoroa.

 Mwaka huu 2016 ameachia wimbo mpya uitwao Mapenzi Nivute aliofanya na Sajna. Wimbo huo umefungua milango mipya kwani baada ya Baraka Da Prince kuusikia, hakusita kukubali kufanya kazi na Nyasa Boy ambaye anatokea kundi la Tanzania One la Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kusikiliza ama bonyeza Play hapo chini.
Kwa maswali/ Ushauri wasiliana nasi kwa nambari 0768175985

WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA KAMPENI YA FAHARI YA TANZANIA NA UTOAJI TUZO KWA CHAPA BORA 50 ZA KITANZANIA MLIMANI CITY DAR

October 09, 2016
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage(MB) akimkabidhi Tuzo ya  Chapa bora  Bi. Mercy Kitomary ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Nelwas Gelato katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na TPSF Mlimani city jijini Dar es Salaam Oktoba 7 2016. Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte na Kaimu Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Egid Mabofu. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogs).

Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.

Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.

Tuzo

Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.

Makamu Mweyekiti wa TPSF, Salum Shamte akiongea kumkaribisha mgeni Rasmi, Mhe. Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais kuzungumza, kuzindua kampeni ya Fahari ya Tanzania na kutoa Tuzo za Chapa bora 50 za Kitanzania kwa mwaka 2016.

Mshereheshaji, katika Uzinduzi wa Fahari ya Tanzania na Utoaji wa Tuzo za Chapa bora 50 za Kitanzania Bw.  Taji Liundi akiwa mimbarini.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Superdoll Bw. Seif  Seif akiwa na timu nzima ya wafanyakazi waandamizi wa Superdoll wakifuatilia kwa makini Shugjuli nzima ya Uzinduzi wa Kampeni ya Fahari ya Tanzania na utoaji wa Tuzo wa Chapa Bora 2016

Meza ya Washirika wakubwa CRDB Bank iliongozwa na Bi Tully Esther Mwambapa Mkurugenzi wa Utafiti,Masoko na Huduma kwa Kwa Wateja akiwa na timu yake wakifuatilia kwa makini Shughuli ya
 Uzinduzi wa Kampeni wa Fahari ya Tanzania na Utoaji wa Tuzo wa Chapa bora 50 za Kitanzania

MBUNGE WA CHALINZE AKABIDHI MAGODORO 200 KWA SHULE YA MORETA

October 09, 2016
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani  Kikwete akikabidhi  magodoro kwa wanafunzi na mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Moreto ,Justine Lyamamu ,ambapo  bweni la  wasichana katika shule hiyo liliungua wiki iliyopita.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya chalinze, Mkurugenzi na maafisa wengine wa halmashauri ya Wilaya Chalinze.
Mbunge wa chalinze ametimiza ahadi yake ya kuchangia magodoro 200 na Halmashauri ya wilaya ya chalinze kwa shule ya Sekondari ya Moreto.
Mbunge akisema neno la ushauri na kuwatia moyo vijana kwa tukio lililowakuta na kwa utulivu uliotokea.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Moreto  iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo, Mwanahamis Msonde na Sekion Mponela wakimshukuru Mbunge wa jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete na mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi  Zikatimu kwa msaada wa magodoro. Na Mwamvua Mwinyi.
 
 
MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze,wametoa magodoro 200  yaliyogharimu zaidi ya mil.8 ili kuwasaidia wanafunzi wa shule ya sekondari ya Moreto iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo.
 
Aidha Ridhiwani ameahidi kushirikiana na wadau pamoja na halmashauri hiyo,kujenga bweni jipya la wanafunzi wa kike,shuleni hapo baada ya kuunguliwa na bweni wiki iliyopita.
Sambamba na hayo tathmini imebaini hasara ya sh.mil 74 baada ya bweni hilo kuungua  na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.
 
Akikabidhi magodoro hayo ,kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo,Justine Lyamuya ,mbunge huyo alisema kati ya magodoro hayo 136 yatatumiwa na wanafunzi wa kike na yatakayobaki yatatumika na wanafunzi wa kiume.
 
Ridhiwani alisema mara baada ya kutokea kwa janga hilo, alitoa magodoro 50 yenye thamani ya mil.2.2 kwa nguvu zake mwenyewe.
 
Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kushirikiana na serikali na vyombo vya dola kuwafichua waliohusika na tukio la kuchoma moto bweni.
 
Ridhiwani alielezea kuwa serikali itahakikisha waliohusika kuchoma moto bweni hilo,wanatafutwa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Alisema tukio hilo linasikitisha na kurudisha nyuma juhudi za serikali na wadau mbalimbali wa elimu wanaohakikisha  wanafunzi wanakaa bweni .
 
“Tumeweka mikakati ya kuhakikisha tunawakamata wale wote waliohusika na tukio hili baya na matukio haya ni mwendelezo wa uunguzaji wa shule ambapo Chalinze imechomwa mara mbili,” alisema Ridhiwani.
 
Ridhiwani aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushirikiana kutatua changamoto zilizojitokeza shuleni humo.
 
Nae  mwalimu mkuu wa shule hiyo Justine Lyamuya alifafanua kuwa vitu vyote viliungua ikiwa ni pamoja na vitanda na magodoro 75 vyenye thamani ya mil. 24.
 
Alisema bweni hilo lilijengwa hivi karibuni kwa thamani ya mil.50 ambalo limeungua lote na halifai tena kutumika.
 
“Moto huo uliunguza vitu vyote vilivyokuwemo ikiwepo magodoro, vitanda 75, madaftari, vitabu, nguo na vifaa vingine lakini mungu alisaidia kati ya wanafunzi 196 wanaolala bweni hili,hawakuwepo bwenini,” alisema Lyamuya.
 
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze,Said Zikatimu alisema licha ya kuchangia magodoro hayo tayari wameitisha kikao na wazazi, walezi na wadau wa elimu ili kujadili namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
 
Baadhi ya wanafunzi Sekion Mponela na Mwanahamis Msonde walimshukuru mbunge wa Chalinze na halmashauri kwa msaada walioutoa na kuahidi kutunza magodoro hayo.
 
Octoba 5 mwaka huu majira ya asubuhi moto ulizuka katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni humo na kusababisha hasara kubwa.

BENKI YA NMB TAWI LA MLIMANI CITY YAWAFARIJI WATOTO YATIMA WA MAKAO YA CHAKUWAMA, SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

October 09, 2016
 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Urio 
akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo  cha Yatima cha Chakuwama kilichopo Sinza wakati wa hafla fupi ya kutoa msaada iliyofanyika Dar es Salaam leo.
 Katibu Mtendaji wa Kituo hicho, Hassan Hamisi (kulia), akitoa historia fupi ya kituo hicho.
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakiwa wamewabeba watoto katika hafla hiyo.
Mfanyakazi bora wa benki hiyo, kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba, Amani Mgweno akishiriki kubeba zawadi za watoto hao.
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kushoto), akishiriki kutelemsha zawadi hizo kutoka kwenye gari.
Zawadi zikiendelea kutelemshwa.
Zawadi zikitelemshwa. Kulia ni mtoto wa mfanyakzi wa benki hiyo, Asha Mayuva, akionesha upendo kwa watoto wenzake kwa kuwapelekea zawadi.
Wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa wamewabeba watoto mapacha wanaolelewa katika kituo hicho.
Zawadi zikipangwa. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Seka Urio, Asha Mayuva, Raphael Mlute na Magreth Lwiva. ' Hapa ni Kazi Tu kwa kwenda'
Taswira ya keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ' Hakika NMB Tawi la Mlimani City mmeonesha upendo wa hali ya juu kwa watoto hao barikiweni sanaaa'
Mwonekano wa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na watoto hao.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa kwenye hafla hiyo fupi.
Hapa ni furaha tupu.
Hapa ni nani kama baba?
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ikikatwa.
Hapa ndipo unapoweza kuutambua utamu wa keki.
"Hapa ni kama wanafikiria sijui tuondoke na mtoto huyu"

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB Tawi la Mlimani City imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Makao ya  Kulea Watoto Yatima ya Chakuwama yaliyopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni  moja ya njia ya kujumuika na jamii inayo wazunguka.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo ambao ni vyakula na vifaa vya shule kwa ajili ya wanafunzi Meneja wa benki hiyo wa tawi hilo, Seka Urio alisema ni kawaida kwa benki hiyo kushiriki shughuli za kijamii na kutoa faida wanayoipata kwa wananchi ambao ndio wateja wao.

"Tunajisikia faraja kutoa vitu vichache kwa watoto wetu ambao mnawalea katika kituo hiki pia ni kurudisha faida tunayoipata kwa jamii" alisema Urio.

Urio alisema vitabu vyote vya dini vinaelekeza kuwajali na kuwafariji wenzetu wenye uhitaji ikiwa ni agizo lake mwenyezi mungu.

Katibu wa Kituo hicho, Hassan Hamisi alisema kituo hicho chenye watoto 60,000 wakike wakiwa 25 na kiume 35 tangu kianzishwe kwake mwaka 1998 kimepata mafanikio ya kupata nyumba yao ya kuishi watoto hao, malezi huduma za elimu na afya.

"Kwa kweli tukiangalia tulipoanzisha kituo hiki na sasa tumepiga hatua licha ya kuwepo changamoto kwani tunasomesha watoto katika shule mbalimbali za sekondari na msingi na wengine wapo vyuo vikuu ni jambo la kujivunia" alisema Hamisi.

Alisema watoto wengine wamepata kazi baada ya kuhitimu elimu katika ngazi mbalimbali na baadhi yao wameoa na kuolewa na sasa wanaendesha familia zao.

Hamisi alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuanzisha utaratibu wa wanafunzi kupata elimu bure kwani umewapunguzia changamoto ya kuwalipa ada wanafunzi 47 wanao walea katika kituo hicho.

Hamisi alisema pamoja na kupiga hatua bado wanachangamoto mbalimbali kama chakula na nyumba kwani kila siku watoto wamekuwa wakiongeza katika kituo hicho kutokana na migogoro ya kifamilia, wazazi au walezi kufariki na kuwaacha watoto na watoto kutelekezwa hivyo akawaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia kama ilivyofanya benki hiyo.

Hafla hiyo ilihudhuria na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo waliwafariji watoto yatima kwa kuwapa vitu mbalimbali na kuzungumza nao ambapo waliwasisitizia kuzingatia masomo.