SPIKA WA BUNGE MH. JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI LEO

SPIKA WA BUNGE MH. JOB NDUGAI AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI LEO

February 29, 2016

J1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai akizungumza na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hawapo pichani kutoka Tanzania wakati walipomtembelea katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es salaam na kumpa salaam maalum za kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake na watanzania na kuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano ikiwa ni pamoja na kupongeza utendaji kazi wake kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
J2
Baadhi ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutoka kulia ni Mh. Adam Kimbisa, Mh. Shy Rose Banjhi na Mh. Abdallah Mwinyi wakizungumza na Spika wa Bunge.
J3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Job Ndugai kulia akizungumza na wabunge hao.
J5
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa ofisi ya Bunge Bw. Josey Mwakasyuka akijitambulisha katika mkutano huo.
J7
Mh. Shy Rose Banjhi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kushoto ni Afisa habari wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya.
POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA SONGEA

POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA SONGEA

February 29, 2016

01
Mmoja wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa na serikali  akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Baadhi ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na Mipango Posta  jijini Dar es salaam.
2
Wanafunzi hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila kibali kwenda kumuona  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
3
Wanafunzi hao wakitoka mbio baada ya kuamriwa na polisi kuondoka eneo hilo na kutawanyika.
4
Askari polisi wakizunguka maeneo mbalimbali kuangalia hali ya usalama.
5
Polisi wakiwazuia wanafunzi hao na kuwaamuru kutawanyika kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
6
Mmoja wa polisi akiwaamuru wanafunzi hao kutawanyika eneo hilo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI KILIMANJARO

February 29, 2016

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.

Mhe. Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.

Vilevile, Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha. 

Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
Jiwe la msingi likiashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga (kulia) na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na viongozi na wataalamu aliombatana nao kwenye ziara yake kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Inj. Ruth Koya akimuonyesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge moja ya miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo, Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI

February 29, 2016
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.
“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.
Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)
dk kigwa
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
dk hk 888Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
dk hk55Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Kigwangalla akitoa maagizo
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
dk hkna
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
dk kigwa
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
dk hk iio
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
dk hk67
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).
HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI (AUDIO)

HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI (AUDIO)

February 29, 2016
Imeelezwa kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji ya mtoto.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
Dkt. Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.
Amesema kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine kama uji na maji.
“Hali sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema Dkt. Kaganda.
Aidha Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama yake.
Nae Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama.
Alisema watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.
“Watoto wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,” alisema Bi. Zaman.
Alisema baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.
Katika makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog
DSC_0599Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
DSC_0630Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
DSC_0622Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
DSC_0654Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
DSC_0655Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet linalohusika na kuandika habari za afya.
DSC_0661Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0665Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
DSC_0674Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0696Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
DSC_0711Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha hiyo.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA WARSHA YA PILI YA KIMATAIFA YA UNESCO MKOANI TANGA LEO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA WARSHA YA PILI YA KIMATAIFA YA UNESCO MKOANI TANGA LEO

February 29, 2016

su1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.(Picha na OMR)

BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

February 29, 2016
Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna  


Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.

Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya  Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .

Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .

Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa  nje kusbiri utaratibu mara baada  waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.Picha na David Nyembe