RC SHIGELLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA 47 LA WAFANYAKAZI WA TANESCO NCHINI MJINI TANGA LEO

October 05, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua Baraza kuu la 47 la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Tanga kulia ni Katibu wa Baraza hilo,Asmaa Myale

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco) Dkt  Tito Mwinuka akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi huo uliofanyika mjini Tanga 
Mwenyekiti wa Tuico Taifa,Paul Sangeze akizungumza wakati wa Baraza hilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,Dkt Tito Mwinukakatika mkutano huo uliofanyika mjini Tanga
Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Dkt Tito Mwinuka  na Mwenyekiti wa wa Tuico Taifa,Paul Sangeze


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akipongezwa na Mwenyekiti wa Tuico Taifa,Paul Sangeze mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza kuu la 47 la wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) leo mjini Tanga anayeshughudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka  kushoto ni Katibu wa Baraza kuu la wafanyakazi,Asmaa Myale

 Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakiufuatilia kwa umakini

Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa umakini mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Tanzania,Leila Muhaji wa pili kushoto aliyevaa koti jeusi akichukua baada ya dondoo wakati Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella alipofungua Baraza Kuu la 47 la Wafanyakazi wa Tanesco nchini mjini Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kulia akitoa nje ya ukumbi mara baada ya kufungua baraza hilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Dkt Tito Mwinuka katikati ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze 

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Tanesco kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale mara baada ya kufungua mkutano wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi wa Tanesco
 Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo mara baada ya kufungua baraza kuu hilo
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dkt Tito Mwinuka kushoto akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza Kuu la 47 la Wafanyakazi wa Tanesco
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tenesco,Dkt Tito Mwinuka akiuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa baraza hilo leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella

Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale akizungumza na waandishi wa habari

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, yatoa msaada wa vifaa vya intaneti kwa shule za mkoa wa Njombekondari Njombe leo

October 05, 2017

Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga (kushoto) Mkuu wa wilaya Wanging'ombe Ally Kasinge Katikati) Mkuu wa shule ya Sekondari Njombe Benard William  wakikata utepe kufungua kufungua  darasa la kusomea wanafunzi kwa njia ya mtandao. Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ally Kasinge (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe akipokea kifaa cha kupokelea mawimbi ya intaneti kutoka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga,   msaada huo umtolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya Shule ya sekondari Njombe.

Mkuu wa Wilaya Wanging'ombe Ally Kassinge (wa pili kushoto) akipata maelekezo ya matumizi ya kompyuta zinazo tumia mtandao wa Intanet toka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga katika Darasa la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe, Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA OFISI ZA URATIBU ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

October 05, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika kikao wa watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Waziri Makamba amepata wasaa wa kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Luthuli.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri January Makamba mara baada ya kutembea Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo amefanya ziara ya kikazi kutembelea Ofisi za Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Katika Ziara hiyo Mhe. Makamba amepata fursa ya kuongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo na kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano zaidi baina yao.
Awali, akimkaribisha Waziri Makamba, Mratibu Mkuu Bw. Issa Mlingoti amemshukuru Waziri Makamba kwa kufika na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Elimu, ajira na fursa kwa pande zote za Muungano.
"Sisi tumefarijika sana kwa ujio wako na tunategemea kuwa huu ni mwanzo na mwelekeo mzuri wa kuzidi kuimarisha mashirikiano baina yetu ikiwa sisi ni waratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" Alisisitiza Bw.Mlingoti
Katika ziara hiyo Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.

DC MTATURU AKEMEA VIASHIRIA VYA MGOGO WA WAKULIA NA WAFUGAJI

October 05, 2017

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itigi, Kata ya Itigi waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Damwelu Kata ya Ipande.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji na Kata ya Kitaraka
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwasili Kijiji cha Damwelu Kata ya Ipande kwa ajili ya mkutano wa hadhara na wakulima na wafugaji.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya serikali wakati wa Mkutano wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Na Mathias Canal, Singida

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekemea vikali viashiria vya mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo ya malisho na mashamba vinavyoanza kuchipuka na kuibua hisia za sintofahamu.

Migogoro ya wakulima na wafugaji huanza kwa majibizano ya mara kwa mara kati ya wananchi wenyewe kwa kuingiliana katika maeneo yao jambo ambalo likipuuzwa ingali dogo hukomaa na kupelekea serikali kutumia nguvu nyingi katika kulimaliza.

Akizungumza na wakulima na wafugaji kwenye ziara ya kikazi katika vijiji korofi vinavyochagiza mgogoro huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuacha haraka kuibua hasira baina yao jambo ambalo linawezekana kutatulika.

Aliwataka wakulima ambao wamevamia katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kuondoka haraka katika maeneo hayo na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya kilimo kwani endapo kama watakiuka maelekezo hayo serikali itachukua hatua dhidi yao.

Aliwataka wakulima hao waliovamia maeneo hayo kufika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji ili kubaini kama wanastahili kupatiwa maeneo mengine kutokana na kukutwa katika maeneo hayo mara baada ya kuanzishwa sheria ya matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007.

Mhe Mtaturu alisema kuwa Mgogoro wa kimaeneo ya malisho na mashamba ambao umeanza kumea katika kipindi cha hivi karibuni Wilayani Manyoni unahusisha Vijiji jirani vya Itigi Mjini, Doroto na Damwelu vinavyochangia maeneo hayo.

Alisema kuwa ni lazima kila mwananchi kuwa wakala wa kuhifadhi na kutunza mazingira katika maneo yanayotuzunguka ikiwa ni pamoja na kutolima katika maeneo ambayo yamehifadhiwa au kupangwa kwa ajili ya mambo mengine.

Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kufatilia ili kubaini aliyetoa maeneo ya wafugaji kwa wakulima ili achukuliwe hatua za kisheria kwani jambo hilo lina dalili zote za rushwa na uhujumu wa maeneo.

Sambamba na hayo pia Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliwataka wananchi kuelekea msimu wa kulima mazao ya kipaumbele ambayo ni Pamba, Korosho, Chai, Kahawa na Tumbaku.

Aidha, alisema kuwa pamoja na mazao hayo ya kipaombele lakini wanapaswa kuongeza kasi katika kilimo cha mazao ya chakula na Biashara hususani mahindi, mtama, Dengu na zao la Alizeti.

Aidha, Mhe Mtaturu aliwashauri  wafugaji kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa kuuza na kununua au kujenga nyumba za kuishi ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kukidhi maeneo ya malisho yaliyopo.