DIAMOND PLATNUMZ, MZEE YUSUF WAAHIDI KUANGUSHA SHOO YA KUFA MTU DAR LIVE SIKUKUU YA X-MAS

DIAMOND PLATNUMZ, MZEE YUSUF WAAHIDI KUANGUSHA SHOO YA KUFA MTU DAR LIVE SIKUKUU YA X-MAS

December 24, 2014

Wanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mzee Yusuf (kushoto) wakipozi baada ya kufanya mahojiano na wanahabari leo.
Wanamuziki hao wakionyesha mbwebwe zao mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akihojiwa na wanahabari leo katika ofisi za Global Publishers Ltd tayari kwa Tamasha la Wafalme kesho, Dar Live.
Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akihojiwa na mwanahabari wa Channel Ten, Freddy Mwanjala.

Mzee Yusuf naye akihojiwa na Freddy Mwanjala wa Channel Ten.

Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd na Dar Live, Abdallah Mrisho (kulia) akielezea kwa wanahabari jinsi Dar Live walivyojipanga kwa ajili ya kuwapa burudani safi mashabiki hapo kesho.
Diamond akifurahia jambo na Mzee Yusuf aliyekuwa ‘busy’ na simu yake baada ya mahojiano.
WASANII mahiri nchini Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mzee Yusuf wamewaahidi mashabiki wa burudani hususani wa Jiji la Dar es Salaam kutokosa kesho katika Ukumbi wa Dar Live kushuhudia shoo ya kibabe inayotambulika kama Tamasha la Wafalme.
Wakiongea na wanahabari katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar, wakali hao wamesema wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya shoo hiyo itakayoacha historia katika pande za Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Naye Meneja wa Dar Live, Abdallah Mrisho amewataka mashabiki wa burudani kuhudhuria kwa wingi kesho katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live maana kila kitu kiko safi kuanzia ulinzi na huduma zote muhimu.
Shoo hiyo ya aina yake itaanza asubuhi kwa burudani za watoto ambapo kundi la sarakasi la Masai Worriors litahakikisha linatoa burudani ya nguvu kwa watoto wote kwa kuwapa staili mbalimbali za sarakasi na mazingaombwe.

Pia watoto wataburudika na michezo kibao kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza huku kila mmoja atakayehudhuria kurudi na zawadi kemkem nyumbani kwao.
Kiingilio cha Tamasha la Wafalme kitakuwa shilingi 10,000 kawaida wakati kwa VIP kiingilio kikiwa shilingi 20,000.
WOTE MNAKARIBISHWA!
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

December 24, 2014

tff_LOGO1 
Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara.
Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa kuanzia saa 10 jioni. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza
Januari 10 mwakani ndipo zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan Mwinyi), Simiyu vs Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).
Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma vs Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi vs Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.
Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwakani, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.
Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.
Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano hayo.
SDL KUTIMUA VUMBI KRISMASI
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayochezwa katika makundi manne tofauti inaingia raundi ya nne kesho (Desemba 25 mwaka huu) kwa mechi ya kundi C kati ya Kiluvya United na Abajalo itakayochezwa Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Mshikamano FC na Transit Camp yenyewe itachezwa keshokutwa (Desemba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Kundi A litakuwa na mechi Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) ambayo itazikutanisha timu za Ujenzi Rukwa na Mji Mkuu (CDA) kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Desemba 28 mwaka huu ni kati ya Mvuvumwa FC na Milambo SC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) kundi B litakuwa na mechi kati ya Arusha FC na Pamba (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha), na Mbao FC vs JKT Rwamkoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Kundi D siku ya Jumamosi hekaheka itakuwa kati ya Mkamba Rangers na Volcano (Uwanja CCM Mkamba), Njombe Mji vs Wenda FC (Uwanja wa Amani, Njombe) na Town Small Boys vs Magereza FC (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Ratiba ya michuano ya Taifa Cup Wanawake pamoja na msimamo wa SDL vimeambatanishwa (attached).

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii chachu ya Maendeleo Wilaya ya korogwe

December 24, 2014

Kikosi kazi maalum kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakiongea na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Bw.Lucas Mweri walimpotembelea leo ofisini kwake kwa ajili ya kufuatilia na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Bw.Lucas Mweri akielezea changamoto mbalimbali wanazopata kutoka katika Mfuko wa maendeleo ya Vijana ikiwemo fedhaza mkopo kuwa ndogo, kwa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake leo kufuatilia na kufanya tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Bw.Yohana Ngao akiongea na wajumbe wa kikundi cha HEKIMA walipowatembea leo katika kata ya Mazinde kujua changamoto gani wanakutana nazo tangu wapewe mikopo kutoka katika mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Sabitina Maneto akitoa maoni kwa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(hawapo Pichani),kuhusu jinsi ya kuboresha mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Kuufanya uwe bora zaidi uku akikazia pesa kwenda moja kwa moja kwenye SACCOS baada ya kuja kwenye vikundi.
Wajumbe wa kikundi cha HEKIMA kutoka kata ya Muheza wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembea leo ili kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikopo iliyokwishatolewa kwa kikundi hicho.
Mjumbe wa kikundi cha HEKIMA kata ya Mazinde Rashid Salum(mwenye shati la bluu),akiwaonyesha Mradi wa Matofali uliotokana na pesa za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana,Bw.Yohana Ngao ambae ni Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(katikati) na Afisa Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Wizara ya Korogwe Bw.Mhinzi.
Wajumbe wa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakiskiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu wa kikundi kisicho cha kiserikali-MOIDES(hayupo pichani),Bw.Nurdin Imam jinsi walivyotumia pesa walizopewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Bw.Yohana Ngao(wa kwanza kulia) akiskiliza maoni kutoka kikundi cha Nyota Alfajiri ambao wameanzisha mradi wa kutengeneza Matofali na kuuza Asali ambapo walichukua mkopo wa shilingi milioni mbili na kurudisha kiasi cha shilingi laki 732,000 wakiwa wamefata taratibu zote za kurudisha mkopo ndani ya mwezi mmoja.
Wajumbe wa Kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakiaangalia moja ya mradi wa matofali kutoka kikundi cha Nyota Alfajiri uliofanikiwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.Kikundi hicho kimetengeneza matofali elfu kumi na nne(14,000) na wanajiandaa kuyauza ili kujiendeleza kimaisha.

DK. SHEIN ATOA VIFAA VYA MCHEZO WA RIADHA LEO

December 24, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwapa mawaidha yake mafupi viongozi wa mchezo wa Riadha walipofika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo katika hafla ya kuwakabidhi vifaa alivyoviandaa kwa Mchezo huo katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba katika mpango wake wa kuimarisha na kuupa nguvu mchezo huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya Riadha Katibu wa mchezo huo Wilaya ya Magharibi Unguja Othman Ali wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi vifaa vya Riadha kwa Mwenyekiti wa mchezo huo Wilaya ya Kaskazini B Unguja Juma Hassan Ali wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya Afisa Michezo Wilaya ya Kaskazini A pia mjumbe wa Riadha Taifa Faida Salim Juma wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja.
Sehemu ya viongozi mbali mbali.
Vifaa vya Mchezo wa Riadha vikiwa katika utaratibu uliopangwa ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alivigawa kwa wawakilishi wa Mchezo huo katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba katika hatua zake za kuupa nguvu mchezo huo ikiwemo na michezo mbali mbali hafla ya kukabidhi vifaa hivi ilifanyika ikulu Mjini Unguja leo.Picha na Ikulu.