ABSALOM KIBANDA ATWAA TUZO YA DAUDI MWANGOSI;AANGUA KILIO UKUMBINI

November 07, 2013
Mjane  wa Daudi  Mwangosi Itika  Mwangosi kulia  akifuatilia matukio  yanayoendelea  katika ukumbi  huo



WANAHABARI  nchini  wametakiwa  kujenga  umoja katika  kupinga sheria  kandamizi  ya  vyombo  vya habari  na  wanahabari nchini inayatarajia  kupitishwa na  wabunge wa  bunge la jamhuri ya  muungano wa Tanzania.

Meneja  wa uthibiti  wa ubora  kutoka  baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa  kauli hiyo  leo  jijini Mwanza wakati  wa hafla  ya  kukabidhi tuzo  ya  kishujaa na uandishi  uliotukuka  ya  Daudi Mwangosi .

Mtambalike  amesema  kuwa  idadi ya  waandishi  kutekwa na kuuwawa  imezidi  kuongezeka  hapa nchini  huku kasi  ya  serikali  kuvifungia vyombo  vya habari  pia  inaendelea  kuongezeka .

Hivyo iwapo wanahabari  nchini  hawataungana  katika  kupinga  manyanyaso  dhidi  ya  vyombo vya habari na  kupinga  sheria  kandamizi  dhidi ya  vyombo  vya habari na wanahabari suala  la uhuru  wa  vyombo  vya habari nchini  litaendelea  kubaki ndoto.

Kwa  upande wake rais  wa umoja  wa  vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania  (UTPC) Keneth Simbaya alisema  kuwa tuzo  hiyo  inayotolewa ni  tuzo ya  kwanza  kutolewa nchini Tanzania  kwa  waandishi  wanaopata  matatizo wakati  wanatekeleza wajibu  wao.

Simbaya  alisema kuwa UTPC  imeamua  kuanzisha  tuzo  hiyo kama  njia ya  kuwapa  moyo  wanahabari na  kuuthibitishia umma kuwa  wanahabari  nchini  hawatakata tama katika  kutumikia tasnia  hiyo.

Alisema iwapo  jamii inapaswa  kujua ni vema  serikali  kukubali  kutoa habari kwa jamii inayopasa  kujua na  inayo haki ya  kupata  habari.

“ Serikali itambue  kuwa  inapohitaji  wananchi  kuchangia maendeleo ni vema itambue  kuwa  wananchi hao  wana haki ya kupata  taarifa  mbali mbali  ya kile  walichochangia….ndani  ya  tukio la mauwaji  ya  Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi  zetu  wapo  wasiopenda  kuona  tunafanya kazi  zetu hiyo”

Pia  alisema  ni vizuri wananchi  kutambua  kuwa wakati  wanahabari nchini  wakitetea  kupata  habari wasifikiri  wanahabari  wanajipangani  wao  .

Kwani  alisema  kuwa  jitihada za  wanahabari  kupigania  uhuru  wa kupata  habari zinapaswa  kuungwa mkono na kila raia  wa Tanzania  ambayo ana haki ya  kupata  habari.

Jaji mkuu  tuzo  hiyo Hamza Kasongo alisema  kuwa mchakato  wa kumpata  mshindi  ulifanyika kwa kipindi  cha miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba mwaka  huu.

Tuzo   hiyo ya  uandishi  wa  habari wa  kishujaa na utumishi  uliotukuka  ya Daudi Mwangosi  imetolewa kwa  Absalom Kibanda mahariri  wa kampuni ya  new habari (2006) Ltd  na mwenyekiti  wa  jukwaa la  wahariri nchini (TEF).

Rais Kikwete awazodoa Kenya, Uganda na Rwanda na kuwaambia Tanzania haitajiondoa EAC ng'o

November 07, 2013

Na Rahimu Kambi, Dodoma  

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewashangaa majirani zake, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kwa kufanya vitendo vinavyoashiria ubinafsi na kuitenga nchi ya Tanzania, bila sababu za msingi.


Rais Kikwete aliyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akilihutubia Bunge, ikiwa ni miaka kadhaa tangu alipofanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2010 alipozindua Bunge hilo lilipotoka katika Uchaguzi Mkuu.  

Akizingumza kwa hisia kali, Kikwete alisema kwamba pamoja na nchi hizo kutaka kuitanga nchi yake, ila Tanzania itaendelea kuipenda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kamwe haitaweza kuondoka, licha ya dalili za ubinafsi wa Kenya, Uganda na Rwanda kuongezeka.



Rais Kikwete alisema kwamba wao kama wakuu wan chi wamekuwa wakikutana na kubadilisha mawazo ya kuinga jumuiya hiyo, hivyo inashangaza kuona wapo watu wanaotaka kufanya mambo yanayoshangaza kwa mustakabali wan chi za Afrika.


"Inashangaza kama kuna watu wanaona sisi hatufai kuwa kwenye makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ukizingatia kuwa tunatumia gharama kubwa katika bajeti yetu kutenga mambo ya Jumuiya hii.


"Na kama wenzetu kuna kosa tumelifanya, nadhani njia nzuri ingekuwa kuwa wawazi na sio kufanya mambo ambayo si mazuri kwa mustakabali wan chi zetu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza Tanzania itaendelea kuwa kwenye jumuiya hiyo na kamwe hawatakuwa tayari kutoka.


Awali Rais Kikwete pia alitumia muda huo kuzungumzia juhudi za kupambana na majangili Tanzania na duniani kote ili kuweka mkakati sahihi wa kuzuia majangili wanaongamiza rasilimali za Tanzania, wakiwamo wanyama aina ya faru na tembo pamoja na mbao.


Pia alizungumzia mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya, akisifia taratibu zote zilizotumika hadi kufikia wakati huu ambapo rasimu ya kwanza imepatikana, huku siku chache zijazo wakitarajiwa kupatikana wajumbe wa Bunge la Katiba.

TAARIFA NA PICHA - DKT. SENGONDO MVUNGI APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI LEO - ALHAMISI NOVEMBA

November 07, 2013

 Mke wa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, …(kulia) pamoja na marafiki wakiomba dua leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere dakika chache kabla na Dkt. Mvungi hajasafishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Dkt. Mugisha Clement Mazoko wa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) (kushoto), Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (mwenye tai) na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (wa pili kulia) pamoja na ndugu na jamaa wa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi wakiangalia wakati Mjumbe huyo akipandishwa ndani ya ndege kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) amesafirishwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) saa 5:45 asubuhi kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.


Akiwa nchini Afrika Kusini, Dkt. Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg.


Itakumbukwa kuwa Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013. Tukio hilo la uvamizi linaendelea kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini. 


Tangu siku alipojeruhiwa, Dkt. Mvungi alikuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI). Hata hivyo, Madaktari waliokuwa wakimtibu MOI, walishauri afanyiwe uchunguzi na matibabu zaidi. 


Dkt. Mvungi ameondoka na ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Flightlink na ameambatana na Dkt. Mugisha Clement Mazoko kutoka MOI; Muuguzi Bi. Juliana Moshi; na mtoto wa kaka yake Bw. Deogratias Mwarabu. Serikali inagharamia gharama zote za matibabu ya Dkt. Mvungi.


Tume inawaomba wananchi wote waendelee kumuombea kwa Mungu Dkt. Mvungi ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na hatimaye kuendelea majukumu yake.

AZAM FG NA MBEYA CITY NANI KUONGOZA LIGI LEO

November 07, 2013

Ligi kuu soka Tanzania bara inaendelea leo kumalizia mzunguko wa kwanza lakini macho na masikio ya wengi yakiwa Azam Complex Chamazi mchezo utakaowakutanisha wenyeji Azam FC dhidi ya Mbeya City.

Mchezo huo una utamu wa aina yake kutokana na vita iliyopo baina ya timu hizo mbili ambazo zipo kileleni na ndizo zitaamua hatima ya timu itakayokaa kileleni wakati mzunguko wa kwanza unamalizika.
Timu hizo zinakutana huku zikiwa ndizo timu pekee ambazo hazijui karaha ya kufungwa katika msimu huu na zikiwa zina pointi 26 kila mmoja.
Kama zitatoka sare na Yanga ikashinda katika mchezo wake dhidi ya JKT Oljoro utakaopigwa uwanja wa Taifa,Yanga watakaa kileleni na kama mmoja wao atashinda ndiye atakayekaa kileleni bila kusikilizia matokeo ya Yanga ambao wana pointi 25 kabla ya mchezo wake wa leo,ikiwa ni pointi moja nyuma ya Azam FC na Mbeya City.

Mchezo huo pia umekuwa na mvuto wa aina yake kutokana na mwenendo wa Mbeya City ambao hakuna timu iliyopata dawa ya kuwafunga na timu iliyobaki kuthibitisha kama ina dawa hiyo ama imekosekana ni Azam FC.

Mvuto mwingine ni kwa timu iliyopanda daraja msimu huu Mbeya City kuonekana kutoa upinzani mkubwa na ikiwa tayari imeweka rekodi ya kushinda mechi sita mfululizo.

Lakini kinachoongeza utamu wa mechi hiyo ni kutokana na matokeo ya mechi tano zilizopita kwa timu hizo ambapo Azam FC imeshinda mechi zote tano zilizopita na Mbeya City pia wameshinda mechi zao zote tano zilizopita.

Tiketi za kuwaona P-Square zaanza kuuzwa

November 07, 2013

Uuzwaji wa tiketi za tamasha la kundi maarufu zaidi la muziki wa kizazi kipya barani Afrika, P-Square, umeanza kufanyika jijini Dar es salaam ambapo zitauzwa kwa awamu tatu kwa bei tatu tofauti.

Wadhamini wakuu wa tamasha hilo, kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, wamekuwa wa kwanza kuuza tiketi hizo ambapo kupitia M-pesa wanauza tiketi kwa shilingi 30,000, zoezi litakalodumu hadi tarehe 17 mwezi huu.

Akiongea na gazeti hili, Alex Galinoma, Afisa masoko wa kituo cha EATV, amesema baada ya tarehe 17 tiketi zitapanda bei na kuuzwa shilingi 35,000 ambapo safari hii zitakuwa zikiuzwa kwenye maduka mbali mbali jijini Dar es salaam ambayo yatatangazwa.

"Bei hii itaendelea mpaka mchana wa siku wa tamasha ambapo sasa, ukienda eneo la tamasha(Leaders Club) kununua tiketi mlangoni zitakuwa zikiuzwa shilingi 50,000, alifafanua Galinoma.

Mara ya mwisho kundi hilo lilipokuja jijini Dar, walikuja kwenye tamasha liloandaliwa na kituo cha EATV, tamasha hilo lilipewa jina la kibao chao kilichokuwa kikitamba wakati huo "Do Me".

Katika tamasha hilo lililofanyika Agost 31, mwaka 2008, katika viwanja vya Leaders Club, kiingilio kilikuwa ni 20,000 ambapo walifanya onyesho la dakika 45 huku wakitumia mtindo wa Playback.

Kwa mujibu wa Galinoma, safari hii wanamuziki hao watakuja na bendi nzima na watatumia mtindo wa ala na watakuwa jukwaani kwa masaa mawili bila kupumzika.

Galinoma alisema tamasha hilo la P-Square litaanza rasmi kuanzia saa moja jioni mpaka saa 7 usiku, ili kuwapa mashabiki muda wa kupumzika na kuendelea na mambo mengine.

Milango ya Leaders club itakuwa wazi kuanzia saa 12 jioni na mashabiki wataweza kuingia. Washabiki wanashauriwa kufika mapema Leaders club kwa sababu kutakuwa na ukaguzi wa kutosha na ulinzi mkubwa kwenye tamasha hili. 
Taarifa hii kwa hisani ya Handeni kwetublog.
KARETI PEMBA WAWEKA MIKAKATI YA MCHEZO HUO.

KARETI PEMBA WAWEKA MIKAKATI YA MCHEZO HUO.

November 07, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba .07/11/2013.
Wadau wa mchezo wa Kareti Wilaya  ya Wete ,  wameweka bayana mbinu na mikakati ya kuimarisha mchezo huo ili uweze kusaidia kupatiakana kwa ajira kwa vijana na kupunguza tatizo ka vijana kutegemea ajira kutoka Serikalini .

Wakizungumza kwenye kikao cha kujadili mbinu na mikakati ya kuimarisha mchezo huo , uliofanyika kwenye ukumbi wa Jamhuri , wamesema kuwa moja ya mikakati hiyo ni kuweka viwanja sehemu za wazi ili kuwafanya vijana wengi kujiunga na mchezo huo .

Kikao hicho ambacho kiliwashirikisha makatibu na wenyeviti wa vikundi vya kareti Wilaya hiyo , ambao walipitisha azimio la kufanya bonanza la mchezo huo ili kuitangaza na kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa mchezo huo .

Afisa Michezo Wilaya hiyo Suleiman Shavuai , akizungumza kwenye kikao hicho amewataka walimu wa mchezo wa karati Wilayani humo , kutafuta maeneo ya wazi na kuacha kufanya mazoezi sehemu za msituni jambo ambalo linawafanya vijan wengi kushindwa kujiunga na mchezo huo .

Amesema kuwa mchezo wa karati unaweza kuiletea sifa nchi , endapo vijana watakuwa tayari kujiunga , huku pia alitoa wito kwa wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo .

Akizungumza kwa niaba ya wenzake katibu wa kikundi cha Scopion karate gruop cha Ole , ameitaka jamii kuelewa kwamba mchezo huo ni kama ilivyomichezo mingine , na kuwataka vijana kujiunga kwa wingi kwa ajili ya kujenga miili pamoja na kujipatia ajira .

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA LEO

November 07, 2013
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,JULIANA MALANGE AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI LEO AMBACHO KILIFANYIKA UKUMBI WA MIPANGO MIJI JIJINI TANGA.

NAIBU MEYA WA JIJI LA TANGA,MH.SHEMDOE AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI LEO KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,JULIANA MALANGE.


WAHESHIMIWA MADIWANI WAKIFUATILIA MAMBO KWENYE KIKAO HICHO.

WATAALAMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAKIFUATILIA MIJADALA MBALIMBALI

MHESHIMIWA DIWANI WA KATA YA MSAMBWENI ABDURAHAMANI AKISIKILIZA HOJA ZA BAADHI YA MADIWANI WENZAKE



MADIWANI WA VITI MAALUMU WAKIFUATILIA MAKABRSHA YA KIOA HICHO

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,JULIANA MALANGE KULIA NA KUHSOTO NI NAIBU MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA TANGA,SHEMDOE