Na Oscar Assenga, Tanga.
WAREMBO
wanaowania umalkia wa Mkoa wa Tanga “Redd’s Miss Tanga 2013”wanatarajiwa
kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira mkoani Tanga “Kalembo Day” June
15 mwaka huu na baadae kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga
Bombo kuwaona wagonjwa na kutoa zawadi.
Shughuli
hizo za usafi watazifanya katika maeneo mbalimbali jijini Tanga siku hiyo
ambayo ni siku maalumu ya usafi katika mkoa wa Tanga wakati wakiwa wanajiandaa
na shindano hilo ambalo litafanyika June 22 mwaka huu kwenye uwanja wa
Mkwakwani.
Siku
mbili baada ya warembo hao kumaliza zoezi hilo watakwenda kutembelea vivutio
vya utalii na maeneo ya kihistoria yaliyopo mkoani hapa June 17 mwaka huu lengo
likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuweza kupata fuksa nzuri ya kuweza
kuutangaza kwa wageni na wenyeji.
Vivutio ambavyo warembo hao wanatarajiwa
kutembelea ni Mbuga ya Wanyama ya Sadani na Mapango ya kihistoria ya Amboni
yaliyopo jijini Tanga ambapo watapata fursa ya kuona na kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusu maeneo hayo.
Shindano hilo linatarajiwa
kufanyika 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa ambapo litapambwa na
wasanii nguli wa muziki wa bongo fleva nchini ili kuweza kuwapa burudani wakazi
wa mkoa huu ambao watajitokeza kushuhudia kinyang’anyiro hicho.
Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, ambaye ndiye
muandaaji wa shindano hilo alisema shindano hilo linatakuwa la aina yake
kutokana na kuwa na warembo bomba.
Alisema kuwa warembo hao tayari
wanaedelea na mazoezi kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga ambapo tayari
wameshaanza kuwateka wadau wa tasnia hiyo ambao wamekuwa wakijitokeza kila siku
kushuhudia mazoezi hayo.
“Ninachoweza kusema shindano la mwaka
huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na
hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Kigundul.
Shindano hilo litaanza saa 2,
usiku na kueleza kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na jumla
ya warembo 12 watashindania taji hilo ambalo hivi sasa linashikiliwa na Miss
Tanga 2012 Teresia Kimolo.
Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack
Emannuel (18),Wahida Hashimu(20), Tatu Athumani (19), Mwanahamis Mashaka(20),
Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21),Azina
Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moreli (21) na Hawa Twaybu(21)
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani
humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini
hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
Redd's, Miss Tanga, imedhaminiwa na Dodoma Wine,CXC Africa,Executive
Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD,
Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group, pamoja
na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu
na assengaoscar.blogspot.com.
Mwisho.