TICTS FAMILY DAY BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DAR

December 03, 2017
 Kamati ya Maandalizi ya Bonanza la Familia za Wafanyakazi wa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es salaam (TICTS), ikiwa katika picha ya pamoja wanati wa sherehe hiyo, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es salaam.
MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA AITAKA JAMII KUHAKIKISHA KUWA WATU WENYE ULEMAVU HAWAACHI NYUMA KWENYE NYANJA ZOTE ZA MAENDELEO

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA AITAKA JAMII KUHAKIKISHA KUWA WATU WENYE ULEMAVU HAWAACHI NYUMA KWENYE NYANJA ZOTE ZA MAENDELEO

December 03, 2017
11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu vya ngozi wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoa wa Kusini,Unguja.

WAZIRI KIJAJI AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

December 03, 2017


NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji
ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza juzi katika mahafali ya Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha ambapo pamoja na mambo mengine amewaonya wahitimu nchini kujiepusha na rushwa kwa kutaka utajiri wa haraka kuacha tabia hiyo kwani hawatabaki salama katika utawala huu. (Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo ya chuo cha Uhasibu Arusha katika mahafali chuoni hapo juzi
 
Mkuu wa kitivo cha uhandisi,mazingira na Computer Paul David Greening kutoka Uingereza akizungumza katika mahafali yao juzi katika Chuo cha Uhasibu NjiroArusha
Kushoto ni mgeni rasmi ambaye ni NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akisoma maelezo mafupi ya chuo cha Uhasibu Njiro Arusha katika mahafli juzi chuoni hapo

ASYA IDAROUS KHAMSIN KUFUNIKA SHEREHE ZA UHURU OAKLAND!

December 03, 2017

Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2017 Mama wa mitindo maarufu hapa Tanzania kama Asya Idarous Khamsin, ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Marekani.  Ifikapo December 9th 2017  ataiwakilisha Tanzania kwa kuonyesha mitindo yake kwenye sherehe za uhuru Oakland Carlifonia.

Hivyo tukiwa kama Watanzania ni jambo la kujivunia maana Tasnia ya mitindo imekuwa ni moja kati ya vyanzo vizuri vya kuitangaza nchi yetu. Tunapaswa kuonyesha ushirikiano kwa wabunifu (Designers)  wetu wanao jituma kama Mama yetu Asya Idarous Khamsin na wengineo.

Ukiguswa unaombwa kusambaza ujumbe huu kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wanao penda Fashion  Asante.
SIMBA SC KWENDA NA KASI YA RAIS MAGUFULI KWA KUZALISHA AJIRA

SIMBA SC KWENDA NA KASI YA RAIS MAGUFULI KWA KUZALISHA AJIRA

December 03, 2017

Rabi Hume,Dar es Salaam

Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO amesema amejipanga kushirikiana na wanahisa wenzake wa klabu hiyo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia kampuni ya Simba Sports Club Limited. Dewji aliyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanachama na mashabiki wa Simba kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo, baada ya kutangazwa na kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba, kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo. Alisema klabu ya Simba inampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, na wao wamedhamiria kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi yake kupitia mchezo wa mpira kwa kutoa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mpya itakayosimamia timu hiyo katika mfumo wa hisa. Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere. "Tamati yangu nielekeze kwa sisi sote kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuongoza taifa hili. Wote tumtakie kila la kheri, baraka na fanaka tele katika utumishi wake uliotukuka, "Pamoja na kupongeza sera yake ya ujenzi wa viwanda nchini, ambapo sisi kwa upande wetu, klabu ya Simba inamuunga mkono kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa kabisa cha soka yaani Simba Sports Club Limited, ambacho licha ya kuongeza ajira lakini pia tutaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Dewji. Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises, alitumia mkutano huo kuelezea mipango ambayo wameipanga ili kuiwezesha Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika kuliko ilivyo sasa, huku malengo ikiwa ni kuwania mataji makubwa barani Afrika.
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah akimkabidhi cheti cha ushindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu ya Simba mfanyabiashara na mwanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji MO kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.
"Katika mwaka wa kwanza, nawaahidi kwa kushirikiana na ninyi tutakuwa na kiwanja cha nyasi asilia, na kiwanja cha nyasi za bandia ambapo viwanja hivi tutavitumia kwa mazoezi kwa kadri ya mahitaji ya mechi tunayokwenda kucheza, "Pia tutajenga hosteli ambayo itakuwa na vyumba 35 ambavyo wataishi wachezaji 30 na support staff, kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 35 square- meter... ili kufanya eneo hilo kuwa bora kwa wachezaji wetu," alisema Dewji na kuongeza. "Wote tunaopenda mpira, tunajua kama ukitaka kuwa na wachezaji bora lazima utumie pesa. Nia yetu kwa mwaka wa kwanza, tunatarajia kiwango cha chini cha pesa ya usajili iwe bilioni moja. Pia tumetenga milioni 500 kuboresha benchi la ufundi, kwa kushirikiana na benchi liliopo sasa." Hata hivyo Dewji, alisema klabu ya Simba itajenga kituo cha kukuzia vipaji ambacho kitakuwa na wachezaji vijana. Jambo ambalo litaisaidia Simba kuwa na wachezaji bora vijana ambao wamefundishwa kucheza soka katika kituo cha timu hiyo. "Ili kuwa na wachezaji bora kwa miaka ijayo tunahitaji kuwa na kituo cha kukuzia vipaji kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 14, 16, 18. Na mipango yetu ya baadae ni kushirikiana na timu kubwa za ulaya kutuongoza na kutuelemsha jinsi gani ya kujenga kituo chenye hadhi ya kimataifa na mungu akipenda tutakuwa na kituo bora barani Afrika." alisema Dewji.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wakishangilia baada ya kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba kumtangaza Mohammed Dewji MO kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA ATOA MIEZI MITATU WANANCHI WALIPWE FIDIA WAPISHE ENEO LA HIFADHI

December 03, 2017
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, David Kanyata na Kaimu Meneja wa pori hilo, Stanslaus Odhiambo.

Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya
.......................................................................................
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.

Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.

“Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.

Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.

Alisema mazungumzo yalishafanywa kupitia vikao halali vya uongozi wa viijiji na halmashauri ambapo wananchi hao waliridhia kulipwa fidia ili kuachia maeneo hayo ya hifadhi.

Alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa pori hilo ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji yanayotiririka kwenda mto Ruaha na kwenye mabwawa ya kidatu na mtera yanayotumika kuzalisha umeme nchini.

Akizungumzia malipo ya fidia kwa vijiji na vitongoji vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo alisema kijiji kimoja kilishalipwa mwaka 2015 jumla ya shlingi milioni 500 na vijiji vilivyosalia vitalipwa kwa awamu ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 fedha zimetengwa kwa ajilia ya kulipa wananchi wa kitongaoji cha Machimbo ambao tayari walishafanyiwa uthamini mwaka 2015.

Awali akizungumza na watumishi wa Pori hilo katika ofisi zao zilizopo Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Naibu Waziri Hasunga aliwataka watumishi hao kuongeza nguvu na ubunifu kwenye kuzuia mifugo isiiingie hifadhini badala ya kusubiri iingie ndipo waikamate na kuitoza faini au kuitaifisha.

“Nyie ni watalaamu, tumieni mbinu na ubunifu wenu wote muhakikishe mnazuia mifugo isiingie hifadhini, sitaki kusikia mmekamata au mmetaifisha mifugo hifadhini, hiyo siyo sifa, sifa ni kuzuia isiingie kabisa, na nitawapima kwa hilo,” alisema Hasunga.

Aidha aliwataka watumishi hao kuimarisha uhifadhi shirikishi, kujiepusha na vitendo vya rushwa, kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuongeza ubunifu utakaowezesha ongezeko la mapato ya Serikali.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwatembelea wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo ambao awali waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo.

MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO

December 03, 2017
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa, Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017. 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea Bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017.Kulia kwake ni binti yake, Zuleikha Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWANJELWA AWATAKA WAJUMBE MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MBEYA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI

December 03, 2017
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo,Mary Mwanjelwa akizungumza  na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mary Mwanjelwa akisalimiana  na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo,Mary Mwanjelwa akitoa salamu za wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017 amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa cha uongozi.

Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.

Alisema kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana, Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi.

Mbele ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote wa Mkoa wa Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012-2017.

WAFANYAAKAZI MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB), WAJIPANGA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA MWAKA 2018

December 03, 2017
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAKATI Mwaka 2017 ukifikia ukingoni taasisi mbaliombali nchini zimeanza kuwakusanya watumishi wake na kufanya tathmini ya utendaji na kujadili namna ya kuzikabili changamoto walizokutana nazo ili hatimaye kuongeza ufanisi mwaka ujao 2018.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Mwalimu Commercial Bank, (MCB), ambao wamekutana jijini Dar es Salaam, ili kufanya tathmini ya kiutendaji na kuweka mikakati mipya waingiapo mwaka 2018.
Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali wakiongozwa na Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi pia walipatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kiuwajibikaji katika maeneo tofauti kutoka kwa mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka.
Ili kuonyesha ushirikiano wafanyakazi hao walibadilishana zawadi mbalimbali ambapo kila mfanyakazi alimuandalia zawadi mfanyakazi anayemvutia zaidi kiutendaji.

 Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
 Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHIMIZA MFUMO WA ELIMU YA JUU UANDAE RASILIMALI WATU ILI KUFIKIA TAIFA LA UCHUMI WA KATI

December 03, 2017

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimpongeza Balozi Nicolous Kuhanga mara baada ya kutunukiwa na Mhe Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, shahada ya heshima ya uzamivu kutokana na mchango wake mkubwa hasa wakati wa kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim akimpongeza Mke wake Mama Mary Majaliwa mara baada ya kutunukiwa shahada ya uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera kutokana katika Chuo Kikuu Huria Tanzania mapema jana Mjini Singida.
Siku ya Ukimwi Duniani 2017, Timu za Sanvik na Mantrac zachuana vikali Mwanza

Siku ya Ukimwi Duniani 2017, Timu za Sanvik na Mantrac zachuana vikali Mwanza

December 03, 2017
Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Sandvik Fc imetoa kichapo cha goli 4-3 dhidi ya wapinzani wao Mantrac Tanzania  za jijini Mwanza katika mchezo wa  kirafiki uliotimua vumbi katika uwanja wa Nyamagana.
Mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Sandvik Mining and Construction (T) LTD ambao waliwakaribisha wenzao wa Mantrac Tanzania, kwa ajili ya kuungana na watanzania na dunia kwa ujumla katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani inayofanyika kila mwaka Disemba Mosi.
Sandvik FC ilifunga magoli kupitia washambuliaji wake Petro Ng’ oko dakika ya 13, Samwel  Manga dakika ya 48 na Hamis Luhenga dakika ya 60 na 72, huku Mantrac ifunga kupitia Emmanuel Joel dakika ya 10, na Hamfrey Kirutu dakika 30 na 52.
Akizungumza na BMG, Afisa Rasirimali Watu (HR) wa Sandvik Mining and Construction (T),  Deogratias Sendama  ambaye ni Nahodha Msaidizi wa timu hiyo,alisema, mchezo huo ni kwa ajili ya kuungana na watanzani na dunia katika kuadhimisha siku ya ukimwi dunia, pia ulikua mzuri na amefurahi kuwafunga wapinzani wao na hatimaye kuibuka na ushindi.
Sendama alisema wataendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha kikosi zaidi, kwani mchezo ni afya na husaidia kuimarisha mahusiano kama walivyofanya wao.

COUNCIL OF EAST AND CENTRAL AFRICA FOOTBALL ASSOCIATIONS CECAFA

December 03, 2017

The CECAFA Congress convening here at Four Point Hotel in Nairobi City this Saturday December 2nd 2017 has elected the five new Executive Committee members to run the region’s top football office for the next two calendar years.
The five who have been unanimously elected will now join CECAFA President Eng. Mutasim Gafar (Sudan) whose constitutional term runs till November 2019. These include Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia), Wallace Karia (Tanzania) and Doris Petra a woman representative hailing from Kenya.
The race that had earlier attracted eight candidates had Eng. Moses Magogo (Uganda), Vincent Nzamwita (Rwanda) and Kourecha Ali Gued from Djibouti withdrawing their candidature just minutes before the polls.
CECAFA COMPETITIONS:
The Congress emphasized the need to have annual tournaments and the following member federations have offered to host the 2018 events as below. 

No.
TOURNAMENT
COUNTRY
01
Beech Soccer & Women
Uganda
02
Kagame Cup
Djibouti
03
Youth U17
Tanzania
04
Youth U20
Sudan/Kenya



This year’s delayed CECAFA WomenCup will still take place in Rwanda early next year. The hosts for the Senior Challenge Cup 2018 will be decided at a later date.  Ten out of twelve countries participated except Sudan and Eritrea.



Rogers Mulindwa

CECAFA Media Manager
+256 772 751 829/ +256 701 520 115

Member countries: Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, South Sudan, Sudan, Tanzania, Uganda and Zanzibar.

SERIKALI YA MKOA WA TANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA LA AGPAHI

December 03, 2017
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi amesifu jitihada zinazofanywa na Shirika la  Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Care Initiative (AGPAHI) kwa kuhakikisha watoto wanapata huduma stahiki za afya na kisaikolojia.
Mhandisi Zena (pichani)aliyasema hayo leo wakati akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani iliyoadhimishwa kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga.
“Ninayo furaha kubwa sana kuwepo hapa kushiriki na kuona jitihada zinazofanywa na shirika la AGPAHI kwa watoto wa mkoa wa Tanga ….Nafahamu kuwa mkusanyiko huu una watoto,vijana na wahudumu wa afya kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo  Hospitali),vituo vya afya vya Ngamiani, Makorora na Pongwe.

Shirika hilo ambalo lilianza kufanya kazi mwezi Oktoba 2016 katika mkoa wa Tanga kwa kutoa huduma za matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU) limekuwa ni chachu kubwa kuwafikia watoto na vijana kupitia vikundi.

Mhandisi Zena alisema “mara tu baada ya shirika hilo kuanza kazi mkoani Tanga, taratibu za uundwaji wa vikundi vya watoto (maarufu kama Ariel Clubs) ulianza na sehemu ambazo vikundi vilikuwepo awali viliimarishwa na Shirika la AGPAHI na kupewa mbinu za kuwafanya waendelee kuwa imara”.  Pia, shirika la AGPAHI lilitoa mwongozo kwa wahudumu wa afya jinsi ya kuanzisha vikundi vya watoto  na vijana vinavyoundwa kwenye vituo vya kutolea huduma za matunzo na matibabu (CTC) husika vinavyohusisha watoto wenye umri wa kuanzia miaka 6-17.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja Mawasiliano  wa Shirika la AGPAHI Jane Shuma alisema katika kusheherekea siku ya Ukimwi duniani kwa mkoa wa Tanga waliona washirikiane na serikali ya mkoa na kuandaa mjumuiko huo ambao utakuwa ni fursa ya kuwakutanisha watoto na vijana kuweza kupata elimu kwa njia ya michezo .

Alisema mjumuiko huo una watoto na vijana wapatao 200 waliotoka katika klabu za vituo vya Afya Ngamiani,Makorora,Pongwe na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo. Aliongeza kuwa lengo la mjumuiko huo ni kuwaweka pamoja watoto na vijana walio katika huduma za matunzo na matibabu kutoka vituo vya Afya Ngamiani,Makorora,Pongwe na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ili kuweza kufahamiana,kujenga urafiki kati yao,kupata burudani,furaha na matumaini.

Vilevile lengo lingine ni kuwapa fursa watoto na vijana kushiriki kwenye michezo kwa pamoja,kupeana matumaini kwa njia ya michezo na kusaidia kuwahamasisha watoto na vijana wenzao kuendelea kubaki kwenye huduma za matunzo na matibabu kwenye maeneo mbalimbali wanapotokea.

“Lakini pia kupata elimu ya Afya ya ziada kwa pamoja kulingana na umri wao ….elimu zaidi kuhusu uwazi na ufuasi mzuri wa dawa na afya ya makuzi. Hata hivyo alisema dhamira yao ni kuona huduma hizo wanazozitoa kwa watoto na vijana zinaleta mtazamo chanya kwenye maisha yao na jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Moses Kisibo alisema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau wote likiwemo Shirika la AGPAHI katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi ili kuhakikisha maambukizi yanashuka. Aliongeza kusema kuwa, Halmashauri ya Jiji la Tanga imetenga fungu kwa ajili ya watoto wanaoishi naVVU hivyo wataona namna nzuri ya kuweza kuwafikia walengwa.

Aidha pia aliitaka jamii kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga vijana na watoto wanaoishi na maambukizi ya VVU badala yake tuwape ushirikiano ili waweze kutimiza ndoto zao.

Kuhusu vikundi vya watoto -- watoto wanapokuwa kwenye vikundi wananufaika na mambo mbalimbali ikiwemo kupata huduma za kisaikolojia,kupata elimu ya afya,lishe,stadi za maisha ikiwemo kupata marafiki na kupeana moyo na wenzao ambao wako katika hali sawa ya maambukizi. Hadi sasa, Shirika la AGPAHI  limeweza kuunda jumla ya vikundi vya watoto vipatavyo 11 katika mkoa wa Tanga vyenye watoto wapatao 1119.

Meneja Mawasiliano  wa Shirika la AGPAHI Jane Shuma akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo

 Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoa wa Tanga,Ben Nahayo akitoa neno kwenye maadhimisho hayo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Moses Kisibo
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Selemani Msangi akizungumza 
 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Moses Kisibo akizungumza
 Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Moses Kisibo kushoto akiwa na Mratibu wa Shirika la  AGPAHI mkoa wa Tanga,Ben Nahayo
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akiagana na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Selemani Msangi
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akiagana na watoto hao
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akipiga picha na miongoni mwa watoto 
 Mmoja kati watoto akizungumza katika maadhimisho hayo
 Sehemu ya watoto wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho hayo
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya maadhimisho hayo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Moses Kisibo kushoto ni
Meneja Mawasiliano  wa Shirika la AGPAHI Jane Shuma
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akiondoka kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlal kushoto ni  Meneja Mawasiliano  wa Shirika la AGPAHI Jane Shuma
 michezo ikichukua nafasi yake kwa watoto
 Michezo ikiendelea kwa watoto hao
 sehemu ya watoto wakiwa wanashiriki kwenye michezo