KAMATI KUU YA CCM YASISITIZA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UENDELEE

August 21, 2014
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alisema,
Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa na kufanya tathimini juu ya maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini, ndani na nje ya Bunge.

Kamati Kuu vilele imepokea na kujadili taarifa kuhusu mazungumzo na mashauriano kati ya vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI  na CCM. Mazungumzo ambayo yalisimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Aidha Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya kikao cha Baraza la Vyama vya siasa na pia taarifa ya kikao cha Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD). Vikao hivyo vyote vilihusu maendeleo ya mchakato wa Katiba nchini.

Kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba, Kamati Kuu imearifiwa maendeleo ya majadiliano na upigaji kura katika kamati za Bunge hilo. Kwa ujumla Kamati Kuu imeridhishwa na namna wajumbe wa Bunge Maalum wanavyoshiriki katika kujadili na kujenga hoja na wanavyoshughulikia tofauti za kimtazamo na kimawazi katika vikao vyao na hatimaye uhutimishaji wa majadiliano kwa kura.

Kamati Kuu inawahimiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kuhudhuria vikao vya kamati na vile vya Bunge na kushiriki katika mijadala kwa kutanguliza masilahi mapana ya taifa na hatimae kuipatia nchi katiba inayotarajiwa na watanzania wote. Chama Cha Mapinduzi kinautakia kila lakheri mchakato huu.


Aidha Kamati Kuu imeridhishwa na juhudi za vyama na wadau mbalimbali katika kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano kwa lengo la kupata muafaka. Hata hivyo Kamati Kuu imesikitishwa na kuvunjika kwa mazungumzo kati ya CCM, CUF,CHADEMA na NCCR-MAGEUZI yaliyokuwa yanasimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kengo la kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano ili kupata muafaka.

Kamati Kuu imepokea na kuridhishwa na taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD) pamoja na vyama vinavyounda TCD katika kutafuta muafaka wa kisiasa kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na kuaminiana kati ya wadau mbalimbali na hasa kati ya vyama vya siasa.

Kamati Kuu inaunga mkono juhudi za TCD za kuendeleza mashauriano kati ya vyama na ndani ya vyama kwa lengo la kupunguza mivutano, kujenga uaminifu na ustahimilivu na umoja kati yao.

Hivyo Kamati Kuu imempongeza Katibu Mkuu wa CCM kwa namna alivyoshiriki na kukiwakilisha Chama kwenye vikao hivyo.

Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu aendelee kukutana na vyama na wadau wengine katika kufanikisha lengo la maridhiano hayo.

Mwisho Kamati Kuu inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuendelea kushikamana na kuvumiliana pale wanapopishana kimtazamo juu ya hoja mbalimbali za katiba kwani Amani,  Utulivu na Utanzania wetu ni muhimu kuliko tofauti zetu za kimitazamo. Mchakato wa Katiba nchini uendelee kuwa fursa ya kuijenga nchi yetu badala ya kutumika kutugawa na kututenganisha.

NANI KUIBUKA MISS TEMEKE 2014

August 21, 2014

Mshiriki Nambari 1 (Subira Ally).
Mshiriki Nambari 2 (Hellen Eugen).
Mshiriki Nambari 3 (Rehema Jabiry).
Mshiriki Nambari 4 (Catheline Alex).
MKUTANO WA APECSA ARUSHA

MKUTANO WA APECSA ARUSHA

August 21, 2014

IMG_1244 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Serikali ya Muungano Dr.Seif Rashid (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo,alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro Mkoani Arusha leo.[Picha na Ramadhan Othman Arusha.] IMG_1375 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki,Kati na Kusini mwa Bara la Afrika katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jumuiya ya Afika ya mashariki Mjini Arusha leo.[Picha na Ramadhan Othman Arusha.]
IMG_1390 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Apecsa kwa kanda Mashariki,Kati na Kusini mwa Bara la Afrika katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jumuiya ya Afika ya mashariki Mjini Arusha leo.[Picha na Ramadhan Othman Arusha.]
RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO

August 21, 2014

k (1)
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
PICHA NA IKULU
k (2)
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014. 
k3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)
k4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni  Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa  Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
k5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete
k6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
k7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
mo28
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule  ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 201
mo29
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete  na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani Morogoro Agosti 20, 2014.
KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM MKOA WA ARUSHA CHAKUTANA KUMJADILI NAIBU KATIBU UVCCM MKOA

KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM MKOA WA ARUSHA CHAKUTANA KUMJADILI NAIBU KATIBU UVCCM MKOA

August 21, 2014

???????????????????????????????
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi mabaya ya fedha za umoja huo.
???????????????????????????????
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za UVCCM mkoa wa Arusha.
CCM 1
Mwenyekiti wa UCVVM Mkoa wa Arusha Robnson Meitinyiku  na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakisikiliza maazimio yaliyopitishwa na wajumbe wakati yalipokuwa yakisomwa mbele ya waandishi wa habari mjini hapa
CCM 2
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi katikatika pamoja na wajumbe wenzake wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji lie linaangalia watendaji wenye sifa.
CCM 3
Sehemu ya mkutano wa waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kikiendelea leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose