NHC YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 KUBORESHA MAJENGO YAO TANGA

July 21, 2024

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoani Tanga Mhandisi Mussa Kamendu

Na Oscar Assenga, TANGA

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 wametumia zaidi ya Milioni 300 kwa ajili ya matengenezo makubwa ya majengo yao katika Jiji la Tanga.

Hayo yalibainishwa leo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoani Tanga Mhandisi Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba matengenezo hayo yatahusisha nyumba za Ngamiani, Nguvumali, Bombo mpaka Raskazone.

Mhandisi Kamendu alisema kwamba shirika hilo limefanya mkakati huo maalumu makusudi kuhakikisha majengo yao yanaboreshwa na kuwa na muonekano mzuri ikiwemo kupakwa rangi ili wapangaji wao waishi kwenye mazingira mazuri.

“Katika miji yote ya Tanzania Shirika hilo linamiliki nyumba katikati ya Miji na Majiji kwa hiyo nyumba zinapokuwa kwenye hali mbaya zinafanya miji ionekane vibaya na taswira ya majiji inakuwa haipo vizuri kwa kuliona hilo shirika limekuja na mkakati maalumu wa kuzipaka rangi ili ziweze kuwa na muonekano mzuri na kubadilisha mifumo ya maji taka na maji safi “Alisema

Aidha allisema pia katika matengenezo hayo wamebadilisha pia mifumo ya umeme ambayo imechakaa na kurekebisha miundombinu mbalimbali mingine ikiwemo milango na madirisha ili kuhakikisha wanapangaji wanakuwa kwenye mazingira mazuri.

Katika hatua nyengine Meneja huyo aliwataka wapangaji wao kuhakikisha wanabadilika na kufuata mikataba yao inavyowataka walipe kodi kwa wakati ili waweze kuepukana na usumbufu wanataokumbana nao.

Mhandisi Kamendu alisema kwamba mikataba yao inawataka wapangaji wao kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na pia waweze kuepukana usumbufu watakaoupata maana pale ambao hawajalipa kodi kufuatia na mikataba yao itafikia wakati watatolewa kwenye nyumba hizo.

“Wapangaji wasumbufu ambao wanasubiri mpaka kufuatwa na madadali kwenye kwenye nyumba sasa wanapotelewa kwenye nyumba ni usumbufu na aibu kwa familia na jamii inaweza kuona ni mtu wa ajabu tusisburi mpaka kufukia hatua hii”Alisema

Katika hatua nyengine Meneja huyo alisema kwamba shirika hilo limejiwekea malengo la kukusanya Sh. Bilioni 2,444,183,556.96 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kutokana na makusanyo yao ya Pango la Kodi kutoka katika nyumba zao.

Alisema kwamba hayo ndio malengo yao na mwaka huu wa fedha kwa sababu hiyo kama mkoa wanaendelela kuboresha huduma zao.

Alisema kwamba wanafanya hivyo kama shirika ili kuhakikisha wapangaji wanakuwa kwenye mazingira mazuri na kuwa sawa ili kodi zao wanazolipa ziendane na thamani ya mahali wanapoishi.

Maneja huyo alisema kwamba malengo yao ya Bajeti katika Mwaka wa Fedha wa 2023/2024 waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 2,040,727,435 kutokana na kodi ya pango kutoka kwa wapangaji wao walioishi kwenye nyumba za shirika hilo.

Alisema katika mwaka wa fedha kuanzia Julai 2023 mpaka June 2024 waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 2,040,727,435 na malengo waliokuwa wamejiwekea kwenye bajeti yao ya mwaka 2023/2024 ilikuwa ni kukusanya kodi Bilioni 2,046 ,528,000 .

“Kwa hiyo utaona ukiangalia kiasi tulichokusanya wao Biloni 2,040,727,435 tumekusanya kwa asilimia 99.7 ya malengo ya bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 kwa hiyo katika majengo yetu na idadi ya wapangaji wao na kodi tunavyokusanya kwa ufupi tumefikia malengo ya kwa sababu asilimia 99.7 ni sawa asilimia 100 kiasi cha 5,856,400 ndio ambacho hakijaweza kukusanywa”Alisema

Aidha alisema na hivyo inatokana na madeni ya wapangaji wao ambao wanadaiwa na ni wajibu wao kuendelea kuyadai na kuchukua nafasi hiyo kuwapongeza wapangaji ambao wanalipa vizuri huku wakiendelea kuwasisitizia kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi.

WAZIRI AONYA UDOKOZI WA FEDHA ZA HATIFUNGANI

July 21, 2024

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati halfa ya utiaji saini ya ya mikataba utekelezaji wa miradi ya maji kwa fedha za hati fungani kati ya Tanga Uwasa na Wakandarasi STC Contracstion Limited na China Railway 7 Group Limited katika halfa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo


Na Oscar Assenga, TANGA 

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema hatarajii kuona fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya hati fungani zinadokolewa au kuchezewa badala yake wahakikishe zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na kurejeshwa kwa utaratibu waliojiwekea.

Aweso aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya utiaji saini ya mikataba utekelezaji wa miradi ya maji kwa fedha za hati fungani kati ya Tanga Uwasa na Wakandarasi STC Contracstion Limited na China Railway 7 Group Limited katika halfa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo

 

Alisema kwamb wanapaswa kuhakikisha wanazilipa ili wapate nguvu na maeneo mengine waweze kufaidika na huo ndio uelekeo wa Serikali kwa mamlaka za maji nchini.

 

Alisema kwamba jambo ambalo limefanywa na mamlaka hiyo ni kubwa huku akimuangiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes Meena kumfikisha salamu katibu Mkuu lazima utendaji wake na usimamizi katika mradi huo pamoja na ufuatiliaji uwe wa kipekee ili kufanikisha dira na dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu.

 

“Tunapozungumza fedha za wananchi wameweza katika hati fungani na mwananchi namba moja aliyetoa fedha kwa ajili ya kusapoti maji katika Jiji la Tanga ni Rais Dkt Samia Suluhu hivyo niwasihi tusidokee na tusichezee huu mradi tuende kutumiza malengo ya Rais “Alisema Waziri Aweso

 

Hata hivyo aliwataka wakandarasi ambao wamepata dhamana ya kutekeleza mradi huo wao kama Wizara jicho lao litakuweo hapo muda wote kusimamia  na kufuatilia hivyo wanahitaji kuona tija kubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

 

“Bodi ya Tanga Uwasa tunapozungumzia hati fungani ni fedha za wananchi wamesema hivyo fedha kama wamekopeshwa lazima kuzirejesha  na faida wasije wakawa watu wa maneno hawataeleka ile nia njema nzuri ambayo waliopanga kuifanya itabadilisha taswira ya Taasisi yenu…niwapongeze Tanga Uwasa ukiwa baba au mzazi ukiona mtoto wako anafanya kazi nzuri jukumu lao ni kumuombe dua hivyo mimi ninawaombe dua”Alisema

 

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa  Dkt Ally Fungo alisema kwamba wameingia kwenye historia katika miradi waliosaini hapo wanakwenda kuitekekeza ni sehemu ya mradi mkubwa wa hati fungani kama alivyoeleza Waziri kinachotokea ni wananchi kuwekeza kwenye huduma ya maji.

 

Alisema fedha zao zinaende kutoa huduma ya maji na hivyo baadae kupata faida jambo hilo ni la kwanza kufanyika hapa nchini kupitia mamlaka hiyo huku akimshukuru Rais  Dkt Samia Suluhu wazo hilo lilipofika kwake aliona ni njia nzuri ya kusaidia serikali kugharamia miradi ambayo serikali inapata ugumu kuigharami kwa sababu ya uwepo wa miradi mingine mikubwa ya kipaumbele .

 

“Hivyo akikubaliana na wazo hilo litekelezwe na amekuwa pamoja nasi muda wote mpaka sasa na Rais amewekeza ni moja ya watu waliowekeza kwenye hati fungani na wengine ambao wamewekeza ambao wamejitokeza na kukudhi kwa muda mfupi kupata kiasi cha zaidi ya Sh.Bilioni 53 walichokuwa wakikihitaji lakini kimevuka lengo mpaka Bilioni 54 “Alisema Mkurugenzi huyo wa Bodi ya Wakurugenzi.

 

“Niwashukuru wawekezaji ambao wamewekeza kwenye hati fungani niwaambie fedha zenu sipo salama na hazitapotea na hakuna hata moja na zitafanya kazi iliyokusudiwa na tumejipanga kufanya mradi huo na Mhe Waziri usiwe na wasiwasi ikifika wakati wa kulipana faida na tutaanza na mwezi Octoba mwaka huu na Aprili mwakani  kila mwaka  na wamejipanga kutekeleza hilo” Alisema

 

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes Meena akizunguma katika halfa hiyo alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelela kuipa kipaumbele cha hali ya juu sekta ya maji na hivyo kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.

 

Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Gilbert  alisema kwamba mkoa huo umeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wananchi ambapo miradi mbalimbali ya kimkakati inaendelea kukamilika na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora

 

“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu sekta ya Maji kwa mkoa wa Tanga jumla ya miradi 67 yenye thamani ya Bilioni 89.67 inatekelezwa kupitia Ruwasa na miradi 13 yenye thamani ya Bilioni 11.32 inatekelezwa na Tanga Uwasa hivyo tunaendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupambania wananchi wa mkoa huu na kuendelea kuimarisha shughuli za kijamii na kichumi”Alisema