AZAM, SIMBA, YANGA ZAPIGWA FAINI

March 27, 2015
Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es salaam, kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom.
Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom  kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado.
Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika ishirini.
Mchezo namba 117 uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya  Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kukataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Nayo klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(11) baada ya timu yake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano kwenye mchezo dhidi ya Simba SC, huku mshambualiji wake Dany Mrwanda  akipigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(12) kwa kutopeana mikono na wachezaji wa timu hiyo.
Mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 37(f) kwa kupiga teke meza ya   mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Suala la mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe kumshika korodani beki wa Simba SC Murshid Juuko limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu.
Kipa wa timu ya Simba SC, Ivo Mapunda amepewa onyo kwa kufunika tangazo la mdhamini wa Ligi Kuu  (Vodacom) kwa kutumia taulo lake wakati wa mechi dhidi ya Yanga, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake iwapo atarudia kufanya tukio la aina hiyo.
Nao wachezaji Salum Abubakar wa Azam FC na Richard Maranya wa JKT Ruvu wamepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja na kusimamishwa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) kwa kupigana uwanjani kwenye mechi namba 123 ambapo walitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Klabu ya Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) baada ya timu yake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo namba 130 dhidi ya Young Africans uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mechi namba 132 iliyozikutanisha Azam na Ndanda SC kwenye uwanja wa Chamazi, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) baada ya washabiki wake kuwamwagia maji na kuwarushia chupa za maji washabiki wa Azam.
Aidha klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi namba 134 dhidi ya timu ya Mbeya City,  pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo.
Kiongozi wa Stand United, Muhibu Kanu amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu baada ya kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumia lugha ya kuhamasisha vurugu kwa timu yake na kupinga uamuzi wa refarii.
Katika mchezo namba 135 uliochezwa jijini Tanga na kuwakutanisha wenyeji Mgambo Shooting dhidi ya Yanga SC, Yanga SC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuvamia uwanja baada ya mechi namba 135 dhidi ya Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
RIPOTI YA CAG IKULU DAR ES SALAAM MACHI 27,2015

RIPOTI YA CAG IKULU DAR ES SALAAM MACHI 27,2015

March 27, 2015

unnamed

2gdhedhdh
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akimkabidhidhi Ripoti yake Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam machi 27,2015
3jgghh
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikifungua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad (kushoto) Ikulu jijjini Dar es Salaam Machi 27, 2015 Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
unnamed-4
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuju wa Hesabu za Serikali mufa mfupi kabla ya mkuu wa taasisi hiyo Profesa Musa Assad (Watatu kushoto) kuiwasilisha Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watano Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

TRENI YAGONGWA NA GARI ENEO LA KARUME JIJINI DAR

March 27, 2015


Hii ni maeneo ya karume tren limegongana na gar. Yani ni baraa tupu! 

WAJUMBE WA VIONGOZI WA SUDAN KUSINI WAVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA TANROADS

March 27, 2015


Mkurugenzi wa Mipango wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Jason Rwiza, akielezea namna TANROADS inavyofanya kazi za ujenzi wa barabara hapa nchini kwa ujumbe wa viongozi kutoka Sudan Kusini katika ofisi za Wakala hao jijini Dar es salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Barabara wa Sudan Kusini Eng. Kenyata Warille, akifafanua namna Mamlaka yake inavyofanya kazi za ujenzi wa barabara nchini kwao. (Nyuma wa kwanza kulia) ni Mwakilishi wa JICA wa Sudan Kusini Tomoki Kobayashi, akifatilia kwa makini.
Naibu Waziri wa Usafirishaji, Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mh. Simon Mijok (Wa kwanza kulia), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wa Sudan Kusini Eng. Gabriel Makur, baadhi ya vitabu walivyopewa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha taasisi zao za ujenzi.
Ujumbe wa viongozi kutoka Sudani Kusini wakiangalia namna magari yanavyopimwa uzito kwa kutumia njia ya kigitali yenye uwezo wa kurekodi taarifa zote za vipimo na kupatikana katika mtandao wa TANROADS. Mzani huo unapima gari moja kwa muda wa sekunde 30 tofauti na wa zamani.
Gari lililozidisha uzito likipimwa katika mzani mpya wa kisasa wa Vigwaza mkoani Pwani. Magari kama haya yanayozidisha uzito huharibu miundombinu ya barabara nchini.

Ujumbe wa viongozi wa sekta ya ujenzi na mazingira toka Sudan Kusini umepongeza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), kwa namna unavyofanyakazi na kuahidi kushirikiana nao ili kuimarisha sekta ya barabara na madaraja nchini mwao.

Akizungumza katika ziara ya mafunzo inayoendelea hapa nchini Naibu Waziri wa Usafirishaji,Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mhe. Simon Mijok amesema mfumo wa uendeshaji wa TANROADS ni mzuri na unaofaa kuigwa na nchi yake kwani unatoa uhuru kwa wakala kuwa na mtandao wa utendaji nchi nzima.

“Kutokana na miaka mingi ya vita nchini kwetu miundombinu mingi ya barabara na madaraja imeharibika hivyo njia nzuri ya kuifufua kwa haraka ni kuwa na taasisi yenye mfumo wa utendaji kama TANROADS na Mfuko wa Barabara”, amesisitiza Naibu Waziri Mijok.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Barabara ya Sudan Kusini (SSRA) Eng.Kenyata Warille amesema mafunzo wanayoyapata hapa nchini yatawawezesha kufanya mabadiliko muhimu katika taasisi zao za ujenzi na watawatumia watanzania kuwashauri ili watumie muda mfupi kuboresha miundombinu ya nchi yao na kwenda na kasi ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki na Kati. 

Amesema Sudan Kusini licha ya kuwa nchi kubwa kwa eneo bado ina mtandao wa barabara wa Km 19,073 zinazounganisha majimbo kumi ya nchi hiyo yenye watu takriban milioni 12.

Aidha ujumbe huo umepata nafasi ya kujionea namna mizani ya kisasa ya Vigwaza mkoani Pwani inavyofanya kazi na kuahidi kujenga mizani ya namana hiyo nchini mwao kutokana na utendaji kazi wa haraka na unaozingatia teknolojia.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo wa Usafirishaji,Ujenzi na Madaraja ameishukuru Tanzania kwa hatua mbalimbali inazochukua kuipatanisha nchi yake ili amani na utulivu viwepo. Pia amesisitiza kuwa ziara za mafunzo za viongozi wa nchi hiyo zitaendelea na kuwaalika watanzania nao kwenda Sudan Kusini kujifunza.

Naye Mkurugenzi wa Mipango wa TANROADS Eng. Jasson Rwiza ameuhakikishia ujumbe huo kuwa ushirikiano uliopo baina ya taasisi zao utaendelezwa ili kubadilishana uzoefu na hivyo kuwezesha barabara za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zipitike kwa urahisi na kukuza uchumi wa nchi zao.
KATIBU MKUU- UTUMISHI BW. GEORGE D. YAMBESI ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA

KATIBU MKUU- UTUMISHI BW. GEORGE D. YAMBESI ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA

March 27, 2015

1
Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akikabidhi ofisi kwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu baada ya kustaafu Utumishi wa Umma.Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwake.
2
Katibu Mkuu -Utumishi Bw. George D. Yambesi (katikati) akipongezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bw. Aloyce Msigwa, (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. HAb Mkwizu. Bw. Yambesi amestaafu Utumishi wa Umma.
………………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi amestaafu Utumishi wa Umma.
Akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi Bw. Yambesi amewashukuru Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ushirikiano katika kutekeleza majukumu na kufikia mafanikio na malengo yaliyopangwa.
 
“Nimefurahi kufanya kazi na kila mmoja wenu katika kipindi chote hata pale rasilimali zilipokua chache kila mmoja wenu alijitahidi kufikia lengo la kuwahudumia wadau wetu” 

Bw. Yambesi alisema na kuongeza jambo la msingi ni kuhakikisha Watumishi wanaendelea kujengewa uwezo ili ubora wa kazi na huduma uendelee kuwa wa kiwango stahili.
 
Katibu Mkuu Bw. Yambesi aliainisha kuwa amekua Mtumishi wa Umma kwa muda wa miaka 38 na kwa hilo anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kutekeleza majukumu mbalimbali kwa muda wote aliotumikia Umma.
 
Wakati huohuo, Naibu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. HAB Mkwizu alimpongeza Bw. Yambesi kwa utendaji wake mzuri. “Unastaafu lakini umejenga uwezo kwa wanaobaki ofisini hivyo kiwango cha huduma zinazotolewa na ofisi na ushirikiano tutaendeleza” Bw. Mkwizu alisema.

KUIONA STARS, THE FLAMES 5,000/

March 27, 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.

Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa kuwakabili the Flames.

Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba,ikiwa na kikosi  kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.

Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.

Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.


MALAWI YAWASILI MWANZA
Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo - Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini),  Harry Nyirenda (Black Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe)

Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.

Kesho jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij na kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa siku  ya jumapili.

   
 ASILIMIA 40 YA WANAWAKE Z’BAR WANAISHI MAISHA DUNI

ASILIMIA 40 YA WANAWAKE Z’BAR WANAISHI MAISHA DUNI

March 27, 2015

DSC_0081
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (aliyefunikwa mwamvuli) akiwasili kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika ndani ya ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UTAFITI uliofanywa na taasisi ya wanawake nchini Zanzibar ya Zanzibalicious Women umeonyesha kuwa asilimia 40 ya wanawake Zanzibar, wanaishi katika mazingira duni ya umasikini kwa kutojitambua na kukosa elimu ya uelewa jinsi ya kukabiliana na mazingira waliyomo.

Akisoma risala siku ya wanawake mbele ya mgeni rasmi mke wa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mama Mwanamwema Shein , katika siku ya wanawake hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal alisema hali hiyo ni changamoto kubwa na sasa kunatafutwa namna ya kumfikia mwanamke huyu ambaye ameshagota katika jamii yetu.

“Mama Shein asilimia hii ni kubwa saana, na sisi kama wanawake ambao tayari tumejaaliwa elimu na tunajitambua, ikiwa ni pamoja na tayari tumepiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali, tumeguswa sana sana na suala hili.” Alisema Shekha.

Zanzibalicious ni umoja wa wanawake wanaoishi Zanzibar,ulioanzishwa mwaka 2011,na kusajiliwa rasmi mwaka 2013, ikiambatana na uzinduzi uliofanyika tarehe 28 Machi 2014.
DSC_0227
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akiwasili kwenye sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel.

Mweka hazina huyo alisema kwamba wanajiuliza maswali mengi kama mwanamke huyo elimu ya kujikwamua imemfikia au kama kuna jitihada zozote za kumfikishia elimu hiyo.
“Je hili ni jukumu la serikali peke yake? Au sisi tunatakiwa tujumuike na serikali? mheshimiwa mgeni rasmi tumeona ya kwamba tuungane pamoja na serikali katika kutekeleza suala hili.” Alisema Shekha akielezea nia ya taasisi hiyo ya kuondoa umaskini miongoni mwa wanawake nchini Zanzibar.

Alisema taasisi yao inajipanga kutoa elimu za aina mbili ili awali kumuwezesha kujikimu kupitia ujasiriamali, kwa kumpatia elimu kwa vitendo,kwa mfano:-ushonaji,ufugaji na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali na pili kumtoa katika hali ya upweke ili elimu atakayopata imfikishe kwenye mifuko mbali mbali pamoja na mfuko wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein .
Alisema katika program hiyo wanatarajia baada ya miaka 2 wanawake 100 watakuwa wanajitegemea wenyewe na kuwa mabalozi katika kuelimisha wanawake wengine zaidi.
DSC_0471
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akisoma hotuba wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Zanzibalicous Women Group na kufanyika ndani ukumbi wa Salama, Bwawani hoteli mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Ummukulthum Ansel.

“Na kama kila mwanamke akiweza kuelimisha wanawake katika kaya yake ,baada ya miaka kadhaa, Zanzibar itakuwa na wanawake walioweza kujikomboa katika dimbwi hili la kuishi maisha duni.” Alisema.

Akizungumzia mafanikio ya asasi hiyo alisema kwamba imefanikiwa kutoa elimu na kuwawezesha kina mama kuunda vikundi vidogo vidogo vya maendeleo kwa kuanzisha miradi mbalimbali, kwa mfano kina mama wa Chaani na Matemwe.

Aidha imetoa misaada ya hali na mali kwa waathirika wa madawa ya kulevya ikiwa ni moja ya kumkwamua mwanamke na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wasiojiweza ikiwemo hospital kuu ya Mnazi mmoja na kina mama wajane.

Alisema pamoja na mafanikio hayo bado wanawake wanakabiliwa na changamoto za ndoa za utotoni, uzazi salama, ukatili wa kijinsia,mfumo dume, ubaguzi na mimba za utotoni.
Mhe.Mgeni rasmi, Umoja huu umekuwa ukiendesha shughuli zote tokea mwaka 2011 kwa kutegemea michango yetu sisi binafsi.
DSC_0314
Baadhi ya wakinama waliohudhuria sherehe hiyo wakionekana kufurahishwa na hotuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani).

Changamoto hii imesababisha kutokutimiza kwa malengo yetu kwa muda tulioupanga kutokana na kukosa fedha za kutosheleza utekelezaji wa malengo hayo.

Akijibu risala hiyo Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, ameikumbusha jamii kuunganisha nguvu zao kuwakomboa wanawake kujiendeleza kimaisha na kujiongezea kipato.

Alisema hatua hiyo itaongeza kasi ya kuimarisha ustawi wa familia na jamii hususan wanawake wanaoishi vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto zaidi.

Alisema sherehe ya siku ya wanawake duniani inakuwa na maana zaidi kama juhudi zitafanyika kuangalia changamoto na kujipanga kuzifanyia kazi.

“Rai yangu ni kuwa tuwazingatie zaidi akina mama wanaoishi vijijini na wenye mahitaji maalum kutokana na kukosa fursa kama hizo za kuwaendeleza kimaisha”, alisisitiza.
DSC_0344
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Bi. Shekha Hilal akisoma risala kwa mgeni rasmi Mke wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani) Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicous Women Group, Bi. Evelyne Wilson.

Aidha, aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiandaliwa vyema linaweza kushinda katika mapambano yanayokusudiwa huku akisisitza mshikamano ili kufikia malengo yanayowekwa.

Akizungumzia ujumbe wa sherehe hizo ambao ni kuhamasisha hatua mathubuti kumwendeleza na kumtambua mwanamke, alitoa rai kwa wanawake kushirikiana na serikali katika kampeni za kupambana na madhila wanayokabiliana nayo ikiwa ni pamoja na ukatili wa watoto na wanawake.

Kuhusu uzoefu wake katika maisha na malezi ya watoto, alisema amebahatika kupata watoto 11 ambao amewalea katika mazingira mbalimbali ikiwa ni kwenda na kurudi kazini na kuwa pekee huku mumewe akiwa safarini kikazi.

Aidha, aliwataka wanawake kuwa wastahamilivu katika malezi ya watoto hasa watoto Njiti ambao huzaliwa kabla ya kufikisha muda.
Hata hivyo aliwaonya wanawake wanaojali kujiremba na kuwa sahau watoto na kukumbusha kwa ‘watoto ni wageni’ kwamba wanahitaji matunzo na ukarimu mkubwa kutoka kwa wazazi wao.
IMG_6571
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Mfuko wa Zanzibalicious Women Group kwa kuchangia shilingi milioni tano, wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wanawake duniani visiwani Zanzibar yaliyoandaliwa na Zanzibalicious Women Group na kufanyika katika ukumbi wa Salama uliopo Bwawani Hotel Zanzibar. Kulia ni Mwenyekiti wa Zanzibalicious Women Group, Bi Evelyne Wilson Baruti.
DSC_0082
Mweka hazina wa Zanzibalicious Women Group, Shekha Hilal akinakili majina ya watu waliokuwa wakichangia kwenye harambe ya mfuko wa Zanzibalicous Women Group uliozinduliwa rasmi na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani).
DSC_0074
Mbunifu nguli wa mavazi Mama wa mitindo, Asia Idarous akinadi moja ya nguo alizotengeneza kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Zanzibalicious Women Group.
DSC_0075
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo akitangaza dau la kununua nguo hiyo iliyokuwa ikinadiwa kwenye harambe ya mfuko wa ZWG iliyozinduliwa na Mama Mwanamwema Shein.
DSC_0091
Meza kuu kwenye picha ya pamoja na Zanzibalicous Women Group.
Unaweza kutembelea mtandao wao na kuona shughuli mbalimbali walizozifanya hapa http://www.zanzibalicious.org/
DSC_0388
Mmoja wa wadhamini ZANLINK wanaotoa udhamini kwa Zanzibalicious Women Group wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo
William Lukuvi aanza ziara mkoani rukwa

William Lukuvi aanza ziara mkoani rukwa

March 27, 2015

1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya alipowasili uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuanza ziara ya kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo. 
New Picture (7)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kuweka jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na NHC kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (1)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na Kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya nyanda za juu kusini Bw. Msigwa mara alipowasili Mkoani Rukwa kutatua migogoro ya ardhi.
New Picture (5)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoa msimamo wa dhati wa serikali (kwa wananchi waliofurika kumsikiliza hawapo pichani) wenye nia ya kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kati ya mwekezaji na wananchi wa vijiji vya Skaungu na Mawensuzi alipofika katika eneo la Malonje Wilayani Sumbawanga.
New Picture (12)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwenye nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Mkoani Rukwa. Alisisitiza Halmashauri nchini kutenga ardhi kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuu.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi (hayupo pichani) jana.
New Picture (13)
Mbunge wa Sumbawanga Mhe. Hilal Aeshi akiishukuru NHC kwa kujenga nyumba za makazi eneo la Jangwani kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (4)
Mwenyekiti wa kijiji cha Skaungu Bw. Pascal Mwanakatwe akisoma risala kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi kuelezea mgogoro wa ardhi unaokabili kijiji hicho na mwekezaji kanisa la Efatha baada ya Waziri Lukuvi kufika eneo la Malonje kuwasikiliza wananchi ili serikali ipate mwelekeo wa kutatua mgogoro huo.
New Picture (2)
Watendaji wa sekta ya ardhi wakiratibu mazungumzo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa Mkoa wa Rukwa (hawapo pichani ) juu ya migogoro ya ardhi inayowasumbua wananchi.
New Picture (3)
  Wananchi wa kijiji cha Skaungu wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipofika kijiji kilichopo kilomita 50 kutoka mjini Sumbawanga kueleza nia ya serikali ya kumaliza mgogoro wa wananchi na Kanisa la Efatha ambalo ni mwekezaji na mmiliki wa mashamba yanayolalamikiwa na wananchi na kukisababisha mauaji ya mara kwa mara.
New Picture (9)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka rasmi jiwe la msingi katika nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani mjini Sumbawanga kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
New Picture (8)
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya ujenzi unaofanyika eneo la Jangwani kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili kuweka jiwe la msingi la nyumba hizo jana.
New Picture (6)  
Kikundi cha ngoma za kifipa kikiburudisha wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za makazi zinazojengwa na NHC eneo la Jangwani Sumbawanga muda mfupi kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi kuwasili eneo hilo.
     New Picture (14)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisikiliza na kupokea barua za malalamiko ya wananchi waliofurika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa jana ili kuwasilisha kero zao za ardhi.